read

Jambo La Nane: Atoacho Imam Mahdi (a.s.)

Miongoni mwa mambo yasiyo na shaka kabisa ni kuwa uadilifu kwa maana yake yote utatimia chini ya utawala wa Mahdi (a.s.), ardhi na mbin- gu zitamwaga kheri zake na dola yake itakuwa ni dola ya mfano bora tuliyoahidiwa na Mola, dola ambayo ndani yake mwanadamu atakuwa mwema kwani hakutokuwa na dhuluma, unyang’anyi, ufakiri wala ufisadi. Hakika maelezo ya riwaya zifuatazo yanaashiria ukweli huu halisi:

1- Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri (r.a.) kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Umma wangu utaneemeka zama za Mahdi kwa neema ambayo katu hawajawahi kuneemeka kwa mfano wake, watatumi- wa mvua nyingi na ardhi haitoacha mmea wowote ila itauotesha, na mali yenye kulundikana, itakuwa mtu anasimama na kusema: Ewe Mahdi nipe, naye anamjibu chukua.”1

2- Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri (r.a.) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ndani ya umma wangu atakuwemo Mahdi, ikipungua ni miaka saba na kama si hivyo ni miaka tisa, ndani ya muda huo umma wangu utaneemeshwa kwa neema ambazo katu haujaneemeshwa kwa mfano wake. Ardhi itapatwa na mazao yake na wala hawatowekeza chochote. Kipindi hicho mali itakuwa imelundikana na hivyo mtu anasi- mama na kusema: Ewe Mahdi nipe, naye anamwambia chukua.”2

3- Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri (r.a.) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakika ndani ya umma wangu yumo Mahdi, atatokeza na kuishi mitano au saba au tisa.” Amesema: Tukasema ni nini hiyo? Akasema: “Miaka.” Akasema: “Atakuwa anajiwa na mtu na kusema: Nipe, nipe.” Akasema: “Ndipo anapomjazia nguo yake kwa kadiri atakavy- oweza kubeba.”3

4- Kutoka kwa Jabir bin Abdullah Al-Ansariy kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Zama za mwisho atakuwepo khal- ifa anawajazia mali nyingi bila kuzihesabu mara kwa mara.”4

5- Muslim ametoa ndani ya Sahih yake kutoka kwa Jabir bin Abdullah Al- Ansariy kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuwa alise- ma: “Zama za mwisho atakuwepo khalifa anayegawa mali bila kuzihesabu.”5

  • 1. Ibnu Hammad: 253, Hadithi ya 992. Al-Bayan: 145, mlango wa 23. Uqad Ad- Durar: 225, mlango wa 8. Al-Fusul Al-Muhimmah: 288 na 289, sura ya 12. Nurul- Absar: 189, mlango wa 2.
  • 2. Sunan Ibnu Majah 2: 1366 – 1367, Hadithi ya 4083. Mustadrak Al-Hakim 4:558. Burhanul-Muttaqiy: 81, mlango wa 1, Hadithi ya 25 na 82 mlango wa 1, Hadithi ya 26.
  • 3. Sunan At-Tirmidhi 4: 439, mlango wa 53, Hadithi ya 2232. Al-Bayan: 107, mlango wa 6. Al-Ilal Al-Mutanahiyah 2: 858, Hadithi ya 1440. Mishkatul- Maswabihi 3: 24, sura ya 2, Hadithi ya 5455. Muqaddimatu Ibnu Khalduni: 393, sura 53. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 215. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 164, mlango wa 11, sura 1. Kanzul-ummal 14: 262, Hadithi ya 38654. Mirqatul-Mafatihu 9:352. Mashariqul-An’war: 114, sura ya 2. Tuhfatul-Ahwadhiy 6: 404, Hadithi ya 2333. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5: 342 – 343.
  • 4. Maswabihus-Sunnah 3: 488, Hadithi ya 4199. Pia kuna Hadithi nyingine muhimu ndani ya kitabu Muswannaf cha Abdur-Ridhaq 11: 371, Hadithi ya 20770, mlango wa Mahdi, ameitoa mwandishi wa kitabu Difau Anil-Kafiy 1: 266.
  • 5. Sahih Muslim ufafanuzi wa An-Nawawiy 18: 39.