read

Sura Ya Pili

Sifa mahususi kuhusu uwelewa wa Mahdi kwa Ahlul-Bait wenyewe (a.s.).

Baada ya kutimia uthibitisho wa kiimani juu ya uwelewa wa Mahdi kwa madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s.) sasa tunaingia hatua mpya ya uchunguzi, nayo ni hatua ya uchunguzi juu ya sifa muhtasi zinazohusu uwelewa huu ili tuweze kuthibitisha kuwa zenyewe ni sifa halisi kivitendo na zina uwepo wa nje kihistoria na kisharia, na kuwa kuziamini sifa hizo hakupelekei kutia doa imani wala kutengana na historia. Na sifa hizo ni kama zifuata- zo:

Sifa ya kwanza: Kuzaliwa kwa Imam Mahdi kulitimia katika mazingira ya siri yaliyokuwa ni lazima kutimia.

Ukithibiti uwelewa wa wazo la Mahdi kwa mujibu wa Ahlul-Bait basi inabainika kuwa miongoni mwa sifa barizi mno za lazima za uwelewa huu ni kuzali kwa Imam wa kumi na wawili kuwe kumeambatana na siri na ufi- cho ili baada ya hapo iwezekane kwake ghaibu na kujificha mbali na macho akiwa sehemu yenye amani atakayoichagua Mwenyezi Mungu kwa ajili yake mpaka pale atakapomruhusu kudhihiri.

Hiyo ni kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye nyota ya mwisho katika mbingu ya uimamu na Imam ambaye waisilamu hawana Imam mwingine baada yake. Hivyo maana hii inalazimu kupatikana maisha ya uficho, umri mrefu na mazazi ya siri ili nafasi ya uimamu iendelee kutumikiwa muda wote na Imam miongoni ma maimamu kumi na wawili (a.s.) aliye hai aliye ghaibu.

Basi haifai kabisa kusema kuwa: Kwa nini kuzaliwa kwa Imam na kuwe- po kwake baada ya baba yake hayakuwa ni mambo ya wazi yanayoshuhudiwa na kuguswa na kila anayetaka kusadikisha? Kwa sababu laiti ingelikuwa hivyo basi ghaibu na kujificha mbali na macho visingekuwa rahisi kwake kwa sababu yeye ndiye Imam wa kumi na waw- ili, na hatimaye maimamu wangekuwa wengi kuliko idadi hii, na suala hili linapingana na dalili zilizotoka kwa Mtume zilizotajwa mwanzo. Hivyo mazazi ya siri ni miongoni mwa mambo ya lazima yanayotokana na hali halisi ya dalili hizo.

Suala hili linabainisha kuwa kuthibitisha uwepo wa nje wa kadhia ya kuza- liwa Imam Mahdi, kuwepo kwake na maisha yake hakuwezi kukomea tu kwenye uchunguzi wa kihistoria madamu tu tunaamini tangu mwanzo kuwa kadhia hiyo imeambatana na usiri na ufichaji wa kiwango cha juu sana, bali wenyewe ni uthibitisho wa kiakida ndani ya historia ambao ndani yake akida ina nafasi ya msingi, wakati historia yenyewe ina nafasi ya kukamilisha tu.

Kwa sababu sisi tuna yakini tangu mwanzo kuwa wapo wakanushaji wa kadhia hiyo na wenye shaka nayo maadamu tu kadhia ni ya siri iliyofich- wa, na wenye kuitambua ni watu wachache kiasi kwamba inawapa mwanya wengine kuikanusha na kuitilia shaka maadamu tu wako mbali na hali halisi iliyo ya siri iliyofichwa, hali hiyo ni hata kama watakuwa ni ukoo wa karibu na Imam na wafuasi wa dhati, kiasi kwamba lau mtu atawahoji kuhusu kuzaliwa kwa Imam Mahdi, kuwepo kwake na maisha yake wangekanusha, na wao wangewanukulia watu kuwa hawajamwona na wala hawajasikia habari za kuzaliwa na kuwepo kwake.

Hivyo sisi hatuzungumzii suala la kimaada lenye kutambulika vipengele vyake vyote kwa njia ya milango ya fahamu, linalo tutaka tufuate nukuu kamili za historia ili katika uthibitisho wake na ukanushaji wake tuwa- tegemee wanahistoria na wapokezi, hapana si hivyo, bali sisi kimsingi tunazungumzia kadhia ya ghaibu, isipokuwa tu ughaibu huo si ule usio na mipaka, bali wenyewe ni ule wenye miale yenye kutambulika kwa kupitia milango ya fahamu unaofahamika na watu maalumu waliyoteuliwa, hivyo wao wameshuhudia mazazi yake na kuyathibitisha na wameshuhudia ghaibu ndogo na wameithibitisha na wakashuhudia ghaibu kubwa kisha wakaithibitisha. Na kwa ajili hii ndio maana tukasema kuwa uwelewa wa wazo la uwepo wa Mahdi kwa mujibu wa madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s.) ni uwelewa wa kiitikadi.

Hii ina maana kuwa kukanusha kwa wakanushaji katika kadhia ya Imam Mahdi hakuwi hoja ya kihistoria ya kimantiki inayoweza kuthibitisha kutokuwepo kwake (a.s.) maadamu tu tumeshaamini tangu mwanzo kuwa kadhia hii ni kadhia ya siri iliyofichwa. Dharura ya uchunguzi wa historia ni kuthibitisha uwepo wa yule aliyemwona Mahdi (a.s.) na akasikia habari za kuwepo kwake na akaziamini, hilo ni bila kujali ukanushaji wa wakanushaji, ukanushaji ambao ni suala la kawaida kupatikana kwenye kadhia ya siri iliyofichwa.

Basi kuanzia hapa tutazama ndani ya uchambuzi wa aina wawili: Kwanza uchambuzi juu ya ushahidi unaothibitisha kuzaliwa kwa Imam na kuende- lea kwake kuwepo. Uchambuzi mwingine ni kuzijadili dalili za wenye kumkanusha (a.s.).

Vielelezo vya kihistoria vinavyothibitisha uwepo wa Imam Mahdi (a.s.)

Upande huu ni mpana mno umejaa namba nyingi sana za vielelezo vya kihistoria, nasi tunavihariri katika nukta mbalimbali:

1. Uthibitisho wa Imam Hasan Al-Askarii (a.s.) kuhusu kuzaliwa mwanae

Imam Mahdi (a.s.):

Katika hilo kuna Hadithi nyingi zilizothibitishwa na Shia na wapokezi wake, nasi tunanukuu baadhi tu:

Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Muhammad bin Yahya kutoka kwa Ahmad bin Is’haqa kutoka kwa Abu Hashim Al-Jafariy, amesema: “Nilimwambia Abu Muhammad (a.s.): Heshima yako inanizuia nisiku- ulize, je unaniruhusu nikuulize? Akasema: “Uliza.” nikasema: Ewe bwana wangu! Je, una mtoto wa kiume? Akasema: “Ndiyo.”1

Ndani ya Hadithi hii kuna njia ya upokezi na madhumuni vinavyoji- tosheleza, kwani ni hivi hapa vitabu vya wapokezi vinathibitisha heshima ya Muhammad bin Yahya Abu Jafar At-Tar Al-Qummiy ambaye kaburi lake mpaka leo bado ni maarufu na mashuhuri watu wakilizuru. Pia vinathibitisha hadhi ya juu ya Ahmad bin Is’haqa bin Abdullah bin Saad bin Malik bin Al-Ahwas Al-Ash’ari Abu Ali Al-Qummiy kwa Imam Hasan Al-Askarii (a.s.). Pia vinathibitisha nafasi ya Daud bin Al-Qasim Ibnu Is’haqa bin Abdullah bin Jafar bin Abu Talib Abu Hashim Al-Jafariy…. Kisha tazama uchache wa mtiririko wa wapokezi katika njia ya upokezi wa Hadithi hii, Hadithi ambayo inaonyesha hali ya wahusika kwa ule ufupi wa njia ya upokezi ambao unaheshimika kama ushahidi unaoipa nguvu Hadithi hii.

2. Uthibitisho wa Al-Qabilah

Yeye ni dada wa Imam na shangazi wa Imam na binti wa Imam, anatokana na ukoo wa Ali uliotoharika. Hakimah binti Muhammad Al-Jawwad ni dada wa Imam Al-Had na shangazi wa Imam Al-Askarii, yeye amethibitisha waziwazi kuwa alishuhudia kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.) ndani ya usiku aliyozaliwa2, na yeye ndiye aliyesimamia uzazi wa Nargis mama wa Imam Mahdi (a.s.) kwa kupata idhini kutoka kwa baba yake Hasan Al-Askarii (a.s.)3.

3. Uthibitisho wa watu mbalimbali waliomwona Imam (a.s.):

Hapa tuna orodha ndefu ya majina ya watu waliomwona Imam Mahdi na wakakutana naye na wakathibitisha kuwa wamemwona, orodha hiyo ime- sajiliwa na historia na baadhi ya waandishi wameisajili ndani ya vitabu vyao muhtasi, mfano kitabu “Tabsiratul-Waliy Fiman’raa Al-Qaimu Al- Mahdiy” cha Sayyid Hashim Al-Bahrani, humo amewataja watu sabini na tisa waliothibitisha kuwa wamemwona Imam (a.s.) utotoni mwake au kipindi cha ghaibu ndogo, na ametaja majina ya rejea alizozitegemea kati- ka hilo.

Sheikh Abutalibi At-Tajlili At-Tabrizi Zahau yeye amehesabu watu mia tatu na nne waliomwona Imam (a.s.) na wakathibitisha kumwona4.

Sheikh As-Suduq aliyefariki mwaka 381 A.H. na aliyeishi zama za ghaibu ndogo ya Imam Mahdi (a.s.) yeye amehesabu majina ya watu sitini na nne waliothibitisha kuwa wamemwona Imam (a.s.), na wengi miongoni mwao walikuwa mawakala wake5, na wenyewe ni kutoka miji mbalimbali.

Miongoni mwa mawakala wake ni: Kwa watu wa Adhribayjani ni Al- Qasim bin Al-Alau. Kwa watu wa Ahwaz ni Muhammad bin Ibrahim bin Mahziyar. Kwa watu wa Baghdad ni Hajiz Al-Balaliy, Uthman bin Said Al-Amriy, Muhammad bin Uthman bin Said Al-Amriy na Al-Atar. Kwa watu wa Kufa ni Al-Asimiy. Kwa watu wa Qum ni Ahmad bin Is’haqa. Kwa watu wa Nisabur ni Muhammad bin Shadhan. Kwa watu wa Hamdan ni Al-Basamiy, Muhammad bin Abu Abdullah Al-Kufiy Al-Asadiy na Muhammad bin Salih.

Ama wengine waliomwona wasokuwa mawakala wake miongoni mwao ni: Kutoka Isfihan ni Ibnu Bashadhalah. Kutoka Ahwaz ni Al-Huswayniy. Kutoka Baghdad ni Ahmad bin Hasan, Is’haqa mwandishi wa ukoo wa Nawbakhat, Abu Abdullah Al-Khaybariy, Abu Abdullah bin Farukh, Abu Abdullah bin Al-Kindiy, Abul Qasim bin Abu Halis, Abul Qasim bin Dabis, Masrur At-Tabakh mtumwa wa Abu Hasan (a.s.), An-Nayliy na Harun Al-Fazariy.

Kutoka Daynawar ni Ahmad mtoto wa kaka yake na Hasan bin Harun na ami wa Hasan bin Harun. Kutoka Ray ni Abu Jafar Ar-Rafau, Ali bin Muhammad, Al-Qasim bin Musa, mtoto wa Al-Qasim bin Musa, Abu Muhammad bin Harun na Muhammad bin Muhammad Al-Kulayniy.

Kutoka Kazwin ni Ali bin Ahmad na Murdasi. Kutoka Qum ni Hasani bin An-Nadhru, Husayn bin Yaaqub, Ali bin Muhammad bin Is’haq, Muhammad bin Is’haq na Muhammad bin Muhammad. Kutoka Misri ni Abu Rajai. Kutoka Nasibayn ni Abu Muhammad bin Al-Wajnau An- Naswibiy. Kutoka Hamdan ni Jafar bin Hamdan, Muhammad bin Kashmirda na Muhammad bin Harun. Kutoka Yemen ni Ibnu Al-Aajamiy, Al-Jafariy, Hasani bin Al-Fadhlu Ibnu Yazid, baba yake Al-Fadhlu bin Yazid na Shamshati. Pia amewataja waliomwona kutoka Shahruzur, Swaymara, Faris, Qabis na Murwu.

Je, akili inakubali kuwa hawa wote walikubaliana na kuafikiana juu ya kuzua uongo? Ilihali miongoni mwao wapo wasimulizi waaminifu ambao vitabu vya wapokezi wa Hadithi vimethibitisha waziwazi uaminifu wao?

4. Utawala wa koo wa Abbas ulicheza mchezo mchafu juu ya tukio hili

Bila shaka utawala wa ukoo wa Abbas baada ya kufariki Imam Hasan Al- Askarii uliamiliana na familia yake muamala unaoonyesha hofu yao dhidi ya mtoto hatari aliyefichwa dhidi yao, hivyo wakaanza kumtafuta kwa kila nguvu na njia waliyo nayo, kiasi kwamba Al-Muutamid Al-Abbasiy aliye- fariki mwaka 279 A.H alimwamuru mkuu wake wa polisi kuipekua nyum- ba ya Imam Hasan Al-Askarii msako mkali sana huku wakimsaka Imam Mahdi. Akaamuru majirani wa Abu Muhammad wawekwe rumande na familia yake ikamatwe, alifanya hivyo huku akisaidiwa na Jafar mwongo, kwa ajili hiyo watu wa karibu wa Abu Muhammad wakapatwa na kila tati- zo kuanzia kukamatwa, kuwekwa mahabusu, kutishwa, kuvunjiwa heshi- ma na kudhalilishwa.6

Haya yote yalifanywa Imam akiwa na umri wa miaka mitano, wala Al- Muutamid hakujali umri baada tu ya kujua kuwa kijana huyu ndiye Imam Mahdi atakayeangusha jukwaa la muovu kutokana na habari zilizoenea na kutapakaa kuwa Imam wa kumi na wawili wa Ahlul-Bait ataijaza dunia usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhuluma na ujeuri, hivyo msimamo wake dhidi ya Mahdi ni sawa na msimamo wa Firaun dhidi ya Musa (a.s.) ambaye mama yake alimweka ndani ya mto akiwa mchanga kwa ajili ya kumuogopa Firaun.

Si Al-Muutamid pekee ndiye aliyekuwa amejua ukweli huu bali hata Al- Muutazu na Al-Muhtad waliujua kabla yake, kwa ajili hii Imam Hasan Al- Askari alikuwa katika tahadhari sana ili habari za kuzaliwa Imam Mahdi zisitapakae isipokuwa kati ya watu wateule kutoka kwa mashia wake na wafuasi wake.

Harakati za utawala zimefichua kuwa wenyewe na watu wengine wote walitambua vizuri kuwa Hadithi ya Jabir bin Samra haiwahusu wao wala yeyote aliyetangulia miongoni mwa ukoo wa Umaiya, bali mfano halisi pekee wa Hadithi hiyo ni watu wa nyumba ya utume ambao ni shukio na teremkio la ufunuo.

Kama si hivyo basi ni hatari gani kutoka kwa mtoto asiyevuka umri wa miaka mitano inatishia utawala wao? Kama si kule kuamini kuwa mtoto huyu ndiye yule Mahdi aliyezungumziwa ndani ya Hadithi mbalimbali mutawatiri!

