read

Udondozi wa Ubashiri

1657. Kutoka dalili na mabashiri ya kudhihiri kwa Imam Mahdi a.s. hapa kuna madondoo machache ambayo yamechambuliwa:

                        1. Uasi wa Sufiani

2. kuuawa kwa mtu mashuhuri kutoka katika kizazi cha Imam Hasan as1

3. Ikhitilafu baina ya Bani Abbas kwa matakwa ya dunia.

4. Kupatwa kwa jua katika mwezi wa Ramadhani, ikifuatiwa na kupatwa kwa mwezi mwishoni mwa mwezi huo wa Ramadhani.

5. Beyda (mahala baina ya Makkah na Madina) itadidimia ardhini,

6. Ardhi katika upande wa Mashariki na upande wa Magharibi zitadidimia,

7. Jua wakati wa asubuhi litaonekana liko papo hapo bila kutembea hadi wakati wa mchana na baadaye litachomoza kutoka Magharibi.

8. Mcha Mungu atauawa nyuma ya msikiti wa Kufa pamoja na watu sabini wengine.2

9. Mtu mwema kutoka ukoo wa Bani Hashim atachinjwa baina ya Rukn na Makam huko Makkah

10. Kuta za Msikiti wa Kufa zitaporomoka.

11. Bendera nyeusi zitatokezea huko Khorasan.

12. Mtu kutoka Yemen ataongoza uasi.

13. Mtu atakayetokea nchi za Maghreb ataonekana huko Misri na ambapo atapata mamlaka makubwa.

14. Warusi watafika Bara la Arabia

15. Wazungu watafika Palestina

16. Upande wa Mashariki kutaonekana kwa nyota yenye mkia. Mwanga wake utaonekana kama ule wa mwezi na ncha zake zote zitakuwa moja (zitaungana).

17. Kutaonekana uwekundu mkubwa sana mbinguni.

18. Kutazuka moto mkubwa sana katika Mashariki ya kati ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu hadi saba.

19. Wale wasio Waarabu watawafukuza Waarabu kutoka ardhi zao.

20. Utawala wa kifalme utakwisha nchini Iran

21. Wamisri watamuua kiongozi wao.

22. Bendera tatu zitakusanyika Syria

23. Kutazuka mizozo mikubwa na Syria itateketezwa.

24. Bendera za Waarabu na Bani Qais zitatoka Misri.

25. Bendera ya Banu Kinda itapepea Khorasan.

26. Jeshi kubwa sana litapita Hira.

27. Mabango meusi yatafika kutokezea Mashariki.

28. Maji ya mito ya Furat yatafurika katika mitaa ya Kufa.

29. Kutatokezea watu sitini watakaodai kuwa wao ni Mitume.

30. Sayyid kumi na wawili watadai kuwa wao ni Imamu Mahdi

31. Mtu mwenye heshima kubwa kutoka Bani Abbas atachomwa moto hai karibu na Khankin.

32. Kutajengwa na daraja katika Baghdad katika sehemu za Kharah.

33. Kutakuwa na tufani ya upepo mkali katika Baghdad wakati wa asubuhi na kutafuatiwa na kupasuka kwa ardhi ambamo baadhi ya sehemu itadidimia ardhini.

34. Mauti, vifo na maangamizo yatakithiri huko Iraq kiasi kwamba watu watakuwa kama wamewehuka.

35. Vikundi vitapigana mno huko Iran.

36. Sura za jumuia zitachafuliwa.

37. Watumwa wataanza kutawala nchi za Mabwana wao.

38. Sura kama ya binadamu itaonekana karibu na jua.

39. Makaburi yatafumuliwa na

40. Waliokufa watapewa uhai.

41. Kutakuwa na mvua itakayonyesha kwa mfululizo wa siku ishirini na nne ambayo itahuisha ardhi iliyokuwa imekufa. Kwa hakika wakati huo ndio utakuwa wakati wa kudhihiri kwa Imam Mahdi Sahib az-Zamaan a.s.

  • 1. Tazama maelezo hapa chini na 45
  • 2. Inasemakana hili limetukia: Ayatullah Muhammad-Baqir Al Hakim aliuwawa Najaf August 29, 2003 pamoja na watu zaidi ya 70 baada ya Kuswalisha swala ya Ijumaa. Sayyid al Hakim pia litokana na kizazi cha Imam Hasan (as)(Mji wa Najaf ambao uko nyuma ya mji wa Kufa haukuwepo zamani)