read

Jambo La Tatu: Sifa za Imam Mahdi

Baada ya kubainika jina la Imam Mahdi na nasaba yake, basi katika jambo hili tutazungumzia riwaya zilizopatikana ndani ya vitabu vya Sunni zina- zohusu sifa za kimaumbile za Imam (a.s), kuanzia sifa ya uso, rangi yake, nywele na mfano wa hayo. Tutabainisha hayo ndani ya riwaya mbalimbali.

1- Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudri, kutoka kwa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Mahdi wa kutoka kwangu ni mwenye paji bapa na pua nyembamba yenye mwinuko, ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa ukatili na dhuluma…”1

2 - Imepokewa kutoka kwa Hudhayfa amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Mahdi ni mtu kutoka ndani ya kizazi changu, uso wake ni kama mwezi ung’aao, rangi yake ni rangi ya kiarabu, kiwili- wili chake ni kiwiliwili cha kiisraeli, ataijaza ardhi uadilifu, kama itakavyokuwa imejaa dhulma. Wataridhia ukhalifa wake watu wa mbingu- ni na aridhini na ndege wa angani….” 2

3- Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudri kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Mahdi ni kutoka kwetu Ahlul-Bayt, ni mwenye pua nyembamba yenye mwinuko ulionyooka, mwenye paji bapa, ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa ukatili na dhuluma. Ataishi hivi.” Akawa amefungua mkono wake wa kushoto na vidole viwili – kidolegumba na kidoleshahada – vya mkono wa kulia na akawa amefumba vitatu vilivyobaki.3

4- Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Al-Harthu amesema: “Mahdi ata- jitokeza akiwa na miaka arubaini kama mtu kutoka kizazi cha Israil.”4

5- Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Jubayri amesema: “Mahdi ni mwenye nyusi laini zilizolala kwa urefu, paji bapa na macho meusi mno, atakuja kutokea Hijazi na kutulia juu ya mimbari ya Damascus akiwa kijana wa miaka kumi na minane.5

6- Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Bashir kutoka kwa Kaab amese- ma: “Mahdi ni mnyenyekevu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama unyenyekevu wa mbawa za furukombe.”6

7- Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Mahdi ni kijana kutoka kwetu Ahlul-Bait.”7

8- Imepokewa kutoka kwa Abdur-Rahmani bin Awfi kutoka kwa baba yake amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu atamleta mtu kutoka ndani ya kizazi changu, ana mwanya na paji bapa, ataijaza ardhi usawa na uadilifu na ataimwagia mali nyingi.”8

9- Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Ja’far kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Hakika mwana wa huyu ni bwana kama alivy- omwita Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na Mwenyezi Mungu ata- toa kwenye mgongo wake mtu mwenye jina la nabii wenu, anafanana naye kwa maumbile na tabia, atatoka wakati ambao watu watakuwa katika mghafala, wakiifisha haki na kudhihirisha dhulma. Wallahi laiti angekuwa hatokei basi ningemkata shingo yake. Kwa kutokeza kwake watafurahia watu wa mbinguni na wakazi wake, na yeye ni mtu mwenye paji bapa, pua nyembemba yenye mwinuko, tumbo pana, mwenye matege huku paja lake la kulia likiwa na weusi na ni mwenye mwanya, ataijaza ardhi uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhuluma na ukatili.”9

10- Imepokewa kutoka kwa Sulayman bin Habib amesema: “Nilimsikia Abu Umamah Al-Bahiliy akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Kati yenu na Rum kutakuwa na vituo vinne vya kupumzika kwa siku, cha nne atakifungua mikononi mwa mtu kutoka jamaa wa mteule na atadumu miaka saba.” Basi mtu mmoja kutoka ukoo wa Abdul-Qaysi aliyekuwa akiitwa Al-Mustawradu bin Ghaylan aka- muuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani atakuwa Imam wa watu zama hizo? Akasema: “Mahdi kutoka ndani ya kizazi changu, mwenye miaka arubaini, uso wake kama nyota ing’aayo huku kwenye shavu lake la kulia kukiwa na weusi….10

11- Imepokewa kutoka kwa Al-Haytham bin Abdur-Rahman kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) amesema: “Mahdi sehemu ya kuzaliwa kwake ni Madina, ni kutoka Ahlul-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), jina lake ni jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), eneo atakalohamia ni Baytul-Maqdas, ana ndevu za msokotano, mwenye macho ya wanja, meno yake ya mbele ni yenye kung’aa, usoni mwake ana weusi, mwenye pua nyembamba yenye mwinuko, mwenye paji bapa, begani kwake kuna alama ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). bendera yake inatokana na kitambaa kisichoshonwa yenye utande wa nyuzinyuzi, ni nyeusi ya pembe nne na imekunjwakun- jwa, haijapepea tangu afariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na haitopeperush- wa mpaka atokeze Mahdi (a.s.). Mwenyezi Mungu atampa msaada kwa Malaika elfu tatu watakaowapiga mbele na nyuma wale waliowakhalifu.”11

