read

Jambo La Tano: Mahdi (a.s.) khalifa wa Mwenyezi Mungu na hitimisho la maimamu (a.s.)

Ikiwa Imam Mahdi tuliyeahidiwa ndiye Muhammad bin Hasan Al-Askari (a.s.), na nafasi yake kwa Mwenyezi Mungu ni khalifa wa haki ambaye ni lazima kumtii. Basi tunajiuliza: Je, kuna Imam mwingine atakuja baada yake? Au yeye ndiye khalifa wa mwisho kutoka Ahlul-Bayt (a.s.) na hitimisho lao, kama wanavyoamini Shia Imamiyya na kumngojea?

Riwaya zifuatazo ambazo ni kutoka kwenye vitabu vya Sunni zinazungumza kuwa Mahdi tuliyeahidiwa ndiye Imam wa mwisho na hitimisho la makhalifa (a.s.).

1- Kutoka kwa Thawbani amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Watatu watagombana kwenye hazina yenu wote wakigombania ukhalifa, kisha hakuna hata mmoja miongoni mwao atakayeupata, kisha zitatokeza bendera nyeusi upande wa Mashariki na kuwauwa mauaji yasiyowahi kufanywa na kaumu yoyote.” – kisha akase- ma jambo ambalo silikumbuki – Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Mkimuona basi mpeni kiapo cha utii angalau kwa kutambaa juu ya thelu- ji, kwani hakika yeye ni Mahdi khalifa wa Mwenyezi Mungu.”1

2- Imepokewa kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Nilimwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mahdi ni kutoka kwetu sisi maimamu wa uongofu au ni kutoka kwa asiye sisi? Akasema: “Bali ni kutoka kwetu, dini inahitimishwa kupitia kwetu kama ilivyofun- guliwa kupitia kwetu, na kupitia kwetu wataokolewa dhidi ya upotovu wa fitina kama walivyookolewa dhidi ya upotovu wa shirki. Kupitia kwetu Mwenyezi Mungu ataunganisha kati ya nyoyo zao ndani ya dini baada ya uadui wa fitina kama alivyounganisha nyoyo zao na dini Yake baada ya uadui wa shirki.”2

3- Ibnu Hajar Al-Haythamiy aliyefariki mwaka 974 A.H. Amesema: “Abu Hasan Al-Abiriy amesema: Zimekuwa nyingi mno habari na zikazidi kwa uwingi wa wapokezi wake kutoka kwa Al-Mustafa (s.a.w.w.) kuhusu kutokeza kwake – Mahdi – na kuwa yeye ni kutoka ndani ya Ahlul-Bayt wake, na kuwa ataijaza ardhi uadilifu, na kuwa yeye atatoka pamoja na Isa (a.s.) na hivyo atamsaidia katika kumuuwa Dajjal huko kwenye mlango wa Ludi kwenye ardhi ya Palestina, na kuwa yeye atasalisha umma huu akiwa Imam na Isa ataswali nyuma yake.”3

4- Sheikh As-Swabbani aliyefariki mwaka 1206 A.H. Amesema: “Zimekuwa nyingi mno habari kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu kutokeza kwake – Mahdi – na kuwa yeye ni kutoka ndani ya Ahlul- Bayt wake, na kuwa ataijaza ardhi uadilifu, na kuwa yeye atamsaidia Isa (a.s.) katika kumuuwa Dajjal huko kwenye mlango wa Ludi kwenye ardhi ya Palestina, na kuwa yeye atasalisha umma huu akiwa Imam na Isa atasali nyuma yake.”4

5- Hadithi ya Abu Saidi Al-Khudri: “Ardhi itajaa ukatili na dhuluma, ndipo atatokeza mtu kutoka ndani ya kizazi changu…5

  • 1. Al-Bayan: 104, mlango wa 3. Sunan Ibnu Majah: 2 / 1367, Hadithi ya 4084. Al- Mustadrak: 4 / 463. Talkhisul-Mustadrak: 4 / 463 na 464. Musnad Ahmad bin Hanbal: 5 / 277, japo kuna tofauti kidogo.
  • 2. Al-Muujamu Al-Awsatu 1: 136, Hadithi ya 157. Al-Bayan: 125, mlango wa 11. Uqadu Ad-Durar: 192, mlango wa 7. Majmauz-Zawaidi 7: 316 – 317. Muqaddimati Ibnu Khalduni: 396 na 397, mlango wa 53. Al-Fusul Al-Muhimmah: 288, japo kuna tofauti kidogo, sura ya 12. Urufus-Suyutiy Al-Hawi 2: 217. Jam’ul- Jawamiu 2: 67. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 163, mlango wa 11, sura 1. Kanzul- ummal 14: 598, Hadithi ya 39682. Burhanul-Muttaqiy: 91, mlango wa 2, Hadithi ya 7 na 8. Faraidu Fawaidul-Fikri: 3, mlango 1. Nurul-Absar: 188.
  • 3. As-Sawaiq Al-Muhriqah cha Ibnu Hajar: 165, chapa ya Misri.
  • 4. Is’afur-Raghibina cha As-Swaban: 140.
  • 5. Mustadrak Al-Hakim 4: 558.