read

Sura Ya Kwanza

Uthibitisho wa kiimani juu ya uwelewa wa wazo la

Mahdi upande wa Ahlul-Bait (a.s.)

Dalili ya kiimani juu ya wazo hili inapatikana ndani ya mamia ya riwaya zilizopatikana kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)1 ambazo zinamwainisha Mahdi kuwa ni miongoni mwa Ahlul-Bait (a.s.)2…. Na kuwa ni kutoka kizazi cha Fatima3… Na ni kutoka kizazi cha
Husein4…. Na kuwa ni wa tisa kutoka kizazi cha Husein5….

Na kuwa ni Khalifa wa kumi na mbili.6

Haya ni makundi matano ya riwaya zinazoshindana katika kubainisha uwelewa wa wazo la Mahdi na kumwainisha Imam Mahdi, na yule atakayezichunguza atazikuta zinakwenda hatua kwa hatua zikianzia kwenye anuani kuu mpaka kwenye kifungu kidogo mpaka zinafika kumwainisha mhusika mwenyewe.

Sayyid Shahid Muhammad Baqir As-Swadri (q.s.) amebainisha kuwa: “Zimefikia kiwango cha juu cha uwingi na kuenea licha ya kuwa Maimamu (a.s.) walijizuia na kuchukua tahadhari katika kueneza fikira hii kwa watu wote, walifanya hivyo kwa ajili ya kumlinda mrithi mwema (a.s.) dhidi ya njama mbaya zinazolenga kuutoa uhai wake haraka iwezekanavyo.7 Wala uwingi wa idadi ya wapokezi wake sio kigezo pekee cha msingi cha kuzikubali, bali zaidi ya hapo ni sifa na vielelezo vinavyothibitisha usahihi wake.

Hivyo baadhi ya waandishi wamehesabu riwaya za Mtukufu Mtume kuhusu Maimamu au Makhalifa au Watawala baada yake, na kuwa wao ni Maimamu au Makhalifa au Watawala kumi na wawili wakazikuta ni zaidi ya riwaya mia mbili na sabini8, huku zikiwa zimechukuliwa kutoka kwenye vitabu mashuhuri vya Shia na Sunni, vikiwemo Bukhari9, Muslim10, Tirmidhi11, Abu Dawdi12, Musnad Ahmad13 na Mustdrakul-Hakim Alas-Sahihayni14.

Hapa tunakuta kuwa Bukhari ambaye amenukuu Hadithi hii aliishi zama za Imam Al-Jawwad na maimamu wawili Al-Hadiy na Al-Askari, hilo lina makusudio makubwa; kwa sababu hilo linathibitisha kuwa Hadithi hii ilisajiliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kabla ya madhumuni yake kutimia kivitendo ambayo ni fikira ya maimamu kumi na wawili. Hii inamaanisha kuwa hakuna shaka yoyote kuwa unakili wa Hadithi hii ume- tokana na ukweli wa wazo la uimamu wa maimamu kumi na wawili; kwa sababu Hadithi za uzushi ambazo zinanasibishwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni matukio au uhalalishaji wa hali iliyochelewa, Hadithi ambazo hazijaitangulia hali hiyo katika kudhihiri kwake na kusajiliwa ndani ya vitabu vya Hadithi.

Maadamu tumemiliki dalili ya kimaada kuwa Hadithi iliyotajwa ilitangu- lia kabla ya mfululizo wa kihistoria wa maimamu kumi na wawili, na ikad- hibitiwa ndani ya vitabu kabla ya kutimia maimamu kumi na wawili, basi tunaweza tukazidi kuamini kuwa Hadithi hii haitokani na hali hiyo bali yenyewe ni maelezo ya uhalisia kutoka kwa Mola ambayo ilielezwa na yule asiyetamka kwa matamanio yake,15 akasema: “Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili.”16 Na hali halisi ya maimamu kumi na wawili ikaanzia kwa Imam Ali na kukomea kwa Mahdi (a.s.) ili iwe ni uoanishaji wa pekee wa Hadithi hiyo tukufu17 wenye kukubalika kiakili.”18

Muslim ametoa ndani ya Sahih yake kwa njia ya Qutaybah bin Said kuto- ka kwa Jabir Ibnu Samara, amesema: “Niliingia na baba yangu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) nikamsikia akisema: “Jambo hili halitotoweka mpaka litawaliwe na makhalifa kumi na wawili.” Kisha akasema: Akazungumza maneno ambayo sikuyasikia, nikamwambia baba yangu: Amesema nini? Akasema: “Wote ni kutoka kwa makurayshi.”19

