read

Jambo La Pili: Jina la Imam ni lipi, na nasaba yake ni ipi?

Mwenye kufuatilia Hadithi sahihi zilizopatikana kuhusu jina na nasaba ya Mahdi ndani ya vitabu vya Sunni atazikuta nyingi mno zikisisitiza uhalisia mmoja nao ni: Nasaba ya Mahdi inarejea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kuwa yeye ni miongoni mwa Ahlul-Bait na miongoni mwa maimamu kumi na wawili walio watakasifu, na yeye ndiye wa mwisho wao. Naye ni Muhammad bin Hasan Al-Askari (a.s.) Ibnu Ali Al- Hadi bin Muhammad Al-Jawad bin Ali Ar-Ridha bin Musa Al-Kadhim bin Jafar As-Sadiq bin Muhammad Al-Baqir bin Ali As-Sajjad bin Husein As- Shahid wa Karbala bin Ali bin Abi Talib (a.s.).

Na ndiyo mwenye lakabu ya Al-Mahdi Al-Muntadhar anayeoana na ile imani ya Shia Imamiyya. Zifuatazo ni riwaya zinazozungumzia jina lake na nasaba yake:

Mahdi ni: Mkinana, Mkurayshi na Hashimia

Imepokewa kutoka kwa Qatadah amesema: “Nilimwambia Said bin Al- Musayyab: Mahdi ni haki? Akasema: ‘Ndio ni haki.’ Nikamwambia: Anatokana na nani yeye? Akasema: ‘Anatokana na Kinana.’ Nikasema: Kisha kutoka kwa nani? Akasema: ‘Kutoka kwa Kurayshi.’ Nikasema: Kisha kutoka kwa nani? Akasema: ‘Kutoka kwa wana wa Hashim.”1

Hivyo kwa mujibu wa riwaya hii Mahdi ni mkinana, mkurayshi na muhashimia, na wala hakuna mgongano katika lakabu hizi, kwa sababu kila muhashimia anatokana na mkurayshi na kila mkurayshi anatokana na mkinana, kwa sababu Kurayshi ni An-Nadhar bin Kinanah, kwa itifaki ya wasomi wote wa nasaba za watu.

Mahdi ni kutoka kwa watoto wa Abdul-Muttalib

Ibnu Majah amepokea kutoka kwa Anas bin Malik amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Sisi ni kizazi cha Abdul-Mutwalib mabwana wa watu wa Peponi, mimi, Hamza, Ali, Jafar, Hasan, Husein na Mahdi.”2 Kwa mujibu wa riwaya hii Mahdi anakuwa miongoni mwa watoto wa Abdul-Mutwalib.

Mahdi ni kutoka kizazi cha Abu Talib

Imepokewa kutoka kwa Saif bin Umayrah amesema: Nilikuwa kwa Abu Jafar Al-Mansur akaanza kuniambia: “Ewe Saif bin Umayrah! Ni lazima atapatikana mwenye kunadi tokea mbinguni kwa jina la mtu kutoka kizazi cha Abu Talib.”

Nikamwambia: Ewe kiongozi wa waumini! Mimi ni fidia kwako; hii ni riwaya? Akasema: “Ndiyo, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika nimeisikia kwa masikio yangu mawili.”

Nikamwambia: Ewe kiongozi wa waumini! Hakika Hadithi hii sijaisikia kabla ya muda huu. Akasema: “Ewe Saif! Hakika yenyewe ni kweli, na iki- tokea basi mimi nitakuwa wa kwanza kumkubali, kwani hakika wito ni kuelekea kwa mtu kutoka wana wa ami yetu.”

Nikamwambia: Ni mtu kutoka kizazi cha Fatima? Akasema: “Ndiyo ewe Saif, laiti nisingeisikia kutoka kwa Abu Jafar Muhammad bin Ali akiniha- dithia basi nisingeikubali kutoka kwa mtu yeyote hata kama wangenisimu- lia watu wote wa aridhini, lakini aliyenisimulia ni Muhammad bin Ali.”3

Na Hadithi hii inasisitiza kuwa Mahdi ni kutoka kizazi cha Abu Talib.

