read

Sura Ya Tatu

Umuhimu wa uwelewa wa wazo la Mahdi kiakida katika madhehebu ya Ahlul-Bait

Akida yoyote sawa iwe ya kidunia ambayo chanzo chake huwa ni mwanadamu mwenyewe au iwe ya kimola ambayo chanzo chake ni Mwenyezi Mungu mtukufu ni lazima iwe na maana ya kibinadamu, hivyo ikiwa ni ya kidunia basi huwa imetokana na mazingira ya mwanadamu na huwa inaonyesha kuelimika kwake na shauku yake ya kutaka kufikia maisha bora zaidi.

Na kama ni ya kutoka kwa Mola basi yenyewe huonyesha rehema za Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu na jinsi anavyompenda na kuwa na pupa ya kutaka kumfikisha kwenye ufukwe wa mafanikio. Hili ndilo analoliamini kwa yakini muumini katika msingi wa akida ya kiisilamu, hiyo ni sawa maana hii ya kibindamu iwe wazi kwake kwa ufafanuzi au vipengele vyake viwe bado ni muhtasari vikiwa vimeji- ficha ndani.

Mwanadamu huamiliana na akida mara kiakili kwa hoja na dalili na mara nyingine kimaada kulingana na jinsi akida hizi zinavyomtimizia malengo yake na kumfanikishia na kutatua matatizo ya mwanadamu katika maisha yake ya kila siku. Akida hizi vyovyote vile zitakavyokuwa wazi na timilifu kihoja na kidalili lakini bado kutoeleweka kwake kwa upande wa mwanadamu huzifanya zishakiwe na kutiliwa wasiwasi, au kwa uchache huwa ni nukta isiyo na msuku- mo na isiyokuwa na mwangaza ndani ya nafsi ya mwanadamu.

Akida ya kiisilamu ni kama akida nyingine za kutoka kwa Mola hatu- taraji kuwa zitafafanua malengo yake ya kibinadamu kwa undani zaidi

kwa sababu ufafanuzi wa ndani zaidi hupelekea kutilia umuhimu upande wa maada katika utu wa mwanadamu na hivyo kupingana na msingi wa akida unaoonekana waziwazi upande wa kiakili huku uki- tilia umuhimu upande wa kiroho katika utu wa mwanadamu, hivyo kwa kawaida inapasa akida hii ikomee kubainisha malengo yake ya kibinadamu kwa kiwango cha chini na kwa muhtasari, kama kauli ya Mwenyezi Mungu: “Nasi hatukukutuma ila uwe rehema kwa walimwengu.”1

Lakini wakati huohuo mwanadamu muumini kwa kuzama kiakili na kimazingatio ndani ya matokeo anaweza kufanikiwa kupata hekima inayotarajiwa na malengo ya kibinadamu ya ndani zaidi yanayotaraji- wa kwenye nyanja mbalimbali za kiakida na kisharia toka ndani ya Uislamu.

Sisi tumechambua suala la wazo la Mahdi upande wa dalili na hoja, na imetubainikia kuwa uwelewa wa wazo la Mahdi kwa madhehebu ya Ahlul-Bait ukilinganisha na uwelewa wa wazo la Mahdi kwa madhe- hebu ya madhehebu manne kwa upande wa dalili na hoja basi hulifik- isha suala hili kwenye kiwango chake cha ukamilifu na utimilifu.

Ukamilifu wake upande wa kiakida na dalili unatulazimisha na kutupelekea kuamini ukamilifu wake katika yale unayompa mwanadamu. Tofauti ambayo inapelekea mara nyingi kushakia na kuzua utata kuhusu uwelewa wa wazo la Mahdi kwa upande wa Ahlul-Bait ina- tokana na hawa kutokutazama upande wa dalili na hoja, kiasi kwamba wanatilia umuhimu upande wa kibinadamu ambao unawafanya waji- ulize: Ni faida ipi inayotokana na kuamini uwelewa wa wazo la Mahdi wenye maana zisizo za kawaida kama vile ghaiba, umri mrefu na uimamu wa mapema?

Wanaposhindwa kufikia jibu lenye kutosheleza na huku upande wa kibinadamu wa uwelewa huu ukiendelea kuzingirwa na giza na utata hupelekea kutoutambua uwelewa huo. Na kule kushindwa kwao kusawiri uelewa huu huwapelekea kukanusha uelewa huu na kuushutumu kuwa ni upenzi wa kupindukia na kitu kisicho na uwepo, na sehemu yake huleta uwelewa mwingine mbadala kuhusu wazo la Mahdi usiokuwa na vipengele hivi na wala usiohitaji ghaibu kubwa.

Wanafanya hivyo bila kujua kuwa kwa kitendo chao hiki wao wame- toka kwenye ukamilifu na kuingia kwenye upungufu na kuwa kupinga kwao vipengele hivi vya ughaibu ni kupinga johari yenye thamani ya uwelewa wa wazo la Mahdi ndani ya Uislamu, ukiachia mbali kule kupingana kwake na upande wa mantiki ambao katika mlango wa akida unalazimisha kufuata dalili na hoja popote vitakapoelekea, na wala si kuvipinga kwa kufuata hatinafsi, malengo na itikadi binafsi.

