read

Kupeleka Macho Chini na Kulinda Heshima.

877. Allah swt anatwambia katika Qur'an Tukufu, Sura An Nuur, 24, ayah ya 30.

قُلْ لِلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ

Waambieni waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Allah swt anazo khabari za wanayo yafanya.

878. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anatuambia, Man la Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 18:

“Kutazama kiharamu kwa wale walio haramishwa kwetu ni sawa na mshale kutoka upinde wa Shaytani ambao imejaa sumu. Yeyote anayejiepusha nao kwa ajili ya Allah swt, na wala si kwa sababu zinginezo, basi Allah swt atampa imani ambamo yeye ataipata furaha ndani mwake.”

879. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J. 5, Uk. 559:

“Zinaa ya macho ni kuangalia yale yaliyo haramishwa, kwa mtazamo wa matamanio,
Zinaa ya midomo ni kuwabusu wale walio haramishwa (wasio maharimu), na
Zinaa ya mikono ni kuwagusa (mikono na sehemu zingine za wale walio haramishwa) bila kujali iwapo atakuwa na hamu au hatakuwa na hamu ya kujamiiana.”

880. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Al-Kafi, J. 5, Uk. 559:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amemlaani yule mtu ambaye anaangalia sehemu za siri za mwanamke ambaye si halali kwake, na vile vile amemlaani yule mtu ambaye anafanya khiyana pamoja na mke wa ndugu yake, na vile vile yule mtu ambaye anachukua rushwa kwa watu kwa msaada wanaohitaji kutoka kwake.”