read

Neno La Mchapishaji

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la: Al-Hijab Saa'datun laa shiqaaun, kilichoandikwa na, Sheikh Muhammad Ibrahim El-Qazwiniy

Kitabu hiki kinahusu vazi la Hijabu: vazi ambalo ni rasimi kwa wanawake wa kiislamu kwa ajili ya kustiri maungo yao. Maadui wa Uislamu wanalibeza sana vazi hili kiasi cha kutaka kuwakatisha tamaa wavaaji wake ambao ni wanawake wa kiIslamu. Mazingira ya sasa tayari yanaonesha kwamba, azma ya maadui hawa wa Uislamu kiasi fulani inafanikiwa. Kwani sasa hivi katika miji yetu asili mia kubwa ya wanawake wanatembea nusu uchi, na hali ni mbaya sana. Hivyo tulipo kiona kitabu hiki, tukaona ni wakati muafaka tukitoe kwa lugha ya kiswahili, kwa kutekeleza amri ile ya Mwenyezi Mungu ya, "kuamrisha mema na kukataza maovu."

Mwandishi wa kitabu hiki ameelezea kwa ufasaha sana falsafa na hekima ya vazi hili, na kuvunja hoja za wale wote wanaolipinga. Katika kufanya hivyo ametumia elimu, akili na hoja zenye mantiki.

Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Msabah S. Mapinda kwa kukubali kwake kuchukuwa jukumu hili la kutarjum kitabu hiki, kutoka lugha yake ya asili ya Kiarabu kwenda lugha ya Kiswahili. Halikadhalika tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa kwa wasomaji wetu, hususan wanawake wa kiislamu na kuiokoa jamii yetu kutokana na maovu.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 1017
Dar-es-Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2127555 / +255 784 786 121
Barua Pepe: alitrah@raha.com
Tovuti: www.ibn-tv.com
Katika Mtandao: www.alitrah.info