Yanayoharibu Saumu

Kwa kuwa Mwislamu huwa na hamu kubwa ya kuukaribisha mwezi wa Ramadhani, kadhalika anatakiwa kuwa na hamu ya kujichunga na mambo ambayo huenda yakamharibia saumu yake. Na mambo yenyewe ni haya:

1. Kula japo kitu kidogo sana;

2. Kunywa hata kama ni tone moja;

3. Kumwingilia mwanamke mchana hata kama manii hayakutoka;

4. Kujitoa manii kwa kujichezesha, au kwa kumchezesha mwanamke hata kama ni mkeo pia kunatengua;

5. Kutooga Janaba, Hedhi, au Nifasi hadi alfajiri pasina sababu ya udhuru maalumu pia kunabatilisha Saumu;

6. Kujifikisha vumbi - zito - kooni makusudi na kadhalika moshi wa sigara pia hubatilisha;

7. Enema-Kupigwa bomba yenye kitu cha majimaji (dawa) kwenye tundu ya nyuma pia kutaharibu;

8. Kujitapisha makusudi;

9. Kumkadhibisha Mwenyezi Mungu au Mtume wake Mohammad (s.a.w.) au Maimamu watakatifu kuwa katika jambo fulani walisema hivi hali ni uongo kunabatilisha Saumu;

10. Kujitosa majini makusudi kwa kupiga mbizi, au kukitumbukiza tu kichwa pekee majini pia kunaharibu Saumu.