read

Shahidi na Shahada.

966. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J. 10, Uk. 100:

“Kuna jema kwa kila jema hadi wakati mtu anapouawa katika njia ya Allah swt na zaidi ya hapo hakuna tena jema lingine juu yake. (Kupigana dhidi ya maadui Waislam ambao wanawaua Waislam)”

967. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Furu'i al-Kafi, J. 5, Uk. 54:

“Yeyote yule anayeuawa katika njia ya Allah swt kama shahidi, basi yeye kamwe hataulizwa chochote kuhusu madhambi yake. (Madhambi yake yote yatakuwa yamesamehewa kwa ujumla).”

968. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 149:

“…kwa kiapo cha yule ambaye maisha na roho yangu iko mikononi mwake, iwapo viumbe vyote vya duniani na angani vikijumuika pamoja kumuua muumin ambaye hana kosa hata moja au watakapo shawishiwa kufanya hivyo, basi Allah swt atawatia wote kwa pamoja katika moto wa Jahannam.”

969. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Wasa'il ush-Shi'ah, J. 15, Uk. 14:

“Hakuna tone ambalo linalopendwa na Allah swt kuliko tone la damu ya yule, linalomwagika akiwa anakuwa shahidi katika njia ya Allah swt.”