Mmoja wa watafiti anasema: “Ingekuwa kweli hajazaliwa basi kuna maana gani kuwaweka majirani rumande na kutuma vikosi kwenda kuwapekua wanawake wajawazito na kuwapeleleza muda mrefu usiokubalika, kwani mwingine alikuwa chini ya upelelezi muda wa miaka miwili, yalifanywa yote haya huku maswahaba wa Imam Askari wakiteswa na kutumiwa majasusi ili kupeleleza habari za Mahdi (a.s.) na mara kwa mara nyumba zikivamiwa?

Kisha kwa nini utawala haukuridhika na dai la Jafar kuwa kaka yake (a.s.) amefariki bila kuacha mtoto? Hivi haikuwa inatosha kumpa haki yake ya mirathi na mambo yote yaishe kuliko harakati hizi za kipumbavu ambazo zinaonyesha jinsi ulivyokuwa na woga na hofu dhidi ya mwana wa Hasan (a.l.f.s.)?!!

Ndiyo, inaweza kusemwa kuwa nia ya utawala ilikuwa ni kumpa kila mwenye haki haki yake na hiyo ndiyo sababu iliyoupelekea kufuatilia ili kujua uwepo wa mtoto wa kiume ili Jafar asimiliki mirathi peke yake kwa ushahidi wake tu.

Tunasema: Haikufaa kwa utawala wa zama hizo kufatilia jambo hili kwa vitendo hivi vyenye kutia shaka, bali ilipasa Khalifa wa ukoo wa Abbas aliache dai hilo la Jafar mwongo mikononi mwa makadhi, na hasa ukizinga- tia kuwa suala lenyewe ni mirathi, suala ambalo hutokea kila siku mara nyingi, na hapo ingekuwa ni jukumu la kadhi muhusika kufungua mlango wa kuletwa shahidi wa kuthibitisha, kwa mfano angeitwa shangazi yake na Imam Hasan Askari (a.s.) na mama yake na watu wa ukoo wa Hashimu walio karibu na Hasan Askari na kisha asikilize kauli zao achunguze ushahidi wao na hatimaye amaleze kila kitu.

Lakini suala hili kufika kwa mtu wa juu kiutawala na kwa haraka ya namna hii hata kabla Imam Hasan Al-Askari hajazikwa huku suala likitoka kwenye uwezo wa Mahakama ilihali ndiyo yenye jukumu hilo, na kisha utawala unalikabili kwa nguvu kama tuliyoifafanua mwanzo, hayo yote yanathibitisha kwa yakini kuwa utawala ulikuwa ukiamini kwa yakini kabisa kuwa Mahdi tuliyeahidiwa ndiye mzunguko wa mwisho wa cheni toharifu ambayo haiwezi kukatika kwa kufariki Imam wa kumi na moja, hasa baada ya kauli ya (s.a.w.w.) “Hivyo viwili – Kitabu na Kizazi – hav- itoachana mpaka vitakaponifikia kwenye Hodhi.” kuenea kwa watu wote.

Kwani kutokuzaliwa Mahdi au kutoendelea kuwa hai maana yake ni kutoweka kwa kizazi, na hii ni kauli isiyosemwa na yeyote yule anayejiita kiongozi wa waumini miongoni mwa wana wa Abbas, kwa sababu kauli hiyo ni kumkadhibisha Mtukufu Mtume wetu (s.a.w.w.) bali haisemwi na mwisilamu yeyote ila yule tu asiyejali ukadhibishaji huu au mwenye kuji- danganya kuwa anaawili Hadithi na kuyapeleka malengo ya Hadithi kwenye kitu ambacho hakijaletewa hoja yoyote ya wazi.”7

5. Wanachuoni wa Sunni wamekiri kuwa Imam Mahdi (a.s.) ameshaz- aliwa.

Sayyid Thamir Al-Amidiy amezungumzia suala hili akasema: “Kauli za kukiri za Wanachuoni wa sharia, wafasiri, wanahistoria, watafiti, wafasihi na waandishi wa kisunni zimefikia zaidi ya mia moja, wote wakikiri wazi- wazi kuwa Imam Mahdi (a.s.) ameshazaliwa. Zaidi ya nusu yao wametam- ka waziwazi kuwa Imam Muhammad bin Hasan Al-Mahdi (a.l.f.s.) ndiye Imam tuliyeahidiwa kuwa atadhihiri mwishoni mwa zama.

Kauli hizi za kukiri zimepangwa kulingana na vifo vya wenye nazo, hivyo tumezikuta zimeungana kizama kiasi kwamba haishindikani mwenye tamko la sasa kuwepo zama za mwenye tamko lililopita, hivyo ni kuanzia zama za ghaibu ndogo mpaka leo hii, ishaallah tutataja kauli za baadhi yao ambazo tumezipata ndani ya vitabu vyao pindi zamu yao itakapofika, na kwa wengine tutaishia kutaja majina yao tu bila kugusia kauli zao hiyo ni kutokana na kushindikana kuzinukuu katika sura hii.

Kauli zao zimefikia ishirini na tisa huku ya mmoja kati yao ikiwemo ndani ya kitabu “Ilzamun-Naswibu” kwenye kurasa zaidi ya mia moja.8 Je hali ingekuwaje laiti angesajili kauli zao wote? Zaidi ya hapo ni kuwa tutakayo itaja kwenye matamshi bila kuonyesha rejea yake kwenye pambizo ni dalili kuwa tumeichukua kutoka kwenye vitabu vya Shia Imamiya ambavyo vimetangulia kuzungumzia suala hili, na tutakazania kusajili namba ya juzuu, namba ya kurasa, sehemu na mwaka wa chapa.

Kitabu kikubwa mno katika mlango huu ni kitabu “Al-Mahdiyyu Al- Muntadhar Finahjil-Balagha” cha Sheikh Mahdiyyu Faqihi Iymaniy, ambaye humo ametaja wapokezi mia wawili na wawili miongoni mwa wapokezi wa kisuni ambao wamekiri hilo9 huku akiishia kutaja majina yao na vitabu vyao kwa kuainisha juzuu zake pamoja na kurasa zake bila kugusia kauli zao.

Nyakati nyingine alilazimika kuainisha kwa umakini kiunganishi kati yake na wao, na yaliweza kumpita karibuni majina thelathini. Sana tumemtege- mea yeye na wala hatukurudia tena ili kutafuta chochote kilichompita kwani tayari kuna mwingine asiyekuwa mimi alisharudia na kukusanya kile kilichompita10, akarudia kwa mzunguko katika dalili hii huku akiishia kukusanya na kupangilia kulingana na karne.”11

Kisha akataja majina mia moja ishirini na nane ya waandishi miongoni mwa waandishi wa kisunni ambao ndani ya baadhi ya vitabu vyao wamem- taja Imam Mahdi kwa kichwa cha habari: Imam wa kumi na wawili mion- goni mwa maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.). Miongoni mwa waandishi hao wamo walioishi zama za kuzaliwa kwake na zama za ghaibu ndogo, ushahidi wa hawa una hadhi maarufu ya kihistoria.

Miongoni mwa hao ni:

1. Abubakri Ar-Riwayaniy, Muhammad bin Harun aliyefariki mwaka 307
A.H ndani ya kitabu chake “Al-Musnad”.

2. Ahmad bin Ibrahim bin Ali Al-Kindiy, yeye ni kati ya wanafunzi wa
Ibnu Jarir At-Tabari aliyefariki mwaka 310 A.H.

3. Muhammad bin Ahmad bin Abu Thalji, Abubakri Al-Baghdadiy aliye- fariki mwaka 322 A.H. ndani ya kitabu “Mawalidul-Aimah”, hiki kimechapwa ndani ya kitabu “Al-Fusulul-Asharat Fil-Ghaybah” cha Sheikh Al-Mufid, pamoja na kitabu “Nawadiru Ar-Rawandiy kili- chochapwa Najaf tukufu mwaka 1370 A.H. Na miongoni mwa Wanachuoni wakubwa waliokuwa karibu na zama za kuzaliwa kwake ni Al-Khuwarazimiy aliyefariki mwaka 387 A.H. ndani ya kitabu chake “Mafatihul-Ulumi: 32 na 33” chapa ya Lidan mwaka 1895 A.D.

Hebu tujadiliane na wakanushaji

Kutokana na maelezo yaliyotangulia imebainika kuwa suala la Mahdi ni suala la kiitikadi kabla halijakuwa la kihistoria, na dalili ya kulithibitisha ni ya kiitikadi kabla haijakuwa ya kihistoria. Pia imebainika kuwa baadhi ya dalili za kihistoria zimelithibitisha na pia imebainika kuwa kadhia ya siri isiyoonekana kama ile ya Imam Mahdi kwa kawaida hulazimu kupatikana wakanushaji wa kadhia kama hiyo.

Hakika yule anayejificha mbali na macho ya watu kwa ajili ya kutimiza lengo lolote miongoni mwa malengo yake basi kwa kitendo hicho huwa amekusudia asionwe na mtu yeyote kiasi kwamba kama watu wataulizwa kuhusu yeye watasema: “Hatujamwona” hata kama walioulizwa ni watu wa karibu mno na yeye. Na tumesema kuwa ukanushaji wa watu kama hawa katika kadhia ya siri iliyofichikana hausihi kuwa dalili ya kutokuwe- po kwa kadhia hiyo.

Hiki ndio kitofautishi cha msingi walichoteleza wale wenye kukanusha kuzaliwa na kuwepo kwa Imam Mahdi (a.s.), kwani wao wamekuwa wak- itafuta ushahidi wa namna hii ndani ya historia na pale wanapopata cho- chote mfano wa hicho basi hukifanya dalili ya kutokuzaliwa na kutokuwe- po Imam Mahdi (a.s.), hivyo wao hushikilia mambo kama vile, kitendo cha Shia kutofautiana juu ya muda wa kuzaliwa na juu ya jina la Imam na ushahidi wa Jafar mwongo ami yake na Imam Mahdi aliyedai kuwa kaka yake amefariki bila kuacha mtoto.

Na mjadala wetu wa msingi na hawa ni kuwa, mfumo wa historia unaweza kutoa uamuzi kwenye masuala ya kimaada ambayo vipengele vyake vyote viko chini ya mtazamo wa wapokezi na wanahistoria tu, mfano vita vya Siffin, vita vya Karbala na vinginevyo, lakini wenyewe hauwezi kuamua kwenye masuala yenye msingi wa ghaibu na itikadi yale yenye miale ya kimaada kwa wateule tu kiasi kwamba laiti watu wa kawaida wakiulizwa kuhusu suala hilo watalikanusha.

Basi inakuwaje mnafanya ukanushaji wa watu wa kawaida kuwa ni dalili ya kutokuwepo kadhia ambayo tangu mwanzo inaaminiwa kuwa si kadhia inayokubali kushuhudiwa kwa milango ya fahamu isipokuwa kwa wateule tu?

Ni wajibu kwa mtu anayetaka kujadili suala la Mahdi aanzie mwanzo wake ambao ni itikadi na wala asianzie mwisho wake ambao ni historia, kwa sababu kadhia ya siri iliyofichwa kwa lengo maalumu dhidi ya macho ya watu wa karibu haikosi tofauti kama zile za muda wa kuzaliwa Imam na tofauti juu ya jina la mama wa Imam, na pia ushahidi kama wa Jafar mwongo haudhuru kadhia hiyo.

Kwa sababu jibu la kawaida katika hali kama hii ni isemwe: Hakika tofau- ti juu ya mwaka wa kuzaliwa na jina la mama wa Imam ilikuwa ni hali ya kawaida inayotokana na juhudi za Imam Hasan Al-Askari katika kuficha vipengele vya kadhia, ufichaji kamili kabisa dhidi ya macho ya watu wa karibu, akiwa anazuia habari zisiufikie utawala wa ukoo wa Abbas.

Hivyo hata ushahidi wa Jafar mwongo kuwa kaka yake alikufa bila ya kuacha mtoto ulikuwa ni wa namna hii, kiasi kwamba Imam Hasan Al- Askari alitaka kuficha mazazi yake hata kwa kaka yake na bila kudhi- hirisha hilo mbele yake. Hata kama Imam angekuwa hana mtoto baada yake basi utaratibu huu wa Imam Hasan Al-Askari mbele ya kaka yake ungekuwa ni wa kimantiki hata kama kaka yake asingekuwa mwongo ambaye ufasiki wake umethibitishwa, sembuse katika hali hii ambayo Jafar mwongo ufasiki wake umethibitishwa?12

Sifa ya pili: Uimamu wa udogoni

Miongoni mwa sifa za lazima zinazoambatana na uwelewa wa wazo la Mahdi kwa mujibu wa upande wa Ahlul-Bait ni kuamini uimamu wa uto- toni wa Imam Mahdi (a.s.), sifa hii kuna kipindi tunaitazama kwa upande wa Uislamu, tukikusudia kutoa dalili na kuthibitisha huku tukijibu utata wowote wa kidini unaoweza kujengwa. Mwingine ni upande wa tukio lenyewe, tukikusudia kubainisha kuwa uimamu huu ni uimamu halisi wenye sifa zote zinazostahili, na wala si uimamu wa dhana au madai matupu.

Tunapoitazama kwa upande wa Uislamu tunakuta kwanza kuna dharura ya kufafanua je, wenyewe ni suala la kiitikadi au wenyewe ni suala la kisharia (kifiqihi)? Ikiwa suala ni la kiitakidi kama wanavyoamini Shia basi sisi tunaikuta Qur’an tukufu inathibitisha waziwazi unabii kwa mtoto, na unabii ni suala la kiitikadi. Mwenyezi Mungu anasema: “Ewe Yahya shika kitabu kwa nguvu, na tukampa hekima angali mtoto.”13

Na kama ni suala la kisharia (kifiqihi) basi ni wazi kabisa kuwa sharia (fiqihi) ya kiisilamu imemzuia mtoto kujiendeshea muamala wowote, na aliyezuiliwa kujiendeshea muamala hana utawala juu ya nafsi yake, basi ikiwa hivyo ndivyo itawezekanaje tena yeye awe mtawala wa mwingine? Hivyo uimamu wa mtoto si halali.

Waisilamu wametofautiana katika suala hili na hatimaye madhehebu ya madhehebu manne ikaufanya ukhalifa na uimamu kuwa miongoni mwa majukumu ya kisharia (kifiqihi) na vitendo vya mukalafina.

Kambi ya Ahlul-Bait yenyewe ikaamini kuwa ni suala la kiitikadi na ni miongoni mwa misingi ya dini ambayo ndio majukumu ya Mola mlezi wa ulimwengu na wala si miongoni mwa majukumu ya mukalafina na viten- do vya waja.

Hivyo madhehebu ya Ahlul-Bait inapoamini uimamu wa utotoni kwa baadhi ya maimamu akiwemo Imam Mahdi yenyewe huwa na uhakika katika hilo na wala hakuna utata wowote upande wa akida maadamu Qur’an tukufu inathibitisha waziwazi unabii wa utotoni kwa Yahya (a.s.), pia hakuna utata wowote upande wa sharia (fiqihi) maadamu suala hili kwa mtazamo wa Ahlul-Bait liko nje na wigo wa sharia (fiqihi) na liko kwenye wigo wa akida. Hukumu za sharia katika mlango wa kumzuia mtoto kujiendeshea mambo unawahusu mukalafina na haumuhusu Mwenyezi Mungu, kwa sababu sharia ni maamrisho ya Mwenyezi Mungu yanayoelekezwa kwa mukalafina.

Hivyo inabainika kuwa lengo letu katika kutoa ushahidi kupitia unabii wa Yayha (a.s.) ni kutaka kubainisha kuwa uimamu ni kama unabii yote maw- ili ni masuala ya kiakida, na kuwa suala la kiakida haliko chini ya vipimo vya kibinadamu, bali hua haliwi hata chini ya vipimo vya sharia ambayo imekuja ili kuratibu mwenendo wa mukalafina na hivyo haisihi kuioanisha na Mola mlezi wa walimwengu.