Kisha ameitoa kutoka kwa Ibnu Abu Umar, kutoka kwa Hudabu bin Khalid kutoka kwa Nasru bin Ali Al-Jahdhamiy kutoka kwa Muhammad bin Rafiu wote kwa njia moja. Na ameitoa kutoka kwa Abubakr bin Abu Shayba kwa njia wawili. Na kutoka kwa Qutaybah bin Said kwa njia wawili nyingine. Hizi ni njia tisa za Hadithi hii ndani ya kitabu Sahih Muslim tu, tusikwambie njia zake nyingine nyingi ndani ya vitabu vya Hadithi vya Sunni na Shia.20

Kambi ya Sunni yatapatapa katika tafsiri ya Hadithi hii

Swali hapa ni akina nani hawa makhalifa? Kabla hatujachagua jibu husi- ka la swali hili ni lazima kwanza tutoe dhana mbalimbali zinazotarajiwa katika maana ya Hadithi hii, na makusudio ya Mtukufu Mtume hapo. Hapa kuna dhana wawili tarajiwa na wala hakuna ya tatu, nazo ni:

1. Makusudio ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kubainisha hali ya kisiasa itakayoupata umma baada yake, akiwa katika hali ya kufichua na kuonye- sha mustakabali ikiwa ni mfululizo wa tabiri mbalimbali zilizotoka kwa (s.a.w.w.) kuhusu masuala mbalimbali. Hivyo malengo ya Hadithi hii ni kutoa habari za hali halisi ya mustakabali wa umma. Dhana hii tuipe jina la “ufafanuzi juu ya hali ya mustakabali.”

2. Makusudio ya (s.a.w.w.) ni kutoa azimio kwa kuainisha Imam na Khalifa baada yake, hivyo malengo yake ni kuanzisha na kusimika kwa mujibu wa sharia, na si kuelezea hali halisi ya mustakabali. Dhana hii tuipe jina la “ufafanuzi juu ya imani.”

Kwa muktadha wa elimu tunawajibika kuchunguza dhana hizi wawili na mwisho tuchague ile inayoungwa mkono na dalili na hoja za kiakili na za kinukuu. Ispokuwa madhehebu ya Sunni tangu mwanzo ilipoamini sheria ya utaratibu wa ukhalifa ilikataa nadharia ya uteuzi na hatimaye theiolojia yao na fikihi yao vikajengeka juu ya msingi huu na hivyo ikajikuta mbele ya dhana moja tu bila kuwa na kiwawilio lingine, nayo ni dhana ya kwan- za, na mwisho ikalazimika kukiletea tafsiri nyingine kila kinachopingana nayo, na kulazimika kuchukua tafsiri hizi hata kama hazioani na Hadithi na ziko mbali mno na kanuni za kiakili na za kijamii, kwa sababu ni jambo lisilokuwa na njia mbadala.

Kambi hii ilitakiwa iichunguze Hadithi hii kwa uchunguzi wa kielimu huru usioegemea fikira yoyote ili iweze kupata uhakika wa ubovu wa tafsiri ya “dhana ya ufafanuzi juu ya hali ya mustakbali”. Kwani ikiwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lengo lake ni kutoa hali itakayotokea basi ni sababu ipi iliyopelekea kuweka kikomo cha idadi ya makhalifa kumi na wawili ilihali mustakabali bado unaendelea zaidi ya hapo?

Ikiwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilenga ukhalifa sahihi unaooana na vip- imo vya sharia basi jua hakika madhehebu ya Sunni haiamini na wala hai- jakongamana ila kwa makhalifa wanne. Na kuanzia hapa ndipo mitazamo yao ikatapatapa katika kuainisha watu maalumu walio makhalifa kumi na wawili.

Kwa Ibnu Kathir makhalifa kumi na wawili ni wale wanne pamoja na Umar bin Abdul-Aziz na baadhi ya wana wa Abbas, na akadhihirisha kuwa Mahdi ni miongoni mwao.21

Kwa Kadhi Ad-Damashqiy makhalifa kumi na wawili ni wale wanne pamoja na Muawiya, Yazid bin Muawiya, Abdul-Malik bin Mar’wan na wanae wanne: Al-Walid, Sulayman, Yazid na Hisham. Na wa mwisho ni Umar bin Abdul-Aziz.22

