read

Back Cover

Mahitaji ya zama zetu hizi yanalazimisha kutathmini maswali mengi yenye umuhimu na sio kuridhika na tathmini zake za awali. Mfumo wa haki za ndoa na majukumu ya kifamilia ni miongoni mwa masuala haya.

Suala la msingi kabisa juu ya haki za kifamilia, ni iwapo mfumo wa ndoa unajitegemea na hautangamani na mifumo mingine yote ya kijamii na una vigezo na mantiki yake maalum, au ni moja tu ya mifumo mingi ya kijamii na kuwa vigezo na falsafa zile zile ndizo zinazotumika kulishughulikia suala hili kama ilivyo kwa mifumo mingine ya kijamii.

Tatizo la mahusiano ya kifamilia katika zama zetu sio rahisi sana kiasi kwamba mtu anaweza kulitatua kwa kuandaa kura za maoni ya vijana wa kike na wa kiume, au kwa kuendesha semina. Sio tatizo la nchi wala hakuna nchi iliyodai kulitatua kabisa.

Inakubaliwa na kila rafiki na adui kuwa Qur’ani Tukufu ilifufua haki za wanawake. Hata maadui wanakiri angalau kwamba Qur’ani wakati wa kuteremshwa kwake ilichukua hatua kubwa katika kuboresha hali ya mwanamke na kurejesha haki zake za kibinadamu. Qur’ani ilifufua haki za mwanamke kama mwanadamu na kama mwenzi wa mwanaume katika utu na haki za binadamu lakini haikupuuza jinsia yake wala jinsia ya mwanaume.

Kwa maneno mengine Qur’ani haikupuuza maumbile ya mwanamke. Ndio maana kuna kuwafikiana kikamilifu kati ya kanuni za maumbile na kanuni za Qur’ani. Mwanamke katika Qur’ani ni sawa na mwanaume katika maumbile. Vitabu hivi viwili vikubwa vya kimungu (Qur’ani na maumbile), kimoja kikiwa kimeumbwa na kingine kikiwa kimekusanywa, vinakubaliana na kuafikiana kabisa. Nia ya kitabu hiki ni kuangazia na kuelezea kuafikiana huku.

Kimetolewa na kuchapishwa na:
Alitrah Foundation
P.O. Box 19701
Dar es Salaam, Tanzania
Simu:+255 22 2110640
Fax: +255 22 2131036