Hivyo unabii wa Yayha (a.s.) unatufidisha kuwa suala la kiakida linasima- ma kwa dalili na hoja, hivyo iwapo itathibiti hoja ya kiakida inay- outhibitisha uimamu wa mtoto mdogo basi ni lazima kuuamini kama tulivyoamini unabii wa mtoto mdogo pindi iliposimama hoja kuuthibitisha, na hapo haitokuwa na maana yoyote kauli ya mwenye kusema kuwa kuthibitisha kupitia unabii wa Yahya haiwezekani kwa sababu wenyewe umetamkwa waziwazi ndani ya Qur’an kinyume na suala la Mahdi.

Kuanzia hapa utaona hauna msingi wowote ukanushaji wa Ibnu Hajar Al- Haythami na mfano wake juu ya uimamu wa Imam Mahdi bali umeangu- ka, kwani yeye ameandika kwa njia isiyonasibu kuwa: “Kisha kina- chokubalika ndani ya sharia takatifu ni kuwa utawala wa mtoto mdogo hausihi, nawashangaa hawa wapumbavu walioghafilika imekuwaje wadai

kuwa uimamu wake ulianzia umri wa miaka mitano…..14 Imeshakuwa wazi kuwa hili si miongoni mwa uamuzi wa sharia bali ni uamuzi wa fiqi- hi yao ambayo haisihi kutulazimisha sisi.

Tunapolitazama suala hili upande wa hali halisi ya kihistoria tunakuta kuwa Mahdi (a.s.) alichukua nafasi ya baba yake katika uimamu wa waisil- amu akiwa ni mtoto wa umri wa miaka mitano, hii inamaanisha kuwa alikuwa ni Imam aliyekamilika katika kila linalohusu uimamu, kuanzia uwezo wa kifikra hadi wa kiroho ikiwa ni mapema mno katika uhai wake mtukufu.

Sayyid Shahid As-Swadri anasema katika suala hili: “Uimamu wa mape- ma ni hali iliyotangulia kuwapata baadhi ya baba zake, kwani Imam Muhammad bin Ali Al-Jawad (a.s.) alichukua uimamu akiwa na umri wa miaka minane15 na Imam Ali bin Muhammad Al-Hadi alichukua uimamu akiwa mna umri wa miaka tisa16 na Imam Abu Muhammad Al-Hasan Al- Askari mzazi wa kiongozi anayengojewa alichukua uimamu akiwa na umri wa miaka ishirini.17

Hivyo inaonekana kuwa tukio la uimamu wa mapema lilishamiri kwa Imam Mahdi na Imam Al-Jawad, sisi tunaliita kuwa ni tukio la wazi kwa sababu kwa kule kuwatokea baadhi ya baba zake lilikuwa limetengeneza dalili ya kivitendo ya kimaada iliyoishi ndani ya jamii ya waisilamu na hivyo kipindi cha Imam wakawa wameijua na kuizowea, na hivyo hai- wezekani kuombwa dalili iliyo wazi na yenye nguvu kuliko uzoefu wa umma18 ili tushibitishe tukio miongoni mwa matukio.

Hilo tutalibainisha ndani ya nukta zifuatazo:

a. Uimamu wa Imam yeyote wa Ahlul-Bait haukuwa makao makuu ya ufalme na utekelezaji ambao unarithiwa kutoka kwa baba hadi kwa mtoto, ambao unapewa nguvu na utawala wa mtawala kama ilivyokuwa uimamu wa makhalifa wa kifatimiyya na ukhalifa wa makhalifa wa kiabbasia, bali sera zake pana za kiraia zilikuwa zikipendwa kupitia njia ya kiroho waliyokuwa nayo, ukinaishaji wa sera hizo kifikra kuwa wao ndio wanao- faa kwa uimamu huu ili kuongoza Uislamu, na uongozi wao uliyokuwa kwa misingi ya kiroho na kifikra.

b. Sera hizi za kiraia ziliasisiwa tangu mwanzo wa Uislamu na zikashamiri na kuenea zama za maimamu wawili Al-Baqir na As-Sadiq (a.s.) na hivyo madhehebu hii iliyolelewa na maimamu hawa wawili ndani ya sera hizi za kiraia ikawa imetengeneza mkondo mpana wa kifikra ndani ya ulimwengu wa kiisilamu, mkondo uliyojumuisha mamia ya Wanachuoni wa sharia, wanathaiolojia, wanatafsiri na Wanachuoni katika fani mbalimbali za maarifa ya kiisilamu na kibinaadamu yaliyokuwa maarufu zama hizo, mpaka Hasan bin Ali Al-Washa akasema: “Mimi niliingia msikiti wa Kufa humo nikawaona masheikh19 mia tisa kila mmoja akisema ametusimulia Jafar bin Muhammad.”

c. Hakika masharti waliyokuwa nayo madhehebu hii pamoja na sera za kiraia walizoziwakilisha ndani ya jamii ya kiisilamu yenyewe tu yalivyo yanauamini uimamu na kuweka mipaka katika kumwainisha Imam na kutambulisha uwezo wake katika jukumu la uimamu, ni masharti makali mno kwa sababu yenyewe yanaamini kuwa Imam hawi Imam ila anapokuwa ni mjuzi kuliko watu wote wa zama zake.20

d. Hakika madhehebu na sera zake za kiraia ilikuwa ikitoa muhanga mkub- wa katika kuimarisha akida yake kuhusu uimamu, kwa sababu kwa mtazamo wa ukhalifa wa zama hizo ulikuwa ukiiona madhehebu hiyo ni adui, kwa uchache ni upande wa kifikira, jambo lililopelekea utawala wa zama hizo kuwatokomeza na kuendelea kuwauwa, hivyo akauwawa aliyeuwawa, akafungwa aliyefungwa na mamia wakafia ndani ya giza la magereza, hii inamaanisha kuwa itikadi ya uimamu wa Ahlul-Bait ilikuwa ikiwakalifu gharama ghali,21 na mtu hakuwa na kishawishi chochote isipokuwa ile hisia ya kujikurubisha karibu mno na Mwenyezi Mungu mtukufu aliyonayo mwenye kuamini au kutarajia.

e. Hakika maimamu wenyewe ambao sera hizi za kiraia zilikuwa karibu nao kupitia uimamu hawakujitenga nazo na wala hawakutegemewa kujik- weza kama ilivyo kwa wafalme mbele ya raia wao na wala hawakuwa wamejificha labda wafichwe na utawala uliokuwa madarakani zama hizo kwa kuwafunga na kuwafukuza, hili tunalifahamu kupitia idadi kubwa ya wapokezi na wasimulizi wa Hadithi wa kila mmoja miongoni mwa maima- mu kumi na moja na pia kupitia barua kati ya Imam na watu wa zama zake, pia kupitia safari alizokuwa akisafiri Imam upande mmoja na wawakilishi wake sehemu mbalimbali za ulimwengu upande mwingine, na kupitia kile kitendo kilichozoeleka na wafuasi wao cha kwenda kuwajulia hali maima- mu wao na kuwazuru huko Madina tukufu pindi wanapokuja nyumba tukufu toka kila sehemu kwa ajili ya kutekeleza faradhi ya hija.22 Hayo yote yanalazimu kuendelea kuwa pamoja kwa kiwango cha wazi kati ya Imam na sera zake zilizoenea sehemu zote za ulimwengu wa kiisilamu katika matabaka mbalimbali ya Wanachuoni na wasiokuwa Wanachuoni.

f. Ukhalifa wa zama za maimamu ulikuwa ukiwatazama wao na uongozi wao wa kiroho na kiimamu kama chimbuko la hatari kubwa dhidi ya utawala wao na mikakati yao, kwa ajili hii ulitumia kila juhudi katika kuu- tokomeza uongozi huu, na katika kutimiza hilo wakalazimika kuwa na njia mbalimbali hasi, na kuna muda ulidhihirisha chuki na ujeuri pale unapo- lazimika kulinda nafasi yake, na hivyo viliendelea vitendo vya kuwaweka maimamu gerezani na kuwafukuza bila kujali hisia za machungu na kuk- erwa kwa waisilamu na watu wa viwango mbalimbali wenye kuwatawal- isha.

Tukichukua nukta hizi sita kwa uangalifu ambazo ni ukweli halisi wa kihistoria usiokuwa na shaka yoyote tunaweza kupata natija ifuatayo, nayo ni: Tukio la uimamu wa mapema lilikuwa ni tukio lililotokea kweli wala si ndoto miongoni mwa mambo ya ndoto, kwa sababu Imam ambaye anaji- tokeza mbele za watu ilihali akiwa mdogo kisha anajitangaza kuwa ni Imam wa kiroho na kifikra kwa waisilamu ni lazima awe katika uwezo wa wazi unaoonekana bali awe na elimu kubwa na maarifa, mtazamo wa juu, umakini katika sharia, tafsiri na akida.

Kwa sababu asingelikuwa hivyo basi asingeliweza kuwakinaisha raia hao juu ya uimamu wake, ilihali imeshatangulia kuwa maimamu walikuwa katika nafasi ambayo inawaruhusu raia kuwa nao pamoja na kuyamiliki maisha yao na kuchunguza shakhsia zao.

Hivi unaona inawezekana mtoto mdogo adai uimamu na ajisimike kama kiongozi wa Uislamu mbele ya macho na masikio ya umma kisha watu wote wamwamini na kutoa kila kilicho ghali na thamani kwa ajili ya kuutetea na kuundeleza bila ya watu hao kujilazimisha kuchunguza hali yake? Na bila ya kutetemeshwa na tukio hili la uimamu wa mapema ili kujua undani wa tukio na kumtathmini kijana huyu mdogo aliye Imam23?

Hebu tujalie kuwa watu hawakujishughulisha na kitendo cha kutaka kujua undani, je suala hili linaweza kuendelea miaka yote na miezi yote bila ya ukweli kugundulika na hasa ukizingatia kuwa kuna ushirikiano halisi wenye kuendelea kati ya mtoto ambaye ndiye Imam na watu wengine? Je akili inakubali kijana yule kwa akili yake na fikira yake awe ni Imam laki- ni hilo lisionekane ndani ya uhusiano wake wa muda mrefu?

Tukijalia kuwa sera za kiraia za uimamu wa Ahlul-Bait hazikutoa nafasi ya kugundua hali halisi ya mambo basi ni kwa nini ukhalifa uliokuwa madarakani ulinyamaza bila kufichua hali halisi kwa faida yake? Hivi uoni hivyo ingekuwa ni rahisi sana juu ya utawala uliyokuwepo madarakani laiti kweli Imam mtoto angekuwa ni mtoto kifikira na kielimu kama ilivyo kwa watoto wengine.

Hivi huoni njia ya kufanikiwa zaidi ingekuwa ni hii ya kutoa hali halisi ya mtoto huyu kwa wafuasi wake na wasiokuwa wafuasi wake, na kisha kuthibitisha kutokufaa kwake kwa uimamu na uongozi wa kiroho na kifiki- ra? Kwani hata kama ni vigumu kukinaisha kuwa mtu fulani mwenye miaka arubaini au hamsini aliyekusanya elimu kubwa zama zake hafai kuchukua uimamu lakini hakuna ugumu wowote katika kukinaisha kuwa mtoto wa kawaida hafai kuchukua uimamu kwa maana ile waijuayo Shia Imamiya24, hiyo ni vyovyote vile atakavyokuwa mwerevu na mwenye kipaji. Njia hii ingekuwa ni nyepesi na rahisi mno kuliko njia hizo za utokomezaji na uuwaji zilizochukuliwa na utawala wa zama hizo.

Hakika tafsiri pekee ya kitendo hiki cha kunyamaza kwa ukhalifa wa zama hizo dhidi ya mchezo huu mwepesi25 ni kuwa wenyewe ulijua fika kuwa uimamu wa mapema ni tukio dhahiri la kweli na wala si mbinu za kuund- wa. Ni kweli kabisa kuwa wenyewe uliujua fika ukweli huo kivitendo baada ya kuwa umejaribu kucheza mchezo huo mwepesi lakini ukashindwa. Historia inatusimulia majaribio ya namna hii na jinsi yalivyofeli, ilihali katu haijatusimulia jinsi tukio la uimamu wa mapema lilivyotetereka au jinsi mtoto aliye Imam alivyokumbana na kikwazo kilicho juu ya uwezo wake au kilichotetemesha na kuwafanya watu wakose imani naye.

Na hii ndio maana ya ile kauli tuliyosema kuwa uimamu wa mapema ni tukio la kweli lililotokea ndani ya maisha ya Ahlul-Bait (a.s.) na wala si ndoto tupu, pia tukio hili lililotokea lina mizizi na hali mbalimbali ndani ya utamaduni utokao mbinguni ambao umedumu ndani ya ujumbe na uongozi wote utumwao na Mola mlezi.

Yahya (a.s.) anatosha kuwa mfano halisi wa tukio hili la uimamu wa mapema wa Ahlul-Bait (a.s.) uliyomo ndani ya utamaduni huu wa Mola mlezi pale Mwenyezi Mungu aliposema: “Ewe Yahya! Shika kitabu kwa nguvu, na tukampa hekima angali mtoto.”26 Basi itakapothibiti kuwa uimamu wa mapema ni tukio lilitokea na lipo kivitendo ndani ya maisha ya Ahlul-Bait hakutokuwa tena na kizuizi chochote kinachohusu uimamu wa Mahdi (a.s.) na ukhali wake baada ya baba yake akiwa angali mdogo.”27

Sifa ya tatu: Ghaiba inalazimu umri mrefu unaolingana na urefu wa zama.

Miongoni mwa mambo ya lazima na sifa za uelewa wa wazo la uwepo wa Mahdi kwa mujibu wa upande wa Ahlul-Bait (a.s.) ni kuamini ghaibu ya Imam (a.s.) dhidi ya macho na kuendelea kuwa katika hali hiyo mpaka Mwenyezi Mungu atakapomwidhinia kudhihirika. Ili tuthibitishe sifa hii basi tunaizungumzia ndani ya hatua wawili:

Ya kwanza: Hatua ya kuthibitisha uwezekano wa umri mrefu mpaka mwisho wa zama.

Hakika tatizo la msingi ambalo uwelewa wa uwepo wa Mahdi kwa mujibu wa Ahlul-Bait unakumbana nalo ni ile hali ya umri mrefu inayolazimu uwelewa huu, pamoja na urefu wa zama wenye kuendelea sanjari na umri wake. Tatizo hili limetatuliwa kwa majibu mengi nasi hapa tutatoa jibu la Sayyid Shahid alipoandika kuwa:

“Je, inawezekana mwanadamu akaishi karne nyingi kama inavyoonekana kwa huyu kiongozi anayengojewa atakayeubadili ulimwengu, ambaye hivi sasa umri wake umefikia zaidi ya miaka elfu moja mia moja na arubaini, yaani zaidi ya mara kumi na nne ya umri wa mwanadamu wa kawaida anayetimiza hatua za kawaida kuanzia utotoni mpaka ukongweni?

Neno uwezekano hapa linamaanisha moja ya maana tatu: Uwezekano wa kivitendo, uwezekano wa kielimu na uwezekano wa kimantiki au kifilosofi. Nisemapo uwezekano wa kivitendo, nakusudia kuwa kitu kiwe kinawezekana lakini ili kitimie kinamuhitaji mtu ima mimi au wewe au mwanadamu mwingine ili akitimize kivitendo. Mfano, kupiga mbizi baharini hadi kufika chini ya kina cha bahari, au kupanda mwezini ni vitu ambavyo vina uwezekano wa kivitendo unaoweza kutimia, na hivyo hivi sasa wapo wanaofanya vitendo hivyo na kuvitimiza kwa namna fulani.