Kwa Waliyullah msimulizi kwenye viburudisho vya macho mawili, kama ilivyokuja ndani ya kitabu ‘Awnul-Maabud’ makhalifa kumi na wawili ni wale wanne pamoja na Muawiya, Abdul-Malik bin Mar’wan na wanae wanne na Umar bin Abdul-Aziz na Walid bin Yazid bin Abdul-Malik. Kisha akanukuu kutoka kwa Malik bin Anas kuwa yeye alimjumuisha Abdullah bin Zubayr katika orodha hiyo, lakini mwandishi akaikataa kauli ya Malik akitoa dalili kupitia riwaya iliyopokewa kutoka kwa Umar na Uthman kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) inayoonyesha kuwa kutawala kwa Ibnu Zubayri kulikuwa ni miongoni mwa misiba mikubwa ya umma huu. Kisha akampinga yule aliyemjumuisha Yazid katika orodha hiyo huku akitamka waziwazi kuwa alikuwa na mwenendo mbaya mno.23

Ibnul-Qayyim Al-Jawziyy amesema: “Ama kuhusu makhalifa kumi na wawili ni kuwa jamaa akiwemo Abu Hatim na Ibnu Habban na wengineo wamesema: Wa mwisho wao ni Umar bin Abdul-Aziz, hivyo wakawataja makhalifa wanne kisha Muawiya kisha mwanae Yazid, kisha Muawiya bin Yazid kisha Mar’wan bin Al-Hakam, kisha Abdul-Malik na mwanae, kisha Al-Walid Ibnu Abdul-Malik kisha Sulayman bin Abdul-Malik kisha Umar bin Abdul-Aziz na kifo chake kilikuwa mwishoni mwa mwaka wa mia moja, nayo ndio karne iliyofadhilishwa ambayo ndio karne bora, na dini katika karne hii ilikuwa katika kilele cha utukufu kisha ndipo yakatokea
yaliyotokea.”24

An-Nur Bashtiy amesema: “Njia katika Hadithi hii na inayofatia katika maana hii, hutafsiriwa kuwa inawalenga waadilifu miongoni mwao, kwani wao ndio wanaostahiki jina la Khalifa kwa maana yake halisi, na wala hailazimu wawe ni watawala. Na hata kama ikikadiriwa kuwa wao ni watawala basi hakika makusudio ni wale wanaoitwa hivyo kwa kinaya, na ndio hali hiyo hiyo kwa waasi.”25

Kwa Al-Muqriziy makhalifa kumi na wawili ni wale wanne kisha Imam Hasan (a.s.), amesema: “Kwake yeye (a.s.) ndiko kulikomalizikia siku za makhalifa waongozaji.” Yeye hajamjumuisha yeyote miongoni mwa wana wa Umayya, kwani ametamka waziwazi kuwa baada yake ukhalifa uligeu- ka ufalme wenye kung’ang’aniwa.

Amesema: “Yaani kulikwa na nguvu na dhuluma!!” Pia hajamjumuisha yeyote miongoni mwa wana wa Abbas akitamka waziwazi kuwa ukhalifa wao “ulifarakisha nguvu ya Uislamu na jina la waarabu likatoweka ndani ya shajara, wakaingizwa waturuki ndani ya shajara hiyo, wakaimarika madaylum kisha waturuki, hatimaye wakawa na dola kubwa mno na tawala za ardhi zikagawika sehemu mbalimbali na kila eneo likawa na mtawala anawaendesha watu kwa dhuluma na kuwatawala kwa nguvu.”

Inaonekana waziwazi jinsi gani madhehebu ya Sunni inavyotapatapa kati- ka kutafsiri Hadithi hii na kuingia kwenye tope ambazo inashindikana kuji- nasua maadamu tu bado inang’ang’ania maana ya tafsiri ya ‘ufafanuzi wa hali ya mustakabali’.

As-Suyutiy amesema ndani ya kitabu Al-Hawi: “Mpaka leo bado hawa- japatikana kumi na wawili ambao umma wote umekongamana juu ya kila mmoja miongoni mwao.”26

Laiti tafsiri ya ‘ufafanuzi wa hali ya mustakabali’ yenyewe binafsi ingekuwa ni sahihi na inakubalika basi maswahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wangeiamini kabla ya mwingine yeyote na imani hiyo ingeonekana kupitia ndimi za makhalifa wenyewe, na wa kwanza wao angesema: Mimi ndiye wa kwanza kati ya makhalifa kumi na wawili, na wa pili na wa tatu mpaka wa kumi na wawili wote wangesema mfano wa maneno hayo, na dai kama hili lingekuwa ni fahari kwao na ushahidi tosha wenye kusaidia kuthibitisha uhalali wa kila mmoja miongoni mwao. Lakini historia haijasajili dai la namna hiyo kutoka kwa yeyote miongoni mwa majina hayo yaliyotajwa katika orodha ya makhalifa kumi na wawili wa bandia.