Laiti wangetuliza akili ndani ya uwelewa wa Ahlul-Bait kuhusu Mahdi (a.s.) wangeukuta upande wa kibinadamu ni kamilifu kuliko uwelewa wa madhehebu ya Sunni kuhusu wazo hilo.

Sayyid As-Shahid Muhammad Baqir As-Sadri amechukua jukumu la kubainisha upande huu ubainifu mzuri akaandika akisema:2 “Hivi sasa tunazungumzia swali la pili, nalo linasema: Kwa nini mwenyezi Mungu amjali sana mwanadamu huyu, hadi kanuni za kifizikia zisi- tishwe ili kurefusha umri wake? Kwa nini uongozi wa siku hiyo tuliyoahidiwa asiachiwe mtu atakayekuzwa na mustakabali na kuwivishwa na misukosuko ya siku hiyo tuliyoahidiwa na hatimaye abarizi uwanjani na kutekeleza jukumu lake linalongojewa. Kwa lugha nyingine ni kuwa ni ipi faida ya ghaibu hii ndefu na ni upi uhalali wake?

Watu wengi wanauliza swali hili huku wakiwa hawataki kusikia upande wa nguvu za kimola, basi sisi tunaamini kuwa maimamu kumi na wawili ni kundi la kipekee3 haiwezekani kumbadili yeyote mion- goni mwao, isipokuwa hawa wenye kuuliza wanataka ufafanuzi wa kijamii juu ya suala hili kwa mujibu wa mambo ya kimaada kwa ajili ya kazi hii ya mabadiliko makubwa na mahitaji ya uwelewa wa siku tuliyoahidiwa.

Kwa msingi huu tunasitisha kwa muda sifa tunazoamini kuwa hawa maimamu watakasifu wanazo4, na hapa tunatoa swali lifuatalo: Bila shaka sisi tunaelekea kwenye mabadiliko tunayotaraji siku tuliyoahidi- wa kwa namna ambayo unaeleweka kulingana na mwenendo wa maisha na uzoefu wake, sasa je umri huu mrefu wa kiongozi wake aliyetunzwa tunaweza kuuchukulia kuwa ni sababu miongoni mwa sababu za kufanikisha mabadiliko hayo? Na inawezekana kwake kuyatimiza na kuyaongoza kwa kiwango kukibwa zaidi?

Hilo tunalijibu kwa kukubali, hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali, miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Mabadiliko makubwa yanahitaji mazingira ya kisaikolojia ya pekee ya kiongozi mwenye kufanya mabadiliko hayo, mazingira yaliyojaa utambuzi juu ya ushindi na hisia juu ya vilimwengu ambavyo kaandaliwa ili avitokomeze na kuvibadili kiustaarabu na kuvifanya ulimwengu mpya.

Kwa kadiri ambavyo moyo wa kiongozi utakavyojaa utambuzi juu ya uduni wa ustaarabu anaopambana nao na akawa na hisia za wazi kuwa wenyewe ni nukta tupu juu ya msitari mrefu wa ustaarabu wa mwanadamu ndivyo atakavyokuwa na uwezo mkubwa upande wa kisaikolojia5 katika kupambana nao na kusimama imara mbele yake na kuendeleza mabadiliko mpaka ushindi upatikane.

Ni wazi kuwa ukubwa huu wa utambuzi unaohitajika wa kisaikolojia hunasibiana na ukubwa wa mabadiliko yenyewe na ule ukubwa wa jamii na ustaarabu anaotaka kuuteketeza, hivyo kila mapambano ya jamii yanapokuwa makubwa na ustaarabu imara na mzito ndivyo unavyohitaji asilimia kubwa zaidi ya utambuzi huu wa kisaikolojia.

Na kwa kuwa ujumbe wa siku tuliyoahidiwa ni wa kuubadili ulimwen- gu uliojaa dhuluma na ujeuri mabadiliko yaliyojumuisha kila ustaarabu wa thamani na miundo yake mbalimbali basi kwa kawaida ni lazima ujumbe umtafute mtu mwenye utambuzi mkubwa wa kisaikolojia
kuliko huo ulimwengu wote, mtu ambaye si katika vizazi vya ulimwengu huo ambavyo vimekulia ndani ya ustaarabu huo ambao anataka kuutokomeza na kuubadili kwa ustaarabu wa uadilifu na haki. Kwa sababu anayekulia ndani ya ustaarabu imara uliyojaa dunia kwa utawala wake na thamani yake na fikra zake huwa anaishi akiwa na uoga ndani ya nafsi yake mbele ya ustaarabu huo kwa sababu yeye kazaliwa ukiwa umesimama, akakuwa ukiwa imara na akafumbuwa macho yake juu ya dunia bila kukuta chochote ila nyanja mbalimbali za ustaarabu huo.

Hali hiyo ni kinyume na mtu aliyekulia ndani ya historia, ameishi duni- ani kabla ya ustaarabu huo kuiona hiyo nuru, ameona ustaarabu wa namna mbalimbali ulio mkubwa uliotawala ulimwengu mmoja baada ya mwingine kisha ukatoweka,6 ameona hayo kwa macho yake na wala si kwa kusoma ndani ya vitabu vya historia.

