Dua

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na watu wangu watakapokuuliza juu yangu, basi hakika Mimi Nipo karibu Nayaitikia maombi ya mwobaji anaponiomba, basi waniombe na waniamini ili wapate kuongoka." 2:186.

Kumwomba Mwenyezi Mungu kama Alivyotuhimiza ni katika mambo muhimu kabisa kwa mja anayemcha Mola wake. Pia Mtume Muhammad (s.a.w.) katika mafunzo yake ya mara kwa mara alisema: "dua ni kiini cha ibada".

Baada ya kuthibiti umuhimu wa kumwomba Mola hapana wakati ambao ni bora zaidi wa kuomba na kuitikiwa kwa haraka kama mwezi wa Ramadhani maana milango yote ya Rehema na Toba huwa wazi.