Nisemapo uwezekano wa kielimu, nakusudia kuwa kuna vitu ambavyo havina uwezekano wa kivitendo unaowezwa kutimizwa na mimi au wewe wala kutimu kupitia vifaa vya kisasa, lakini elimu haina kauli wala haiashirii rai yake inayoweza kutafsiriwa kuwa inakanusha uwezekano wa kutokea na kutimia vitu hivyo kupitia vifaa maalumu. Mfano, ndani ya elimu hamna kauli inayokanusha kutokea kwa kitendo cha kupanda hadi

kwenye sayari ya Zuhura, bali nadharia ya sasa inaonyesha kuwa hilo linawezekana japokuwa hivi sasa haijakuwa rahisi kwangu au kwako kufanya hivyo. Kwa sababu hakuna tofauti ila ndogo kati ya kupanda hadi kwenye sayari ya Zuhura na kupanda hadi mwezini, na wala kupanda hadi kwenye sayari ya Zuhura si kingine bali ni kuushinda ugumu wa ziada utokanao na masafa ya mbali zaidi.

Hivyo kitendo cha kupanda hadi sayari ya Zuhura kinawezekana kielimu japokuwa hivi sasa kivitendo haiwezekani28, hiyo ni kinyume na kitendo cha kupanda hadi kufika kwenye jua huko mbinguni, jambo hilo hali- wezekani kielimu, yaani elimu haina matarajio ya kutokea hilo kwani uwezekano wa kutengeneza chombo chenye uwezo wa kuzuia joto la jua hausawiriki kielimu na kitafiti.

Nisemapo uwezekano wa kimantiki na kifilosofi, nakusudia kuwa akili haioni kizuizi kinachopelekea kuhukumu kuwa jambo fulani ni muhali na haliwezekani kabisa, hiyo ni kutokana na kanuni za uwezekano ina- zozidiriki. Kwa mfano, kugawa machungwa matatu kwa uwiano sawa ni kitendo kisichokuwa na uwezekano wa kimantiki, kwa sababu akili inajua kuwa tatu ni idadi tasa na wala si idadi shufwa hivyo haiwezekani kugawanyika kwa uwiano sawa, kwa sababu kugawanyika kwa uwiano sawa kutakuwa kunamaanisha yenyewe ni shufwa na hapo itakuwa ni tasa na shufwa wakati mmoja, na hali hii ni mpingano na mpingano ni muhali kimantiki.

Lakini mwanadamu kuingia ndani ya moto bila kuungua au kupanda hadi kwenye jua bila ya kuunguzwa na joto la jua ni jambo lisilokuwa muhali kimantiki, kwani hamna mpingano katika kufikiria kuwa joto halitoki kwenye umbo lenye joto kali na kuingia kwenye umbo lenye joto dogo, bali ni kinyume na utafiti uliyothibiti sasa kuwa joto hutoka kwenye umbo lenye joto kali mpaka kwenye umbo lenye joto dogo hadi pale maumbo yote mawili yatakapolingana kwa joto. Na hivyo tunagundua kuwa uwezekano wa kimantiki una wigo mpana kuliko uwezekano wa kielimu na ule wa kielimu una wigo mpana kuliko wa kivitendo.

Hamna shaka kuwa kurefuka umri wa mwanadamu hadi maelfu ya miaka ni jambo linalowezekana kimantiki kwa sababu hilo si muhali kwa mtazamo wa kaikili, wala katika hali kama hii hakuna mpingano wowote kwa sababu uhai kama uhai haulazimu kifo cha haraka, na wala hakuna mjadala katika hilo.

Pia hamna shaka wala mjadala kuwa umri huu mrefu hauwezekani kivi- tendo kwa namna ile ya uwezekano wa kivitendo wa kuteremka mpaka chini ya kina cha bahari au kupanda hadi mwezini, hiyo ni kwa sababu elimu na vitendea kazi vyake na nyenzo zake zilizopo sasa, na ule uwezo wa uzoefu wa mwanadamu wa zama hizi, vyote haviwezi kurefusha umri wa mwanadamu hadi mamia ya miaka, kwa ajili hii tunawakuta watu wengi wenye kujali uhai na wenye uwezo wa kuandaa nyenzo za kielimu hawafanikiwi kufikia umri ila ule wa kiwango cha kawaida.

Ama kwa upande wa uwezekano wa kielimu ni kuwa mpaka leo hakuna rai inayokanusha hilo.29 Mada hii ina uhusiano na tafsiri ya kifasiolojia kuhusu hali ya uzee na ukongwe wa mwanadamu, je hali hii inatokana na kanuni ya maumbile inayolazimu nyama za mwili wa mwanaadamu na chembechembe zake kukauka kidogokidogo na kupungua uwezo wa kuen- delea katika utendaji mpaka kufikia kiwango cha kusimama katika muda maalumu hata kama tutautenga na sababu za nje?

Au ukaukaji huu na upungufu wa uwezo huu katika nyama na chem- bechembe za mwili hutokana na kule kupambana na sababu za nje kama vile bakteria au sumu inayoingia mwilini kupitia chakula anachokula au sababu nyingine yoyote?

Elimu inajiuliza yenyewe swali hili hivi sasa na ina uwezo wa kulijibu, swali hili lina jibu zaidi ya moja kwa mtazamo wa kielimu. Kwani iwapo tukichukua mtazamo wa kielimu unaotafsiri uzee na udhaifu wa ukongwe kuwa unatokana na mapambano dhidi ya sababu maalumu za nje, hii ita- maanisha kuwa kwa uwezekano wa kielimu ni kuwa iwapo nyama ambayo inatengeneza mwili wa mwanaadamu itatengwa mbali na sababu hizo maalumu basi ina uwezo wa kuendelea na uhai na kujiepusha na hali ya uzee na kuishinda kabisa.

Na kama tukitafsiri uzee kuwa unatokana na kanuni ya kimaumbile ya chembechembe hai na nyama yenye uhai binafsi, kwa maana kuwa yenyewe ina nguvu yenye ukomo maalumu inayopitia ukongwe na uzee na kuishia kifo. Basi nasema: Kama tukitafsiri kwa mtazamo huu haitomaan- isha kuwa kwa kanuni hii ya kimaumbile hakuna udhaifu. Bali yenyewe inaonyesha udhaifu upo, kwa sababu katika uhai wetu wa kawaida tunaku- ta uzee ni hali ya kifasiolojia isiyokuwa na wakati maalumu na hivyo huweza kuja mapema, na wasomi wanathibitisha hilo katika tafiti zao za kielimu.

Na pia inaweza kuchelewa kiasi kwamba akawa na miaka mingi ya kupin- dukia lakini akawa bado viungo vyake vina nguvu na wala havitokezi kwake viambata vya uzee, kama matabibu wanavyoeleza hilo.30 Bali wasomi wameweza kivitendo kutumia udhaifu kwa kanuni hiyo ya kimaumbile na hivyo wakajua umri wa baadhi ya wanyama kuwa ni zaidi ya mamia ya miaka ukilinganisha na umri wa kawaida, hiyo ni kutokana na kutengeneza mazingira na sababu zinazochelewesha utendaji wa kanuni ya uzee.

Kwa maelezo haya inathibiti kielimu kuwa kuchelewesha kanuni hii kwa kutengeneza mazingira na sababu maalumu ni jambo linalowezekana kie- limu japokuwa elimu haijafanikiwa kutimiza ucheleweshaji huu kivitendo kwa kiumbe maalumu kama mwanaadamu, hakuna kitofautishi ila ni kwa sababu ya tofauti ya kiwango cha ugumu kilichopo kati ya utimizaji huu kwa mwanadamu na kwa viumbe wengine.

Hii inamaanisha kuwa upande wa nadharia ya kielimu na kulingana na maelekezo ya mitazamo yake kamwe hakuna kinachokanusha uwezekano wa kurefuka umri wa mwanadamu, hiyo ni sawa tutafsiri uzee kuwa una- tokana na mapambano na vita dhidi ya sababu za nje au tutafsiri kuwa ni matokeo ya kanuni ya kimaumbile ya chembechembe hai zenyewe binafsi huelekea kwenye kutoweka.

Muhtasari wa hali hiyo ni kuwa urefu wa umri wa mwanaadamu na kuen- delea kwake kuishi karne nyingi ni jambo linalowezekana kimantiiki na kielimu, lakini lenyewe halijawezekana kivitendo isipokuwa mitazamo ya kielimu ipo mbioni kulitimiza hili kivitendo baada ya juhudi ndefu.

Kutokana na maelezo haya tunauzungumzia umri wa Mahdi (a.s.) na mshangao na maswali yanayouzunguka, tunasema: Baada ya kuthibiti kuwa umri huu unawezekana kimantiki na kielimu, na baada ya kuthibiti kuwa elimu ipo mbioni kidogo kidogo kuubadili uwezekano huu wa kinad- haria na kuugeuza kuwa wa kivitendo basi hakuna nafasi ya mshangao labda kushangaa jinsi gani Mahdi ameitangulia elimu yenyewe, na hivyo uwezekano wa kinadharia unabadilika na kuwa wa kivitendo kwa Mahdi mwenyewe kabla ya elimu kufikia kiwango cha uwezo huo wa kivitendo katika maendeleo yake kuhusu mabadiliko haya, hii ni sawa na mtu anayei-

tangulia elimu katika kugundua dawa ya kansa.

Na ikiwa suala ni vipi Uislamu umezitangulia harakati za elimu katika sekta hii ya mabadiliko? Basi jibu ni kuwa: Hiyo si sekta pekee ambayo Uislamu umezitangulia harakati za kielimu, kwani sisharia yote ya kiisila- mu imezitangulia harakati za elimu na maendeleo ya kimaumbile ya fikra za mwanadamu kabla ya karne nyingi?31

Kwani haijatoa changamoto kwa kutoa kanuni mbalimbali zinazohitaji utekelezaji ambao bado uwezo wa mwanadamu haujaufikia katika harakati zake binafsi ila baada ya miaka mingi?

Hivi haujaleta sheria ambazo ziko katika kilele cha hekima ambazo mwanadamu hajaweza kutambua siri zake na hekima yake ila baada ya muda fulani? Hivi ujumbe wa Mola haujafichua siri za ulimwengu ambazo hazikuweza kugonga ndani ya mawazo ya mwanadamu, kisha baadae ndipo elimu ikathibitisha na kuunga mkono?

Ikiwa kweli tunayaamini haya yote basi ni kwa nini tunakanusha kitendo cha huyu aliyeutuma ujumbe huu kuwa ameitangulia elimu kupitia umri wa Mahdi?32 Mimi hapa sijazungumzia ila hali ya utanguliaji ambayo sisi tunaweza kuidiriki moja kwa moja na hapo tunaweza kuongezea hali ya utanguliaji ambayo inazungumziwa na ujumbe wa Mola wenyewe.

Mfano wa hali hiyo ni: Wenyewe unatupa habari kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipelekwa usiku kutoka msikiti mtukufu hadi msikiti wa mbali, safari hii33 ikiwa tutataka kuifahamu kupitia kanuni za kawaida za kiulimwengu basi yenyewe inaonyesha jinsi ya kutumia kanuni za kawai- da za kiulimwengu kwa namna ambayo elimu haikufanikiwa kutimiza matumizi hayo ila baada ya mamia ya miaka.34 Hivyo ujuzi huu wa Mola ambao ulimwezesha Mtukufu Mtume kusafiri kwa haraka mno kabla ya elimu kufanikiwa kitimiza hilo ndio uliomwezesha Khalifa wake wa mwisho awe na umri huu mrefu kabla ya elimu kufanikiwa kutimiza hilo.

Ndio, umri huu mrefu ambao Mwenyezi Mungu amemtunuku mwokozi anayengojewa unaonekana ni kitu kigeni ndani ya mipaka iliyozoeleka na hata leo katika maisha ya kawaida ya watu na hata ndani ya maendeleo ya kisasa yaliyotimizwa kwa uzoefu wa wasomi. Lakini je, jukumu gumu la mabadiliko aliloandaliwa huyu mwokozi nalo sigeni ndani ya mipaka ya kawaida ya maisha ya watu ukilinganisha na maendeleo mbalimbali yaliy- owapitia katika historia ya maisha?

Hivi si kakabidhiwa mabadiliko ya ulimwengu na kurejesha hali yake ya kiustaarabu kama ilivyokuwa mwanzo kwa msingi wa haki na uadilifu?

Kwa nini basi tunashangaa pindi jukumu hili kubwa linapokuwa na baad- hi ya hali ngeni zilizoko nje ya mazoea yetu kama vile urefu wa umri wa mwokozi anayengojewa? Kwani ugeni wa hali hizi na kuwa kwake nje ya mazoea hata kama utakuwa ni mkubwa wa kiasi gani bado haujaushinda ugeni wa jukumu lenyewe kubwa ambalo ni lazima huyu tuliyeahidiwa alitekeleze.

Ikiwa tunaridhika na jukumu hilo la kipekee35 la kihistoria japokuwa ndani ya historia ya mwanadamu halina mfano wake uliotangulia basi ni kwa nini haturidhii umri huo mrefu ambao ndani ya maisha yetu ya kawaida hatu- japata umri mfano wake? Na wala sijui je, ni bahati au la, kitendo cha watu wawili tu kusimama na kumaliza ustaarabu mbovu wa mwanadamu kwa kujenga ustaarabu mpya, huku kila mmoja kati yao akiwa na umri mrefu unaouzidi mara elfu umri wetu wa kawaida ?

Mmoja kati ya hao wawili tayari alishamaliza jukumu lake katika historia iliyopita ya mwanadamu, naye ni Nabii Nuh ambaye Qur’an Tukufu imemwelezea36 kuwa aliishi ndani ya jamii yake miaka elfu moja kasoro hamsini, na kwa kupitia mafuriko akafanikiwa kuutengeneza ulimwengu upya.

Mwingine ni yeye atakayetekeleza jukumu lake huko mbele kwenye mus- takabali wa maisha ya mwanadamu, naye ni Mahdi (a.s.) ambaye mpaka sasa ameishi ndani ya jamii yake zaidi ya miaka elfu moja, na siku aliyokadiriwa ataujenga ulimwengu upya.

Basi ni kwa nini tunakubali umri wa Nuh ambaye ulikaribia miaka elfu moja kwa kadirio la chini lakini hatukubali umri wa Mahdi (a.s.)?37

Mpaka sasa tumeshajua kuwa umri mrefu ni jambo linalowezekana kie- limu, lakini hebu tujalie kuwa ni jambo lisilowezekana kielimu na kuwa kanuni ya uzee na ukongwe ni jambo lisilowezekana kwa mwanadamu wa sasa na wala hata baada ya juhudi ndefu haiwezekani kuushinda na kubadili kanuni zake na masharti yake, hali hiyo inamaanisha nini?

