read

Jambo La Nne: Nafasi ya Imam Mahdi (a.s.) mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu

Baada ya kuwa tumejua jina la Imam Mahdi na sifa zake, basi ndani ya kifungu hiki tutazungumzia hadhi ya kiroho aliyonayo Imam Mahdi na nafasi yake mbele ya Mola ambayo humsukuma kutekeleza jukumu lake, na kuwa yeye ni khalifa wa Mwenyezi Mungu tuliyeahidiwa, ambaye ni wajibu kumtii kwa amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Tutazungumzia hilo ndani ya riwaya mbalimbali.

1- Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Sisi kizazi cha Abdul-Muttalib ni mabwana wa watu wa Peponi, mimi Hamza, Ali, Ja’far, Hasan, Husein na Mahdi.”1

2- Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kutoka kwa Mtukufu Mtume
(s.a.w.w.) amesema: “Mahdi ni tausi wa watu wa Peponi.”2

3- Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Umma huu utakuwa na khalifa, Abubakri na Umar si bora kuliko yeye.”3

4- Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Umar amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mahdi atatokeza huku juu ya kichwa chake kukiwa na wingu. Na kuna mnadi atakayenadi: Huyu ndiye Mahdi khalifa wa Mwenyezi Mungu mfuateni.”4

5- Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Amru kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Atatokeza Mahdi huku juu ya kichwa chake kukiwa na Malaika akinadi: Hakika huyu ndiye Mahdi mfuateni.”5

  • 1. Sunan Ibnu Majah 2: 1368, mlango wa 34, Hadithi ya 4087. Mustadrak Al- Hakim 3: 211. Tarikh Baghdad 9: 434, Hadithi ya 5050. Matwalibus-Suul 2: 81, mlango wa 12. Al-Bayan: 101, mlango 3. Dhakhairul-Uqba: 15 na 89. Ar-Riyadh An-Nadhirah 3: 4 na 182, sura ya 8. Uqad Ad-Durar: 194, mlango wa 7. Faraidu As-Samtwayn 2: 32, mlango 7, Hadithi ya 380. Muqaddimati Ibnu Khalduni: 398, mlango wa 53. Al-Fusulu Al-Muhimmah: 284, chapa ya Darul-Adh’wai, sura ya 12. Jam’ul-Jawamiu 1: 851. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 160, mlango wa 11, sura ya 1 na ukurasa wa 187, mlango wa 11, sura ya 2, Hadithi ya 19. Burhanul- Muttaqiy: 89, mlango wa 2, Hadithi ya 3. Is’afur-Raghibina: 124. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 214.
  • 2. Al-Firdawsu 4: 222, Hadithi ya 6668. Al-Bayanu: 118, mlango wa 8. Uqad Ad- Durar: 199, mlango wa 7. Al-Fusul Al-Muhimmah: 284, sura ya 12. Burhanul- Muttaqiy: 171, mlango wa 12, Hadithi 2. Kunuzud-Daqaiq: 152. Nurul-Absar: 187. Yanabiul-Mawaddah: 181, mlango wa 56.
  • 3. Ibnu Abi Shaybah 15: 198, Hadithi ya 19496. Al-Kamil cha Ibnu Adiy 6: 2433. Uqad Ad-Durar: 199, malngo wa 7. Burhanul-Muttaqiy: 172, mlango wa 12, Hadithi ya 6.
  • 4. Al-Bayan: 132, mlango wa 15. Uqad Ad-Durar: 183, mlango wa 6. Faraidu As- Samtwayni 2: 316, mlango 61, Hadithi ya 566 – 569. Al-Fusul Al-Muhimmah: 298, sura ya 12. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 217. Tarikhul-Khamis 2: 288. Nurul-Absar:
  • 5. Takhlisul-Mutashabihi 1: 417. Al-Bayan: 133, mlango wa 16. Faraidu As- Samtwayni 2: 316, mlango 61, Hadithi ya 569. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 217. Al- Qawlu Al-Mukhtasar: 39, mlango wa 1, Hadithi ya 24. Burhanul-Muttaqiy: 72, mlango wa 1, Hadithi ya 2. Yanabiul-Mawaddah: 447, mlango wa 78.