Mwanamke naKujipamba.
881. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Wasa'il ush-Shi'ah, Volume 14, Uk. 10:
“Neno asemalo mwanamme kumwambia mke wake:
‘Nakupenda basi kamwe halitatoka moyoni mwa mke wake’.”
882. Amesema Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., Al-Kafi, J. 4, Uk. 119:
“Haijali chochote au vyovyote vile mwanamke ajirembavyo kwa ajili ya bwana wake.”
883. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Man la Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 6:
“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameharamisha kujiremba kwa mwanamke kwa ajili ya mwanamme mwingine mbali na mume wake mwenyewe na akasema:
‘Na kama atafanya hivyo, basi ni haki ya Allah swt kumchoma moto katika Jahannam. (Hadi hapo atakapofanya Tawba1 )”
884. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Wasa'il ush-Shi'ah, J. 14, Uk. 11:
“Yeyote yule anayezidisha mapenzi yetu (Ahlul Bayt a.s.) basi na atazidisha mapenzi yake kwa mke wake vile vile.”
885. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Wasa'il ush-Shi'ah, J. 20, Uk. 30:
“Bora katika wake zenu ni yule ambaye ni mcha Allah swt na mtiifu kwa mume wake katika mapenzi na kujirembesha (lakini sio kuwavutia wanaume wengine).”
- 1. Mimi nimekitarjumu kitabu kimoja cha Ayatullah Sayyed Dastaghib Shiraz kinacho zungumzia Tawba kwa kirefu na mapana kwa hiyo ukitaka kusoma zaidi kuhusu Tawba tafadhali sana tafuta kitabu hicho ambacho kitakufaidisha sana.