Mahdi ni kutoka Ahlul-Bayt (a.s.)

Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudri amesema: Mtume wa
Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Kiyama hakitosimama mpaka ardhi ijae dhuluma na uadui.” Akasema: “Kisha atokee mtu kutoka ndani ya kizazi changu au watu wa nyumba yangu atakayeijaza usawa na uadilifu kama ilivyojaa dhuluma na uadui.”4

Na mfano wake ni ile iliyotoka kwa Abdullah kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Kiyama hakitosimama mpaka aje mtu miongoni mwa watu wa nyumba yangu, jina lake linalingana na jina langu.”5

Imepokewa kutoka kwa Ali kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amese- ma: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mahdi ni kutoka kwetu sisi Ahlul-Bayt, Mwenyezi Mungu atamleta ndani ya usiku mmoja.”6

Mahdi ni kutoka kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)

Kutoka kwa Ibnu Umar amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Zama za mwisho atatokea mtu kutoka kwenye kizazi changu, jina lake ni jina langu, kuniya yake ni kuniya yangu, ataijaza ardhi uadili- fu kama itakavyokuwa imejaa ujeuri, na huyo ndiye Mahdi.”7

Mahdi ni kutoka kizazi cha Fatima (a.s.)

1- Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mahdi ni kweli na yeye ni kutoka kizazi cha Fatima.”8

2- Kutoka kwa Ummu Salamah amesema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Mahdi ni kutoka ndani ya kizazi changu kutoka kwenye kizazi cha Fatima.”9

Mahdi ni kutoka kizazi cha Husein (a.s.)

Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah bin Al-Yamani (r.a.) amesema: “Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alituhutubia, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akatutajia yatakayotokea, kisha akasema: “Hata kama dunia itabakiwa na siku moja, basi Mwenyezi Mungu ataire- fusha siku hiyo mpaka amlete mtu kutoka ndani ya kizazi changu, jina lake ni jina langu.”

Salman Al-Farsi (r.a.) akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni kutoka kwa mwanao yupi? Akasema: “Ni kutoka kwa huyu.” Akawa amempiga Husein (a.s.) kwa mkono wake.10

Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudri amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu aliugua ugonjwa ambao ulimdhoofisha, basi Fatima (a.s.) akaingia kumtembelea na mimi nikiwa nimeketi kuliani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.w.w.), basi alipoona udhaifu alio nao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianza kulia mpaka machozi yakafika mashavuni. Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia: “Ewe Fatima! Kitu gani chakuliza? Hivi hujui kuwa Mwenyezi Mungu aliitazama ardhi yote mara moja akamchagua baba yako kutoka humo na kumfanya nabii, kisha akaitazama mara ya pili akamchagua mume wako, ndipo akanifunulia na nikakuoza kwake na nikamfanya wasii. Hivi hujui kuwa wewe uko katika heshima ya Mwenyezi Mungu kwa kuwa baba yako alikuoza kwa mtu mwenye elimu mno zaidi yao, mvumilivu mno kuliko wao na wa kwanza wao kuukubali Uislamu.”

Ndipo Fatima akacheka na kufurahi. Mtume wa Mwenyezi Mungu akata- ka kumuongezea nyongeza ya kheri ambayo Mwenyezi Mungu aliigawa kwa Muhammad na kizazi cha Muhammad, akamwambia: “Ewe Fatima! Ali ana fadhila nane: Kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hekima yake, mke wake, watoto wake Hasan na Husein, kuamrisha kwake mema na kukataza kwake maovu.

“Ewe Fatima! Sisi Ahlul-Bayt tumepewa vitu sita, ambavyo hajapewa yeyote vitu hivyo kati ya watu waliotangulia kabla yetu na wala hatovipa- ta yeyote atakayekuja baada yetu asiyekuwa Ahlul-Bayt: nabii wetu ndiye mbora wa manabii, naye ni baba yako. Wasii wetu ndiye mbora wa mawasii, naye ni mume wako. Shahidi wetu ndiye mbora wa mashahidi, naye ni Hamza ami ya baba yako. Na wajukuu wawili wa umma huu wana- toka kwetu, nao ni wanao wawili.

