read

Salaa ya Jama’a.

1012. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.,amesema Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 4:

“Allah swt huheshimu sana yule mja anayesali sala kwa Jama’a na baada yake anapoomba kitu chochote basi Allah swt lazima humtimizia.”

1013. Al Imam Musa al-Kadhim a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 4 na Wasa'il ush-Shi'ah, J. 8, Uk. 290:

“Fadhila za sala ya Jama’a kwa sala ya mtu anayesali peke yake ni kila raka’a moja katika Jama’a ni bora kuliko raka’a elfu moja (1000) zinazosaliwa na mtu peke yake.”

1014. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Mustadrak-ul-Wasa'il, J. 6, Uk. 446:

“Sala moja ya mtu katika Jama’a ni bora kuliko sala za miaka arobaini anazosali akiwa nyumbani kwake (peke yake).”

1015. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 6:

“Safu ya mistari katika sala ya Jama’a inayosaliwa juu ya ardhi ni sawa na safu za Malaika huko mbinguni; na Raka’a moja inayosaliwa katika Jama’a ni sawa na Raka’a ishirini na nne na kila raka’a moja inayosaliwa na wapenzi wa Allah swt kuliko sala za miaka arobaini. Hivyo, siku ya Qiyamah ambayo ni siku ya uadilifu wakati Allah swt atakapo wakutanisha wanaadamu wote kuanzia mwanzoni hadi mwisho, basi hakutabakia na muumin yeyote ambaye amesali sala ya Jama’a, kwamba Allah swt atampunguzia shida zake za siku ya Qiyamah na ataambiwa aingie Jannah.”

1016. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. siku moja aliijiwa na Kipofu mmoja ambaye alisema, At-Tahdhib, J. 3, Uk. 266:

“Kulikuwa hakuna mtu yeyote wa kumchukua Msikitini ili aweze kushiriki katika sala ya Jama’a pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pale aliposikia Adhana ikitolewa.

Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia:
“Funga kamba kutoka nyumbani kwako hadi Msikitini na ushiriki katika sala ya Jama’a.”

1017. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 11:

“Mtu yeyote ambaye anaiacha sala ya Jama’a bila ya kuwa na Udhuri inayokubalika bali bila sababu yoyote, kwa misingi ya kutotaka kushiriki katika mkusanyiko wa Waislam, basi atakuwa hana Sala yoyote.”

1018. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 88, Uk. 12:

“Kwa hakika sala ya Jama’a imefaradhishwa ili kuwepo imani halisi katika umoja, katika Islam, na katika kumwabudu Allah swt kiwazi wazina ambayo imedhihirishwa kuwa bayana, kwa sababu, ili iweze kuwadhihirikia watu wa mashariki na wa magharibi (wa dunia hii).

Hivyo ukweli na asili wa Uislam utadhihirika na kujulikana na makafiri na mapagani kabla ya Uislam utakuwa ni kama kiza mbele ya nuru, kiza ambacho hatimaye kinapotea.

Vile vile sala ya Jama’a husababisha watu kutambuana na kuelewana na inawezekana wengine wakawa mashahidi kuhusu wengineo kuhusu Uislam wao, ambamo kuna uwezekano na vile vile kushirikiana katika mambo mema na ya kumfurahisha Allah swt mambo ambayo yanawazuia wasimuasi Allah swt kupita kiasi.”