read

Ulafi Na Matumaini Ya Kipuuzi.

945. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Nahjul Balagha Barua no. 52:

“Ingawaje uchoyo, uoga na uroho ni vitu vyenye sifa tofauti, lakini vyote viko sawa katika mambo ya kufikiria kwao kuhusu Allah swt.”

946. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Man la Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 418:

“Iwapo mwanaadamu atakuwa na mabonde mawili ambamo kumejazwa dhahabu na fedha, basi yeye hatatosheka nayo bali atakwenda kuitafuta ya tatu.”

947. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Al-Usul-i- Kafi, J. 2, Uk. 320:

“Yeyote yule anaye uendekeza moyo wake kwa dunia hii basi atapatwa na hali tatu:
Mateso yasiyoisha, kiu ya matamanio isiyoisha na matumaini yasiyo timika.”

948. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 240:

“Wako kiasi gani cha watu ambao ni waovu na siku zao ziko zinahesabika lakini bado wanaendelea kwa juhudi zao zote za kuitafuta hii dunia.”