“Na Mahdi wa umma huu ambaye Isa ataswali nyuma yake anatoka kwetu.” Kisha akapiga mkono wake juu ya bega la Husein (a.s.) na kuse- ma: “Mahdi wa umma huu atatoka kwa huyu.”11

Jina la mzazi wa kike wa Mahdi na kuwa Mahdi ni kutoka kizazi cha As-Sadiq (a.s.)

Imepokewa kutoka kwa mfafanuzi wa lugha ajulikanaye kwa jina la Ibnul-Khashabu, amesema: Alinisimulia Abu Qasim At-Tahir bin Harun bin Musa Al-Kadhim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, amesema: Bwana wangu Jafar bin Muhammad alisema: “Mrithi mwema ni kutoka kizazi changu naye ni Mahdi, jina lake ni Muhammad na kuniya yake ni Abu Qasim, atatokea zama za mwisho, mama yake ataitwa Nargis na juu ya kichwa chake (a.s.) kutakuwa na wingu likimkinga na jua, litazunguka pamoja naye popote atakapokwenda huku likinadi kwa sauti fasaha huyu ndiye Mahdi mfuateni.”12

Mahdi ni kutoka kizazi cha Ar-Ridha (a.s.)

Imepokewa kutoka kwa Hasan bin Khalid, amesema: Ali bin Musa Ar- Ridhaa alisema: “Hana dini asiyekuwa na ujidhibiti, na hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni mcha Mungu kuliko nyinyi.” Kisha akase- ma: “Hakika mtu wa nne kutoka katika kizazi changu ni mwana wa bibi wa watumwa, kupitia yeye Mwenyezi Mungu atatoharisha ardhi dhidi ya kila ujeuri na dhuluma….”13

Jina la mzazi wa kiume wa Imam Mahdi (a.s.)

Ar-Riwayyaniy na At-Tabaraniy na wengineo wametoa: “Mahdi ni kutoka kizazi changu, uso wake ni kama nyota ing’aayo, rangi yake ni rangi ya kiarabu, na kiwiliwili cha kiisraeli – yaani mrefu – ataijaza ardhi uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhulma. Watu wa mbinguni na ardhini watarid- hia ukhalifa wake.”

Pia katika kitabu chake Al-Hilyatu imepatikana: “Yeye ni kijana mwenye macho yenye wanja, mwenye nyusi laini zilizolala kwa urefu, mwenye pua nyembamba yenye mwinuko, mwenye ndevu fupi zilizosokotana, na juu ya shavu lake la kulia kuna weusi.”

Sheikh Al-Qutub Al-Ghawthiy Sayyidiy Muhyid-Din Ibnul-Arabiy amese- ma ndani ya kitabu Al-Futuhati: “Fahamuni kuwa ni lazima atatokeza Mahdi, lakini hatoki mpaka ardhi ijae ukatili na dhuluma na ndipo aje kui- jaza uadilifu na usawa, na yeye ni kutoka kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kutoka kizazi cha Fatima Mola awe radhi naye, babu yake ni Husein bin Ali bin Abu Talib na mzazi wake wa kiume ni Hasan Al-Askari mwana wa Imam Ali An-Naqiy mwana wa Imam Muhammad At-Taqiy mwana wa Imam Ali Ar-Ridhaa mwana wa Imam Musa Al- Kadhim mwana wa Imam Ja’far As-Sadiq mwana wa Imam Muhammad Al-Baqir mwana wa Imam Zaynul-Abidina mwana wa Imam Husein mwana wa Imam Ali bin Abu Talib, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote.

