Kwa hakika kitabu hiki kinazungumzia maadili ya vijana kwa mtazamo wa Kiislamu. Kama tujuavyo Uislamu ni dini na mfumo wa maisha, kwa hiyo, haukuacha chochote kinachomhusu mwanadamu katika maisha yake ya hapa duniani na ya kesho Akhera.

Mwandishi wa kitabu hiki amejaribu kwa uwezo wake kuwakumbusha vijana juu ya wajibu wao katika jamii na kuwarejesha katika maadili mema. Na katika kuikamilisha kazi yake hii amerejea sana kwenye mafunzo ya Uislamu ambayo chimbuko lake ni Qur’ani na Sunna. Hivyo basi, huu ni mwongozo halisi kwa vijana unaolenga kuwaokoa katika harakati zao za maisha na hatimaye wawe ni wenye kufuzu kesho Akhera.