Hakika Hadithi inaonyesha kuwa kipindi cha uimamu wa maimamu kumi na wawili kitajumuisha umri mzima wa Uislamu mpaka mwisho wake kiasi kwamba baada yao ardhi haitokuwa na mtu yeyote. Sunni wame- pokea kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Dini hii itaendelea kusimama mpaka watimie kumi na wawili wote kutoka kwa makurayshi, wakitoweka basi ardhi haitokuwa na mtu.”27

Ardhi haikutoweka wakazi wake baada ya kifo cha Umar bin Abdul-Aziz, bali kuenea kwa elimu mbalimbali za dini kama vile elimu ya sharia, Hadithi na tafsiri kuliimarika ndani ya karne wawili za hijiriya, ya tatu na ya nne, mpaka elimu za dini zikafikia kilele cha ubora katika kuenea ikiwa ni baada ya kufariki hawa makhalifa kumi na wawili wa Sunni, wakati ili- takiwa ardhi isiwe na wakazi wake!

Pia wamepokea kutoka kwa Jabir bin Samra kuwa: “Umma huu utaende- lea kuimarika katika jambo lake, ukiwa na nguvu juu ya adui wake mpaka watimie makhalifa kumi na wawili miongoni mwao, wote ni kutoka kwa makurayshi, kisha ndipo itapatikana ‘maraji.’”2828

Ikiwa makusudio ya neno “maraji” ni moyo kuuma, msukosuko na utata basi inapasa kusema kuwa hakikutokea kitu kama hicho hata mpaka zama za Umar bin Abdul-Aziz. Lakini historia haijui fitina kubwa ambayo mau- mivu ya moyo yalizidi, msukosuko uliongezeka na utata kati ya haki na batili ulikuwa ila ni ile ya Muawiya na kitendo chake cha kutoka kwenda kumpiga Khalifa wa waisilamu.

Hii inaonyesha kuwa muradi wa neno “maraji” ni kitu kikubwa zaidi kuliko maumivu ya moyo, msukosuko na utata, na huenda muradi ikawa ni kitendo cha kuachwa dini yote, na hili halijatokea ila litatokea Kiyama kitakapokaribia, Kiyama ambacho kitatanguliwa na udhihiri wa Imam Mahdi na matukio mengine yatakayotokea baada ya kufariki kwake.

Kisha akinamaanisha nini kitendo cha kuwajumuisha wafalme kwenye orodha ya makhalifa?! Bila shaka Sunni wamepokea kutoka kwa Saad bin Abu Waqqas mmoja wa kumi waliobashiriwa, na mmoja wa wajumbe wa kamati aliyoiteua Umar, kuwa aliingia kwa Muawiya huku akiwa amekataa kumpa kiapo cha utii, akasema: “Amani iwe juu yako ewe mfalme.” Akamjibu: “Je, hakuna jingine lisilokuwa hilo? Ninyi ni waumini na mimi ni kiongozi wenu.” Akasema: “Ndiyo, iwapo tukikupa uongozi.” Katika tamko lingine: “Sisi ni waumini na hatujakupa uongozi.”

Aisha alimkanusha Muawiya juu ya dai lake la ukhalifa, kama ambavyo pia Ibnu Abbas alikanusha dai hilo, na hata Imam Hasan (a.s,) aliendelea kukanusha hata baada ya suluhu29, hivyo yeye ni miongoni mwa waovu kwa itifaki ya wote kwa mujibu wa Hadithi: “Ewe Ammar litakuuwa kundi ovu.” Sasa sijui vipi imesihi muovu aliyetoka kumpiga Khalifa halali kuwa Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu juu ya waumini!

Kinamaanisha nini kitendo cha kumjumuisha Yazid muovu kwenye orod- ha ya makhalifa?! Ambaye alikuwa akidhihirisha waziwazi ufasiki wake na uvunjaji wa heshima ya Mwenyezi Mungu, na kweli hili ni ajabu ya maajabu! Vipi inasihi kwa mwislamu amfanye kuwa Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) mtu ambaye anamwaga damu za watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), mtu ambaye jeshi lake linalivamia Jiji la Madina na kuwaua maelfu ya wakazi wake kiasi kwam- ba baada ya tukio hilo hakubaki hai sahaba yeyote yule aliyepigana vita vitukufu vya Badri!