“Jina lake linaoana na jina la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), waislamu watampa kiapo cha utii eneo la kati ya Ruknu na Maqam. Anafanana na Mtume wa Mwenyezi Mungu katika maumbile na anakarib- iana naye katika maadili, watu wema kupitia yeye ni watu wa Kufa, ata- gawa mali kwa usawa, atafanya uadilifu kwa raia na maisha bora yatakuwa mikononi mwake.”14

 • 1. Uqadud-Durari: 42 – 44, mlango wa kwanza. Mustadrak Al-Hakim 4: 553. Maj’mauz
 • 2. Sunanu Ibnu Majah 2: 1368, Hadithi ya 4087, mlango wa kutokeza kwa Mahdi.
  Mustadrak Al-Hakim 3: 211. Maj’maul-Jawamiu cha As-Suyuti 1: 851.
 • 3. Uqadu Ad-Durar cha Al-Muqaddasiy As-Shafiiy: 149 – 150, mlango wa nne.
 • 4. Musnad Ahmad 3: 424, Hadithi ya 10920. Musnad Abu Yaala 2: 274, Hadithi ya 987. Al- Mustadrak 4: 577. Uqadu Ad-Durar: 36, mlango wa 1. Mawaridu Ad-Dham’ani: 464, Hadithi ya 1879 na 1880. Muqadimah cha Ibnu Khalduni: 250, sura ya 53. Jam’ul-Jawamiu
  1: 902. Kanzul-ummal 14: 271, Hadithi 38691. Yanabiul-Mawaddah 433, mlango wa 73.
 • 5. Musnadul-Bazzaz 1: 281. Musnad Ahmad: 3761. Sunan At-Tirmidhiy 4: 505, mlango wa
  52, Hadithi ya 2230. Al-Muujam Al-Kabir 10: 135, Hadithi ya 10221 ikiwa na tofauti kido- go. Tarikh Baghdad 4: 388. Uqad Ad-Durar: 38, mlango wa 3. Matwalibu As-Suul 2: 81. Al-Bayan fi Akhbari Swahibuz-Zaman cha Muhammad An-Nawfaliy Al-Qurayshiy Al- Kunjiy As-Shafiiy: 91. Faraidu As-Samtwayn 2: 327, Hadithi ya 576. Ad-Durul-Manthur 6:58. Jam’ul-Jawamiu 1:903. Kanzul-ummal 14: 271, Hadithi ya 38692. Burhanul-Muttaqiy: 90, mlango wa 2, Hadithi ya 4.
 • 6. Ibnu Abu Shayba 8: 678, Hadithi 190. Futunu Ibnu Hammad. Musnad Ahmad 1: 84. Tarikh Al-Bukhari 1: 371, Hadithi ya 994. Sunan Ibnu Majah 2: 1367, mlango wa 34, Hadithi ya 4085. Musnad Abu Yaala 1: 359, Hadithi ya 465. Hilyatul-Awliyai 3: 177. Al- Kamil cha Ibnu Adiy 7: 2643. Al-Firdawsu 4: 222, Hadithi ya 6619. Al-Bayani fi Akhbari Swahibuz-Zaman cha Al-Kunjiy As-Shafiiy: 100. Uqadu Ad-Durar: 183, mlango wa 6. Al- Ilalu Al-Mutanahiyah 2: 2856, Hadithi ya 1432. Faraidu As-Samtwayni 2: 331, Hadithi ya 583. Mizanul-Iitidal 4: 359, Hadithi ya 9444. Muqadimah Ibnu Khalduni 1: 396, mlango 53. Tahdhibu At-Tahdhibu 11: 152, Hadithi ya 294. Urufus-Suyutiy Al-Hawiy 2: 213. Ad- Durul-Manthur 6: 58. Jam’ul-Jawamiu 1: 449. Al-Jamiu As-Saghir 2: 672, Hadithi ya 9243. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 163, mlango wa 511, sura ya 1. Kanzul-ummal 14: 264, Hadithi ya 38664. Burhanul-Muttaqiy: 87, mlango wa 1, Hadithi ya 43, na ukurasa wa 89, mlango wa 2, Hadithi ya 1. Mirqatul-Mafatihi 9: 349 humo mna tofauti kidogo. Faydhul-Qadir 6: 278, Hadithi ya 9243.
