"Ni jambo la wajibu juu ya kila mtu kujiunza masiala ambayo yanamtokea mara kwa mara." (Hii ni kauli ya wanavyuoni wa kifikihi iliyodondolewakutoka vitabu vya fatwa au hukumu za kifikihi). Hakika kipindi cha ujana kinahesabika kuwa ndiyo fursa yenye thamani katika kujipatia maarifa na kuyavuta kutoka kwenyvyanzo vya elimu ambavyo mtu atafidika navyo muda wote wa uhai wake. Kila umri wa mwanadamu unavyosonga mbele, ndivyo majukumu yake yanavyozidi na maisha yake kuwa na msongamano. Kwa hali hiyo, basi hukosa fursa ya faragha itakayoruhusu kujifunza yale yanayomlazimu miongoni mwa hukumu za sheria za Kiislamu, na maoni ya wanavyuoni wa sheria, ambazo nyingi miongoni mwa hizo huenda atazihitaji katika maisha yake hapo baadaye. Bila shaka mwanadamu anahitaji kuwa na wigo katika kufanya mabadiliko ya kibinadamu ndani ya safari yake ya maisha.