Na ndio hali hiyo hiyo kwa wafalme toka mti uliolaniwa na Qur’an tuku- fu, bila shaka Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliwaona usingizini, na kama ujuavyo ndoto ya Mtume ni kweli, aliwaona wakichezea mimbari yake kama wachezavyo ngedere (tumbir). Hilo ni kwa mujibu wa itifaki ya wafasiri wengi wa Qur’an wa kisunni pindi wanapoifasiri Aya ya sitini ya Sura Al-Israi, wala hatuna haja ya kunukuu maneno yao.

Hivyo kwa uwazi kabisa yanadhihiri matokeo matatu:

1. Kufeli kwa tafsiri ya “ufafanuzi juu ya hali ya mustakabali” kwenye Hadithi ya ukhalifa wa maimamu kumi na wawili.

2. Mchango wa sababu ya kisiasa katika kuisababisha madhehebu ya Sunni ikiwawilie tafsiri hiyo.

3. Tafasiri ya kweli ya halali ya Hadithi imekomea kwenye tafsiri ya “ufafanuzi juu ya imani” ambayo inasema Hadithi iliyotajwa inaonyesha kuwekwa kwa maimamu kumi na wawili wa waisilamu, na hiyo ndiyo tafsiri iliyothibitishwa na dalili za kiakili na Aya nyingi za Qur’an ambazo zimefafanuliwa sana kwenye vitabu vya Shia Imamiya vya sasa na vya zamani, tazama hilo kwenye ulingo wa tafsiri, Hadithi, theiolojia na historia.

Inaonekana wazi kuwa historia haijataka kitu ila kuwabakisha maimamu kumi na wawili kutoka nyumba ya Mtume (a.s.) ili wawe mfano halisi pekee wa Hadithi iliyotajwa kiasi kwamba hawapingwi katika hilo hata katika kiwango cha madai. Wa kwanza wao ni kiongozi wa waumini (a.s.) na wa mwisho wao ni Imam Mahdi mwana wa Hasan Al-Askarii (a.s.), na hazihesabiki kwa wingi wake Hadithi tukufu zinazothibitisha hilo.

Hapa tutaashiria moja kati ya hizo, nayo ni ile aliyoitoa Al-Juwayniy As- Shafiy ndani ya kitabu Faraidu As-Samtwayni, kutoka kwa Ibnu Abbas kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa yeye alisema: “Mimi ni bwana wa manabii na Ali bin Abu Talib ni bwana wa mawasii, na bila shaka mawasii wangu baada yangu ni kumi na wawili, wa kwanza wao ni Ali bin Abu Talib na wa mwisho wao ni Mahdi.”30

Kuanzia hapa ndipo baadhi ya wahakiki wakaona kuwa, huenda ndani ya jibu la baba kuna opotoshaji. Imesemwa na vitabu vya Hadithi kuwa, pindi baadhi ya maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yalipokosa kusikika kwa Jabir bin Samara, na akawa amemuuliza baba yake kuhusu maneno yaliy- ofichikana kwake, baba yake alimjibu kuwa (s.a.w.w.) amesema: “Wote ni kutoka kwa makurayshi.”

Kwa sababu riwaya imetoa sababu iliyosababisha jibu lisisikike, ikasema: “Kisha jamaa wakainua sauti na kuongea.” Na “Watu wakapiga kelele.” Na “Akasema neno ambalo watu walinifanya nisilisikie.” Na “Watu wakainua sauti hivyo sikusikia alilosema.” Na “Watu wakatoa takbira na kupiga kelele.” Na “Watu wakaanza kusimama na kukaa.” Sababu zote hizi hazi- afikiani na ibara ambayo mpokezi hakuisikia, kwa sababu kuufanya ukhalifa uwe kwa makurayshi ni jambo linalowapendeza wala halipelekei fujo na kelele, na hivyo dhana inayonasibiana na hali hii iliyoelezwa ni ile ya kuwa uimamu umekabidhiwa kwa kundi maalumu na si makurayshi.

Hili ndilo alilolisema Al-Qunduz ndani ya kitabu chake Yanabiul- Mawaddah kwani amesema, ibara aliyoitamka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni “Wote ni kutoka kwa wana wa Hashim.”31

Baada ya kubainika kuwa upande mmoja tafsiri ya “ufafanuzi wa hali ya mustakabali” imefeli kwenye Hadithi ya uimamu wa maimamu kumi na wawili, na upande wa pili umethibiti ukweli wa tafsiri ya “ufafanuzi wa imani” na upande wa tatu limethibiti jina la Imam Mahdi ndani ya orodha ya mfululizo wa maimamu wa Ahlul-Bait na kuwa yeye ni Imam wa kumi na wawili ambaye kupitia kwake Mwenyezi Mungu ataitengeneza ardhi baada ya kuwa imejaa uharibifu, basi baada ya hapo haibaki shaka yoyote juuu ya kuthibiti wazo la imani ya uwepo wa Mahdi anayehimizwa na madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s.).

