read

Utangulizi

Hamna shaka kuwa historia ya mwanadamu ndio chemchemu na chanzo cha maarifa, chanzo ambacho mataifa yanakihitaji katika safari yake yenye kuendelea. Na ndio chanzo pekee chenye uwezo wa kuhuisha na kulisukuma taifa mbele na kulipa sifa na hadhi maalum huku kikilifunganisha taifa hilo na mizizi yake ya ustaarabu ambayo hulizuwia taifa dhidi ya mmong'onyoko.

Qur'ani imemhimiza kila mwanadamu ikamtaka azame ndani ya his- toria ya mwanadamu na azingatie yaliyomo ili awaidhike na kuongoka, hivyo Mwenyezi Mungu akasema: "Je, hawatembei katika ardhi ili wapate nyoyo za kufahamia au masikio ya kusikilizia?"1 Baada ya Mwenyezi Mungu kutoa historia ya Adi, Thamudi, Firauni, watu wa miji iliyopinduliwa na watu wa Nuh akasema:
"Ili tuifanye ukumbusho kwenu na sikio lisikialo lisikie."2

Historia ya ujumbe mbalimbali wa Mwenyezi Mungu imejaa masomo na mazingatio, masomo ambayo yameonyesha jinsi manabii watukufu walivyojali mataifa yao ili kuyaokoa toka kwenye matatizo mbalimbali.

Pia ujumbe huo umeonyesha lengo na mwelekeo wake wenye kujaa nuru na manufaa. Kwa ajili hiyo sera ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake huwa ni tafsiri ya kivitendo ya misingi na sheria za kiislamu.

Hivyo kusoma sera yao na historia ya maisha yao ni chanzo muhimu cha kuifahamu Qur'ani na Sunna, na ni chemchemu ya maarifa ya wanadamu wote, kwa sababu ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu alioutuma kwa wanadamu huku Nabii wa mwisho na mawasii wake wateule wakiwa ni viongozi wa wanadamu wote bila kubagua.

Tumeona ni vizuri tuweke silabasi kwa ajili ya kusoma historia ya kiislamu kwa kufuata hatua moja baada ya nyingine, kwani masomo ya historia ya nukuu hutangulia kabla ya masomo ya uchambuzi.

Na kwa kuwa umma wote umekongamana juu ya wema na utakaso wa viongozi wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu basi inafaa tuingize historia ya maisha yao ndani ya maisha ya wanafunzi, kwani Qur’ani imetamka wazi kuhusu umaasumu na utakaso wao ili wawe ni kiigizo chema kwa yule anayetarajia fadhila za Mwenyezi Mungu na malipo mema ya Siku ya Kiyama.

Lengo La Silabasi Ya Kitabu Hiki

Kitabu Masomo ya utangulizi katika historia na sera ya viongozi wema” kimetungwa ili kiwe hatua ya mwanzo ya kuelekea kwenye masomo mbalimbali ya lengo la kina zaidi, huku kikitegemea kufikia lengo hilo kwa kutumia wepesi wa ibara, usalama wa nukuu na vyanzo vyenye kukubalika ili kitoe picha ya wazi isiyokuwa na utata, shaka au hisia ambazo huenda zikamchanganya msomaji wa sera na historia mwanzoni tu mwa safari yake hii.

Masomo haya sitini yataanza kuzungumzia historia na sera kwa mtazamo wa Qur’ani, kisha yatatoa maisha binafsi na ya kijamii ya kila mmoja kati ya maasumina kumi na wanne (a.s.), na mwisho yataishia kwenye uwanja kati ya viwanja vya urithi wao wenye kunukia manukato.

Mwisho kabisa tutatoa faida ya maisha yao ya ujumbe huku tukionyesha mavuno ambayo yamepatikana ndani ya karne tatu bali ni zaidi ya karne kumi na nne za mapambano yenye kuendelea kwa ajili ya kuuokoa umma wa kiislamu na jamii ya wanadamu toka kwenye yale yaliyowapata na waliyonasa ndani yake.