Kisha akaona ustaarabu ambao unakadiriwa kuwa ndio sehemu ya mwisho ya kisa hiki cha mwanadamu kabla ya siku iliyoahidiwa, ameuona ukiwa bado punje ndogo iliyongumu kuonekana, kisha akau- tazama ukiwa tayari umeshachukua nafasi yake ndani ya jamii ya mwanadamu ukisubiri fursa ili uchipue na kudhihiri

Kisha akaishi nao zama moja ukiwa umeshaanza kuchipua na kutam- baa huku mara ukianguka na mara nyingine ukufanikiwa kwa taufiki. Kisha akauongoza huku ukistawi, ukijikita na kumiliki nguvu yote ya ulimwengu kwa ukamilifu kidogokidogo, hakika mwanadamu kama huyu aliyeishi ndani ya hatua zote hizi kwa akili na uangalifu kamili

huitazama nguvu hii anayotaka kuitokomeza kwa mtazamo wa msa- fara wa historia hiyo ndefu ambayo ameishi nayo na akaishuhudia na si kwa mtazamo wa yaliyomo ndani ya vitabu vya historia tu.

Haitazami kama nguvu ya mwisho na wala haitazami kama John Jack Rusuw7 alivyokuwa akiutazama ufalme wa Ufaransa, imepokewa kuwa kitendo tu cha kuiwaza Ufaransa kilikuwa kikimtetemesha hata bila kuangalia ufalme, japokuwa alikuwa miongoni mwa wanaharakati wa kifikra na kifalasafa waliokuwa wakililia uboreshaji wa mazingira ya kisiasa zama hizo; hiyo ni kwa sababu huyu Rusuw alikulia ndani ya ufalme na akavuta pumzi yake muda wote wa uhai wake.

Ama mwanadamu huyu aliyebobea ndani ya historia yeye ana haiba ya historia, nguvu ya historia na utambuzi zaidi kuwa jamii na ustaarabu unaomzunguka ni matokeo ya siku moja miongoni mwa siku za histo- ria, kuna sababu zilizoandaliwa ndipo ukapatikana, na kuna sababu zitaandaliwa utatoweka na hivyo hautobakiwa na chochote kama ambavyo juzi na majuzi haukuwa na chochote, na kuwa vyovyote utakavyorefuka umri wa kihistoria wa ustaarabu mbalimbali na jamii mbalimbali lakini wenyewe si chochote ila ni siku chache ndani ya umri mrefu wa historia.

Je, umesoma sura ya vijana wa pangoni? Na je, umesoma kuhusu vijana hao waliomwamini Mola wao Mlezi na Mwenyezi Mungu akawazidishia uongofu?8 Wakakumbana na utawala wa ushirikina uliokuwa ukitawala zama hizo usiohurumia wala kusita kunyonga mbegu yoyote miongoni mwa mbegu za Tawhidi na yenye kujiepushana umoja wa shirki, basi nafsi zao zikaumia na wakapatwa na hali ya kukata tamaa huku madirisha ya matarajio yakifungika mbele ya macho yao, ndipo wakakiwawilia pangoni wakitafuta ufumbuzi wa matatizo yao kutoka kwa Mwenyezi Mungu baada ya ujanja wote kuwaishia huku kitendo cha batili kuendelea kutawala, kudhulumu, kuigandamiza haki na kumteketeza kila aliye na haki ndani ya moyo wake kikizidi kuwauma.

Je, unajua Mwenyezi Mungu aliwafanyia nini? Yeye aliwalaza ndani ya pango hilo miaka mia tatu na miaka tisa9 kisha akawaamsha kuto- ka kwenye usingizi wao huo na kuwapeleka kwenye mapambano ya maisha baada ya kuwa tayari umeshadondoka ule utawala uliowatisha kwa nguvu zake na kuwadhulumu, na historia ikawa haimtishi mtu wala haimtingishi aliyetulia, yote hayo ni ili vijana hawa washuhudie kudondoka kwa batili hiyo ambayo ilikuwa ikionekana kubwa juu yao kuanzia uwezo wake, nguvu yake na kuendelea kwake, na watazame mwisho wake kwa macho yao na ionekane ndogo ndani ya nafsi zao.

Na ikiwa kupitia tukio hilo la kipekee ambalo lilirefusha maisha yao miaka mia tatu mtazamo huu wa wazi ulitimia kwa vijana wa pangoni kwa kila ukubwa na uimara wa kisaikolojia basi ni jambo hilohilo lita- timia kwa kiongozi anayengojewa kupitia umri wake mrefu ambao utamwezesha kuona nguvu hizo zikiwa bado ndogo, mti mrefu ukiwa bado mbegu, na zama nyingi zikiwa bado roho.10

Zaidi ya hapo ni kuwa uzoefu unaoutoa msafara wa ustaarabu huo wenye kufuatana na mapambano ya moja kwa moja ya harakati zake na maendeleo yake una athari kubwa katika kuandaa fikira na kuimar- isha ujuzi wa kiutawala kwa ajili ya siku tuliyoahidiwa, kwa sababu unamweka mwanadamu aliyeandaliwa mbele ya utendaji mwingi wa wengine wenye kila aina ya nukta ya udhifu na uimara, makosa na usahihi na unampa mtu huyu uwezo mkubwa mno katika kutathmini mambo ya kijamii kwa ujuzi kamili juu ya sababu zake na mazingira yake yote ya kihistoria.