Kwa sababu uhusiano wa ndani kati ya suala la uimamu wa maimamu kumi na wawili na suala la Mahdi unapelekea yahamishiwe kwenye suala la Mahdi matokeo matatu yaliyopatikana ndani ya uchambuzi. Hivyo ikife- li tafsiri ya “ufafanuzi juu ya hali ya mustakabali” kwenye uimamu wa maimamu kumi na wawili maana yake ni kuwa tafsiri hii pia imefeli kwenye suala la Mahdi. Kama ambavyo ikithibiti sababu ya kisiasa katika kuzuka tafsiri hii kwenye uimamu wa maimamu kumi na wawili itamaan- isha imethibiti sababu hiyo kwenye suala la Mahdi.

Kwani madhehebu ya Sunni kama ilivyoifanya Hadithi ya ukhalifa wa makhalifa kumi na wawili kuwa ni habari juu ya hali ya mustakabali ili iwe ni sehemu ya usahihi wa nadharia ya uchaguzi wa sakifa, ukhalifa na uha- lali wake, basi ndivyo hivyo hivyo imeona dharura ya kuunga suala la
Mahdi kwenye tafsiri ya “ufafanuzi juu ya hali ya mustakabali”, wame- fanya hivyo ili kukimbia imani ya uimamu wa Ahlul-Bait (a.s.) na kutosi- hi utaratibu wa ukhalifa. Kama ambavyo kuthibiti ukweli wa tafsiri ya “ufafanuzi juu ya imani” kwenye Hadithi ya uimamu wa maimamu kumi na wawili kunamaanisha ni kuthibiti ukweli kuhusu wazo la imani ya uwepo wa Mahdi.

