read

Jambo La Tisa: Miujiza ya Imam Mahdi (a.s.)

Ikiwa Mahdi tuliyeahidiwa ndiye mmoja kati ya maimamu watakasifu, kwa mujibu wa imani ya Shia Imamiyya ni lazima Imam huyu atakuwa na vipaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kama vile elimu pana na uwezo wake wa kufanya miujiza ambayo ataitoa kwa watu ili kuhimiza uimamu wake na ukhalifa wake wa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), kama vitendo vya nguvu ya ghaibu vilivyokuwa vikitoka kwa baba zake, kwani baba zake kumi na moja watakasifu walikuwa na miujiza na karama mbalimbali iliyosisitiza hadhi yao mbele ya Mola. Maelezo ya riwaya zifuatazo yanaashiria ukweli huu halisi:

1- Kutoka kwa kiongozi wa waumini Ali bin Abu Twalib (a.s.) amesema: “Mahdi atakuwa anamwashiria ndege na kuanguka mikononi mwake, na atakuwa anapanda mti sehemu ndogo ya ardhi basi unastawi na kutoa majani.”1

2- Kutoka kwa kiongozi wa waumini Ali bin Abu Twalib (a.s.) amesema: “Bendera tatu zitatofautiana: Bendera ya Morocco na bendera ya Uarabuni na bendera ya Sham, fitina itadumu mwaka mzima kati yao.” Kisha akazungumzia kutokeza kwa As-Sufyaniy na dhuluma na ujeuri atakao- fanya, kisha akazungumzia kutokeza kwa Mahdi na kupewa kiapo cha utii eneo la kati ya Ruknu na Maqam, kisha akasema: “Atakwenda na jeshi kubwa mpaka afike kwenye mabonde ya vijiji kwa utulivu na upole, na huko mwana wa ami yake Al-Hasaniy ataungana naye akiwa na wapanda farasi elfu moja na kumwambia: Ewe mwana wa ami yangu! Mimi nina haki zaidi na jeshi hili kuliko wewe, mimi ni mwana wa Hasan na mimi ndiye Mahdi. Basi Mahdi (a.s.) atamjibu: “Bali mimi ndiye Mahdi.” Hapo Al-Hasaniy atamwambia: “Je, una muujiza wowote nikupe kiapo cha utii? Ndipo Mahdi ataashiria kwenye ndege na kudondoka mikononi mwake, na atapanda mti sehemu ndogo ya ardhi na ndipo utastawi na kutoa majani. Hapo Al-Hasaniy atamwambia: Ewe mwana wa ami yangu hili (jeshi) lenyewe ni la kwako.”2

Muhtasari

Kutokana na uchambuzi imebainika kuwa imani ya ulazima wa kudhihiri suluhisho la ulimwengu zama za mwisho si imani ya watu wa dini tu, bali inajumuisha hata makundi ya kitheolojia na kifilosofia yasiyokuwa ya kidini. Pamoja na dini kukiri ulazima wa kudhihiri suluhisho hili vilevile uchambuzi wa kielimu umeongeza utabiri mbalimbali uliopatikana ndani ya vitabu vya zama mbili kwa namna ya kipekee kuwa suluhisho hili ndiye Mahdi (a.s.).

Wanavyuoni bila kujali madhehebu yao ya kiisilamu wamesajili matamko ya kukiri kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.) kuanzia mwaka 260 A.H. mpaka wakati tulio nao. Hivyo basi, kulichunguza kundi la Hadithi za Mahdi (a.s.) zinazopatikana ndani ya vitabu vya Waisilamu kunatosha kuleta yakini kuwa zimetoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa wingi bila shaka yoyote ile.

Kwa muhtasari ni kuwa uwingi wake umethibiti ndani ya vitabu vya Sunni3 ambazo wanavyuoni na wasimulizi wamezitoa ndani ya vitabu vyao vingi.4 Wanavyuoni mbalimbali wametamka wazi hilo akiwemo At- Tirmidhiy aliyefariki mwaka 297 A.H.5, Al-Hafidhu Abu Jafar Al-Aqiliy aliyefariki mwaka 322 A.H6, Al-Hakim An-Nisaburi aliyefariki mwaka
405 A.H.7, Imam Al-Bayhaqiy aliyefariki mwaka 458 A.H.8, Imam Al- Baghawi aliyefariki mwaka 510 A.H.9, Ibnu Al-Athir aliyefariki mwaka
606 A.H10., Al-Qurtubiy Al-Malikiy aliyefariki mwaka 671 A.H.11, Ibnu Taymiyya aliyefariki mwaka 728 A.H.12, Al-Hafidhu Ad-Dhahabiy aliye- fariki mwaka 748 A.H.13, Al-Kunjiy As-Shafiy aliyefariki mwaka 658
A.H.14, Al-Hafidhu Ibnu Al-Qayyim aliyefariki mwaka 751 A.H.15, na wengineo waliokiri usahihi wa Hadithi za Mahdi kama vinavyoeleza vitabu vyao.

