read

Jambo La Sita: Mahdi (a.s.) atamswalisha Nabii Isa (a.s.)

Ikiwa dalili za nukuu zilizomo ndani ya Sahih Sita na vitabu vingine zina- sisitiza ukweli wa Imam Mahdi, kuanzia utu wake, jina lake, nasaba yake hadi sifa zake nyingine, hivi je, muislamu wa zama atakazodhihiri ame- ongezewa alama nyingine zitakazoimarisha imani yake kwake na utiifu kwa huyu mtu aliye Imam mwenyewe, na kumwepusha na mafuriko nyuma ya madai na mkondo wa upotovu?

Hakika riwaya zifuatazo zinasisitiza ukweli huu wa kihistoria nao ni kuwa, Nabii Isa (a.s.) atateremka kutoka mbinguni na kusali nyuma ya Imam Mahdi mwana wa Hasan Al-Askari (a.s.).

1- Ile aliyoitoa Ibnu Shaybah ndani ya kitabu Al-Muswannaf, kutoka kwa Ibnu Sirini amesema: “Mahdi ni kutoka ndani ya umma huu, na yeye ndiye atakayemsalisha Isa bin Maryam.”1

2- Ile aliyoitoa Abu Nua’im kutoka kwa Abdullah bin Amru amesema: “Mahdi atateremkiwa na Isa bin Maryam, na Isa atasali nyuma yake.”2

3- Ile aliyoisema Al-Munawi katika kufafanua Hadithi: “Ni kutoka kwetu yule ambaye Isa bin Maryam atasali nyuma yake.” Akasema: “Kutoka kwetu” yaani sisi Ahlul-Bayt. “Ambaye” yaani mtu ambaye. “Isa bin Maryam atasali” yaani Ruhullah pindi atakapoteremka kutoka mbinguni zama za mwisho pindi Dajjal atakapodhihiri. “Nyuma yake” yaani atateremka wakati wa swala ya Asubuhi juu ya mnara mweupe Mashariki mwa Damascus, na kumkuta Imam Mahdi akitaka kusali, hivyo atamuhisi na hapo atarudi nyuma ili (Isa) atangulie, lakini Isa atamtanguliza na kusali nyuma yake. Na hapo umma huu utapata fadhila na sharafu kubwa kupitia kwake.”3

4- Aliyoisema Ibnu Burhani As-Shafiy kuhusu kuteremka kwa Isa (a.s.): “Kuteremka kwake kutakuwa wakati wa swala ya Alfajiri, atasali nyuma ya Mahdi baada ya Mahdi kumwambia: “Tangulia ewe Ruhullah” naye ata- jibu: Tangulia imekimiwa kwa ajili yako.”

Akaendelea mpaka akasema: “Hakika Mahdi atatokeza pamoja na Isa na hivyo kumsaidia kumuua Dajjal. Na imepokewa kuwa Mahdi ni kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kupitia kizazi cha Fatima.”4

5- Ile iliyokuja ndani ya kitabu Fat’hul-Bari: “Abu Hasani Al-Khasaiy Al-Abadiy5 ndani ya kitabu Manaqib Ash-Shafiiy amesema: Zimekuwa nyin- gi mno habari kuwa Mahdi ni kutoka ndani ya umma huu na kuwa Isa ataswali nyuma yake. Amelitaja hilo ikiwa ni kujibu Hadithi ambayo ime- tolewa na Ibnu Majah kutoka kwa Anas isemayo: “Hakuna Mahdi ila ndiye Isa mwenyewe.” Kisha akajibu kauli ya At-Twibiy isemayo kuwa maana yake ni: “Isa atawasalisha akiwa ndani ya dini yenu.” Akajibu kwa kuse- ma: “Inabatilishwa na kauli yake iliyomo kwenye Hadithi nyingine ya Muslim: “Ataambiwa tusalishe. Atasema hapana, hakika wao kwa wao ni viongozi kwa ajili ya kuupa heshima umma huu.”

Kisha akanukuu kutoka kwa Ibnu Al-Jawziy kauli yake: “Laiti Isa ange- tangulia kama Imam basi nafsi ingeingiwa na utata, na ingesemwa: Unaona ametangulia kama naibu au nabii mpya kisheria? Hivyo ataswali kama maamuma ili asichafuliwe na vumbi za utata kutokana na kauli ya (s.a.w.w.): “Hakuna nabii yeyote baada yangu.”

Kisha akasema: “Isa kusali nyuma ya mtu wa kutoka ndani ya umma huu ilihali ikiwa ni zama za mwisho, na ile kukaribia Kiyama ni dalili zithibitishazo usahihi wa kauli zisemazo: Hakika ardhi haikosi khalifa wa Mwenyezi Mungu aliye hoja.” Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.6

6- Aliyoitoa Ibnu Abu Shaybah kutoka kwa Ibnu Sirin: “Mahdi ni kutoka ndani ya umma huu na yeye ndiye atakayemswalisha Isa mwana wa Maryam.”7

  • 1. Al-Muswannaf cha Ibnu Abu Shaybah 15: 198: 19495
  • 2. Al-Hawi Lil-Fatawa cha As-Suyutiy 2: 78.
  • 3. Faydhul-Qadir cha Al-Munawi 6: 17
  • 4. As-Siratu Al-Halbiyah cha Ibnu Burhani As-Shafiy 1: 226 – 227.
  • 5. Hivyo ndivyo ilivyo, na sahihi ni Al-Abariy. Baadhi wamemwita kwa kuniya ya Abu Husein, na sahihi ni Abu Hasani. Alifariki mwaka 363 A.H. Kama ilivyo ndani ya wasifu wake.
  • 6. Fat’hul-Bari Bisharhi Sahih Bukhar cha Ibnu Hajar Al-Asqalaniy 6: 383 – 385.
  • 7. Al-Muswannaf cha Ibnu Abu Shaybah 15: 198, 19495.