Misemo
1231. Utakatifu huambatana na busara
1232. Kutoridhika kwa mtu kutamfutia utulivu
1233. Saumu ya akili ni kuiepusha kutoka matamanio yote yaliyo maovu
1234. Uoga ni kutokana na moyo uliodhoofika na usio na uimara
1235. Vitu vinavyotuharibu sisi ni karibu tu tutakavyo ungana navyo
1236. Kufuatilia mateso na matatizo yamkabiliayo mtu, yanadhihirisha ukubwa wake na ustahimilivu na uwema wake
1237. Yeyote asemaye maneno na misemo ya wale wenye busara, basi ndivyo anavyojivisha utukufu wao
1238. Maisha marefu hukutana na matatizo mengi
1239. Ardhi ni msafishaji bora
1240. Makabiliano ndiyo yanayomsaidia sana mtu
1241. Ukweli na mabishano ndiyo yaliyo bora kabisa
1242. Mtu ajigambaye basi ndiye ajidhalilishaye yeye nafsi yake
1243. Mtu mwenye mafanikio bora kabisa
1244. Yeyote yule mwenye kuhofu ndiye abakiaye salama
1245. Tajiri hasemwi kwa kuongezeka kwa uwema na kuiendeleza subira
1246. Uso wenye mcheko (mcheshi) huuepusha kutoka moto wa uadui
1247. Kwa kukatalia zawadi ndiko kunamaanisha kutokuwa na shukrani
1248. Hakuna chochote mbali na kule kufanya Tawbah ila ni kujipunguzia ule mwenendo unaofutilia
1249. Usiligeuze tumbo lako likawa ni kaburi la wanyama (kwa kula sana nyama)
1250. Ugonjwa ni moja wapo ya aina mbili za kifungo
1251. Kuzuzuliwa kwa ghadhabu ni dhambi pia
1252. Ndugu huongezea na kufurahikia furaha zetu na hutuondolea na kutuponya yale maumivu tuliyonayo
1253. Ubongo (akili) huwa ni mfano wa ghala (stoo) ambayo ilifungwa kabisa na maswali tu ndio zifunguazo kutoka humo
1254. Hata kama pazia itaondolewa mbele yangu ,basi hakuna chochote kile kitachoongezeka katika imani yangu
1255. Pale Allah swt ampendeleapo Mja wake yeyote,Yeye humshugulisha katika mapenzi yake
1256. Nywele za kijivu huelezea kuwa ni hatua ya kuikaribia mauti