Inamaanisha kuwa kurefuka kwa umri wa mwanaadamu kama Nuh na Mahdi (a.s.) kwa kuishi karne nyingi ni kinyume na kanuni za kawaida za Ama kuhusu uyakinifu wa nassi ni kuwa Hadithi za Mahdi zimefika kiwango cha uwingi usiopingika “tawaatur” na hali hiyo huwajibisha uyakinifu na elimu hivyo hakuna tofauti kati ya makundi mawili. Rejea kitabu At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5:341 na 360. Uwingi usiyopingika “Tawaturi” umepokewa kutoka kwa Shawkaniy, na hatimaye Wanachuoni wa makundi yote mawili wamefikia kusema kuwa atakayepinga kuhusu Mahdi basi amempinga Mtukufu Mtume Muhammad. Hawajasema hivyo ila ni kwa ajili ya kuthibiti hali ya uwingi usiyopingika “tawa- turi” wa Hadithi hizo, na kuwa suala hilo ni katika dharura za kidini na atakayezikanusha basi ni kafiri kwa kauli ya wanazuoni wote. Rejea Al-Ishaah Liashratisaah cha Al-Barazanjiy anapomzungumzia Mahdi. Maelezo ya uwingi usiyopingika “tawaturi” tumeyanukuu kwenye utangulizi.

kiulimwengu ambazo zimethibitishwa na elimu, utafiti na majaribio ya kisasa, na kwa ajili hiyo hali hiyo inakuwa ni muujiza ambao umesitisha kanuni ya kiulimwengu katika hali maalumu ili kuhifadhi uhai wa mtu ambaye amekabidhiwa jukumu la kuhifadhi ujumbe wa Mola.

Huu si muujiza pekee wa namna yake au mgeni katika itikadi ya mwisila- mu anayeamini Qur’an na Sunna,38 kwani kanuni ya uzee na ukongwe si nzito zaidi kuliko kanuni ya joto kuhama toka umbo lenye joto kali hadi kwenye umbo lenye joto hafifu mpaka litakapokuwa na uwiano sawa, kwani tayari Mwenyezi Mungu alishasitisha kanuni hii ili kuokoa maisha ya Nabii Ibrahim (a.s.) pindi njia pekee ya kumwokoa ilipokuwa ni kusi- tisha kanuni hiyo.

Moto ukaambiwa pindi alipowekwa ndani ya moto: “Tukasema: Ewe moto, kuwa baridi na salama kwa Ibrahim.”39 Basi akatoka ndani ya moto huo kama alivyoingia akiwa salama bila kupatwa na madhara yoyote. Na kanuni mbalimbali nyingi za kiulimwengu ambazo zilisitishwa ili kuwaokoa manabii na hoja wa Mwenyezi Mungu juu ya ardhi.

Bahari ilipasuliwa kwa ajili ya Musa40 (a.s.), warumi wakafananishiwa Isa41 pindi walipotaka kumshika na hawakuwa wamemshika, Mtume Muhammad (s) akatoka nyumbani kwake akiwa amezingirwa na vijana wa kikurayshi ambao walibaki saa nyingi wakisubiri kumshambulia, basi Mwenyezi Mungu akamsitiri dhidi ya macho yao ilihali akitembea katikati yao.42

Hali zote hizi zinaonyesha kanuni za kifizikia zilivyositishwa ili kum- wokoa mtu ambaye hekima ya Mola ilihitaji kumwokoa, basi na kanuni ya uzee na ukongwe iwe miongoni mwa kanuni hizo.

Na tunaweza kutoa uwelea jumuishi kutoka ndani ya hali hiyo kuwa kila uhifadhi wa maisha ya hoja wa Mwenyezi Mungu unapolazimu kusitisha kanuni za kifizikia basi kurefuka kwa maisha ya mtu huyo kunakuwa ni dharura ili kutimiza jukumu lake aliloandaliwa kwalo, kwa sababu msaada wa Mola uliingilia kati kusitisha kanuni hiyo ili kutimiza jukumu hilo, kinyume na pale mtu anapokuwa tayari keshatimiza jukumu lake aliloan- daliwa kwalo na Mola, yeye hupokea mwito wake na kufariki au hufa kishahidi kulingana na taratibu za kanuni ya kifizikia .

Kwa kawaida huwa tunakutana na swali lifuatalo kutokana na uwelewa huu jumuishi: Inawezekanaje kanuni kusitishwa? Na inakuwaje unakatika uhusiano wa kutoachana (dharura au lazima) uliyopo katika hali ya kifizikia? Huoni hali hii inapingana na elimu iliyogundua kanuni hiyo ya kifizikia na kuainisha uhusiano huu wa kutoachana (dharura au lazima) kwa misingi ya majaribio na utafiti?

Jibu: Hakika elimu yenyewe binafsi imejibu swali hili kwa kuondoa fikira ya kuwepo hali ya kutoachana katika kanuni za kifizikia. Ufafanuzi juu ya hilo ni kuwa: Hakika elimu huzigundua kanuni za kifizikia kwa msingi wa utafiti wa majaribio na utaratibu maalumu, hivyo pindi inapozalisha utokeaji wa tukio la kiulimwengu baada ya tukio lingine basi uzalishaji huu huthibitishwa kwa kanuni ya kifizikia, nayo ni kila linapopatikana tukio la mwanzo baada yake hupatikana tukio la pili.

Isipokuwa ni kuwa elimu haioni kuwa ndani ya kanuni hii ya kifizikia mna hali ya kutoachana kati ya matukio mawili kupitia uhusiano wa tukio hili na lile, kwa sababu kutoachana ni hali ya ghaibu ambayo majaribio na utafiti wa kielimu haviwezi kuithibitisha, na kwa ajili hii mantiki ya elimu ya sasa inasisitiza kuwa kanuni ya kifizikia haizungumzii uhusiano usioachana bali huzungumzia mkutano wenye kuendelea kati ya matukio mawili.43 Hivyo muujiza unapokuja hutenganisha tukio moja dhidi ya lingine na kwenda kinyume na kanuni ya kifizikia na hali hiyo si kukatisha uhusiano usioachana wa matukio mawili.

Ukweli ni kuwa muujiza kwa uwelewa wake wa kidini kwa mujibu wa mantiki ya elimu ya kisasa umekuwa ni uwelewa wa kiwango kikubwa mno kuliko ulivyokuwa zama zile za nadharia ya kilasikia juu ya uhusiano wa sababu na visababishwa. Kwani kwa mujibu wa nadharia ya kale ilikuwa ikiona kuwa kila moja kati ya matukio mawili limezalisha hali ya moja kukutana na lingine, hivyo uhusiano wao ni ule wa dharura. Dharura hapa maana yake ni muhali tukio moja kuachana na tukio lingine.

Lakini ndani ya mantiki ya elimu ya sasa uhusiano huu umegeuka na kuwa kanuni ya mkutano au ya mfuatano unaozalika44 kati ya matukio mawili bila ya kuwepo dharura hiyo ya ghaibu. Hivyo muujiza unakuwa ni hali iliyotoka nje ya kanuni hii ya mkutano au mfuatano bila ya kugongana na dharura au kupelekea hali ya muhali.

Ama kwa misingi ya utafiti wa kimantiki45 sisi tunakubaliana na mtazamo wa elimu ya sasa kuwa utafiti huo hauthibitishi kuwa kuna uhusiano wa dharura kati ya matukio mawili, lakini sisi tunaona wenyewe unaonyesha kuwa kuna tafsiri shirikishi ya uzalikaji wa mkutano au mfuatano kati ya matukio mawili kwa namna ya kuendelea. Tafsiri hii shirikishi kama ambavyo inawezekana kuitengeneza kwa misingi ya dharura ya asili pia vilevile inawezekana kuitengeneza kwa misingi ya hekima iliyopelekea Mnadhimu wa ulimwengu kufunganisha matukio maalumu na matukio mengine maalumu kwa namna yenye kuendelea, na hekima hiihii mara nyingine inalazimu kuvua matukio hayo toka kwenye kanuni na hivyo kupatikana muujiza.”46

Hivyo dalili inabainika wazi kielimu na kimantiki kuwa umri mrefu ni jambo linalowezekana na wala haulazimu dosari ya kielimu wala ya kifal- safa, na kwa maelezo haya tunakamilisha hatua ya mwanzo ya utafiti kati- ka sifa ya ghaiba.

Pili: Hatua ya kuthibitisha kutokea hilo kivitendo kwa Imam Mahdi (a.s.): Uchambuzi katika hatua hii utakamilika kwa njia wawili: Ya kiakida na ya kihistoria.

Njia ya kiakida

Tunaweza kuiunda kwa fafanuzi tatu:

a. Sifa hii ni miongoni mwa vitu vya lazima vya asili ya uelewa wa wazo la Mahdi kwa Ahlul-Bait hivyo kuthibiti uwelewa huu uthibitikaji utokanao na dalili yakinifu, na kule kubainika ubatilifu wa uwelewa usiokuwa huu vinatuongoza kwa namna ya kawaida kuamini ghaiba ya Imam wa kumi na wawili (a.s.). Maadamu maimamu ni kumi na wawili tu na wao ni wenye kuainishwa na Mwenyezi Mungu na watu hawana ruhusa

ya kuwateua basi hatuwezi kusawiri chochote ila kule kuendelea kwa uhai wa Imam wa kumi na wawili na msafara wake katika safari ya wanadamu na baada ya hapo kudhihiri zama za mwisho.

Na ni hali ya kawaida kuwa mwanadamu anayeandaliwa kwa lengo kama hili na kupangiwa maisha marefu kama haya asifanikiwe kuishi maisha hayo kwa sura ya dhahiri, na ni lazima ayaishi kwa sura ya siri mbali na macho ya watu ila iwapo tutasema Imam Mahdi (a.s.) alikufa kifo cha kawaida kama watu wengine kisha atarudi tena kuishi zama atakazodhihiri. Lakini kauli hii inalazimisha hoja ya Mwenyezi Mungu kukatika ndani ya kipindi tenganishi kati ya kufa kwake na kudhihiri kwake, na hali hiyo inapingana na Hadithi ya vizito viwili ambayo inaonyesha Kitabu haki- toachana na Kizazi na kuwa havitoachana hata muda mchache mpaka pale Kiyama kitakaposimama na kuingia kwenye Hodhi. Na italazimu kuamini kurejea Imam Mahdi kwenye uhai baada ya kifo chake, na hii ni kauli isiyosemwa na mwisilamu yeyote.

b. Riwaya zinaonyesha Imam Mahdi ana sifa ya ghaiba, na baadhi ya vyan- zo vya kisunni mfano wa kitabu Yanabiul-Mawaddah na Faraidus- Samtwayni vimeeleza hilo. Ndani ya kitabu Yanabiul-Mawaddah amenukuu kutoka kwenye kitabu Faraidus-Samtwayni kutoka kwa Al- Baqir (a.s.) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake Ali (a.s.) amese- ma: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Mahdi ni kutoka kwenye kizazi changu, atakuwa na ghaiba na atakapodhihiri ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa ujeuri na dhulma.”47

Pia humo mna nyingine kutoka kwa Said bin Jubayri kutoka kwa Ibnu Abbas (r.a.) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakika Ali ni wasii wangu na Al-Qaimu mwenye kungojewa Mahdi ambaye ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhu- luma na jeuri atatoka kwenye kizazi chake. Naapa kwa Yule aliyenituma kwa haki niwe mbashiri na muonyaji hakika wale watakaothibiti katika imani ya kuamini uimamu wake zama za ghaiba yake ni watukufu mno kuliko madini ya yakuti chekundu.”

Akasimama Jabir bin Abdullah akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)! Al-Qaimu kutoka kwenye kizazi chako ana ghaibu? Akasema: “Ndio, naapa kwa Mola wangu Mlezi ili Mwenyezi Mungu awachambue wale walioamini na awaangamize makafiri.” Kisha akasema: “Ewe Jabir! Jambo hili ni jambo la Mwenyezi Mungu na siri miongoni mwa siri za Mwenyezi Mungu, basi jiepushe na shaka kwani hakika kushakia jambo la Mwenyezi Mungu ni ukafiri.”

Pia ndani ya kurasa zilizotajwa imepokewa kutoka kwa Hasan bin Khalid amesema: Ali bin Musa Ridhaa amesema: “Hakika wa nne toka kizazi changu ni mwana wa bibi wa watumwa, kupitia yeye Mwenyezi Mungu atatoharisha ardhi dhidi ya kila ujeuri na dhulma na yeye ndiye ambaye watu watashakia kuzaliwa kwake na ndiye mwenye ghaibu, basi atakapodhihiri ardhi itang’aa kwa nuru ya Mola wake Mlezi.”48

Pia mna: Kutoka kwa Ahmad bin Ziyad kutoka kwa Daabal bin Ali Al- Khazaiy katika Hadithi waliyoipokea kuhusu Ridhaa (a.s.) na alivyosoma shairi mpaka akasema: “Hakika Imam baada yangu ni mwanangu Muhammad na baada ya Muhammad ni mwanae Ali na baada ya Ali ni mwanae Hasan na baada ya Hasan ni mwanae Hoja Al- Qaimu naye ndiye mwenye kungonjewa ndani ya ghaibu yake na mwenye kutiiwa atakapodhihiri, ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa jeuri na dhuluma. Ama ni lini atadhihiri? Ni kuwa habari kuhusu wakati amenisimulia baba yangu kutoka kwa baba zake kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Mfano wake ni sawa na Kiyama hakitowaijia ila ghafla.”49

Na mna: Kutoka kwenye kitabu Ghayatul-Marami kutoka kwenye kitabu Faraidus-Samtwayni kutoka kwa Jabir bin Abdullah, ameivusha: “Mahdi ni kutoka kwenye kizazi changu jina lake ni jina langu na kuniya yake ni kuniya yangu, ndiye mtu afananaye na mimi sana tabia na maumbile, atakuwa na ghaibu na mataifa yatakuwa na mbabaiko mpaka viumbe vipotee dhidi ya dini zao, hapo ndipo atadhi- hiri kama vimondo vyenye kuruka na kuijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhuluma na ujeuri.”

Na mna: Kutoka kwenye kitabu Faraidus-Samtwayni kwenye ukurasa uliotajwa, kutoka kwa Al-Baqir kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.)- ameivusha: “Mahdi ni kutoka kwenye kizazi changu, atakuwa na ghaibu ambayo ndani yake mataifa yatapotea – akaendelea mpaka akasema- na ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhuluma na ujeuri.”50

Na mna: Kutoka kwa Abu Jafar Muhammad Al-Baqir amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Ni uzuri ulioje kwa atakayemdiriki Qaimu wa Ahlul-Bait wangu naye huku akimfuata wakati wa ghaibu yake kabla ya kusimama kwake, huku akiwapenda vipenzi vyake na akiwafanyia uadui maadui zake, basi huyo ni mion- goni mwa marafiki zangu na wenye mapenzi kwangu, na ndiye mbora kwangu siku ya Kiyama katika umma wangu.”

Na mna: Kutoka kwa Abu Basira kutoka kwa As-Sadiq Jafar bin Muhammad kutoka kwa baba zake kutoka kwa kiongozi wa waumini (a.s.) amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Mahdi ni kutoka kwenye kizazi changu jina lake ni jina langu na kuniya yake ni kuniya yangu, ndiye mtu afananaye na mimi sana tabia na maumbile, atakuwa na ghaibu na mataifa yatakuwa na mbabaiko mpaka viumbe vipotee dhidi ya dini zao, hapo ndipo atadhihiri kama vimondo vyenye kuruka na kuijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhuluma na ujeuri.”

Kutoka kwake mfano wa hiyo isipokuwa alisema: “Hapo ndipo ataku- ja kama vimondo vyenye kuruka atakuja na akiba ya manabii (a.s.).”51

Na katika ukurasa wa 494 mna: Kutoka kwake kutoka kwa Jabir bin Yazid Al-Jaafiy amesema: Nilimsikia Jabir bin Abdullah Al-Ansar akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliniambia: “Ewe Jabir! Mawasii wangu na maimamu wa waisilamu baada yangu wa kwanza wao ni Ali kisha Hasan kisha Husein kisha Ali bin Husein kisha Muhammad bin Ali maarufu kwa jina la Al-Baqir na utamdiriki ewe Jabir, basi utakapokutana naye mpe salamu kutoka kwangu.