Kisha mabadiliko yanayomsubiri kiongozi anayengojewa yanasimama kwa msingi wa ujumbe maalumu nao ni ujumbe wa Uislamu, na kwa kawaida hali hii inahitaji kiongozi wa karibu na vyanzo vya mwanzo vya Uislamu. Ambaye utu wake umejengeka kikamilifu kwa sura ya kujitegemea na ya kipekee iliyojitenga na athari za ustaarabu ambao amekadiriwa kuupiga vita siku hiyo tuliyoahidiwa.

Hali hiyo ni kinyume na mtu ambaye anazaliwa na kukulia ndani ya ustaarabu huu na fikira zake na hisia zake vinafunguka ndani ya mazingira yake, hakika aghlabu hanasuki kutoka kwenye ustaarabu huo na malengo yake hata kama akiongoza mapambano ya mabadiliko dhidi ya ustaarabu huo.

Ili kiongozi aliyehifadhiwa asalimike na ustaarabu huo ambao kaan- daliwa kuubadilisha ni lazima utu wake uwe umejengeka kikamilifu katika kipindi cha ustaarabu uliotangulia ulio karibu mno na roho ya jamii yote na atoke upande wa asili mpaka kwenye hali ya ustaarabu ambao siku tuliyoahidiwa inaelekea kuutimiza chini ya uongozi wake.”11

Kisha mheshimwa (r.a.) baada ya hapo akatoa swali jingine linalohu- siana na upande wa kibinadamu kuhusu akida ya Mahdi, nalo ni: Kwa nini kiongozi wa kiulimwengu hajadhihirika muda wote huu? Na ikiwa tayari ameshajiandaa kwa ajili ya kazi ya kijamii basi ni kitu gani kili- chomzuia kudhihiri kwenye uwanja wa maisha zama za ghaibu ndogo au baada yake badala ya kuigeuza na kuwa ghaibu kubwa?

Jibu ni kuwa: a. Hakika Mtume (s.a.w.w.) kivitendo alikuwa chini ya hali ya kujitenga kikamilifu dhidi ya ustaarabu wa kijahiliya, kama ilivyopokewa ndani ya sira ya Mtume kuwa alikuwa akijipwekesha akienda pango la Hira akikaa huko. Na pia manabii walikuwa wakijiepusha na mazingira ya jamii zao na hivyo kujitenga, na hilo limeashiriwa na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Basi alipojitenga nao na wanayoyaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu, tukampa Isihaka na Yakubu, na kila mmoja tukamfanya Nabii.” Sura Maryam: 49.

b. Hakika Nabii Mtume hupewa wahyi na hupewa nguvu moja kwa moja na Mola na hufikia kazi na hatua anazozichukua hatua kwa hatua, na Imam hapewi wahyi na wala hafikii vitu moja kwa moja kutoka kwa Mola. Ndiyo, yuko chini ya uan- galizi wa Mola hivyo yeye anahitaji maandalizi maalumu, wakati ambao anakuwa karibu na mwenye mahusiano na ustaarabu wa kiisilamu akitegemea baba zake katika asili, elimu na maarifa ni wakati huohuo anakuwa mjuzi juu ya mambo ya wanadamu na ustaarabu, anajua jinsi gani unakua, sababu za kujengeka kwake na kupata nguvu yake, na ni jinsi gani unashuka, sababu za kudhoofika na kuporomo- ka. Hivyo anategemea ujuzi, uwezo na uwelewa wa mambo yote, hali hii ni bila kusahau imani yetu kuwa Imam ana uwezo wa asili wa elimu ambayo Mwenyezi Mungu humtunuku na kupewa nguvu na Mola

Kwani zama hizo mazingira ya kikazi kijamii na kimabadiliko yalikuwa mepesi na rahisi, na mawasiliano yake na watu ya kivitendo kupitia utaratibu wa ghaibu ndogo ulikuwa unampa fursa ya kuku- sanya nguvu zake na kuanza kwa nguvu zote, pia nguvu iliyokuwa ikitawala zama hizo ilifikia kiwango cha chini kuliko nguvu na uwezo ambao amefikia mwanadamu baada ya hapo kupitia maendeleo ya kiteknolojia na kiviwanda.12

Jibu: “Kila kazi ya mabadiliko ya kijamii kufaulu kwake kuna uhu- siono na masharti na mazingira ya kadhia husika, malengo yake haya- timii ila baada ya masharti na mazingira hayo kutimia. Mabadiliko ya kijamii ambayo yanafanywa na Mola aridhini yana sifa ya pekee kwa sababu yenyewe upande wake wa kimola hayana uhusiano na mazin- gira ya kadhia husika,13 kwa sababu ujumbe unaotegemewa na mabadiliko hapa ni wa kimola, lakini upande wa utekelezaji unatege- mea mazingira ya kadhia husika na hivyo kufaulu kwake na wakati wake vina uhusiano na mazingira hayo.

Kwa ajili hiyo Mola alisubiri zipite karne tano za ujahiliya ndipo akateremsha ujumbe wake wa mwisho mikononi mwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kwa sababu mahusiano ya mazingira ya kadhia husika ya utekelezaji yalikuwa yakilazimu kuchelewesha ujumbe huo japokuwa ulimwengu ulikuwa na haja nao tokea muda mrefu kabla ya hapo.

