Table of Contents

Sura Ya Kwanza: Baleghe

Mwanzoni mwa kipindi cha ujana hutokea mabadiliko makubwa na ya kina ambapo nguvu za kimwili na kiroho hufunguka.

Si hivyo tu, bali katka kipindi hichi ndani ya akili ya mwanadamu huchomoza matarajio na fikra mpya na kumwonesha kuwa anayo hadhi inayowavutia wengine kushirikiana naye.

Bila shaka kuanzia hapo mtu huyu hukataa kuwa (mwenye) kufuata tu, ambapo sasa hutafuta uhuru katika mambo yake binafsi na katika maamuzi yake anayoyachukua. Hali hiyo humaanisha kuwa amefikia kipindi cha Baleghe na kuwa anataka kuchagua njia moja baina ya njia nyingi mbali mbali.

Na njia hii (anayoitafuta) ni ile itakayo mfikisha kwenye wema wake binafsi, kama ambavyo ni wajibu wake binafsi kuichagua njia hiyo, kwani katika bahari hii yenye wingi wa fikra zinazo gongana huenda akajikuta anamhitajia (mwanachuoni) atakayemsaidia kumuongoza na kumvusha Swalama na kumfikisha ufukweni kwa amani.

Basi ndani ya kipindi hiki, huruma ya Mwenyeezi Mungu humfunika na rehema humteremkia kwa msaada wa ujumbe unaokunjukiwa na muono unaotokana na aina (mbali mbali) za fikra, kwa lengo la kuzingatiwa misingi yake na kusomwa maandiko yake.

Kwa hali hii basi, mara atajikuta anahisi furaha na kuingia katika mazingira mazuri hali ya kuwa uso wake ni wenye nuru na huku ulimi wake ukimhimidi na kumshukuru (Mola) juu ya yale aliyoelezwa na kule kufikia kipindi cha kuwajibika kisharia.

Hakika Baleghe ni kitabu cha habari na matendo ambacho ni lazima kukihifadhi ili nuru yake idumu na usafi wa kurasa zake uendelee mpaka mwisho wa uhai.

Hakika siku ya kubaleghe ndiyo siku ambayo Malaika wana haki ya kukaa kushotoni na kuliani: “Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.” Na hali ya kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu inamjumuisha inasema: “Enyi Mlioamini…..”

Alama Za Baleghe

Kuna baadhi ya watu ambao wanaweza kupitiwa na miezi kadhaa tangu kubaleghe, hali ya kuwa hawalijuwi suala hili muhimu. Na kwa wakati huo utekelezaji wa wajibu wa mambo ya kisharia utakuwa umempita katika kipindi hicho.

Hakika utambuzi wa jambo hili unahitaji kuwa makini kwa namna Fulani, japokuwa ni jambo jepesi kwa upande wa wasichana kwani lina uhusiano na alama tatu ambazo moja miongoni mwa hizo inatosha kuwa dalili ya kubaleghe. Alama hizo ni hizi zifuatazo:-

1. Umri

Nao ni kutimiza miaka tisa ya mwaka unaofuta kalenda ya mwezi mwandamo.1 Na mwaka wa kalenda ya mwezi mwandamo ni pungufu kwa siku kumi na saa kumi na nane ukilinganisha na mwaka unaofuata kalenda ya Jua wa mawiyo.2

2. Nywele ngumu za Sehemu ya Siri:

Hizi ni nywele zinazodhihiri chini ya tumbo.

3. Damu ya Mwezi:

Miongoni mwa alama za kubaleghe, ni kupata damu ya mwezi (yaani hedhi). Na mara nyingine hupatikana alama nyingine kama vile kuongezeka kimo, kuota matiti na kupanuka kwa uke.

  • 1. Mwaka Mwandamo ni Mwaka upatikanao kutokana na mzunguko wa Mwezi Mwandamo. (Mfasiri)
  • 2. Mwaka Mawiyo ni Mwaka wa kawaida uliozoeleka ujulikanao kama Mwaka wa Kizungu. (Mfasiri)