Kisha ni Jafar bin Muhammad kisha Musa bin Jafar kisha Ali bin Musa kisha Muhammad bin Ali kisha Ali bin Muhammad kisha Hasan bin Ali kisha Al-Qaimu. Jina lake ni jina langu, kuniya yake ni kuniya yangu mwana wa Hasan bin Ali, huyo ndiye ambaye Mwenyezi Mungu atafungua Mashariki ya ardhi na Magharibi yake mikononi mwake. Huyo ndiye ambaye atakuwa ghaibu dhidi ya vipenzi vyake, hatothibiti kwenye imani ya kuamini uimamu wake ila ambaye Mwenyezi Mungu ameutahini moyo wake kwa ajili ya imani.”

Hakika Mahdi tuliyeahidiwa akiwa si Imam mtakasifu na akawa ni mtu wa kawaida kama waisilamu wa kawaida basi hakutokuwa na munasaba wowote kati yake na kudhihiri na Masih (a.s.) kwa pamoja, ilihali yeye ni miongoni mwa manabii watano watukufu mno ili ampe nguvu Mahdi na kuwalingania wakristo waamini unabii wa Mtukufu Nabii (s.a.w.w.), hivyo ni lazima Mahdi tuliyeahidiwa awe Imam mtakasifu.

Na kwa kuwa uimamu wenye utakaso si jambo lililopo chini ya madai bali ni jambo linalohitaji uainishaji kutoka kwa Mola na nasi ya Mtume inay- oonyesha hilo, na kwa kuwa hilo halijatokea kwa wasiokuwa maimamu kumi na wawili (a.s.) hata katika kiwango cha madai tu achia mbali dalili na hoja, na kwa kuwa vifo vya maimamu kumi na mmoja waliotangulia vimethibiti na miili yao imezikwa maeneo maalumu na amebakia Imam wa kumi na wawili pekee ndiye hakijajulikana kifo chake mpaka leo basi ni lazima tuamini kuwa uhai wa Imam huyu unaendelea kuanzia pale alipoza- liwa mpaka atakapodhihiri zama za mwisho ili afae kupewa nguvu na Masihi (a.s.).

Sayyid Samiy Al-Badriy amezungumzia hilo kwa kusema: “Hakika kudhi- hiri kwa Isa kutahitaji mjumuisho wa kielimu na kiuongozi kutoka kwa Mahdi tuliyeahidiwa kwa kuzingatia yeye (Isa) atasimama kama shahidi wake na wa ujumbe ambao wito wake utaenezwa (na Mahdi) na atakuwa mfuasi wake. Mahdi kwa mtazamo wa kisunni hatokuwa na uwezo wa kumjumuisha Masihi (a.s.) bali yeye si mwenye uwezo wa kuyajumuisha makundi ya kiisilamu.

Hatokuwa na uwezo wa kumjumuisha Masihi kwa sababu Masihi ni Nabii na Mtume mtakasifu na mwenye kupewa nguvu kwa miujiza ya Mola, na mtu wa mfano huo hawezi kujumuishwa na mwanadamu asiyepewa nguvu na miujiza, wala utakaso na elimu timilifu. Na hatokuwa na uwezo wa kuu- jumuisha umma wa kiisilamu bila ya nguvu ya muujiza wa Mola na utaka- so na elimu timilifu.”52

Njia ya kihistoria

Tunaweza kuiunda kwa fafanuzi tatu:

Hakika historia imethibitisha kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.) na wala haijathibitisha kufariki kwake, jambo linaloonyesha kuwa uhai wake unaen- delea, na kwa kuwa uwepo wake hatuoni na wala hatumwoni mtu yeyote aitwaye Mahdi mwana wa Imam Hasan Al-Askari basi ni lazima atakuwa na uhai wa siri usioonekana kwa watu.

Historia imethibitisha kuwa Imam Mahdi ameonekana kwa macho mara kwa mara zama za ghaibu yake, na vimeandikwa vitabu mbalimbali juu ya hilo mfano wa kitabu Tabsiratul-Waliy Fimanr-Raa Al-Qaim Al-Mahdiy cha Sayyid Hashim Al-Bahraniy. Sheikh Abu Talib At-Tajlil At-Tabriziy ndani ya kitabu chake amewataja watu mia wawili sitini na sita53 waliomwona Imam Mahdi zama za ghaibu yake ndogo na akawa ametaja visa vyao na akatenga sura maalumu ya waliomwona Imam zama za ghaibu yake kubwa.

Akataja vitabu ishirini ambavyo ndani yake waandishi wake wameta- ja visa na habari za kihistoria kuhusu hilo, sisi hapa tutataja kisa ali- chokitoa Sayyid Sadrud-Dini As-Sadr ndani ya kitabu chake Al-Mahdi akinukuu kutoka kwa Sheikh Abdul-Wahabi As-Shaaraniy ndani ya kitabu chake Tabaqatul-Irfai kuhusu hali ya Sheikh Hasan Al-Araqiy amesema: “Nilikwenda kwake pamoja na bwana wangu Abul Abbas Al-Harithiy akasema: Unaniidhinia nikusimulie simulizi yangu kuanzia mwazo wangu mpaka muda huu kama vile ulikuwa rafiki yangu tangu udogoni mwangu?

Nikamwambia: Ndio, akasema: Nilikuwa kijana kutoka Damascus, nilikuwa fundi na siku ya ijumaa tulikuwa tukijikusanya kwa ajili ya upuuzi, michezo na pombe, basi siku moja nikafikiwa na tahadhari kutoka kwa Mwenyezi Mungu, je umeumbwa kwa ajili ya hili? Basi nikaacha waliyokuwa nayo na nikawakimbia wakanifuata nyuma laki- ni hawakunikuta. Nikaingia kasri la ukoo wa Umayya nikamkuta mtu mmoja amekaa juu ya kiti akizungumzia kuhusu Mahdi (a.s.) basi nikatamani nikutane naye.

Nikawa sisujudi sijida yoyote ila humuomba Mwenyezi Mungu aniku- tanishe naye, basi usiku baada ya Swala ya magharibi nilipokuwa nikiswali Swala ya Sunna ghafla nikamwona mtu nyuma yangu na akagusa bega langu na kuniambia: “Mwenyezi Mungu amejibu dua yako ewe mwanangu! Unataka nini mimi ndiye Mahdi.” Nikamwambia: Utakwenda na mimi nyumbani kwangu? Akasema: “Ndiyo” basi akaenda na mimi na kusema: “Niachie sehemu ya faragha nijitenge peke yangu.” Basi nikamtengea sehemu ya faragha na akawa amekaa kwangu siku saba mchana na usiku.”54

Sheikh Ali bin Isa Al-Urbaliy amesema ndani ya kitabu Kashful- Ghummah: “Watu wananukuu visa na habari kuhusu mambo yasiyokuwa ya kawaida ya Imam Mahdi (a.s.) ambayo ufafanuzi wake ni mrefu, mimi hapa nitakutajia visa viwili tu vya karibu na zama zetu ambavyo nimesimuliwa na kundi la ndugu zetu waaminifu.

Cha kwanza: Katika mji wa Al-Hilah kati ya mto Furati na mto Dijlah kulikuwa na mwanaume aitwaye Ismail bin Hasan, akasema: Ndugu yangu Ismail ametusimulia kuwa juu ya paja lake la kushoto kulizuka kipele chenye ukubwa wa shiko la mwanadamu basi matabibu wakashindwa kutibu ndipo akaja Baghdad, matabibu walipomwona wakasema: Hauna tiba. Basi akaelekea Samrau na kuwazuru maimamu wawili Ali Al-Hadi na Hasan Al-Askari (a.s.), akashuka na kuingia nyumba ya chini ya ardhi, akamwomba Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu na kutaka msaada kupitia Imam Mahdi (a.s.) kisha akaenda Dijlah akaoga na kuvaa nguo zake.

Basi akawaona wapanda farasi wanne wakitokea mlango wa uzio wa mji mmoja wao ni mzee aliyebeba mkuki mkononi na mwingine akiwa na upinde wenye rangi, mwenye mkuki alikuwa kuliani mwa njia na kushotini mwa njia kulikuwa na vijana wawili na yule kijana mwenye upinde alikuwa katikati ya njia. Basi mwenye upinde akamwambia: Wewe kesho utaenda kwenye familia yako. Akamwambia: Ndiyo. Basi mwenye upinde akasema: “Njoo kwangu ili nione kinachokuuma.” Basi akaenda kwake na ndipo akanyoosha mkono wake na kumkamua upele kwa mkono wake, akahisi maumivu na baadae akatulia.

Mzee mwenye mkuki akasema: “Umefaulu ewe Ismail, huyu ni Imam.” Kisha wakeendelea kwenda ilihali naye akiwa pamoja nao, Imam akasema: “Rejea.” Akajibu: “Kamwe sitokuacha.” Imam akase- ma: “Masilahi yako yako kwenye kurejea kwako.” Akasema: “Kamwe sitokuacha.” Mzee akasema: “Ewe Ismail! Hauoni aibu! Imamu anakwambia mara mbili rejea nawe unampinga!” Basi Imam akasima- ma na kutangulia mbele baadhi ya hatua, kisha akamgeukia na kumwambia: “Ewe Ismail! Utakapofika Baghdad ni lazima Abu Jafar atakutafuta, yaani Khalifa Al-Mustansir billah basi utakapofika kwake na akakupa kitu chochote usipokee, umwambie mtoto wetu Ridhaa akuandikie ujumbe kwa Ali bin Awdhu hakika mimi nitamsihi akupe unachokitaka.”

Kisha akaondoka pamoja na maswahaba zake, basi akaendelea kuwaona mpaka walipotoweka, kisha akaketi juu ya ardhi saa nzima akihuzunika na kulia kwa kutengana nao, kisha akaja Samrau basi watu wakamzunguka na kumwambia: “Tunaona uso wako umebadili- ka umepatwa na nini?” Akasema: “Je mliwajua wapanda farasi waliotoka mjini na kuelekea ufukweni mwa mto?” Wakasema: “Ndiyo, wao ni viongozi na wamiliki wa kondoo,” basi akawaambia: “Hapana, wao ni Imam na maswahaba zake, kijana mwenye upinde ndiye Imam, baraka za mkono wake zimeondoa maradhi yangu.”

Wakasema: “Tuonyeshe.” basi akafunua paja lake na hawakuona athari yoyote, ndipo wakachana nguo yake na kumwingiza hazina na wakawazuia watu wasiende ili watu wasisongamane kwake, kisha mpelelezi kutoka upande wa Khalifa akaja hazina na kumuuliza kuhusu habari hii na kuhusu jina lake, nasaba yake, mji wake na kuhusu kwenda kwake Baghdad mwanzo wa wiki hii kisha akamwacha.

Ismail akakesha ndani ya hazina akaswali Swala ya asubuhi na akato- ka pamoja na watu mpaka wakafika mbali na Samrau na ndipo watu wakamwaga na kurejea, basi akaendelea peke yake mpaka akafika sehemu fulani akawaona watu wamesongamana kwenye jengo la kale wakiuliza kuhusu mtu aliyewasili kwao, jina lake, nasaba yake na sehemu aliyotokea. Basi walipokutana naye na wakamtambua kupitia alama zilizotajwa walichana nguo yake na kuichukua kwa ajili ya kupata baraka kwani mpelelezi wa alikuwa ameshawaandikia Baghdad na kuwajulisha hali.

Waziri alikuwa keshamwomba As-Said Radhiyu Dini amjulishe kuhusu usahihi wa habari basi Radhiyu Dini ambaye alikuwa miongo- ni mwa marafiki wa Ismail akatoka, na yeye ndiye aliyekuwa mwenye- ji wake kabla ya kwenda Samrau, basi Radhiyu Dini na kundi lake walipomuona wakateremka kutoka kwenye wanyama wao na kuwaonyesha paja lake na hawakuona chochote, ghafla Radhiyu Dini akazimia saa nzima, kisha akamshika mkono na kumwingiza kwa waziri huku akilia na kusema:

“Huyu ni ndugu yangu na mtu wa karibu mno na moyo wangu.” Ndipo waziri akamuuliza kuhusu kisa, naye akasimulia na hatimaye akawahudhurisha matabibu walioona ugonjwa wake, akawauliza mlimuona lini, wakasema kabla ya siku kumi, basi ndipo waziri akawafunulia paja la Ismail wakakuta hakuna athari yoyote, wakase- ma: “Hii ni kazi ya Masihi (a.s.),” waziri akasema: “Sisi tunamjua ni nani aliyemtibu hivyo.”

Kisha waziri akampeleka mbele ya Khalifa naye akamuuliza kuhusu

kisa, basi akamsimulia yaliyotokea na ndipo akampa dinari elfu moja. Akamwambia: “Sina ujasiri wa kuchukua hata punje moja.” Khalifa akamwambia: “Unamwogopa nani?” Akasema: “Yule aliyefanya hivi, kwani aliniambia: Usichukue chochote kutoka kwa Abu Jafar.” Khalifa akalia.

Kisha Ali bin Isa akasema: “Nilikuwa nikiwasimulia kisa hiki jamaa waliokuwa kwangu na Shamsud-Dini mwanae alikuwa kwangu ilihali mimi simjui, akasema: Mimi ni mwanae kutoka kwenye mgongo wake. Nikasema: Je uliliona paja la baba yako likiwa na jeraha? Akasema: “Mimi nilikuwa mtoto mdogo pindi paja lake lilipojeruhika, lakini nilikisikia kisa kutoka kwa baba yangu, mama yangu, karaba zangu na jirani zangu, na nililiona paja lake baada ya kuwa limepona likiwa halina athari yoyote na eneo hilo likiwa limeota vinyweleo.”

Na pia akasema: “Nilimuuliza Sayyid Swafiyud-Dini Muhammad bin Muhammad na Najmud-Dini Haydar Ibnu Al-Aysar, wakaniambia kisa hiki ni sahihi na kuwa wao wawili walimwona Ismail kipindi cha ugonjwa wake na baada ya kupona kwake, na mwanae akanisimulia kuwa baba yake alikwenda Samrau mara arubaini baada ya kupona kwake, akiwa anatamani umrudie tena wakati ule aliomwona.

Cha pili: Alinisimulia Sayyid Baqiy bin At’watu Al-Alawi Al-Hasaniy kuwa baba yake At’watu alikuwa aamini kuwepo kwa Imam Muhammad Al-Mahdi (a.s.) na akisema: “Iwapo Imam ataniijia na kuniponya maradhi haya basi ndipo nitaamini kauli yao.” Alikuwa akikariri kauli hii, basi ndipo siku moja tukiwa tumekusanyika wakati wa Isha ghafla baba yetu akatuita nasi tukaenda haraka, akasema: “Mfuateni Imam ametoka kwangu sasa hivi.” Tukatoka na wala hatukumwona mtu. Tukarudi kwake naye akatuambia: “Mtu aliingia kwangu na kuniambia: “Ewe At’watu!” Nikasema: “Labayka.” Akasema: “Mimi ndiye Mahdi nimekuja kwako kukuponya ugonjwa wako.” Kisha akanyoosha mkono wake wenye baraka akakamua tako langu na kuondoka basi likawa kama kamba iliyofumuliwa.” Ali bin Isa amesema: “Nilimuuliza kisa hiki mwingine asiyekuwa mwanae akakikubali.”55

Kuanzia hapa Wanachuoni wa kisunni wameamini uhai wake na kuen- delea kwake kuishi au ndio matokeo ya maneno yao. Sayyid Sadrud- Dini As-Sadri amewataja baadhi yao akasema: “Miongoni mwao ni Sheikh Muhyid-Dini Ibnul Arabiy ndani ya kitabu Al-Futuhati kwa mujibu wa riwaya ya Sheikh Abdul-Wahab As-Shaaraniy ndani ya kitabu chake Al-Yawaqitu Wal-Jawahir amenukuu kutoka kwenye kitabu Is’afur-Raghibina, kwani kuwepo Imam Mahdi bin Hasan Al- Askari bila kitenganishi cha wakati kama alivyotamka wazi hilo, pia kuwepo kifo cha Imam Hasan Al-Askari mwaka mia wawili na sitini vinalazimu uhai wa Mahdi na kuendelea kuishi mpaka atakapodhihiri, au kusema atakufa kisha Mwenyezi Mungu atamfufua tena kwa uwezo wake. Na wala sidhani Sheikh Muhyid-Dini anaridhia kunasibishwa na dhana hii ya mwisho.

