Hili ni vazi rasmi kwa wanawake wa ki-Islamu kama ilivyoainsihwa katika Qur’an Tukufu, na ni amri sahihi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ni vazi la heshima kwa mwanamke, vazi linalo linda utu wa mwanamke, vazi linalo muondelea mwanamke usumbufu mitaani, vazi linalo linda heshima ya mwanamke, vazi linalo ondoa maovu na uchafu katika jamii, vazi linalo watambulisha wanawake wenye heshima na vazi linalo mlinda mwanamke kutokana na maovu.