read

Imani ya uimamu wa maimamu kumi na wawili ni msingi wa uelewa juu ya Mahdi (a.s.)

Hakika chanzo cha wazo la kudhihiri mwokozi ambaye anawakilisha msingi wa wazo la Mahdi ndani ya Uislamu ni wazo la wanadamu wote wala si la dini fulani au madhehebu mahsusi, na ukweli huu wenyewe binafsi unasaidia kuvunja hoja nne za utata juu ya suala la Mahdi wakati mmoja.

Kwanza: Wenyewe unafafanua ubatilifu wa hoja isemayo kuwa wanaoamini imani ya Mahdi ni Shia tu. Na hasa inapothibiti ijimai ya waislamu juu ya imani yake.

Pili: Unafafanua ubatilifu wa hoja ya ngano isemayo kuwa, imani kuhusu Mahdi ni ngano itokanayo na dhana isiyo na uwepo, kwani hakika ngano ni dhana tupu isiyo na uwepo wowote itokanayo na hali ya kikabila au kitaifa au kundi maalumu. Na hakuna ngano yoyote inayothaminiwa na dini zote za kimungu na zisizo za kimungu, huku ikielezea dhamira ya wanadamu wote na huku wanachuoni na wanafikra pamoja na wanafalsafa mbalimbali wakiikubali.

Tatu: Unafafanua ubatilifu wa hoja isemayo kuwa Mayahudi wana mchango mkubwa katika kupandikiza wazo la kuwepo Mahdi. Ikiwa wazo la Mahdi linaaminiwa na dini zote hata zile zisizokuwa za kimungu, basi ni kwa nini tunachukia wazo hili kuwemo ndani ya Uislamu? Kwani kwa mujibu wa akili salama na mantiki ni kuwa Uislamu unapasa uwe na wazo hili tena kwa uwelewa wa wazi zaidi na uliokamilika zaidi, kama ilivyo ndani ya madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s.).

Hivyo basi miongoni mwa ukamilifu wa dini hii na madhehebu hii ni kule kulimiliki kwa ukamilifu wazo la kuwepo Mahdi, hivi dini za kimungu si zinashirikiana katika duru nyingi za kiimani na kisharia kama vile hija, Swaumu na Swala…? Hivi Mayahudi kuamini ibada hizi inapasa kuwa sababu ya Uislamu kuzikana? Au inapasa kuzihimiza na kuzitolea uwele- wa uliokamilika na wa hadhi ya juu mno? Hakika hoja yao hii inawaletea wenyewe upungufu na kuuletea Uislamu na Ushia ukamilifu.

Nne: Unafafanua ubatilifu wa hoja isemayo kuwa wazo la kuwepo Mahdi limetokana na mazingira ya ugandamizaji wa kisiasa ambao uliwapata Maimamu (a.s.), kwani makhawariji walikumbana na ugandamizaji usioto- fautiana na ule uliowakumba wafuasi wa Maimamu (a.s.) na kama hiyo ingekuwa ni kanuni basi ni wangapi wamedhulumiwa na kugandamizwa lakini hawaamini wazo la Mahdi. Na ni makundi mangapi na watu wan- gapi wameamini wazo hili bila ya kukumbana na dhuluma na ugan- damizaji. Na kama imani hii ingekuwa inatokana na dhuluma na ugan- damizaji kwa nini imani hii imedhihiri kwenye vizazi vilivyofuata visivyogandamizwa?

Ndiyo, tunaweza kuamini kuwa sababu za ugandamizaji na unyanyasaji zinafaa kumsukuma mtu zaidi kushikamana na wazo la Mahdi, lakini si kwamba zenyewe ndizo zinaanzisha wazo hili na kuwa msingi wa kuwepo kwa wazo hili.

Hakika dini ni maelezo kamilifu mno kuhusu uhalisia wa mwanadamu, na Uislamu ni maelezo kamilifu mno kuhusu uhalisia wa dini, na madhehebu ya Ahlul-Bait ni maelezo kamilifu mno kuhusu uhalisi wa Uislamu.

Hivyo basi, pindi dini zinapoeleza waziwazi wazo la mwokozi wa ulimwengu huwa zinafichua dhamira ya mwanadamu iliyohimizwa na huwa ni kwa namna bora mno. Na pindi Uislamu unapoelezea waziwazi wazo hili huwa unaelezea waziwazi ukweli wa kidini uliyohimizwa na huwa ni kwa namna bora zaidi kuliko ulivyoelezwa na dini zilizotangulia.

Na pindi madhehebu ya Ahlul-Bait inapoelezea waziwazi wazo hili huwa inatoa maelezo kamilifu mno kuhusu ukweli wa Uislamu katika dhamira hii.

Hivyo tofauti iliyopo kati ya uelewa wa madhehebu ya kisunni na madhe- hebu ya Ahlul-Bait kuhusu Mahdi ni tofauti kati ya madhehebu inayobain- isha kiwango cha chini cha ukweli na madhehebu inayochukua jukumu la kubainisha ukweli wa Uislamu kwa kiwango cha juu mno. Hivyo madhe- hebu ya kwanza ikadhani kuwa madhehebu ya pili imepita njia ya mapen- zi ya kupindukia na nje ya mstari.

Siri ya Ushia kuwa mashuhuri kwa wazo la Mahdi mpaka likawa kama lin- auhusu Ushia tu na si miongoni mwa imani waliyokubaliana Waisilamu wote, huenda ni ile hali ya Ushia kuhusika kwa kiwango cha ukamilifu mno katika suala la Mahdi, huku uwelewa huo kwake ukiwa na sifa za kipekee ambazo kwazo inatimia ile maana halisi inayohitajika kutoka kwenye wazo la Mahdi.

Na sifa hizi zinatoka ndani ya msingi mmoja nao ni kuwa wazo la Mahdi katika uelewa wa Ahlul-Bait si nadharia tu ya mustakabali na wala si kutoa tu habari za mustakabali mwema kwa binadamu ambao atakuwanao mwisho wa safari kama linavvyoonekana kwa madhehebu ya Makhalifa, bali lenyewe ni sehemu isiyoachana na imani ya uimamu wa Maimamu kumi na wawili ambao Mwenyezi Mungu aliamua utawale ulimwengu tokea sekunde ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka sekunde za mwisho za uhai wa wanadamu. Au kwa maelezo mengine ni kuwa wazo hilo ni suala la Imam wa kumi na mbili ambaye uimamu wake umeanza tangu mwaka 260 A.H. ukaendelea mpaka sasa na utazidi kuendelea mpaka atakapodhihiri mwishoni mwa historia ya mwanadamu.

Sisi tunapochambua suala la Mahdi katika uwelewa wa Ahlul-Bait (a.s.) ni lazima tuhimize msingi huu wa kiimani, na tutazame tena upande wa dalili na hoja kwa lengo la kuthibitisha, na mara nyingine tutazame matokeo ya

imani hiyo, na mara ya tatu tutazame upande wa hadhi ya kiimani iliyon- ayo matokeo hayo, hivyo kuna hatua tatu za uchambuzi na kila hatua tutai- weka kwenye sura yenye kujitegemea.