Na miongoni mwao ni Sheikh Abdul-Wahabi As-Shaaraniy ndani ya kitabu chake Al-Yawaqitu Wal-Jawahir kama ilivyo ndani ya kitabu Is’afur-Raghibina, amesema: “Mahdi bin Imam Hasan Al-Askari amezaliwa usiku wa nusu ya Shaabani mwaka mia wawili hamsini na tano na bado yupo mpaka atakapokutana na Isa bin Maryam. Hivyo ndivyo alivyonipa habari Sheikh Hasan Al-Araqiy kuhusu Imam Al- Mahdi pindi alipokiri na bwana wangu Ali Al-Khawasu56 akamwafiki.”

Miongoni mwao ni Sheikh Abu Abdullah Muhammad bin Yusuf bin Muhammad Al-Kunjiy ndani ya kitabu chake Al-Bayan Fiakhbar Sahibuz-Zaman kama kilivyonukuu kitabu Is’afur-Raghibina, amesema: “Na miongoni mwa dalili za kuthibitisha kuwa Mahdi yu hai mwenye kuendelea na uhai baada ya ghaibu yake mpaka sasa, na kuwa hakuna kizuizi katika kuendelea kwake ni kule kuendelea kwa Isa bin Maryam, Al-Hidhri na Ilyasa miongoni mwa mawalii wa Mwenyezi Mungu, na kuendelea kwa chongo Dajjal na Ibilisi mlaanifu miongoni mwa maadui wa Mwenyezi Mungu, hawa wote imethibiti kuwa bado wanaendelea kuishi kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.57

Miongoni mwao ni Sheikh Al-Arif Al-Fadhil Al-Khawajih Muhammad Barisa ndani ya kitabu chake Faslul-Khitabi kama ilivyo ndani ya kitabu Yanabiul-Mawaddah, baada ya kuelezea kuzaliwa kwa Mahdi anayengojewa, na kuwa Mwenyezi Mungu amempa hekima na ubainifu wa maneno akiwa mtoto mchanga kama alivyomneemesha Yaya na Isa (a.s.) kwa hilo, akasema: “Mwenyezi Mungu amerefusha umri wake kama alivyorefusha umri wa Al-Hidhri (a.s.)”.58

Miongoni mwao ni Sheikh Sadrud-Dini Al-Qawnawiyu katika baadhi ya wasii wake kwa wanafunzi wake pindi alipokuwa akifariki kama ilivyo ndani ya kitabu Yanabiul-Mawaddah, amesema: “Hakika vitabu vya tiba, hekima na falsafa vilivyo vyangu viuzeni na thamani yake wapeni sadaka mafakiri. Ama vitabu vya tafsiri, Hadithi na utawa vihi- fadhini jumba la vitabu, na someni tamko la upweke () mara elfu sabi- ni kila usiku na mnifikishie salamu kwa Mahdi (a.s.).”59

Nasema: Huenda mtu akasema kusema kwake huko hakuonyeshi uwepo wa Mahdi wala uhai wake, kwani huenda alisema hayo kwa kule kutaraji kuwa watadiriki kudhihiri kwake, lakini maana ya mwan- zo ndio inayofahamika.

Miongoni mwao ni Sheikh Saidud-Dini Al-Humawiy kama ilivyo ndani ya kitabu Yanabiul-Mawaddah, imenukuliwa kutoka kwenye kitabu cha Sheikh Azizi bin Muhammad An-Nasafiy pindi anapozungumzia utaratibu wa mawalii: “Hakika Mwenyezi Mungu alichagua mawalii kumi na wawili ndani ya umma huu kutoka Ahlul- Bait akawafanya makhalifa wa Nabii Wake mtukufu (s.a.w.w.).” mpaka akasema: “Ama Walii wa mwisho ambaye ndiye Khalifa wa mwisho wa Nabii, ambaye ni walii, naibu wa kumi na wawili na hitimisho la mawalii ni Mahdi mwenye zama hizi.”60

Miongoni mwao ni Sheikh Shihabud-Dini Al-Hindi maarufu kwa jina la mfalme wa Wanachuoni ndani ya kitabu chake Hidayatus-Suadai kama ilivyo ndani ya kitabu Ad-Durar Al-Musawiyah, amesema anapozungumzia maimamu kumi na wawili: “Wa tisa kutoka katika kizazi cha Husein ni Imam Hoja wa Mwenyezi Mungu Al-Qaimu na yeye ni ghaibu na ana umri mrefu kama walivyo waumini Isa, Ilyasa na Al-Hidhri. Na katika makafiri ni kama Dajjal na As-Samiriy.”

Miongoni mwao ni zaidi ya mmoja kati ya waheshimiwa na wanafasi- hi, kwani linalodhihiri kutoka kwenye mashairi yao ya kiarabu na kia- jemi yaliyotajwa ndani ya kitabu Yanabiul-Mawaddah na vinginevyo katika vitabu vya fadhila ni kuwa wao wanaamini uhai wa Mahdi mwenye kungojewa na kuwa yeye yu hai anaruzukiwa pale wanapom- sifu kuwa ana utawala, uimamu, ukhalifa na unaibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwa yeye ndiye kiunganishi katika rehema za Mola.”61

Katika ufafanuzi wa tatu tutategemea ule aliouandika Sayyid As-Shahid Muhammad Baqir As-Sadri (r.a.) ameandika: “Hakika ghaibu ni uzoefu walioupata baadhi ya watu muda unaokaribia miaka sabini, nao ni muda wa ghaibu ndogo, ili kufafanua hilo tunaanza kukupa fikira fupi kuhusu ghaibu ndogo.62

Hakika ghaibu ndogo huelezea kipindi cha mwanzo cha uimamu wa kiongozi mwenye kungojewa (a.s.), Imam huyu alipangiwa kuwa asionekane kwa watu wote tangu atakapochukua uimamu na aendelee kuwa mbali na matukio kwa jina lake japokuwa yupo karibu nayo kwa moyo wake na akili yake.

Ilionekana kuwa iwapo ghaibu hii ikija ghafla basi italeta tatizo kubwa kwa raia juu ya uimamu ndani ya umma wa kiisilamu kwa sababu raia hawa walikuwa wamezoea kuwasiliana moja kwa moja na Imam ndani ya kila zama, wakiamiliana naye na kurejea kwake katika utatuzi wa matatizo mbalimbali, hivyo iwapo Imam ghafla akiwa mbali na macho ya wafuasi wake na wakahisi mahusiano yao ya kiroho na kifikra yamekatika, basi ghaibu63 hii itasababisha hisia za ghafla zenye mtik- isiko mkali unaoweza kung’oa jamii nzima na kuifarakisha, hivyo ikawa ni lazima kuandaa mazingira ya ghaibu hii ili raia hawa waun- gane nayo hatua kwa hatua na kuwiana nayo kidogo kidogo kwa kufu- ata misingi yake.

Maandalizi haya yalikuwa ni ghaibu ndogo ambayo Imam humo aliji- ficha dhidi ya mazingira ya watu wote isipokuwa daima alikuwa na mawasiliano na wafuasi wake kwa njia ya mawakili wake na manaibu wake na waaminifu miongoni mwa maswahaba zake ambao wanatengeneza kiungo kati yake na watu wanaoamini njia yake ya uimamu.64

Kituo hiki cha unaibu wa Imam zama hizi za ghaiba ndogo kilikuwa chini ya manaibu wanne ambao raia wote wamekongamana juu ya uchamungu wao, udhibiti wao na usafi wao walioishi nao. Na wao ni kama ifuatavyo:

• Uthman bin Said Al-Amri Muhammad bin Uthman Al-Amri Abul Qasim Husein bin Ruh

• Abul Hasan Ali bin Muhammad As-Sumriy

Hawa wanne65 walifanya jukumu hili la unaibu kwa utaratibu huo uliota- jwa, kila alipofariki mmoja mwingine aliyefuata alichukua nafasi yake kwa kuainishwa na Imam Mahdi (a.s.).

Naibu alikuwa akiwasiliana na wafuasi na kupeleka maswali yao kwa Imam na kumpelekea matatizo yao na huku akibeba majibu yake kwao kwa mdomo na mara nyingine kwa maandishi.66 Hivyo jamuhuri iliyokuwa haimuoni Imam ikawa imepata pole na kifuta machozi kwa njia ya barua hizi na mawasiliano haya yasiyokuwa ya moja kwa moja. Saini zote na barua zote zilizokuwa zikitoka kwa Imam Mahdi (a.s.) zilikuwa za hati moja ya namna moja67 muda wote wa manaibu wote wanne ambao ulidumu kipindi cha miaka sabini.

As-Sumriy ndiye aliyekuwa naibu wa mwisho, hivyo alitangaza kumalizika kipindi cha ghaibu ndogo ambacho kilijitofautisha kwa kuwa na manaibu maalumu na hapo ikaanza ghaibu kubwa ambayo haina watu maalumu walioainishwa kwa ajili ya ukiungo kati ya Imam kiongozi na wafuasi wake.

Mabadiliko ya kutoka kwenye ghaibu ndogo hadi ghaibu kubwa yameelezea jinsi ghaibu ndogo ilivyofanikiwa kutimiza malengo yake na jukumu lake kukamilika kwa sababu kitendo hiki cha hatua kwa hatua kiliwazuia wafuasi dhidi ya hisia za ghafla zenye mtikisiko mkali wa kutokwa na Imam kwa sababu ya ghaibu na hivyo ikafaniki- wa kuandaa mazingira ya wafuasi kulingana na ghaibu na kuwazoesha kidogokidogo ili waipokee fikira ya unaibu usio maalumu wa Imam.

Na kwa ajili hii unaibu ulibadilika kutoka kwa watu maalumu waliotangazwa kwa nasi68 mpaka kuwa ni mfumo wa watu wote,69 nao ndio mfumo wa Mujtahid mwadilifu mjuzi wa mambo ya dunia na dini, hiyo ni kutokana na kubadilika ghaibu ndogo na kuwa ghaibu kubwa.

Na sasa unaweza kuchukua msimamo kutokana na maelezo yaliyotan- gulia ili uweze kutambua kwa uwazi kabisa kuwa Mahdi ni ukweli mtupu walioishi nao baadhi ya watu, na manaibu na mabalozi wakau- tambulisha muda wa miaka sabini kupitia muamala wao na watu wengine.

Muda wote huu hakuna mtu yeyote aliyeona kwao mchezo mchafu katika maneno, au ujanja fulani katika hilo au dosari zozote katika nukuu, sasa je unadhani uongo unaweza kudumu miaka sabini na watu wanne wakautumia kwa namna moja tena kwa kufuatana mmoja baada ya mwingine na wote wakiwa wameafikiana juu yake? Na isitoshe waendelee kuutumia kana kwamba ni kadhia wanayoishi nayo wao wenyewe na kuiona kwa macho yao bila kutokea kitu chochote kina- chozua shaka, na bila ya kuwa na uhusiano maalumu wa pekee kati ya wanne unaotoa fursa ya kula njama ya kukubaliana, na huku kutokana na mwenendo wao wanapata sifa ya watu kuwaamini wao wenyewe na kadhia yenyewe wanayodai kuwa wanaiona na kuishi nayo?!

Kuna usemi: Njia ya mwongo ni fupi, na hata mantiki ya maisha inathibitisha hilo kuwa ni muhali kivitendo kwa mujibu wa hesabu za matarajio uongo kudumu kwa namna hii na kwa muda wote huu na ndani ya mahusiano kama hayo ya kuchukua na kutoa, kisha upate kuaminiwa na wote wanaouzunguka.

Hivyo tunatambua kuwa hali ya ghaibu ndogo tunaweza kuichukulia kama uzoefu wa kivitendo ili kuthibitisha hali halisi ya maudhui husi- ka na kumkubali Imam kiongozi kuanzia kuzaliwa kwake, uhai wake, ghaibu yake70 na tangazo lake kuu kuhusu ghaibu kubwa ambayo kwa mujibu wake amefichwa mbali na mazingira ya watu na wala hajajifichua kwa yeyote.7172