Na ili yawe maandalizi mema yenye kuunea na mapinduzi ya kiulimwengu ambayo yanamsubiri kiongozi wake wa kiroho, Imam angojewaye Al-Mahdi (a.s.) ambaye Mwenyezi Mungu aliwaahidi watu wa mataifa yote, ili aje kuunganisha nguvu na kuzifanya vizuri hali zao huku akiwaokoa wanadamu toka kwenye upotevu na kutimiza matarajio ya manabii na akitimiza wema wa ubinadamu, wema ambao bado binadamu anaendelea kuutolea juhudi zake usiku na mchana.

Hivyo mafunzo ya historia yamegawanywa katika sera binafsi na sera ya kijamii, huku yakiwa hayana uchambuzi wa matukio ya kihistoria wala kuzama sana ndani ya matukio makuu ya kihistoria, hiyo ni ili baadaye yafuatiwe na masomo mapana zaidi kuliko mafunzo haya.

Pia tumejiepusha na urudiaji huku tukikomea kwenye historia ya ujumbe wenyewe na yale yaliyopita katika mzunguko na vipindi vya ujumbe na kwenye matokeo yaliyopatikana ndani ya karne zilizopita ambazo ziliupitia Uislamu na waislamu.

Mada hizi zimetimia kwa kufuata uchambuzi wa kielimu dhidi ya matukio yaliyosajiliwa ndani ya vitabu vya historia au yaliyogunduliwa na watafiti. Katika hali zote mbili tumejaribu kutegemea juhudi za wale waliotutangulia, ambazo ni masomo ya waandishi na watafiti ili kupata matunda ya juhudi zao na kuunganisha kati ya watu wa zamani na kizazi cha sasa.

Pia ili tuwafunze vijana dharura ya kupitia rejea za kutegemewa za zamani na za sasa bila kudhulumu haki za waliyotangulia bali ili zionekane juhudi zao na jinsi walivyochangia katika uwanja wa elimu na maarifa ya jamii, na ili kuijua nafasi waliyonayo katika kunukuu urithi na kuvipelekea vizazi vyenye kufuata.

Waandishi wa zama hizi tutakaowataja ni Sheikh Baqir Sharifu Al- Qarashiy, Sayyid Murtaza Al-Askariy, marehemu Sheikh Asad Haydar, mashahidi wawili: Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri na Sayyid Muhamad Baqir Al-Hakim. Kisha Sayyid Jafar Murtaza Al- Amiliy, Sheikh Muhammad Had Al-Yusufiy Al-Gharawiy na wengine ambao tumegusia vitabu vyao mwishoni mwa kila mada ambayo tumenukuu toka kwao.

Ni wajibu wetu kusema: Kitabu hiki ni mjumuisho wa mada mbalim- bali na utunzi unaolenga mafunzo ambayo yamezagaa ndani ya vitabu maalumu vilivyoteuliwa kufundisha sera ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) ili iwe ni mali kwa mtafiti, mwanafunzi, mhutubu, mubali- hghiina, mlezi na mlelewa ili ajiandae na masomo ya juu zaidi katika historia ya Uislamu kwa ajili ya kupambana mapambano ya kielimu dhidi ya matukio ya kihistoria na kijamii, na ili tuzame ndani huku tukipata mafunzo toka humo ili yawe ni mazingatio kwa msomaji na mawaidha kwa mwenye mazingatio, insha’allah.

Kutokana na maelezo yaliyopita, kwa muhtasari tunatoa matokeo yafuatayo:

Kwanza: Katika hatua hii mwalimu anapofundisha historia asitege- mee kukutana na mafunzo ya kihistoria yenye mtiririko wa kuungana na kufuatana kwa maana iliyozoeleka. Kwa kuanzia jografia na histo- ria ya Bara la Uarabu, kisha utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na dola yake, kisha dola ya makhalifa ambao walitawala kwa utaratibu maalumu. Hiyo ni kwa sababu sisi hatukusudii isipokuwa kusoma sera ya viongozi wema maasumina ambao ni lazima kuwaiga ili mwanafunzi afuate nyayo zao, awafuate na kuongoka kwa uongozi wao na sera yao katika maisha yake binafsi na ya kijamii.

