read

Kufunga Mikono Kwenye Sala Kati Ya Bidaa Na Sunna Kwa Mujibu Wa Kitabu Na Sunna.

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu mlezi wa ulimwen- gu. Rehma na Amani zimfikie mbora wa viumbe na hitimisho la mitume Wake, pia kizazi chake kitakatifu ambacho ndio kasha la elimu yake na hazina ya mafunzo yake. Hakika Uislamu ni imani na sheria. Imani ni kuamini Mwenyezi Mungu, mitume Wake na Siku ya Mwisho. Na sheria ni huku- mu za Mwenyezi Mungu ambazo zina jukumu la kumpa mwanadamu maisha bora na kumuhakikishia wema wa dunia na akhera.

Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake, hivyo Mwenyezi Mungu akasema:

الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ{3}

“Leo nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizieni neema Yangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu.” ( 5:3 ).

Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanazuoni wa sheria wamehitilafiana kwa sababu ya kutofautiana kwao kuhusu riwaya ambazo zimenasibishwa kwa Mtume. Jambo ambalo limepelekea kutofautiana kuhusu masuala madodo madogo ya sheria.

Kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti basi hakika katika mtiririko wa masomo haya tumejaribu kuliweka sala hili juu ya meza ya utafiti, kwani huenda ikawa ndio njia ya kuunganisha mtazamo na kusogeza hatua katika uwanja huu. Kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dini hata ipelekee kuwa na uadui na chuki bali tofauti iliyopo ni kuhusu riwaya zilizonasi- bishwa na Mtume, nalo ni jambo dogo ukilinganisha na mambo mengi ambayo tunaafikiana kati ya madhehebu za Kiislamu. Na muongozo wetu katika njia hii ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا{103}

“Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziungan- isha nyoyo zenu, hivyo kwa neema Zake mkawa ndugu.” (3:103)

Sheikh Jafar Subhani
Tasisi ya Imam Sadiq (a.s.)
Qum