 • 7. Tadhkiratul-Khawwas: 363, Uqadu Ad-Durar: 43, mlango wa 1. Minihajus- Sunnah cha Ibnu Taymiyah 4: 86 – 87.
 • 8. Tarikh Bukhari 3: 364. Al-Muujam Al-Kabir 23: 267, Hadithi ya 566. Mustadak
  Al-Hakim 4: 557.
 • 9. Sunan Abu Dawdi 4: 104, Hadithi ya 4284. Sunan Ibnu Majah 2: 1368, mlan- go wa 34, Hadithi ya 4086. Al-Firdawsu 4: 497, Hadithi ya 6943. Maswabihul- Baghawi 3: 492, mlango wa 3, Hadithi ya 4211. Jamiul-Usul 5: 343. Matwalibu As-Suul: 8. Uqadu Ad-Durar: 36, mlango wa 1. Mizanul-Iiitidal 2: 87. Mishkatul- Maswabihi 3: 24, sura ya 2, Hadithi ya 5453. Tuhfatul-Ashraf 13: 7, Hadithi ya 18153. Al-Jamiu As-Saghir 2: 672, Hadithi ya 9241. Ad-Durul-Manthur 6: 57.
  Jam’ul-Jawamiu 1: 449. As-Swawaiq cha Ibnu Hajar: 141, mlango wa 11, sura ya 1. Kanzul-ummal 14: 264, Hadithi ya 38662. Mirqatul-Mafatihi 9: 350. Is’afur- Raghibina: 145. Faydhul-Qadir 6: 277, Hadithi ya 9241. At-Taju Al-Jamiu Lil- Usul 5: 343.
 • 10. Al-Manaru Al-Munifu cha Ibnul-Qayyim: 148, 329, sura ya 50, kutoka kwa At- Tabaraniy ndani ya kitabu Al-Awsatu. Uqadu Ad-Durar: 45, mlango wa kwanza, humo mna: “Ameitoa Al-Hafidhu Abu Nua’im katika sifa ya Mahdi.”. Dhakhairul-Uqba cha Al-Muhibu At-Tabari: 136, humo mna: “Maelezo yasiyoainishi yanatafsiriwa na haya yaliyoainishi.” Faraidu As-Samtwayni 2: 325, 575, mlango wa 61. Al-Qawlu Al-Mukhtasar cha Ibnu Hajar 7: 37, mlango wa 1. Faraidu Fawaidul-Fikri: 2, mlango wa 1. As-Siratul-Halbiyah 1: 193. Yanabiul- Mawaddah 3: 63, mlango wa 94. Na kuna Hadithi nyingine zenye kuelezea sifa hizi mahususi ndani ya kitabu Maqtalul-Imam Al-Husayn cha Al-Khawarazamiy Al-Hanafiy 1: 196. Faraidu As-Samtwayn 2: 310 – 315, Hadithi za 561 – 569. Yanabiul-Mawadah 3: 170: 212, mlango wa 93 na mlango wa 94.
 • 11. Al-Bayanu: 120, mlango 9. Al-Fusulul-Muhimmah: 286, chapa ya Darul- Adh’wai, sura ya 12. Yanabiul-Mawadah: 490 na 493, mlango wa 94, japokuwa kuna tofauti kidogo.
 • 12. Yanabiul-Mawaddah: 491 kutoka kwenye kitabu Al-Arbauni cha Al-Hafidhu Abu Naim Al-Isbihaniy.
 • 13. Yanabiul-Mawaddah: 448 na 489, imenukuliwa kutoka kitabu Faraidu As- Samtwayni.
 • 14. Mashariqul-An’wari Fifawzi Ahlil-Iitibar cha Sheikh Hasan Al-Adawi Al- Hamzawiy Al-Misriy: 476 – 477, sura inayohusu Mahdi. Yawaqitul-Jawahir 562, mlango unaohusu alama zote za Kiyama, imenukuliwa kutoka kwenye kitabu Al-