Mazingira ya kadhia husika ambayo yana mchango katika kutekeleza kazi ya mabadiliko baadhi yake hutengeneza hali munasibu na anga kuu kwa ajili ya mabadiliko yanayolengwa, na baadhi yake huten- geneza baadhi ya vipengele ambavyo harakati za mabadiliko zinavihi- taji kupitia kona zake zote.

Kwa mfano kazi ya mabadiliko aliyoyaongoza Lenin huko Urusi na kufaulu ilikuwa na uhusiano na sababu kama vile vita vikuu vya kwan- za vya dunia na kuporomoka kwa utawala wa Kaysari, na hili lilisaidia kupatikana mazingira munasibu ya kazi hii ya mabadiliko. Pia ilikuwa na uhusiano na sababu nyingine ndogo ndogo kama vile kusalimika kwa Lenin mwenyewe katika safari yake ya uficho kuingia Urusi na kuongoza mapinduzi, kwani angepatwa na tukio lolote ambalo lingemzuia basi inatarajiwa kabisa kuwa mapinduzi hayo yangekosa nguvu zake na kutokudhihiri mapema.

Sera ya Mwenyezi Mungu isiyokuwa na mabadiliko katika kazi ya mabadiliko ya kimola imeendelea kuhitaji mazingira ya kadhia husika upande wa utekelezaji, mazingira ambayo hutimiza hali munasibu na anga kuu ili kufanikisha kazi ya mabadiliko, na kuanzia hapa ndipo Uislamu haukuja ila baada muda fulani wa mitume na baada ya kumalizika uchungu ulioendelea muda wa karne nyingi.

Japokuwa nguvu ya Mwenyezi Mungu ilikuwa na uwezo wa kudhalil- isha kila lililo tatizo na gumu mbele ya ujumbe wa Mola, na kuten- geneza hali munasibu kimuujiza lakini hakutaka kutumia njia hii, kwa sababu mtihani, balaa na matatizo ambayo kupitia kwayo mwanadamu hukamilika yanalazimu kazi ya mabadiliko iwe katika hali ya kawaida na ya kikadhia husika kwa upande huu.

Hili halimzuii Mwenyezi Mungu baadhi ya nyakati kuingilia baadhi ya yale yanayohusu vipengele ambavyo huwa si hali munasibu, bali baad- hi ya nyakati harakati uhitajia hilo ndani ya hali hiyo munasibu, na miongoni mwa mahitajio hayo ni msaada na nguvu za ghaibu ambazo Mwenyezi Mungu huwatunuku mawalii wake ndani ya saa ngumu na hivyo kupitia msaada huo uuhami ujumbe.

Ghafla moto unakuwa baridi na salama juu ya Ibrahim,14 mkono wa myahudi ambao uliinua upanga juu ya kichwa cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) unapooza na kukosa nguzu za kufanya kazi,15 ghafla kimbunga kikali kinang’oa mahema ya makafiri na mushirikina ambao waliuzingira mji wa Madina siku ya vita vya Handaki na kutia woga ndani ya nafsi zao,16 isipokuwa haya yote hayavuki vipengele. Kwani kutoa msaada katika saa ngumu baada ya anga kuwa munasibu na hali kulingana na kazi ya mabadiliko kwa ujumla, kunaweza kukawa kwa sura ya kawaida na kwa kulingana na mazingira ya kadhia husika.

Inajulikana kuwa Mahdi hakuwa amejiandaa kwa ajili ya kazi ya jamii fulani wala kwa ajili ya kazi ya mabadiliko inayokomea eneo fulani la ulimwengu na kuacha eneo jingine, kwa sababu ujumbe wake ambao umehifadhiwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili yake ni mabadiliko kamili ya ulimwengu na kuwatoa wanadamu toka kwenye giza la ujeuri mpaka kwenye nuru ya uadilifu.17

Kazi hii ya mabadiliko makubwa utekelezaji wake hauhitajii kupatikana tu ujumbe na kiongozi msuluhishi kwani ingekuwa hivyo masharti yake yote yangetimia tangu zama za utume, bali ni kuwa unahitaji vilevile hali munasibu ya kiulimwengu na anga kuu la kimataifa ambalo litatimiza mazingira ya kadhia husika kwa ajili ya kazi ya mabadiliko ya kiulimwengu.

Hivyo upande wa binadamu inachukuliwa kuwa kile kitendo cha wanadamu kutambua ustaarabu kwa undani ni sababu ya msingi wa kutengeneza mazingira munasibu ili kupokea ujumbe mpya wa uadili- fu, utambuzi huu wa ndani hujengeka na kuimarika kupitia mazoea ya ustaarabu wa namna mbalimbali ambao humo mwanadamu hutoa ustaarabu mpya huku akiwa mzito kutokana na yale yakuachwa aliyo- jengeka kwayo, huku akijua fika haja yake inahitaji msaada na akiita- mbua nguvu ya ghaibu kwa maumbile yake.

Upande wa kimaada ni kuwa huenda masharti ya maisha ya kimaada ya kisasa yakawa na nguvu mno katika kutimiza ujumbe ulimwenguni kote kuliko maisha ya zamani katika kipindi cha ghaibu ndogo, hiyo nikutokana na ukaribu wa masafa, uwezo mkubwa katika kuamiliana na mataifa mbalimbali ya aridhini na kupatikana vifaa na nyenzo ambazo makao makuu inazihitaji ili kupanua uelewa wa mataifa ya ulimwengu na kuyaelimisha kwa msingi wa ujumbe mpya.

