Table of Contents

Sehemu Ya Nne: Haki Za Vijana

Haki za vijana juu ya wazazi wao: Umuhimu wa haki za mtoto:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mzazi hupatwa kutokana na haki za mtoto wake yale ambayo humpata mtoto kutokana na haki za mzazi wake.” 1
.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Wazazi hupatwa kutokana na kutomtimizia haki mtoto wao yale ambayo humpata mtoto wao kutokana na kutowatimizia haki zao. 2

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Wazazi hupatwa kutokana na kutomtimizia haki mtoto wao iwapo ni mwema yale ambayo humpata mtoto.” 3

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mtoto ni bwana miaka saba, ni mtumwa miaka saba na ni waziri miaka saba.” 4

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Mwache mwanao acheze miaka saba, na huadabishwa miaka saba na mfuatilie miaka saba.” 5

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Ambaye mwanae atafikia umri wa kuoa na akawa ana mali anayoweza kumuozesha lakini hakumuozesha kisha (mtoto) akizua la kuzua madhambi ni juu yake (mzazi).” 6

Uadilifu:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Fanyeni uadilifu baina ya wanenu. Fanyeni uadilifu baina ya wanenu.” 7

Nu’man Bin Bashir amesema: “Baba yangu alinipa kipawa basi Amrat bint Rawaha akasema: ‘Siridhii mpaka umshuhudishe Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Akamjia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kumwambia: ‘Hakika mimi nimempa mwanangu toka kwa Amrat binti Rawaha kipawa, akaniamuru (Amrat) nikushuhudishe wewe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Akamuuliza: ‘Je umewapa wanao wengine kama hivyo?’ akasema ‘La.’ Akamwambia: ‘Mcheni Mwenyezi Mungu na fanyeni uadilifu baina ya wanenu.’ Anasema: Basi akarejea na kumnyang’anya kipawa kile.” 8

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Uadilifu ni mtamu kuliko maji ayanywayo mwenye kiu. Ni upana ulioje wa uadilifu pindi mtu akifanyiwa hata kama ni mdogo.” 9

Dua:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Dua njema ya mzazi kwa mwanae ni sawa na dua njema ya Nabii kwa umma wake.” 10

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Dua njema ya mzazi kwa mwanae ni sawa na maji kwenye mmea kwa manufaa yake.” 11

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mwenyezi Mungu humrehemu anayemsaidia mwanae kumfanyia mema, nako ni kumsamehe makosa yake na kumuombea mema katika yale yaliyopo kati yake na Mwenyezi Mungu.” 12

Kuacha kumuombea mabaya:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Msiwaombee mabaya wanenu ikaja kuwa mwafaka kwa jibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” 13

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Msijiombee mabaya na wala msiwaombee mabaya wanenu, wala msiiombee mabaya mali yenu, msifanye iwe mwafaka na saa ambayo humo huombwa kipawa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na hatimaye akawajibu.” 14

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Msitamani kuhiliki kwa vijana wenu hata kama wana madhara, kwani hakika wao pamoja na hivyo walivyo bado wana vipindi (vya manufaa): Ima watubu na Mwenyezi Mungu awakubalie toba yao, na ima madhara yawapate. Na ima adui aje wamuue, ima janga la moto walizime, na ima maji wayazuie.” 15

Imam As-Sadiq (a.s.) amesema: “Mtu yeyote atakayemuombea mwanae mabaya basi Mwenyezi Mungu humrithisha ufakiri (mtu huyo).” 16

Alama ya kuvuka mipaka katika kumlaumu:

Imam Ali (a.s.) amesema: “Utakapomkemea kijana basi mwachie nafasi katika kosa lake ili kumkemea kusimpelekee kuwa na jeuri.” 17

Imam Ali (a.s.) amesema: “Kuzidisha kukemea huwasha moto wa ubishi (upinzani).” 18

Imam Ali (a.s.) amesema: “Unapokemea kemea kwa wastani.” 19

Haki Za Kijana Kijamii

Kuwakirimu:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Wapeni nafasi vijana katika mabaraza, waelewesheni hadithi, kwani hakika wao ni warithi na watu wa hadithi.” 20

