Table of Contents

Sura Ya Tano: Mas’ala Mbalimbali Ya Akina Dada Na Wanawake

Je ni wajibu mwanamke kujisitiri uso wake kutokana na wanaume wasiyo muhusu kwa mujibu wa Sharia?

Swali: Iwapo Mwanamke atatambua kuwa mwanaume asiye maharimu wake anautazama uso na viganja vyake kwa matamanio, je ni wajibu juu ya mwanamke huyo kujisitiri uso na viganja?

Majibu Ya Waheshimiwa Wanachuoni Wakuu Wa Sharia.

Mheshimiwa Ayatullah Khamenei: Kwa hali kama hiyo ni wajibu juu yake kujisitiri uso na viganja viwili.

Mheshimiwa Ayatullah Sistani: Kwa hali kama hiyo ni wajibu juu yake kujisitiri uso na viganja viwili.

Mheshimiwa Ayatullah Bahjati: Kujisitiri uso na viganja viwili ni wajibu katika hali yoyote ile kwa mujibu wa ihtiyati.

Mheshimiwa Ayatullah At-Tabrizi: Ndiyo, katika hali hii, ni wajibu kujisitiri kwa mujibu wa ihtiyati

Mheshimiwa Ayatullah Lan-karani: Ndiyo, kujisitiri ni wajibu.

Kuficha Mapambo Kutokana Na Asiye Maharimu

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa pete au bangili za dhahabu kwa wanawake pindi (mwana mke) anapotazamwa na asiyekuwa maharimu wake?

Majibu ya Waheshimiwa Marja’a watukufu

Samahatu Ayatullah Bahjati: Ni wajibu kusitiri.

Samahatu Ayatullah Lan-karani: Ni wajibu lazima kuyasitiri dhidi ya asiyekuwa maharimu.

Samahatu Ayatullah Sistani: Hairuhusiwi kuyadhihirisha kwa asiyekuwa maharimu.

Samahatu Ayatullah Makarim Ash-Shirazi: Haisihi kuyadhihirisha kwa asiyekuwa maharimu.

Samahatu Ayatullah At-Tabrizi: Kusitiri vitu mfano wa bangili kwa asiyekuwa maharimu ni wajibu.

Mazungumzo Kati Ya Mwanamke Na Asiyekuwa Maharimu

Maswali:

a. Ni ipi hukumu ya mwanamke anayecheka na kutabasamu pindi anapozungumza na mwanaume asiyekuwa maharimu wake?

b. Ni ipi hukumu ya kucheka kwa sauti ya juu barabarani au kuten- da mambo yatakayovuta macho ya vijana?

Majibu:

Samahatu Ayatullah Khamenei:

a. Ikiwa kuongea na kucheka na yule asiyekuwa maharimu kunaleta uharibifu basi hairuhusiwi.

b. Ni wajibu kujiepusha na kila kitendo kinacho lazimisha kuvuta macho ya asiyekuwa maharimu.

Samahatu Ayatullah Bahjati:

a. Kila kitendo kinachopelekea matamanio au fitina hakiruhusiwi.

b. Hairuhusiwi.

Samahatu Ayatullah Makarimu Ash-Shirazi:

a. Kuna mushkeli, na inapokuwa ni lazima basi hairuhusiwi kuvuka mazungumzo ya kawaida.

b. Ni bora kwa wanawake na wasichana wa ki-Islamu kujiepusha na matendo haya, na kama yanapelekea uharibifu basi hayaruhusiwi.

Samahatu Ayatullah At-Tabrizi:

a. Kutenda kwa ajili ya kuvuta macho ya wanaume wasiyo kuwa maharmu ni mañosa

b. Mwanamke mcha Mungu hafanyi matendo haya, na kuamsha hisia za matamanio hairuhusiwi kwa kila pande zote mbili (Wana ume na Wana wake).

Tofauti Kati ya Wimbo na Muziki:

Imam As-Sadiki (a.s.) amesema: “Mnajimu amelaniwa, kohani amelaniwa, mchawi amelaniwa, mwimbaji amelaniwa, atakayevutiwa naye amelaniwa na mwenye kula pato lake amelaniwa.”1

Swali:

Ni ipi tofauti iliyopo kati ya wimbo na muziki, na ni ipi hukumu yake?