Ama kuhusu kile kilichogusiwa katika swali kuwa kila muda wa kud- hihiri kwake unavyozidi kurefuka ndivyo nguvu za kijeshi na vifaa vitakavyopambana na kiongozi siku hiyo tuliyoahidiwa vinavyozidi kukua, kweli hili ni sahihi, lakini ukuaji wa nguvu kimaada zitasaidia nini ikiwa kisaikolojia ndani ya nafsi umeshashindwa, huku nguvu ya kiroho kwa mwanadamu ambaye ndiye anamiliki nguvu hizo na vifaa hivyo imeshasambaratika? Ni mara ngapi ndani ya historia jamii ya ustaarabu wenye nguvu imesambaratika mwanzo tu wa vita kwa sababu tu kabla ya vita hivyo ilikuwa imeshasambaratika kisaikolojia huku ikiwa haijiamini na wala haina matumaini na muundo wake na imekosa imani na hali yake halisi?”18

Pia tunaweza kuzungumzia faida ya kiakida ya wazo la Mahdi kwa mwanadamu katika uwelewa wa Ahlul-Bait (a.s.) kwa upande mwingine. Hivyo tunasema: Itikadi ya kuamini wazo la Mahdi aliyem- bali na macho lakini aliye hai na mwenye kuingilia baadhi ya matukio kwa ajili ya masilahi ya kundi lenye kuamini huku akiwa ana sifa zote za uimamu kuanzia utakaso, nasi ya Mtukufu Mtume na ukamilifu wa kielimu na kivitendo kwa kawaida ni lazima ieneze ndani ya jamii hali ya uimamu huu na nguvu zake za kimaana na kiroho za hali ya juu.

Na ni lazima imshibishe mwanadamu hisia nzuri kwa kule kuendelea kuwepo mahusiano kati ya ardhi na mbingu na mbingu kuendelea kuitunza ardhi na kubadili hali hiyo na kuwa maana zenye kuonekana kivitendo zenye msukumo mkubwa ndani ya nafsi baada ya awali ndani ya misingi yake ya kiakida kuwa ni maana za akilini.

Na ni lazima iimarishe utawala wa Tawhidi ndani ya uwanja wa kijamii na kisiasa na kuufanya ni utawala ulio karibu na hisia ya mwanadamu kwa kutambua kuwa Mahdi aliye ghaibu si mwanadamu wa kawaida bali yeye ni Imam wa kumi na wawili aliyeteuliwa na Mola ili ashughulikie nafasi ya uimamu mpaka mwisho wa historia.

Sahihi watu hawamwoni moja kwa moja kwa milango ya fahamu laki- ni kule kuamini kuwa yeye ni ukweli wa kimaada kunapunguza hamasa ya milango yetu ya fahamu kutaka kumdiriki, inaifanya nafsi iwe katika hali ya kuamiliana kiroho na kiutii na njia ya uimamu uliy- oteuliwa na Mola na uliyo mtakasifu kwa kuzingatia kuwa wenyewe ni maelezo na mwendelezo wa utawala wa Tawhid aridhini.

Muamala huu unazidi zaidi pale Mahdi mtakasifu aliye ghaibu anapo- tolewa maelezo ya kisiasa yaliyo barizi kupitia msingi wa unaibu maalumu ndani ya kipindi cha ghaibu ndogo na msingi wa unaibu wa wote wa Wanachuoni wa sharia ndani ya kipindi cha ghaibu kubwa ambao ni uongozi wa kisiasa wa kisharia wa jamii ya kiisilamu ambao unahifadhi nafasi ya juu ya uimamu kama msimamizi na mwangalizi anayefatilia uzoefu wa kisiasa na kijamii na kuunusuru na kama chem- chemu inayounywesha sharia pale inapoukuta unaafikiana na Uislamu.

Kutokana na mjumuiko wa ubainifu huu inaonekana wazi maana ya ukamilifu inayotolewa na uwelewa wa wazo la Mahdi kwa Ahlul-Bait (a.s.) wa faida za kibinadamu nazo ni faida zinazooana kikamilifu na asili ya wazo la Mahdi, kwani Mahdi mtakasifu aliye ghaibu ni mwenye harakati na mwenye kuleta athari za utii katika hali halisi ya mwanadamu.

Wakati Mahdi ndani ya uwelewa wa masunni hana athari yoyote kati- ka hali halisi ya mwanadamu, naye si chochote zaidi ya habari za mus- takabali. Kana kwamba Mahdi wa Ahlul-Bait (a.s.) anachukua jukumu la kutimiza unayoahidi kupitia msukumo wa hali halisi ya mwanadamu na muamala wa utii pamoja naye.

Suala hili lenyewe ni jambo bora linalofafanua maana ya utii ya uwele- wa wa kungojea, kwani kungojea faraja si kunyamaza na kushindwa bali ni roho ya utii yenye msukumo kuelekea mabadiliko ya Mahdi yanayohitajika.

