read

Ndoa ‘Ibada Kuu.

810. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 384:

“Raka’a mbili za sala zinazosaliwa na mtu aliyeoa ni nzito kuliko yule asiyeoa ambaye anakesha usiku kucha katika ibada na kufunga saumu nyakati za mchana.”

811. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Usingizi wa mtu aliyeoa ni afadhali mbele ya Allah swt kuliko ibada afanyazo mtu asiyeoa usiku kucha na anayefunga saumu nyakati za mchana.”

812. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Wengi wa watendao wema katika ‘ummah wangu ni wale waliooa na kuolewa wakati watendao maovu wengi wao ni wale wasio oa au kuolewa.”

813. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema, Bihar al-Anwaar J. 103, Uk. 217:

“Siku moja mtu mmoja alimwijia baba yangu naye a.s. alimwuliza iwapo alikuwa ana mke naye akajibu alikuwa hana. Hapo baba yangu a.s. alimjibu kuwa yeye hawezi kulala usiku mmoja bila ya mwanamke hata kama atapewa badala yake dunia nzima na yale yote yaliyomo ndani yake.

Na hapo Imam a.s. alimwambia kuwa Raka’a mbili anazosali mtu aliyeoa ni bora kuliko ibada ya yule asiyeoa kwa kukesha usiku kucha na kufunga saumu katika nyakati za mchana. Na baadaye Imam a.s. alimpa Dinar za dhahabu saba na akamwambia akaolee kwa hayo.”