Sahlu bin Sa’ad amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliletewa bilauri akanywa kilichomo, kuliani mwake kulikuwa na kijana mdogo kuliko wote waliokuwepo, na kushotoni mwake (s.a.w.w.) kulikuwa na wazee, basi akamwambia: ‘Ewe kijana unaniridhia niwape wazee kilichomo?’ akase- ma: ‘Siwezi kumrithisha yeyote fadhila yangu kutoka kwako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Basi akawa amempa.”21

Kuwaomba ushauri:

Imam Ali (a.s.) amesema: “Ukihitaji ushauri wa jambo lililokutokea basi lidhihirishe kwa kuwaanza vijana kwani hakika wao ni moja ya akili na wepesi wa kutafakari, kisha baada ya hapo lirejeshe kwenye rai ya wazee na vikongwe ili walipitie tena, na wafanye uteuzi wa maamuzi mazuri, kwani hakika uzoefu wao ni mwingi.” 499

Kutilia umuhimu mahitaji yao maalumu

Ima Al-Baqir (a.s.) amesema: “Hakika Ali (a.s.) aliwaendea mabazazi na kumwambia aliye mtu mzima: ‘Niuzie nguo mbili.’ Mwanaume yule akasema: ‘Ewe Jemedari wa waumini, kwangu kuna haja yako.’ Alipojua kusudio lake akamwacha na akaenda kwa kijana, akachukua nguo mbili, moja kwa dirhamu tatu na nyingine kwa dirhamu mbili, akasema: ‘Ewe Qanbar chukua ya dirhamu tatu.’ Akasema: ‘Wewe ndiye aula kwayo kwani unapanda mimbari na kuhutubia watu.’ Akamjibu: ‘Nawe ni kijana na bado una mvuto wa ujana, nami naona haya mbele ya Mola wangu Mlezi kuwa mbora juu yako.’” 500

 • 1. Kanzul-UImmal, Juz. 16, Uk. 444, hadithi ya 45344.
 • 2. Al-Kafiy, Juz. 6, Uk. 48, hadithi ya 5
 • 3. Al-Khiswal, Uk. 55, hadithi ya 77.
 • 4. . Makarimul-Akhalq, Juz. 1, Uk. 478, hadithi ya 1649.
 • 5. Man Layahdhuruhul-Faqiih, Juz. 3, Uk. 492, hadithi ya 4743.
 • 6. Kanzul-Ummal, Juz. 16, Uk. 442, hadithi ya 45337
 • 7. As-Sunanu Al-Kubra, Juz. 6, Uk. 293, hadithi ya 11999.
 • 8. Sahih Bukhar, Juz. 2, Uk. 914, hadithi ya 2447.
 • 9. Al-Kafiy, Juz. 2, Uk. 146, hadithi ya 11.
 • 10. Mishkatul-An’war, Uk. 282, hadithi ya 853.
 • 11. Biharul-An’war, Juz. 104, Uk. 98, hadithi ya 3038
 • 12. Al-Firdawsu, Juz. 2, Uk. 213, hadithi ya 3038.
 • 13. Tarikh Isbihan, Juz. 2, Uk. 296, hadithi ya 1784.
 • 14. Sahih Muslim, Juz. 4, Uk. 2304, hadithi ya 3009.
 • 15. Hilyatul-Awliyai, Juz. 5, Uk. 119.
 • 16. Iddatud-Dai, Uk. 80
 • 17. Sharhu Nahjul-Balagha, Juz. 20, Uk. 333, hadithi ya 819.
 • 18. Uyunul-Hikam Wal-mawaidh, Uk. 333, hadithi ya 819.
 • 19. Ghurarul-Hikam, hadithi ya 3977
 • 20. Al-Firdawsu, Juz. 1, Uk. 98, hadithi ya 320
  498 Sahih Bukhari, Juz. 2, Uk. 829, hadithi ya 2224.
  499 Sharhu Nahjul-Balagha, Juz. 20, Uk. 337, hadithi ya 866.
  500 Biharul-An’war, Juz. 40, Uk. 324, hadithi ya 6.
 • 21.