 • 1. Rejea Muujamu Ahadithil-Imam Al-Mahdiy: Juz 1 kwenye Hadithi za Mtukufu
  Mtume (s.a.w.w.).
 • 2. Musnad Imam Ahmad 1: 84, Hadithi ya 646. Ibnu Abu Shaybah 8: 687, kitabu
  cha 40, mlango wa 2, Hadithi ya 190. Ibnu Majah na Naimu bin Hammad ndani ya Al-Futunu kutoka kwa Ali (a.s.) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu ame- sema: “Mahdi ni kutoka kwetu Ahlul-Bait, Mwenyezi Mungu atamtoa ndani usiku mmoja.”. Rejea Sunan Ibnu Majah 2: 1367, Hadithi ya 4085. Al-Hawi Al-Fatawa cha As-Suyuti 2: 213 na 215, humo mna: “Ameitoa Ahmad na Ibnu Shaybah na Abu Daud kutoka kwa Ali kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hata kama ulimwengu utabakiwa na siku moja, ni lazima Mwenyezi Mungu atamleta mtu kutoka ndani ya kizazi changu, atakeyeujaza uadilifu kama utakavyokuwa umejaa dhulma.” Rejea Sahih Sunanul-Mustafa 2: 207. Rejea Muujamu Ahadithil- Mahdi 1: 147 na unaofuata, kwani amenukuu Hadithi nyingi zenye maana hii kutoka kwenye Sahih Sita na Masanid. Rejea Mawsuatul-Imam Al-Mahdi: Usanifu wa Mahdi Faqihi Imaniy, juzuu ya kwanza, humo mna nakala halisi zili- zonukuliwa kutoka ndani ya makumi ya vitabu vya kisuni na wasimulizi wao zik- ihusu Mahdi, sifa zake na yanayomhusu, na humo mna nakala halisi ya muhadhara wa Sheikh Al-Ibad kuhusu Hadithi na athari zinazomhusu Mahdi (a.s.).
 • 3. Al-Hawi Lil-Fatawa cha As-Suyutiy Jalalud-Dini 2: 214. Amesema: Abu Daud
  ametoa na Ibnu Majah na At-Tabaraniy na Al-Hakim kutoka kwa Ummu Salamah alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Mahdi ni kutoka ndani ya kizazi changu kutoka kizazi cha Fatima.”. Rejea Sahih Sunanul-
 • 4. Hadithi zinazosema kuwa Mahdi ni kutoka kizazi cha Husein (a.s.) kama ilivyo ndani ya vyanzo vifuatavyo kama ilivyonukuliwa ndani ya Muujamu Ahadithil- Mahdi, navyo ni: Al-Arbauna Haditha cha Abu Naim Al-Isfahaniy kama ilivyo ndani ya Uqad Ad-Durar cha Al-Muqadasiy As-Shafiiy. Na ameitoa At-Tabaraniy ndani ya kitabu Al-Awsat kama ilivyo ndani ya Al-Manaru Al-Munir cha Ibnu Al- Qayyim na ndani ya kitabu As-Siratu Al-Halbiyah 1: 193. Na ndani ya kitabu Al- Qawlu Al-Mukhtasar cha Ibnu Hajar Al-Haythamiy. Rejea Muntakhabul-Athar cha Shaikh Lutfullah As-Swafiy zile alizozinukuu kutoka kwenye vitabu vya Kishia. Rejea dalili za udhaifu wa riwaya isemayo kuwa yeye ni kutoka kizazi cha Imam Hasan, kitabu cha As-Sayyid Al-Amidiy Difau Anil-Kafiy 1: 296
 • 5. Rejea riwaya ambayo inaelezea kuwa yeye ni wa tisa kutoka kizazi cha Husein (a.s.) ndani ya kitabu Yanabiul-Mawaddah cha Al-Qunduziy Al-Hanafiy: 492 na ndani ya kitabu Maqtalul-Imam Al-Husein cha Al-Khawarazamiy 1: 196. Faraidu As-Samtwayn cha Al-Jawniy As-Shafiiy 2: 310 – 315, Hadithi ya 561 – 569. Rejea Muntakhabul-Athar cha Allamah Shaikh As-Swafiy kwani yeye kazitoa kwa njia za madhehebu zote mbili.
 • 6. Hadithi: “Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili wote ni kutoka kwa Makurayshi.” Au “ Dini hii itaendelea kusimama mpaka itawaliwe na kumi na wawili wote kutoka kwa Makurayshi.”. Hadithi hii ni mutawatiri, imepokewa ndani ya Sahihi sita na Masanid kwa njia mbalimbali japokuwa zinatofautiana kidogo katika matamshi. Ndio wametofautiana katika tafsiri na hivyo waka- hangaika. Rejea Sahih Bukhari 9: 101, kitabu cha hukumu, mlango wa kuacha Khalifa. Sahih Muslim 6: 4, kitabu cha alama, mlango wa kuacha Khalifa. Musnad Ahmad 5: 90, 93, 97.
 • 7. Rejea kitabu Al-Ghaybatul-Kubra cha As-Sayyid Muhammad As-Sadri: 272 na kuendelea.
 • 8. Rejea At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 3: 40, amesema: “Imepokewa na mashekhe
  wawili na Tirmidhi.” Kuhusu uhakiki wa Hadithi, njia zake za upokezi na senten- si zake rejea kitabu Al-Imam Al-Mahdi cha Ali Muhammad Ali Dakhil.
 • 9. Sahih Bukhar: Juzuu ya tatu 9: 101, kitabu cha hukumu, mlango wa ukhalifa, chapa ya Daru ihyaut-Turathil-Arabiy – Beirut.