Jibu:

Wimbo ni maneno yenye kupumbaza yajulikanayo kwa mafasiki na watu waovu, kwa sifa hii hauna tofauti na muziki katika hukumu, na vyote viwili ni haramu.

1. Samahatu Ayatullah Lan-Karani: Wimbo ni sauti inayotokea kooni na inapumbaza. Sauti kama hii ni mashuhuri kwenye vikao vya mambo ya upuuzi, na ni haramu. Na muziki kwa mujibu wa moja ya maana ni kupandanisha sauti zenye kuleta furaha, hivyo ukinasibiana na maeneo ya upuuzi basi ni haramu. (Tunaongeza kuwa kuuza, kununua, kutumia na kuhifadhi vyombo vya muziki ni haramu pia.)

2. Samahatu Ayatullah Bahjati: Ikiwa muziki unapumbaza basi kuusikiliza, kuuza na kununua vyombo vyake ni haramu.

3. Samahatu Ayatullah Makarimu Ash-Shirazi: Sauti zote na miziki ijulikanayo kwa watu wa upuuzi na uharibifu ni haramu, na usiyokuwa huo ni halali. Na uainishaji wa maudhui unatege- mea jamii husika, pia hairuhusiwi kuuza, kununua na kuhifadhi vyombo vyake.

4. Samahatu Ayatullah At-Tabrizi: Wimbo ni sauti yenye kupumbaza, ambayo ni mashuhuri katika vikao vya uharibifu na yenye madhumuni batili. Kuusikiliza ni haramu. Na kwa mujibu wa ihtiyati ya wajibu kama itakuwa unaambatana na urembeshaji wa sauti. Na ni lazima kujizuia dhidi yake hata kama madhumuni yake si batili. Pia muziki, (nao ni kuzalisha sauti kwa kutumia ala maalumu zijulikanazo kwa watu waovu), hairuhusiwi kuusikiliza, wala hamna tofauti kati ya muziki wa kitamaduni na mwingineo.

Kusikiliza Muziki:

Imamu As-Sadiki (a.s.) amesema: “Kusikiliza nyimbo na upuuzi huotesha unafiki ndani ya moyo kama maji yaoteshavyo mmea.”

Swali:

Ni ipi hukumu ya kusikiliza muziki ambao unarushwa na idhaa na Runinga (katika Jamuhiri ya ki-Islamu) au mamlaka ya ki-Isilamu. Ni ni ipi hukumu ya kutengeneza, kujifunza, kuuza na kununua vyombo vya muziki?

Jibu:

1. Samahatu Ayatullah Sistani: Ikiwa muziki hauna uhusiano na maeneo ya upuuzi na uharibifu basi si vibaya.

2. Samahatu Ayatullah Khamenei: Kila aina ya sauti zinazo pumbaza, za upuuzi zijulikanazo kwenye maeneo ya ufasiki na uovu ni haramu. Kuuza na kununua vyombo vinavyotumika ni haramu na hairuhusiwi. Ama kuhusu vipindi vya idhaa na Runinga ili kuainisha maudhui husika kunategemea mtazamaji na msikilizaji. Hivyo akiamini kuwa muziki huu ni wenye kupumbaza na upuuzi au kipindi hiki hupelekea uharibifu, basi ni lazima kutokusikiliza na kutokutazama, (na kwa ujumla ni kuwa, kurusha muziki kunapingana na malengo mema ya utawala wa ki-Islamu).

3. Samahatu Ayatullah Lan-Karani: Ikiwa muziki unapumbaza na una amsha hisia, na ni mashuhuri kwa watu waovu, basi muziki huo utakuwa haramu, na usiyokuwa na sura hii hauna kizuizi, na wala upande unaoutangaza hauathiri hukumu.

4. Samahatu Ayatullah Bahjati: Ikiwa muziki unapumbaza basi kuusikiliza, kuuza na kununua vyombo vyake ni haramu.

5. Samahatu Ayatullah As-Swafi Al-Kulbaygani: Sauti zote na midundo mashuhuri kwa watu wenye (kupendelea) mambo ya upuuzi na waharibifu ni haramu, na zisizokuwa hizo ni halali, na kuiainisha maudhui hii, kunategemea jamii husika.

