Johari Za Hekima

Mambo manne ni mema, lakini manne ni bora zaidi kuyashinda.

1. Haya ni njema kwa waume lakini kwa wanawake ni bora zaidi;

2. Uadilifu kwa kila mmoja ni mwema lakini kwa viongozi (watawala) ni bora zaidi;

3. Mzee kutubu madhambi ni vyema lakini kwa kijana ni bora zaidi;

4. Ukarimu kwa matajiri ni mwema lakini kwa maskini ni bora zaidi.

(Al Hakiim)

Mambo manne ni maovu, lakini manne mabaya zaidi kuyashinda.

1. Kutenda dhambi kwa kijana ni kuovu, lakini kwa mzee ni kubaya zaidi;

2. Mjinga kujishughulisha na Dunia ni kuovu, lakini kwa mwanachuo ni kubaya zaidi;

3. Watu kutojishughulisha na ibada na kuwa wavivu ni kuovu, lakini kwa waalimu na wanafunzi wa dini ni kubaya zaidi;

4. Tajiri kujigamba na kujinaki ni kubaya; na kwa maskini ni kubaya zaidi.

(Al Hakiim)