read

Jambo La Saba: Bendera ya Mahdi (a.s.)

Na miongoni mwa alama alizoongezewa mwislamu wa zama za kudhihiri kwake (a.s.) ili ajikinge na asiweze kuingia ndani ya mikondo ya upotovu ni wasifu wa bendera ya Imam Mahdi na wito wake unaosubiriwa. Kwani bendera yake (a.s.) ina alama itakayowaongoza wenye kungojea kudhihiri kwake, basi hebu tuzitazame riwaya hizi mbili zifuatazo:

1- Kutoka kwa Abdullah bin Sharik, amesema: “Mahdi atakuwa na ben- dera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) iliyohukumiwa kushinda. Natamani ningekutana naye ilhali nikiwa ni mwenye nguvu mno.”1

2- Kutoka kwa Abu Is’haqa kutoka kwa Nufu Al-Bukaiy: “Bendera ya Mahdi imeandikwa: Kiapo cha utii ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”2

  • 1. Ibnu Hammad: 249, Hadithi ya 972. Al-Qawlu Al-Mukhtasar: 100, mlango wa 3, Hadithi ya 35. Burhanul-Muttaqiy: 152, mlango wa 7, Hadithi ya 24.
  • 2. Ibnu Hammad: 249, Hadithi ya 973. Uqad Ad-Durar: 274, mlango wa 9. Al- Qawlu Al-Mukhtasar: 101, mlango wa 3, Hadithi ya 36. Burhanul-Muttaqiy: 152, mlango wa 7, Hadithi ya 25. Faraidu Fawaidul-Fikri: 8, mlango wa 4. Yanabiul- Mawaddah: 435, mlango wa 73.