Table of Contents

Sura Ya Nne: Namna Ya Kuoga

Majosho yaliyotangulia kutajwa hapo kabla, unaweza kuyatimiza kwa namna moja kati ya namna mbili:

Utaratibu Maalum:

Niya: Kisha kuosha kichwa na shingo. Kuosha upande wa kulia wa mwili pamoja na tupu mbili. Kuosha upande wa kushoto wa mwili pamoja na tupu mbili.

Nukta Muhimu

Ili kuwa na yakini (ya ukamilifu) wa kuoshwa kwa maeneo yote ya mwili, basi anapo osha upande mmoja aingie kidogo hadi upande wa pili ili kuhakikisha kuwa ameosha sehemu zote wakati wa kuoga.

Kupiga Mbizi

Niya: Kisha aingize mwili wote ndani ya maji kwa mara moja. Aingie ndani ya maji hatua kwa hatua mpaka maji yafunike mwili wake wote.

Aingize mwili wake ndani ya maji kwa namna yoyote kisha anuwiye na hatimaye atikise mwili wake huku akiwa ndani ya maji.

Nukta Muhimu

i. Inawezekana kwa mtu akanuwiya niya mbali mbali kwenye josho moja.

ii. Majosho yote namna ya kuyaoga ni moja, tofauti iliyopo ni kwenye niya tu.

iii. Majosho yote yanatekelezwa kwa niya ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

iv. Kwenye uogaji wa Utaratibu Maalumu, anapo osha upande mmoja aingie kidogo hadi upande wa pili ili awe na uhakika kuwa ameosha sehemu zote wakati wa kuoga.

v. Iwapo atasahau utaratibu au asipoujua hivyo akawa hakuoga kwa utaratibu sahihi basi josho lake ni batili.

vi. Unyevu nyevu wa mwilini unaokuwepo kabla ya kuoga haudhuru josho, (kwa sharti maji ya josho yawe ni mengi zaidi kuliko unyevu nyevu uliyoko mwilini).

vii. Kila sharti linalohusu kusihi kwa udhu ni wajibu kufuatwa katika kuoga, isipokuwa mfululizo na umwagiaji maji kuanzia juu kwenda chini1

viii. Josho la Janaba linatosheleza udhu, ama majosho mengine hayatoshelezi.2

  • 1. Kuna tofauti kati ya Wanazuoni wa Sharia juu ya suala hili, hivyo Muqalidi arejee kwenye rai ya Mujtahid wake.
  • 2. Kuna tofauti kati ya Wanazuoni wa Sharia juu ya suala hili, hivyo Muqalidi arejee kwenye rai ya Mujahid wake