 • 10. Rejea At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 3: 40, ameongezea kwenye Hadithi kwa kusema: “Imepokewa na mashekhe wawili na Tirmidhi.” Pembezoni akasema: “Ameipokea Abu Dawdi ndani ya kitabu cha Mahdi kwa tamko: “Dini hii itaen- delea kusimama mpaka mtawaliwe na Makhalifa kumi na wawili….”” Na rejea Sunan Abi Dawdi 2: 207.
 • 11. Rejea At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 3: 40, ameongezea kwenye Hadithi kwa kusema: “Imepokewa na mashekhe wawili na Tirmidhi.” Pembezoni akasema: “Ameipokea Abu Dawdi ndani ya kitabu cha Mahdi kwa tamko: “Dini hii itaen- delea kusimama mpaka mtawaliwe na Makhalifa kumi na wawili….”” Na rejea Sunan Abi Dawdi 2: 207.
 • 12. Rejea At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 3: 40, ameongezea kwenye Hadithi kwa kusema: “Imepokewa na mashekhe wawili na Tirmidhi.” Pembezoni akasema: “Ameipokea Abu Dawdi ndani ya kitabu cha Mahdi kwa tamko: “Dini hii itaen- delea kusimama mpaka mtawaliwe na Makhalifa kumi na wawili….”” Na rejea Sunan Abi Dawdi 2: 207.
 • 13. Musnad Imam Ahmad 6: 99, Hadithi ya 20359.
 • 14. Al-Mustadrak Alas-Sahihayni 3: 618.
 • 15. Anaashiria kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hatamki kwa matamanio.* Ila ni wahyi unaofunuliwa.” Sura Najmu: 3 – 4.
 • 16. Hadithi hii tayari tumeshaitoa huko nyuma.
 • 17. Bahthu hawlal-Mahdi cha As-Sayyid As-Shahid As-Sadri: 105 – 107, uhaki- ki wa Dr. Abdul-Jabar Shirara.
 • 18. Baadhi ya Wanachuoni baada ya kukongamana juu ya usahihi wake wame lazimika kuioanisha na mifano ambayo haiwezekani kuikubali, bali baadhi yake kamwe akili haiwezi kuiridhia, kama Yazid bin Muawiya fasiki wa waziwazi ambaye alitoka ndani ya dini na kukufuru, au mwingine mfano wake.
 • 19. Sahih Muslim 6, kitabu cha alama, mlango wa watu wawafuate makurayshi.
 • 20. Rejea Sahih Bukhar 4: 164, kitabu cha hukumu, mlango wa ukhalifa. Musnad Ahmad 6: 94, Hadithi ya 325, 20366, 20367, 20416, 20443, 20503 na 20534. Sunan Abi Dawd 4:106 / 4279 – 4280. Al-Muujam Al-Kabir cha At-Tabaran 2:238/1996. Sunan At-Tirmidhi 4: 501. Mustadrakul-Hakim 3:618. Hilyatul-Awliyai cha Abu Naim 4:333. Fat’hul-Bari 13:211. Sahih Muslim sherehe ya An- Nawawi 12:201. Al-Bidayah Wan-Nihayah cha Ibnu Kathir 1:153. Tafsir Ibnu Kathir 2:24 kwenye tafsiri ya Aya ya 12 ya Sura Maida. Kitabus-Suluki fiduwalil-Muluki cha Al-Maqrizi 1: 13 – 15, sehemu ya kwanza. Sherehe ya Sunan Abi Dawd 11: 363, iliyofanywa na Al-Hafidh Ibnu Qayyim Al-Jawziyah, sherehe ya Hadithi ya 4259. Sherehe ya Al-Aqidah At-Tawahiyah 2:736. Al-Hawi Lil-Fatawa cha As-Suyutiy 2:85. Awnul-Maabud Sharhu Sunan Abi Dawd cha Al-Adhim Abad 11:362, sherehe ya Hadithi ya 4259. Mishkatul-Maswabih cha At-Tabrizi 3:327, 5983. As-Silsilatu As-Sahiha cha Al-Abaniy, Hadithi namba 376. Kanzul-Ummal 12:32, 33848, na 12:33/33858, na 12:34/33861. Hadithi hii pia ime- tolewa na wasimulizi wa kishia akiwemo As-Saduq ndani ya kitabu chake Kamalud-Din 1:272, na Al-Khisal 2:469 na 475, ndani ya kitabu chake Ihqaqul- Haqi 13: 1 – 50 amefatilia njia za upokezi wake na maswahaba walioipokea.
 • 21. Tafsir Ibnu Kathir 2: 34, tafsiri ya Aya 12 ya Sura Maida
 • 22. Sherehe ya Al-Aqidah At-Tahawiyah cha Kadhi Ad-Damashqiy 2: 736.
 • 23. Awnul-Maabud katika kusherehesha Sunan Abi Dawd 11: 246, sherehe yaHadithi ya 427, kitabu cha Mahdi, chapa ya Darul-Kutubi Al-Ilmiyah.
 • 24. Awnul-Maabud katika kusherehesha Sunan Abi Dawd 11: 245.
 • 25. Awnul-Maabud katika kusherehesha Sunan Abi Dawd 11: 244.
 • 26. Al-Hawi Lil-Fatawa 2: 85.
 • 27. Kanzul-Ummal 12: 34, Hadithi ya 33861, Ibnu An-Najar ameitoa kutoka kwa Anas.
 • 28. Kanzul-Ummal 12: 32, Hadithi ya 33848.
 • 29. Rejea kitabu Al-Ghadir cha Al-Allamah Al-Amin 1: 26 – 27, amelitaja hilo akiwa amelitoa kwenye vitabu vya masunni.
 • 30. Faraidu As-Samtwayni 2:313, Hadithi ya 564.
 • 31. Yanabiul-Mawaddah 3: 104, mlango wa 77.