read

Kutoa Sadaka na Ubahili:

767. Mali ya mchoyo huliwa na warithi wake au hupeperuka bila kujulikana.

768. Hakuna mtu mwenye upweke vile alivyo bahili.

769. Mchoyo ni mweka/mtunzi hazina wa warithi wake.

770. Ubahili na uchoyo huangamiza upendo wa urafiki wa kweli.

771. Ubahilifu ni kujipatia ubadhirifu.

772. Kuwa mchoyo kwa kile ulichonacho ni kutomwamini Allah swt.

773. Sifa ya upole na wema huangamizwa kwa ubahili.

774. Fedha haimnufaishi mwenye kuwa nayo hadi hapo atenganapo nayo.

775. Maovu hufichwa kwa ukarimu.

776. Bora wa watu ni yule afaaye watu

777. Hakutakuwa kuwafadhili watu kwa mifuko mitupu.

778. Fadhila huuliwa kwa matumizi fidhuli.

779. Uachie ngome ya Sadaqa iilinde ufanisi wako.

780. Kutoa baada ya kughairi ni bora zaidi kuliko kughairi baada ya kutoa.

781. Uso ulio mcheshi ni mojawapo ya ne’ema mbili.

782. Usimuudhi mtu yeyote yule pale akutakiapo kila la kheri.

783. Fadhila na ukarimu hupatiwa sifa.

784. Fadhila ya kweli (kwa moyo safi) huondoa dhiki zote

785. Makosa ya mwenye kutoa fadhila ni afadhali kuliko dharau ya mchoyo.

786. Fadhila isiongozwe kwa uoga wala kuwa na matumainio ya kupata chochote (tamaa).