Ushauriano.
958. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Manhaj-us-Sadiqiin, Tafsiri, J. 2, Uk. 373:
“Iwapo watawala wenu ni watenda wema, na matajiri ni wale wenye kukushukuruni, na mambo yenu yanakwenda kwa ushauriano miongoni mwenu, basi kwenu nyinyi kuishi duniani ni vyema kuliko chini yake. Lakini iwapo watawala wenu ni waovu kwenu nyie, na matajiri ni mabakhili miongoni mwenu, na mambo yenu yanakwenda bila kushauriana, kwa hivyo kwenu nyie kutakuwa afadhali kuwa ndani ya ardhi kuliko kuishi juu yake.”
959. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Ghurar-ul-Hikam, Uk. 336:
“Yeyote yule anayeshauriana pamoja na wenye busara na akili, kwa ajili ya kupata mwangaza ili aweze kupata mwanga katika masuala yake (na ataweza kuona sahihi kile kilicho sawa kutoka na kile kilicho potofu).”
960. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 105:
“Yeyote yule anayeshauriana pamoja na watu wa maelewano, basi huonyesha maendeleo yake….”
961. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Nahaj-ul-Falsafa, Uk. 533;
“Hakuna muumin atakaye kuwa mwovu kwa ushauriano, na wala hakuna atakayefaidika kwa ukaidi wake.”