 • 1. Sunan Abi Dawdi 4: 107, Hadithi ya 428. Mustadrak Al-Hakim 4: 557, japo ina tofauti kidogo. Maalimus-Sunan 4: 344. Maswabihul-Bahgawi 3: 492, Hadithi ya 4212. Al-Ilalu Al-Mutanahiyah 2: 859, Hadithi ya 1443. Jamiul-Usul 5: 343, mlango 7. Matalibus-Su’ul 2: 80, mlango wa 12. Al-Bayan: 117. Uqadu Ad-Durar: 59, mlango wa 3. Mishkatul-Maswabihi 3: 171, mlango wa 2, sura ya 2, Hadithi ya 5454. Al-Jamiu As-Swaghir 2: 672, Hadithi ya 9244. Jam’ul-Jawamiu 1: 449. Kanzul-ummal 14: 264, Hadithi ya 38665. Mirqatul-Mafatihu 9: 351, Hadithi ya 5454. Faydhul-Qadir 6: 278, Hadithi ya 9244. At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5: 34, mlango wa 7.
 • 2. Al-Firdawsu 4: 496, Hadithi ya 6940. Al-Ilalu Al-Mutanahiyah 2: 858, Hadithi ya 1439. Al-Bayan: 118, mlango wa 8. Dhakhairul-Uqba: 136. Uqadu Ad-Durar:
  60, mlango wa 3, humo mna “Kama nyota ing’aayo.”. Mizanul-Iitidal 3: 449. Lisanul-Mizan 5: 24. Al-Fussul Al-Muhimmah: 284. Al-Jamiu As-Swaghir 2: 672, Hadithi ya 9245. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 164, mlango wa 11, sura ya 1. Kanzul- ummal 14: 264, Hadithi ya 38666. Mirqatul-Mafatihi 9: 350. Lawaihus-Safawiniy 2: 4. Is’afur-Raghibina: 146. Nurul-Absar: 187. Faydhul-Qadir 6: 279, Hadithi ya 9245.
 • 3. Mustadrak Al-Hakim 4: 558. Uqad Ad-Durar: 60, mlango wa 3, japo mna tofauti kidogo. Faraidu As-Samtwayni 2: 330, Hadithi ya 580. Burhanul-Muttaqiy: 98, mlango wa 2, Hadithi ya 28 na 99, mlango wa 3, Hadithi ya 3. Yanabiul- Mawaddah: 488, mlango wa 94.
 • 4. Futunu Ibnu Hammad: 258, Hadithi ya 1008. Urufu As-Suyuti Al-Hawiy 2:232. Burhanul-Muttaqiy: 99, mlango wa 3, Hadithi ya 2. Kanzul-ummal 14: 586, Hadithi ya 39660.
 • 5. Burhanul-Muttaqiy: 100, mlango wa 3, Hadithi ya 5. Uqadu Ad-Durar: 64, mlango wa 3. Urufus-Suyuti Al-Hawi 2: 232. Faraidu Fawaidul-Fikri: 4, mlango 2.
 • 6. Ibnu Hammad: 258. Uqad Ad-Durar: 65, mlango wa 3. Urufus-Suyuti Al-Hawi 2: 232. Al-Qawlu Al-Mukhtasar: 98, mlango wa 3, Hadithi ya 29. Burhanul- Muttaqiy 101, mlango wa 3, Hadithi ya 10.
 • 7. Ibnu Hammad: 102. Urufus-Suyuti Al-Hawi 2: 232. Burhanul-Muttaqiy 98,
  mlango wa 2, Hadithi ya 26 na 27. Kanzul-ummal 14: 585, Hadithi ya 39658, japo kuna tofauti kidogo. Faraidu Fawaidul-Fikri: 2, mlango 1.
 • 8. Al-Bayanu: 139, mlango wa 19. Uqadu Ad-Durar: 37, mlango wa 1. Faraidu As-Samtwayni 2: 331, Hadithi ya 582, japo mna tofauti kidogo. Urufus-Suyuti Al- Hawi 2: 220. As-Sawaiq cha Ibnu Hajar: 164, mlango wa 11, sura ya 1. Al-Qawlu Al-Mukhtasar: 43, mlango wa 1, Hadithi ya 33. Burhanul-Muttaqiy: 84, mlango wa 1, Hadithi ya 32. Is’afur-Raghibina: 146. Yanabiul-Mawaddah: 433, na 436, mlango wa73, sura ya 2. Faraidu Fawaidul-Fikri: 4, mlango 2.
 • 9. Sunan Ibnu Dawdi 6: 162, Hadithi ya 4121. Uqadu Ad-Durar: 45, mlango wa 1. Futunu Ibnu Kathir 1: 38. Muqaddimatu Ibnu Khaliduni: 391, sura ya 53. Urufus-Suyuti Al-Hawi 2: 214. Ad-Durrul-Manthur 6: 39, mwishoni mwa Aya ya 8. Jam’ul-Jawamiu 2:35. Kanzul-ummal 13: 647, Hadithi ya 37636. Mirqatul- Mafatihu 9: 363, Hadithi ya 5462. Yanabiul-Mawaddah: 432, mlango wa72. At- Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5: 343, Hadithi ya 10.
 • 10. Al-Bayan: 137–138, mlango wa 18, kutoka kwenye Al-Muujam Al-Kabir na
  Manaqib Al-Mahdawi cha Abu Nua’im.
 • 11. Al-Bayan: 140, kutoka kwenye Al-Muujam Al-Kabir cha At-Tabaraniy na
  Manaqib Al-Mahdawi cha Abu Nua’im.