Pili: Mwanafunzi anaweza kupata mafunzo muhimu ya kihistoria kupitia njia ya kutoa hatua za maisha ya kila mmoja kati ya maasumina kumi na wanne kwa kiwango kinachonasibiana na hatua ya mwanzo ya utangulizi ambayo imeishia kugusia nafasi na sehemu ya kizazi cha Mtume katika historia na harakati za Uislamu, kwa kuanzia nafasi yao maalumu ya kipekee aliyowapa Mwenyezi Mungu na kumalizia hali halisi ya kihistoria ambayo imetoa harakati zao na mwenendo wao muda wa karne tatu na zaidi.

Tatu: Kwanza hakika mafunzo ya historia ya Bara la Uarabu hayaingii yote katika historia ya Uislamu isipokuwa huwa kama utan- gulizi tu. Pili hutumiwa katika sehemu ya uchambuzi, jambo ambalo hatulikusudii katika hatua hii ya masomo haya. Zaidi ya hapo ni kuwa maelezo ya kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kama vile kauli za Imam Ali (a.s.) toka kwa Mtume (s.a.w.w.) na maelezo ya Zahra (a.s.) ndani ya hotuba yake mashuhuri aliyoitoa baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w.) yameelezea vizuri hali ya waarabu kabla ya Uislamu. Na pia imeunganisha kati ya yaliyopita na yaliyopo ambayo aliyatimiza Mtume (s.a.w.w.), na majukumu makubwa yaliyofuatia yaliyopo juu ya wais- lamu ambao walitolewa na Uislamu toka kwenye shimo la ujinga mpaka kwenye nuru ya mwanga wa Uislamu.

Nne: Hakika anayemaliza kusoma kitabu hiki inampasa azalishe mafunzo ambayo yatampa njia ya kufikia malengo yanayokusudiwa katika kusoma historia ndani ya hatua zote mbili, na wala asitosheke na haya yaliyopo kwenye masomo ya hatua ya utangulizi.

Hatutaki kurudia mafunzo mara juu juu au mara nyingine kwa upana na undani zaidi, kwa ajili hiyo tunategemea waheshimiwa walimu wetu watazingatia malengo ya masomo kabla ya kuhoji silabasi ya kitabu. Na watatilia maanani silabasi ya kitabu kabla ya kuzama ndani ya vipengele vidogo vidogo vya historia ambavyo tumeviteua kwa ajili ya hatua hii. Pia watazingatia kikomo cha wakati na dharura ya kupangilia mafunzo kulingana na ubora ambao ni lazima kuzingatiwa katika silabasi ya mafunzo. Na kwa kuwa hiki si kitabu cha ziada bali kimeandaliwa kama kitabu cha kiada basi walimu watafundisha kulingana na silabasi ya mafunzo iliyopangwa.

Hatuna budi kusema kuwa kitabu hiki kilichapishwa mwanzo kwa jina la: ‘Dondoo za sera za viongozi wema’. Lakini baada ya kupi- tia upya mafunzo ya kitabu, kilibadilishwa jina na kuitwa:
‘Masomo ya utangulizi katika historia na sera ya viongozi wema’.

Mwisho tunatoa shukurani za dhati kwa ndugu zetu kamati ya elimu katika taasisi ya kimataifa inayosimamia vituo vya elimu na shule za kiislamu kwa msaada na juhudi walizozitoa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampe uongofu na nguvu, hakika Yeye ndiye kiongozi bora na Mwenye kunusuru. Pia tunatoa shukuranu za dhati kwa mwandishi wa kitabu hiki Ustadh Sayyid Mundhir Al-Hakim (heshima yake idumu).

Jopo la kamati ya waandishi wa vitabu vya kiada.
1425 A.H.

  • 1. Al-Hajj: 46.
  • 2. Al-Haaqah: 12.