6. Samahatu Ayatullah At-Tabrizi: Hairuhusiwi kusikiliza muziki wenye upuuzi ujulikanao kwenye maeneo ya waovu, na pia hairuhusiwi kutengeneza, kujifunza, kuuza na kununua vyombo vya muziki wenye upuuzi.

Kuhudhuria Maeneo Ya Muziki

Swali:

Ni ipi hukumu ya kuhudhuria kwenye hafla na harusi ambazo muziki unapigwa?

Jibu:

1. Samahatu Ayatullah Bahjati: Ikiwa muziki unapumbao, basi hairuhusiwi kuhudhuria.

2. Samahatu Ayatullah Lan-Karani: Hairuhusiwi kuhudhuria maeneo yenye pumbao na uharibifu.

3. Samahatu Ayatullah Makarimu Ash-Shirazi: Hairuhusiwi kuhudhuria vikao vya maasi.

4. Samahatu Ayatullah At-Tabrizi: Hairuhusiwi kusikiliza muziki wenye upuuzi hata kama ni harusini.

5. Samahatu Ayatullah Sistani: Ikiwa muziki ni ule ujulikanao kwenye hafla za wapuuzi na waharibifu basi hairuhusiwi kuhudhuria.

Kucheza

1. Samahatu Ayatullah Khomeni: Kwa mujibu wa ihtiyati ya wajibu ni kwamba hairuhusiwi kwa wanawake kucheza sehemu yoyote ile, mfano kwenye hafla ya ndoa, harusini au kwenye mashairi (isipokuwa mwanamke kucheza kwa ajili ya mumewe).

2. Samahatu Ayatullah Khamenei: Kwa ujumla kucheza kuna utata isipokuwa mwanamke kucheza kwa ajili ya mumewe mbali na macho ya wengine.

3. Samahatu Ayatullah Bahjati: Kucheza kwa namna yoyote ile kuna utata.
4. Samahatu Ayatullah Makarimu Ash-Shirazi: Isipokuwa kucheza kwa mwanamke kwa ajili ya mumewe tu ndiko kunaruhusiwa. Ama kulikobaki kuna utata.

5. Samahatu Ayatullah Sistani: Kwa mujibu wa ihtiyati ya wajibu hairuhusiwi, isipokuwa mwanamke kucheza kwa ajili ya mumewe mahali ambapo hakuna mtu mwingine yeyote.

6. Samahatu Ayatullah At-Tabrizi: Kucheza ni katika mambo ya upuuzi, na hakumfai muumini.

Kuuza na Kununua Casset na Picha Zenye Mambo Machafu: Kulingana na fatwa za Waheshimiwa wanachuoni wetu watukufu (Samahatu Ayatullah Bahjati, Samahatu Ayatullah Makarimu Ash-Shirazi, Samahatu Ayatullah Lan-Karani, Samahatu Ayatullah Sistani na Samahatu Ayatullah At-Tabrizi) ni kuwa: Kuuza na kununua mikanda na picha mbaya ni haramu na hairuhusiwi kutafuta kipato kutokana na hayo.

Wanawake Kutazama Filamu Za Michezo

Swali:

Ni ipi hukumu ya wanawake kutazama filamu za michezo ambazo hurushwa na Runinga ya Jamuhuri ya ki-Islamu ya Iran na ambazo ndani yake huonekana sehemu kubwa ya mwili wa mwanaume, mfano filamu za michezo ya myeleka na kuogelea?

Jibu:

1. Samahatu Ayatullah Khamenei: Hakuna kizuizi kutazama filamu na picha ikiwa ni bila matamanio na uharibifu.

2. Samahatu Ayatullah Bahjati: Ikiwa kunapelekea uharibifu au matamanio ni lazima kujiepusha.

Mwanamke Kuhudumiwa Na Tabibu Mwanamume

1. Samahatu Ayatullah Lan-Karani: Hairuhusiwi iwapo itawajibika kumgusa na kumtazama.

2. Samahatu Ayatullah Makarimu Ash-Shirazi: Ni katika hali ya dharura tu ndipo mwanamke anaruhusiwa kuhudumiwa na tabibu mwana mume au kinyume chake (mwana mume kuhudumiwa na mwanamke).

