Soma Dua Hizi Ukiuona Mwezi

Ukiuona mwezi umeandama, simama wima huku umeelekea Kibla, na usome:

"Ee Mwenyezi Mungu! Tunakuomba Utuukaribishie mwezi huu kwa amani, imani, na kwa Uislamu kamili (na tunakuomba katika mwezi huu) afya bora, riziki pana, na utuondolee maradhi. Ee Mola wetu! Tujaalie tuufunge wote, tusimame kwa Ibadati, tusome Qur'ani kwa wingi, tujaalie tuupokee, (nao mwezi) Utupokee, na tunakuomba Utuvushe salama.

Pia ni vizuri kusoma Dua hii ya Amiril Muuminina Aly Bin Abi Talib (a.s.) baada ya kuuona mwezi.

“Ee Mola wetu! Ninakuomba heri za mwezi huu na heri za mwanzo wake na ninakuomba mwangaza wake, pia nusura yake, baraka zake, utufuku wake na riziki zake. Pia ninakuomba heri zilizomo katika mwezi huu na heri zijazo, na ninajilinda kwako na shari zitakazokuwemo katika mwezi huu na shari zitakazokuja baada yake.

“Ee Mwenyezi Mungu! Ulete kwetu kwa amani, imani, usalama, na kwa Uislamu, pia tunakuomba baraka, na Utujaalie tukuogope zaidi katika mwezi huu, na mambo yetu yawe ni yenye kuwafikiana na Uyapendayo na Ukayaridhia.”

Dua hizi ni bora zaidi kwa Mwislamu kuzisoma punde tuu baada ya kuonekana mwezi. Na wakati wa kuzisoma ni bora zaidi uwe umeelekea Kibla - yaani huko Makkah.