 • 1. Usulul-Kafiy 1: 327, kitabu cha hoja, mlango wa kielelezo na maelezo kwa mwenye nyumba.
 • 2. Usulul-Kafiy 1: 327, kitabu cha hoja, mlango wa jina la aliyemwona (a.s.).
 • 3. Kamalud-Dini 2: 424, mlango wa 42.
 • 4. Man’huwa Al-Mahdiy cha A Abu Talib Tajlil At-Tabrizi: 460 – 506.
 • 5. Kamalud-Dini 2: 442, na imepokewa kutoka kwake ndani ya kitabu Biharul- An’war 52: 30, mlango wa 26.
 • 6. Al-Irshad cha Sheikh Al-Mufid 2: 336.
 • 7. Difau Anil-Kulayniy 1: 567 – 568, cha Hasan Hashim Thamir Al-Amidiy.
 • 8. Ilzamun-Naswibu Fiithbatil-Hujatil-Ghaib cha Sheikh Ali Al-Yazdi Al-Hairiy 1: 321 –
  440.
 • 9. Al-Mahdiyyu Al-Muntadhar Finahjil-Balagha cha Sheikh Mahdiyyu Faqihi Iymaniy: 16 – 30.
 • 10. Al-Imam At-Thani Ashar cha Sayyid Muhammad Said Al-Musawiy: 27 – 70. Muhakiki wa kitabu hiki pambizoni mwa kitabu amekusanya wapokezi thelathini wa kisunni waliompita mwandishi. Angalia pambizoni mwa kitabu husika: 72 – 89. Al-Mahdiyyu Al-Maw’udu Al-Muntadhar Indaahlis-Sunah Wal-Imamiyah cha
  Sheikh Najmud-Dini Al-Askari 1: 220 – 226.
 • 11. Difau Anil-Kafiy 1:568.
 • 12. Tazama Usulul-Kafiy 1: 421, kitabu cha Hoja, mlango wa mazazi ya Abu Muhammad Hasan bin Ali (a.s.). Kamalud-Dini 1: 40 kwenye utangulizi wa mwandishi. Al-Irshad 2: 321. Iilamul-Waraa Biaalamil-Huda cha Al-Fadhlu bin Hasan At-Tabari: 357. Tazama Kamald-Dini 2: 375, mlango wa 43 aliyemwona Al-Qaimu (a.s.).
 • 13. Sura Maryam: 12.
 • 14. As-Swawaiq Al-Muhriqah: 256, Darul-Kutubi Al-Ilmiyah.
 • 15. Al-Fusulul-Muhimmah cha Ibnu As-Swabagh Al-Malikiy: 253. Al-Irshad cha
  Sheikh Al-Mufid 2: 274 na ufuatao.
 • 16. At-Tatimah Fitawarikhil-Aimah cha Sayyid Tajud-Din Al-Amiliy mwanazuoni wa karne ya kumi na moja hijiriya, kilisambazwa na taasisi ya Al- Biithah ya huko Qum takatifu. Pia rejea As-Swawaiq Al-Muhriqah cha Ibnu Hajar: 312 – 313, pale anapotaja baadhi ya karama za Imam na mwenendo wake.
 • 17. At-Tatimah Fitawarikhil-Aimah cha Sayyid Tajud-Din Al-Amiliy mwanazuoni wa karne ya kumi na moja hijiriya, kilisambazwa na taasisi ya Al-Biithah ya huko Qum takatifu. Pia rejea As-Swawaiq Al-Muhriqah cha Ibnu Hajar: 312 – 313, pale anapotaja baadhi ya karama za Imam na mwenendo wake.
 • 18. Al-Irshad cha Sheikh Al-Mufid 2: 281 na ufuatao. As-Swawaiq Al-Muhriqah: 312 – 313. Ameleta kisa cha mazungumzo yaliyotokea baina ya Imam Al-Jawad na Yahya bin Aktham zama za Al-Maamun, na kuonyesha jinsi gani Imam (a.s.) alivyoweza kuthibitisha ujuzi wake wa kielimu na uwezo wake wa kumfumba mtu mdomo, ilihali Imam akiwa badi na umri mdogo.
 • 19. Rejea Al-Majalis As-Saniyyah cha Sayyid Al-Amin Al-Amiliy 2: 468, kisa hiki ni mashuhuri kimenukuliwa na Sunni na Shia. Rejea Sahahul-Akhbar cha Muhammad Sirajd-Dini Ar-Rifaiy: 44, amenukuu kutoka kwenye kitabu Imam As- Sadiq Wal-Madhahib Al-Arbaah cha Asad Haydar 1: 55. Amesema Ibnu Hajar ndani ya kitabu chake As-Swawaiq Al-Muhriqah kuwa: “Jafar As-Swadiq, watu walinikuu kutoka kwake elimu ambazo zilibebwa misafara na misafara na sauti yake ikaenea miji yote. Maimamu wakubwa kama vile Yahya bin Said, Ibnu Jariji, Malik Sufiyani wawili, Abu Hanifa, Shaabah na Ayubu As-Sakhtiyaniy wote wamepokea kutoka kwake….”
 • 20. Sula la Imam kuwa mjuzi kuliko watu wote wa zama zake ni suala linalokubaliwa na Shia imamiya wote, rejea kitabu Al-Babu Al-Hadi Ashara cha Al-Allamah Al-Hiliy: 44, kuna mitihani mingi waliyofanyiwa maimamu ili kuthibitisha dai hili na hatimaye walifaulu. Rejea As-Swawaiq Al-Muhriqah cha Ibnu Hajar: 312, yeye katika suala hili kanukuu kwa upana zaidi katika kisa cha Yahya bin Aktham na Imam Al-Jawad (a.s.).
 • 21. Hakika imani ya uimamu wa maimamu uliwagharimu wafuasi wao gharama ghali, na hili ni suala lililothibiti ndani ya historia na wala hamna njia ya kulikanusha, na lililopo huthibitisha lisilokuwepo. Rejea kitabu Muqatilu At- Talibina cha Abul Farji Al-Asbahaniy.
 • 22. Maimamu waliwausia hilo wafuasi wao kama riwaya nyingi zisemavyo. Rejea kitabu Usulul-Kafiy 1: 392, kitabu cha hija, mlango wa “wajibu wa watu pindi wanapomaliza kutekeleza ibada zao ni kuja kwa Imam na kumuuliza maswala mbalimbali juu ya dini yao na kumtambulisha mapenzi yao na utawal- ishaji wao kwake.”
 • 23. Isharatu Ilal-Imam Al-Mahdi.
 • 24. Yaani ni lazima awe mbora kuliko watu wote na mjuzi kuliko watu wote kama inavyoaminiwa na Shia Imamiya.
 • 25. Anakusudia kuwa kule kushindwa kumjaribu Imam mbele za watu ili kudhi- hirisha hali yake halisi.
 • 26. Sura Maryam: 12.
 • 27. Bahthu Hawlal-Mahdi cha Sayyid As-Shahid: 93 – 99, uhakiki wa Dk. Abdul Jabarah Shararah. Baadhi ya mashia wapenzi wa karibu walimwona Imam Mahdi na wakawasiliana naye na wakapokea kutoka kwake kama ilivyokuwa kwa njia ya mabalozi wanne. Rejea kitabu Tabsiratul-Waliy Fiman’raa Al-Qaim Al-Mahdi cha Al-Bahraniy. Pia rejea Al-Irshad cha Sheikh Al-Mufid: 345. Rejea kwa undani zaidi kitabu Ad-Difau Anil-Kafiy cha Sayyid Thamir Al-Amidi 1: 535 na ufuatao.
 • 28. Chunguza kwa makini, anachodai ni kuwa inawezekana kielimu lakini haija- tokea kivitendo, ukweli ni kuwa majaribio mengi ya anga na kufika kwenye sayari na viambata vingine vya ardhi ni mambo yaliyotimia mwishoni mwa karne ya ishirini.
 • 29. Ndio, hakuna kigezo cha kielimu kinachokataa nadharia hii, bali ni kuwa wasomi wa tiba hivi sasa wanajishughulisha sana kutaka kurefusha umri wa mwanadamu na mpaka sasa kuna majaribio mengi yamefanywa katika hili. Kitendo hicho ni dalili tosha yenye nguvu ithibitishayo uwezekano wa kielimu.
 • 30. Jaribio hili linasisitizwa sana na matabibu na masomo ya tiba na wao wana ushahidi mbalimbali katika suala hili, na huenda suala hili ndilo lilolowasukuma kufanya majaribio ya kurefusha umri wa kawaida wa mwanadamu, na kama inavyozoeleka kuwa jaribio la kwanza huwa ni kuwafanyia wanyama kwani ni rahisi kwao, na hakuna kizuizi kinachozuia kufanya jaribio hilo kwa mwanadamu.
 • 31. Maswali haya anayoyatoa Sayyid Shahid yanalenga kuimarisha ukweli muhimu nao ni kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anapombashiri Mahdi na hali isiyokuwa ya kawaida kwa wanadamu basi ndani ya utabiri huo anatoa habari za maelezo ambayo tayari yameshatangulia yaliyotimia kwa uwezekano wa kiviten- do baada ya kusisitiza uwezekano wa kielimu. Yaani kitendo cha mwanadamu kubakia muda mrefu usiokuwa wa kawaida tayari kimeshaelezwa na Qur’an na Hadithi tukufu sehemu nyingi katika masuala ya kifizikia, ulimwengu na uhai. Rejea kitabu Al-Qur’an Wal-Ilmi Al-Hadith cha Dk. Abdur-Razaq Nawfal.
 • 32. Anaashiria kuwa hii ni aina pia ya muujiza nao ni kipawa maalumu kutoka kwa Mola, na jambo hili mwisilamu hawezi kulikanusha baada ya Kitabu kituku- fu kuzungumzia jambo kama hilo na hasa Qur’an kama ilivyozungumzia umri wa Nabii Nuhu na mambo mengine ya aghaibu. Zaidi ya hapo masunni wengi watawa na wanairfani wanaamini kuwa karama na miujiza huwatokea mawalii, wachamungu na watu wakaribu na Mola. Rejea At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5: 228, kitabu cha utawa.
 • 33. Anaashiria kauli ya Mwenyezi Mungu: “Utukufu ni wake ambaye alimpeleka mja wake usiku kutoka Msikiti mtukufu mpaka Msikiti wa mbali…” Sura Al-Israi.
 • 34. Anaashiria hali ya hewa angani na urefu wa masafa tokea ardhini na kuyaka- ta kwa muda wa masaa mengi au siku nyingi. Mambo haya yamedhihiri zama zetu hizi mwishoni mwa karne ya ishirini.
 • 35. Anaashiria jukumu la mabadiliko aliloandaliwa Imam Mahdi (a.s.) katika kiwango cha ubinadamu kama isemavyo haditihi tukufu: “Ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhuluma na ujeuri.” Na jukumu hili wameafikiana kwalo Wanachuoni wote wa kiisilamu. Ama tofauti zilizopo ni kwenye baadhi tu ya vipengele visivyokuwa vya asili, na kuanzia hapa swali alilolitoa Sayyid Shahid limekuwa ni la kimantiki sana.
 • 36. Aya tukufu: “Na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini..” Sura Ankabuti: 14.
 • 37. Swali linaelekezwa kwa waisilamu wanaoamini Qur’an na Hadithi tukufu. Wanachuoni wa kisunni wamepokea umri mrefu zaidi ya huo kwa asiyekuwa Nuhu. Rejea kitabu Tahdhibul-Asmai Wallughati cha An-Nawawi 1: 176, wala haifai mtu kujenga hoja kuwa hilo la Nuh limeelezwa na Qur’an kwa uyakinifu na pia linamuhusu Nabii aliyetumwa Nuhu (a.s.), ama hapa kwa Mahdi hatuna nassi yakinifu wala jambo linalohusiana na Mtume.
  Jibu: Kwanza, hakika jukumu ni moja nalo ni kuondoa dhuluma na ufisadi, kama ambavyo jukumu alikabidhiwa Nabii vilevile hapa jukumu amekabidhiwa yule mteule wa Mola mtukufu kama riwaya sahihi zisemavyo. Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Hata kama dunia haitobakiwa ila na siku moja basi ni lazima Mwenyezi Mungu atairefusha siku hiyo mpaka amlete mtu kutoka watu wa nyum- ba yangu atakayeijaza ardhi usawa na uadilifu….” At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5:343.
 • 38. Yaani suala hilo linakuwa muujiza, nalo limezungumzwa na Qur’an na Sunna sahihi. Muujiza ni ukweli ulioambatana na wito wa manabii na dai lao la kuwa mabalozi wa Mola, nalo ni jambo asiloweza mwisilamu kulikanusha au kulitilia shaka, bali hata asiyekuwa mwisilamu hushirikiana na mwisilamu katika kuamini miujiza.
 • 39. Sura Anbiyai: 69.
 • 40. Anaashiria kauli ya Mwenyezi Mungu: “Mara tulimpelekea Wahyi Musa: Piga bahari kwa fimbo yako. Mara ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mwamba mkubwa.” Sura Shuaraa: 63.
 • 41. Anaashiria kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na wala hawakumuua wala hawakumsulubu, lakini alifananishwa kwao…”. Sura Nisaa: 157.
 • 42. Rejea Sirat Ibnu Hisham 2: 483, amenukuu tukio hili.
 • 43. Amefafanua kauli hii kunako suala hii ndani ya kitabu chake Falsafatuna: 295 na 299 rejea huko.
 • 44. Rejea kitabu Falsafatuna: 282 na ufuatao
 • 45. Rejea ufafanuzi wa nadharia hii ndani ya kitabu Al-Ususu Al-Mantiqiya Lil- Istiqrai cha Sayyid Shahid As-Sadri (q.s.), humo Imam kafanikiwa kufichua umuhimu na hatari kwa mujibu wa nadharia ya maarifa kwa ujumla.
 • 46. Ni uchambuzi uliotokana na uchambuzi wa kitabu Bahthu Hawlal-Mahdiy cha Sayyid Shahid As-Sadri (q.s.): 65 – 80, uhakiki na maelezo ya Dk. Abdul Jabbar Shararah.
 • 47. Yanabiul-Mawaddah 3: 296, mlango wa sabini na nane.
 • 48. Yanabiul-Mawaddah 3: 297, mlango wa sabini na nane.
 • 49. Yanabiul-Mawaddah 3: 310, mlango wa 80
 • 50. Yanabiul-Mawaddah 3: 386, mlango wa 94
 • 51. Yanabiul-Mawaddah 3: 397
 • 52. Shubhat Warudud, mzunguko wa nne: 32.
 • 53. Man’huwal-Mahdiy: 460.
 • 54. Al-Mahdiy: 149 cha Sadrud-Din As-Sadri.
 • 55. Yanabiul-Mawaddah 3: 315 – 317.
 • 56. Is’afur-Raghibina: 157.
 • 57. Is’afur-Raghibina: 227.
 • 58. Yanabiul-Mawaddah 3: 352, mlango wa themanini na saba.
 • 59. Yanabiul-Mawaddah 3: 352, mlango wa themanini na saba.
 • 60. Yanabiul-Mawaddah 3: 352, mlango wa themanini na saba.
 • 61. Al-Mahdiy: 146 – 148.
 • 62. Rejea kitabu Al-Ghaybatu As-Sughra cha Sayyid Muhammad As-Sadri, amechambua kwa upana zaidi.
 • 63. Anaashiria ghaibu kubwa.
 • 64. Rejea Tabsiratul-Waliy Fimanraa Al-Qaim Al-Mahdiy cha Sayyid Hashim Al-Bahraniy. Difau Anil-Kafiy cha Sayyid Thamir Al-Amidiy 1: 568 na ufuatao.
 • 65. Rejea wasifu wa hawa wanne ndani ya kitabu Al-Ghaybatu As-Sughra cha Sayyid Muhammad As-Sadri, sehemu ya tatu: 395, kimesambazwa na Darutaaruf Lilmatbuati Bayrut 1980.
 • 66. Tahriri hizi hujulikana kwa jina la ‘Tawqiati”, nazo ni majibu ya maandishi na ya mdomo ambayo yalinukuliwa kutoka kwa Imam Mahdi (a.s.). Rejea kitabu Al- Ihtijaj cha Tabarasiy 2: 523 na ufuatao.
 • 67. Kilichomakinika kwa wanafasihi wa sasa na wazamani ni kuwa “Mfumo ndio mtu mwenyewe” kauli hii ni sahihi. Kuanzia hapa ndio maana tumeona na kusikia kuwa wanafasihi wengi na wanamashairi kwa kusoma tu msitari wa shairi au nathari hutambua kuwa ni la nani au ni la fulani, si kwa chochote ila ni kwa sababu mfumo ndio mtu mwenyewe. Na kuwa kila mwandishi ana alama na chapa maalumu katika maandishi yake ambayo kwayo unaweza kumtofautisha na mwingine, ukiachia mbali kuwa hati ya mtukufu (a.s.) inatofautiana na hati nyingine.
 • 68. Anaashiria manaibu wanne waliotajwa.
 • 69. Kiistilahi unaitwa “Marejeo makuu ya kidini” na hapa zinaonekana sifa ambazo Shahid anaona ni lazima mtu awe nazo ili afae kuwa marejeo makuu ya kidini.
 • 70. Imam Mahdi kukutana na wafuasi wake kwa njia ya manaibu wake na mawakala wake au kwa njia nyinginezo mbalimbali ni ukweli wa kihistoria ambao hauna njia ya kukanushwa, ukiachia mbali dalili nyingine nyingi zina- zotegemea utoaji habari wa yule ambaye ni lazima kumsadikisha. Kisha suala hili ni muktadha wa Hadithi mutawatiri kama vile Hadithi isemayo: “Atakayefariki huku hamjui Imam wa zama zake basi amekufa kifo cha kijahiliya.” Na nyingine- zo, nazo zinakubalika na makundi mengi ya kiisilamu, hizo zote zinabatilisha shaka za wenye kushakia uwepo wa Imam Mahdi na kuendelea kwake kuishi. Rejea kitabu Al-Ghaybatu As-Sughra cha Sayyid Muhammad As-Sadri: 566.
 • 71. Kuna Tawqii tukufu ya Imam Mahdi (a.s.) inayoonyesha kuwa hatoweza kuonekana waziwazi baada ya ghaibu kubwa, suala hili Shia Imamia wote wamekongamana juu ya hilo. Rejea kitabu Munaqashatul-Mas’alah Fil- Ghaybatus-Sughra cha Sayyid Muhammad As-Sadri: 639 na ufuatao.
 • 72. Bahthu Hawlal-Mahdi: 108 – 111, uhakiki na maelezo ya Dk. Abdul Jabbar Shararah.