read

Sifa za Kupendeza za Mwanamke

1022. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Wasa'il ush-Shi'ah,Vo. 20, Uk.172

“Malipo ya mwanamke mcha Allah swt kwa kumpa mume wake bilauri moja ya maji ni zaidi ya kufanya ibada mwaka mzima ambamo mchana anafunga saumu na usiku zake anakesha katika kufanya ibada.”

1023. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Kafi, J.5, Uk. 508:

“Ni kwa mwanamke kujiweka msafi kabisa kwa kujipaka manukato bora kabisa na kuvaa mapambo ambayo yatamfanya yeye amvutie bwana wake na ajiweke tayari kwa ajili ya bwana wake usiku na mchana.” 1

1024. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Nahjul Balagha, Msemo 494:

“Jihadi ya mwanamke (vita katika njia ya Allah swt ) ni kuwa na uhusiano mwema na kuwa mshiriki wa bwana wake.”

1025. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Usuli kafi, J. 5, Uk. 327

“Iwapo ningetaka kukusanya mema yote ya dunia hii na Aakhera kwa ajili ya Mumin basi mimi ningeziweka kwa ajili ya:
moyo mnyenyekevu,

ulimi wenye shukurani na isemayo mema,

mwili ufanyao subira wakati wa shida na dhiki.

(Kwa ajili ya mwanamme mimi ningempa) Mke mcha-Allah swt ili anapouona uso wake anajawa na furaha na yeye (mwanamke) anaihifadhi na kulinda mali yake, pale bwana wake anapokuwa hayupo.”

1026. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J.103, Uk. 252

“Amelaaniwa! Amelaaniwa kabisa mwanamke yule ambaye anautonesha moyo wa mume wake na kumfanya akasirike.

Lakini amebahatika kabisa mwanamke yule ambaye anamheshimu bwana wake wala hamghadhabishi na huwa mtiifu kwa bwana wake.”

1027. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema Bihar al-Anwaar, J.103, Uk. 235

“Bora ya mwanamke ni yule anayezaa, mvutiaji kimapenzi, mtunza siri zenu, na mcha-Allah swt. Na humtii bwana wake na hupendwa na jama’a na ndugu zake. Pale anapokuwa pamoja na bwana wake, anamwonyesha urembo na mavazi yake ambayo kwa hakika huyaficha kwa ajili ya wanaume wengine isipokuwa mume wake tu.

Kwa hakika huwa msikivu na mnyenyekevu kwa mazungumzo yake na huzitii amri zake. Pale anapokuwa faragha anavaa vizuri kabisa na kutimiza mahitaji ya bwana wake kutoka kwake. Daima huwa anakuwa amevaa vizuri na kujirembesha kwa ajili ya bwana wake tu na kamwe huwa si mtu aliyejisahau kwa ajili ya bwana wake (hujiweka tayari kwa ajili ya bwana wake.)”

1028. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J.104, Uk. 98:

“Kutokea kwa furaha ya mwanamme Mwislamu ni kwamba ana mke mcha-Allah swt na
nyumba kubwa ya kukidhi wananyumba, usafiri mzuri na watoto wema.”

1036. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema
“Vita vya Jihad kwa ajili ya mwanamke ni kuwa na uhusiano na kuwa mwema kwa mume wake na haki za mwanamme kwa mke wake ni zaidi ya haki za wote juu yake.”

1029. Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu Surah Al-Baqara, 2, Ayah ya 231:

وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ ۚ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِتَعْتَدُوا ۚ وَمَنْ يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ وَلَا تَتَّخِذُوا آيَاتِ اللَّهِ هُزُوًا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنْزَلَ عَلَيْكُمْ مِنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُمْ بِهِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

Na mtakapo wapa wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakayefanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Allah swt kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Allah swt juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hikima anachokuonyeni kwacho. Na mcheni Allah swt , na jueni kwamba hakika Allah swt ni Mjuzi wa kila kitu.

1030. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Wasa'il ush-Shi'ah, J.22, uk.9:

“Muoe na wala msitoe talaqa kwa sababu ‘Arshi Ilahi hutetemeka kwa talaka.”

1031. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Al-Kafi, J. 6, Uk. 54

“Allah swt hufurahishwa mno kwa nyumba ile ambamo harusi huwapo na hughadhabishwa kwa nyumba ile ambamo huwa na talaka. Na hakuna kinachomkerehesha Allah swt kama talaka.”

  • 1. Ni jambo la kusikitisha kabisa kuona wanawake wa siku hizi ambao wana tabia za kutembea nje ya nyumba iwe kikazi au kimatembezi Wao wanapokuwa nyumbani wanavaa nguo zilizochakaa na chafu na utakuta nywele na nyuso zao zimechakaa na kiasi kwamba utakapomwona hautamtamani lakini iwapo atakuwa akitaka kwenda nje basi utafikiria kuwa bibi harusi yupo nyumbani kwako kwani wataoga na kuvaa mavazi mazuri na kujipaka vipodozi na manukato kiasi kwamba watakapo pita mtaa mzima hujawa kwa manukato mazuri. Hapo ni kwa ajili ya kwenda nje. Hivyo inamaanisha kuwa amejiandaa hivyo kwa ajili ya wengine na wala si kwa ajili ya mume wake aliye nyumbani. Jambo hili Islam inakataa na kupinga. Wavae vizuri nyumbani na wanapotaka kwenda nje. Mume apewe kipaumbele !