Pia kundi lingine la wanavyuoni wa kisuni limetamka wazi uwingi wa Hadithi za Mahdi, na sisi hapa tutafupisha kwa kutaja baadhi yao akiwemo Al-Barbahariy aliyefariki mwaka 329 A.H.16, Muhammad bin Hasan Al-Abariy As-Shafiy aliyefariki mwaka 363 A.H., hili limenukuliwa na Al- Qurtubiy Al-Malikiy17 kutoka kwake. Na Al-Qurtubiy Al-Malikiy aliye- fariki mwaka 671 A.H.18, Al-Hafidhu Al-Mutqinu Jamalud-Dini Al- Mazniy aliyefariki mwaka 742 A.H.19, Ibnu Al-Qayyim aliyefariki mwaka 751 A.H.20, Ibnu Hajar Al-Asqalaniy aliyefariki mwaka 751 A.H.21, na wengineo.

Na nyongeza ya habari zinazounga mkono uwingi wa Hadithi zake ni zile zinazotoa wasifu wake, umbile lake na vitendo vyake, na habari zina- zozungumzia jina lake, nasaba yake, jina la mama yake na jina la baba yake.

Na tunamuainisha kutoka kwenye habari zisizoainisha kwa kupitia habari zinazozungumzia utu wake kama zile zinazosema kuwa Mahdi ni kutoka wana wa Abdul-Mutwalib, na kuwa yeye ni kutoka kizazi cha Abu Talib, na kuwa ni kutoka Ahlul-Bayt (a.s.) na kuwa ni kutoka kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kuwa ni kutoka kizazi cha Fatima, na kuwa ni kutoka kizazi cha Husein na kuwa ni kutoka kizazi cha As-Swadiq na kuwa ni kutoka kizazi cha Ar-Ridha (a.s.), na kuwa yeye ni khalifa wa Mwenyezi Mungu na hitimisho la maimamu, na kuwa yeye atamsalisha Nabii Isa (a.s.).

Maelezo haya yote ambayo yanamuainisha na kumbainisha Imam Mahdi tuliyeahidiwa ambaye hitimisho la Mitume, Muhammad (s.a.w.w.) alibashiri kudhihiri kwake zama za mwisho yanaonyesha kuwa yeye ni Muhammad bin Hasan Al-Askari bin Ali Al-Hadiy bin Muhammad Al- Jawaad bin Ali Ar-Ridha.

Na hivyo inabainika waziwazi kuwa Mahdi tuliyeahidiwa amezaliwa nusu ya pili ya karne ya tatu ya hijiriya na yeye yuko hai anaendelea kuruzuki- wa. Ama kitendo cha sifa zake kuelezwa kwa ufafanuzi zaidi kwa kutilia umuhimu sifa zake za kimwili, kiroho na kimaadili ni uthibitisho wa kweli jinsi gani sheria ilivyotilia umuhimu uainishaji wa mtu huyu kiongozi wa kiulimwengu tuliyeahidiwa na mfano halisi wa mtu huyo ambaye ni Imam Mahdi (a.s.) ili asifanane na mwingine na ili wapotoshaji wasitumie fursa hii kuwapotosha watu. Na zaidi ya hapo uainishaji huu unamzidishia mtafi- ti imani na yakini kuhusu suala la kiulimwengu la Imam Mahdi (a.s.) kupi- tia wasifu wake uliotolewa na Uislam.

Na mwisho wa dua zetu ni kushukuru kuwa kila sifa njema ni ya
Mwenyezi Mungu.

 • 1. Burhanul-Muttaqiy: 76, mlango wa 1, Hadithi ya 14.
 • 2. Burhanul-Muttaqiy: 76, mlango wa 1, Hadithi ya 15.
 • 3. Rejea Ibrazul-Wahmi Al-Maknuni: 437.
 • 4. Ameviorodhesha Ustadh Muhammad Ali Dakhil ndani ya kitabu chake Al- Imam Al-Mahdi: 259 – 365, mpaka kafikisha vitabu thelathini vya kisuni.
 • 5. As-Sunan At-Tirmidhiy 4: 505, 2230, 2231 na 4: 506, 2233.
 • 6. Ad-Dhuafau Al-Kabir cha Al-Aqiliy 3: 253 na 1257.
 • 7. Mustadrak Al-Hakim: 4 / 429 na 465 na 553 na 558.
 • 8. Al-Itiqad Wal-Hidayatu Ilas-Sabilir-Rashadi cha Al-Bayhaqiy: 127.
 • 9. Maswabihus-Sunnah: 492 – 493 / 4210 – 4213 na 4215.
 • 10. An-Nihayatu Figharibil-Hadithi Wal-Athar cha Ibnu Al-Athir 5: 254.
 • 11. At-Tadhkiratu cha Al-Qurtubiy: 704, mlango wa yanayomhusu Mahdi.
 • 12. Minihajus-Sunnah cha Ibnu Taymiya 4: 211.
 • 13. Talkhisul-Mustadrak cha Ad-Dhahabiy 4: 553 na 558.
 • 14. Al-Bayanu Fi-Akhbar Swahibuz-Zaman: 500.
 • 15. Al-Manaru Al-Munif cha Ibnu Al-Qayyim: 130 – 135/ 326 na 327 na 39 na 331.
 • 16. Al-Ihtijaju Bil-Athari Ala Man An’kara Al-Mahdi Al-Muntadhar: 28.
 • 17. At-Tadhkirah 1: 7. Tahdhibul-Kamal cha Al-Mazniy 25: 146 / 5181.
 • 18. At-Tadhkirah 1: 701.
 • 19. Tahdhibul-Kamal 25: 146, 5181.
 • 20. Al-Manaru Al-Munif: 135.
 • 21. Tahdhibut-Tahdhibu 9: 125, 201.