3. Ayatullah Sistani: Hairuhusiwi iwapo kutawajibisha kumgusa au kumtazama (mtazamo) uliyo haramishwa, isipokuwa tu ikiwa kumtibu ndio bora zaidi.

Na Mwisho wa Maombi yetu tunasema: Kila Sifa njema inamstahikia Mwenyezi Mungu Mlezi wa Viumbe.

Jedwali Ya Maasumina Kumi Na Wanne.

JINA TAREHE YA KUZALIWA TAREHE YA KUFARIKI ALIKOZIKWA
Mtume Muhammad bin Abdillahi (s.a.w) Mwezi 17 Shawwal (Mfungo sita) mwaka wa 52 kabla ya Hijrah Mwezi 28 Safar (Mfungo tano) mwaka wa 11 Hijiriyyah Madina ;
Saudi Arabia
Imam Ali bin Abi Talib (a.s) Mwezi 13 Rajab mwaka wa 23 kabla ya Hijrah Mwezi 21 Ramadhan mwaka wa 40 Hijiriyyah Najaf; Iraq
Fatimah binti Muhammad (a.s) Mwezi 20 Jamadil Akhar (Mfungo tisa) mwaka wa 8 kabla ya Hijrah Mwezi 3 Jamadil Akhar (Mfungo tisa) mwaka wa 11 Madina ;
Saudi Arabia
Imam Hassan bin Ali (a.s) Mwezi 15 Ramadhan mwaka wa 3 Hijiriyyah Mwezi 28 safar (Mfungo tano) mwaka wa 50 Madina ;
Saudi Arabia
Imam Hussein bin Ali (a.s) Mwezi 3 Shabaan mwaka wa 4 Hijiriyyah Mwezi 10 Muharram (Mfungo) mwaka wa 61 Hijiriyyah Karbala; Iraq
Imam Ali bin Hussein (a.s) Mwezi 5 Shabaan mwaka wa 38 Hijiriyyah Mwezi 25 Muharram (Mfungo nne) mwaka wa 95 Hijiriyyah Madina ;
Saudi Arabia
Imam Muhammad bin Ali (a.s) Mwezi 1 Rajab mwaka wa 57 Hijiriyyah Mwezi 7 Dhul-hijja (Mfungo tatu) mwaka wa 114 Hijiriyyah Madina ;
Saudi Arabia
Imam Ja’far bin Muhammad (a.s) Mwezi 17 Rabiul-Awwal (Mfungo sita) mwaka wa 83 Hijiriyyah Mwezi 25 Shawwal (Mfungo mosi) mwaka wa 148 Madina ;
Saudi Arabia
Imam Musa bin Ja’far (a.s) Mwezi 6 Safar(Mfungo tano) mwaka wa 128 Hijiriyyah Mwezi 25 Rajab mwaka wa 183 Hijiriyyah Kadhimiyyah; Iraq
Imam Ali bin Musa (a.s) Mwezi 11 Dhul-Qada (Mfungo pili) mwaka wa 148 Hijiriyyah Mwezi 29 Safar (Mfungo tano) mwaka wa 203 Hijiriyyah Khurasaan; Iran
Imam Muhammad bin Ali (a.s) Mwezi 10 Rajab mwaka wa 195 Hijiriyyah Mwezi 29 Dhul-Qada (Mfungo pili) mwaka wa 220 Kadhimiyyah; Iraq
Imam Ali bin Muhammad (a.s) Mwezi 2 Rabil-Akhar (Mfungo saba) mwaka wa 212 Hijiriyyah Mwezi 3 Rabiul-Awwal (Mfungo Sita) mwaka 254 Hijiriyyah Samarraa; Iraq
Imam Hassan bin Ali (a.s) Mwezi 8 Rabil-Akhar (Mfungo saba) mwaka wa 232 Hijiriyyah Mwezi 8 Rabiul-Awwal (Mfungo Sita) mwaka wa 260 Hijiriyyah Samarraa; Iraq
Imam Muhammad bin Hassan Al-Mahdi (a.s) Mwezi 15 Shaaban mwaka wa 255 Hijiriyyah Bado yu hai na yuko katika Ghaiba kuu
  • 1. Al-Biharu, juz 103.