read

Upole na Matokeo Yake Mazuri

996. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ,Bihar al-Anwaar, J. 71, Uk. 373:

“Kwa hakika mja anaweza kujipatia daraja la yule anayefunga saumu katika nyakati za mchana na anayesali usiku kucha, kwa tabia zake nzuri za upole.”

997. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia mtoto wake Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. ,Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 111:

“Ewe Mwanangu !
Hakuna utajiri uliona thamani kuliko akili na
hakuna umasikini uliosawa na ujahili;
hakuna ugaidi ulio mbaya kabisa kama kiburi,na
hakuna maisha yenye raha kuliko kuwa mpole.”

998. Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Khisal-i-Sadduq, Uk. 29:

“Kwa hakika, bora ya bora zote ni tabia njema.”

999. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 71, Uk. 394:

“Tabia njema ipo katika njia tatu:
Kujiepusha na vitu vilivyo haramishwa,
kutafuta yale yaliyo halalishwa, na
kutendea haki wana nyumba wake.”

1000. Al Imam Zaynul 'Abediin a.s., amesema Khisal-i-Sadduq, Uk. 317:

“Kauli njema huongezea mali, utajiri, na riziki, na huahirisha ajali, na hutengeneza mapenzi miongoni mwa wenye nyumba, na humfanya mtu akaingia Jannah.”

1001. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 103:

“Yapo mambo matatu ambayo yeyote yule atakayezifikisha kwa Allah swt, basi Allah swt atamfaradhishia Jannah kwa ajili yake:
Kutoa mchango katika umaskini,
desturi nzuri pamoja na watu wote, na
kujitendea haki nafsi yake.”

1002. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk, 100:

“Kwa mambo ambayo umma wangu utajipatia Jannah ni hasa kwa mema yote, na desturi nzuri.”