Matokeo ya uchambuzi

Mwisho wa uchambuzi tunaweza kufupisha matokeo ya uchambuzi kwa nukta zifuatazo:

Hakika dini ni mabadiliko kamili ya uhalisia wa binadamu na Uislamu ni mabadiliko kamili zaidi juu ya uhalisia wa dini na Ushia ni maelezo kamil- ifu zaidi juu ya uhalisia wa Uislamu na hatimaye Mahdi wa Ahlul-Bait (a.s.) ndiye maelezo kamilifu zaidi kuhusu asili ya wazo la Mahdi ambaye waisilamu wote wamekongamana katika kumwamini.

Asili ya tofauti kati ya Mahdi wa Ahlul-Bait na Mahdi wa Wanachuoni wa kisunni inatokana na uimamu, kwani Mahdi kwa madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s.) ndiye Imam wa kumi na wawili (a.s.) wakati kwa upande wa madhe- hebu ya kissuni ni suala la mustakabali lisilokuwa na kitu.

Kwa kuwa suala la Mahdi kwa Ahlul-Bait ni suala la Imam wa kumi na wawili ambaye hakuna tena baada yake Imam basi kuanzia hapa uwelewa wa wazo la Mahdi kwao (a.s.) limekuwa na sifa tatu muhimu: Kuzaliwa Imam kwa siri kulikofichwa, uimamu wa utotoni na ghaibu yake inayolaz-

imu umri mrefu unaolingana na zama. Sifa hizi tatu zimethibiti kwa kuthibiti asili ya uimamu wa maimamu kumi na wawili watakasifu ambao ndio umezaa wazo la Mahdi, ukiachia mbali dalili za wazi ambazo tumes- hazitaja moja baada ya nyingine.

Hakika sifa hizi tatu si tu kwamba zimethibiti kwa dalili za kiakida, kiak- ili na kimaumbile zilizokamilika na si tu kwamba hazihitajii utata wa kiak- ili na kidini, bali vilevile zenyewe ndizo zinazotoa maana ya ukamilifu ya uwelewa wa wazo la Mahdi, na kuufanya uwe ni uwelewa wenye thamani ya kiakida na faida za juu kwa mwanadamu na kufaa zaidi ndani ya jamii, huku ukikamilika na kuoana na faida za msingi wa dini ndani ya maisha ya mwanadamu.

Na mwisho wa dua yetu ni kumshukuru Allah Mlezi wa walimwengu.

 • 1. Sura Anbiyai: 107.
 • 2. Bahthu Hawlal-Mahdi: 83 – 89, uhakiki na maelezo ya Dk. Abdul Jabbar Shararah.
 • 3. Anaashiria imani ya Shia Imamiya inayotegemea dalili za kiakili na za nukuu, na hasa Hadithi mutawatiri ya vizito viwili: “Mimi nimewaachieni viwili ambavyo laiti mkishikamana navyo kamwe hamtopotea baada yangu: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu.” Rejea kitabu Sahih Muslim 4: 1873. Rejea As-Sawaiq Al-Muhriqah cha Ibnu Hajar: 89, amesema: “Kisha tambua kuwa Hadithi ya kushikamana navyo ina njia nyingi za upokezi, imepokewa kutoka kwa maswahaba zaidi ya ishirini.” Na pia anaashiria kauli ya (s.a.w.w.): “Havitoachana mpaka vitakaponikuta kwenye Hodhi…” na kauli yake (s.a.w.w.): “Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili wote ni kutoka kwa maku- rayshi.” Zote hizo zinatengeneza maana hii.
 • 4. Mtukufu Mtume mara nyingi sana amezungumzia sifa zao, mizunguko yao, jukumu lao na kazi yao na kuwa wao ni wabebaji wa sharia, meli za uongofu, amani ya umma na kinga yake dhidi ya upotovu, kama ilivyoelekeza hilo Hadithi ya vizito viwili na Hadithi ya hivyo viwili havitoachana. Zote wawili zinasisitiza utakaso wao, kwani akili haikubali kuwa wao wasiwe watakasifu kisha wao ni kinga kwa umma dhidi ya upotovu na wasiachane na Qur’ani takasifu. Rejea kitabu Usulul-Amma Lil-Fiqhi Al-Muqarin cha Allamah Muhammad Taqiyu Al- Hakim, uchambuzi wa hoja ya Sunna, Uk 169 na unaofuatia
 • 5. Kiongozi wa kihistoria awe ameandaliwa kisaikolojia maandalizi yanayona- sibiana na jukumu husika. Na laiti tukirudi ndani ya Qur’an tukufu tuitaikuta inazungumzia suala hili ndani ya historia ya manabii kwa sura ya wazi zaidi. Na hasa katika yale yanayomuhusu Nabii Nuhu (a.s.) nalo ni jambo linalozindua na kuvutia, na huenda hilo likatokana na kule kushabihiana katika jukumu walilok- abidhiwa, kama alivyonabihi Shahid As-Sadri. Rejea kitabu Maal-Anbiyai cha Afif Abdul-Fatah Tabarah.
 • 6. Maana hii tunaweza kuiona kwenye muungano wa kisovieti jinsi ulivyokua na kustawi mpaka ukawa nguvu ya pili ulimwenguni, wenyewe na Marekani vik- agombania ustaarabu na nguvu ya kisiasa, wote kwa pamoja wakapanda angani na hatimaye tukashuhudia usambaratikaji wa muungano wa kisovieti na misingi yake kuachana kwa kasi ya ajabu. Hilo lina athari kiasi gani? Hilo lina mafunzo kiasi gani? Hilo ni dalili ya kina kiasi gani?
 • 7. John Jack Rusuw (1712 – 1778 A.D.) mwandishi na mfilosofia wa kifaransa, baadhi ya wanafikra wanamchukulia kama mtu mwenye mchango mkubwa katika fasihi ya kifaransa ya kisasa na filosofia mpya. Maandishi yake na makala zake viliandaa mapinduzi ya kifaransa, na kitabu chake maarufu ni Al-Aqdu Al- Ijtimaiy. Rejea kitabu Mawsuatul-Mawridu cha Muniru Al-Baalabakiy 8: 169.
 • 8. Anaashiria Aya ya Qur’an: “Hakika wao ni vijana waliomwamini Mola wao Mlezi, nasi tukawazidishia katika mwongozo.” Sura Al-Kahfi: 13. Rejea tafsri ya Ayah ii ndani ya kitabu Al-Kashaf cha Az-Zamakhshar 2: 706, kilichosambazwa na Darul-Kitabi Al-Arabi – Beirut.
 • 9. Anaashiria Aya: “Na walikaa katika pango lao miaka mia tatu na wakazidisha tisa.” Sura Al-Kahfi: 25.
 • 10. Hayo yote yana mchango katika kumlea na kumwandaa maandalizi maalu- mu ikiwemo kummlikisha mtazamo wa kina kamilifu, ukiachia mbali kile kitendo cha yeye mwenyewe binafsi kushuhudia kufeli kwa hao waliobobea kwenye dunia na kuwatisha watu. Ushahidi huu unamwezesha mara nyingi katika kutekeleza jukumu lake la kiulimwengu katika mabadiliko, yaani kuijaza dunia uadilifu kama utakavyokuwa umejaa dhuluma. Haya yote ni bila kujali uwezo wake wa dhati na msaada maalumu wa Mola.
 • 11. Wala haifai mtu yeyote kuzua utata kuwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) japokuwa ujumbe wake ulikuwa ni wa kiulimwengu na jukumu lake kubwa la mabadiliko isipokuwa yeye aliishi ndani ya mazingira ya ustaarabu wa kijahiliya na wala haukumuathiri, na ndio hali ya manabii waliomtangulia, sasa ni upi ubora wa rai hii?
 • 12. Bahthu Hawlal-Mahdi cha Shahid Muhammad Baqir As-Sadri, rejea ya 89, uhakiki na maelezo ya Dk. Abdul Jabbar Shararah, chapa ya kituo cha Ghadir kwa ajili ya masomo ya kiisilamu.
 • 13. Pamoja na umuhimu huu ambao Shahid As-Sadri ameuandika kuhusu mazingira ya kadhia husika na pia kuhusu mchango wake katika kuivisha na kuandaa mapinduzi mbalimbali ila ni kuwa Shahid As-Sadri anatoa mtazamo mpya katika kufahamu kazi ya mabadiliko ya kijamii yanayoletwa na Mola kupi- tia ujumbe Wake kuwa, upande wake wa kiujumbe yana uhusiano wake maalumu lakini upande wa utekelezaji yanategemea mazingira ya kadhia husika na hivyo yanahusiana nayo kiwakati na kiufaulu. Tunaposema mazingira ya kadhia husika tunamaanisha kuwa ni hali ya kisiasa na hali ya kijamii ya umma na hali halisi ya dola za wakati huo na kiwango cha nguvu za umma katika uwezo wake binafsi na maandalizi yake ya kisaikolojia.
 • 14. Anaashiria kauli ya Mwenyezi Mungu: “ Wakasema: Mchomeni na muiokoe miungu yenu ikiwa nyinyi ni wenye kutenda.* Tukasema: Ewe moto! Uwe baridi na salama juu ya Ibrahim.* Na wakamtakia ubaya lakini tukawafanya kuwa wenye kupata hasara.” Sura Anbiyau: 68 – 70.
 • 15. Rejea riwaya hii katika tafsiri ya Ibnu Kathir 2: 33 na rejea Al-Bihar cha Al- Majlisiy 18: 47 na 52 na 60 na 75, mlango wa miujiza ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).
 • 16. Tarikh At-Tabar 2: 244, matukio ya mwaka wa tano hijiriya.
 • 17. Kama ilivyo nassi ya Hadithi ya Mtukufu Mtume: “Hata kama dunia haito- bakiwa ila na siku moja tu basi Mwenyezi Mungu atairefusha siku hiyo mpaka amlete mtu kutoka kizazi changu au kutoka watu wa nyumba yangu ili aijaze ardhi usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhuluma na ujeuri.” Rejea kitabu At-Taju Al-Jamiu Lil-Usul 5: 343, amesema: “Ameipokea Abu Dawdi na Tirmidhiy”.
 • 18. Tumeshuhudia mwanzoni mwa miaka ya tisini mfano halisi wa kauli hii aliy- oitoa Shahid As-Sadri kutokana na ujuzi wake wa kina juu ya jamii ya mwanadamu, kwani muungano wa kisovieti umeporomoka haraka sana na kwa namna ambayo iliwashangaza wote, nao ulikuwa ni moja kati ya nguvu wawili zilizokuwa zikiutisha ulimwengu.