read

Mlango Wa 3: Kanuni Muhimu Za Kifiqhi -1 Kwa Wawili Waliooana

Hali Ya Janaba

Janaba ni kunajisika kiibada kunakosababishwa na kutokwa na manii au kwa kujamiiana, na yule mtu ambaye anawajibika kuoga Ghusl al- Janaabat anajulikana kama Mujnib.

Mambo Ambayo Ni Makruh Kwa Mwenye Janaba

Mambo Ambayo Ni Makruh Kwa Mwenye Janaba1

1. Kula

2. Kunywa

Hata hivyo, kama mtu huyu aliyeko kwenye hali ya janaba akiosha mikono yake, uso na kinywa, halafu akala na kunywa, katika hali hiyo haitakuwa makruh. Ni rahisi kwa hiyo basi kwa mtu kutawadha.

3. Kulala

Hata hivyo, kama mwenye janaba hana maji, au kwa sababu ya kutoku- patikana maji, anaweza kufanya tayammam badala ya Ghusl al-Janabat.

4. Kugusa sehemu yoyote ya kitabu, jalada, pambizo au ukingo wa Qur’ani Tukufu au ile sehemu katikati ya mistari yake.

5. Kufanya tendo la kujamiiana wakati mtu yuko kwenye hali ya Ihtilam (yaani aliyetokwa na manii usingizini).

6. Kuweka nywele henna.

7. Kupaka mafuta mwilini mwake mtu.

8. Kuchukua au kukaa na Qur’ani Tukufu.

9. Kusoma zaidi ya aya saba za Qur’ani, mbali na zile ambazo sijdah ya wajibu hutokea (kuzisoma aya hizo ni haram).

DOKEZO: Udhahiri wa ‘Makruh ya Ibada’ ni tofauti na kanuni ya jumla ya makruh, ambayo ni kwamba, ni bora kwamba mtu asilifanye tendo hilo. Kwa mfano, ni makruh kwa msafiri kuswali swala ya Dhuhri, al-Asr, na Ishaai nyuma ya mtu ambaye sio msafiri na kinyume chake,2 au ni makruh kusoma Qur’ani ndani ya sajidah.3

Hii ‘Makruh ya Ibada’ haina maana kwamba ni bora mtu asilifanye tendo hilo, bali hasa ina maana kwamba kama ukikifanya kitendo hicho, basi kiwango cha malipo yake yanayopatikana ni cha chini kulinganisha na kile cha kawaida.

Mambo Ambayo Yanakatazwa Kwa Mtu Mwenye Hali Ya Janaba

Mambo Ambayo Yanakatazwa Kwa Mtu Mwenye Hali Ya Janaba4

1. Kugusa kwa kiungo chochote cha mtu huyo, maandishi ya Qur’ani Tukufu, au jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa lugha yoyote ile iwayo. Ni bora vilevile kwamba yale majina 14 ya Ma’suumin (a.s.) pia yasiguswe katika hali hiyo.

2. Kuingia ndani ya Masjidul-Haraam au Masjidun-Nabii.

3. Kukaa au kusimama katika misikiti mingine yote, na hali kadhalika katika msingi wa tahadhari ya wajib kukaa katika maquba ya Maimam watukufu ni haram pia. Hata hivyo, hakuna madhara iwapo mtu atapita au kukatisha msikiti, kwa kuingia kupitia mlango mmoja na kutokea kwenye mwingine.

4. Kuingia msikitini kwa lengo la kunyanyua kitu au kuweka kitu ndani yake.

5. Kusoma aya za Qur’ani tukufu ambazo ndani yake kuleta sajidah kunakuwa ni wajibu

6. Surat ‘Alif Lam Mim Sajdah (32:15), Surat Haa Mim Sajdah (41:38), Suratun-Najm (53:62) na Surat al-Alaq (96:19).

Josho La Janaba-(Ghuslul-Janaabah)

Nyakati Ambazo Ghuslul-Janaabah Linakuwa Ni Wajib:

1. Wakati mwanaume anapomuingilia mwanamke mpaka kwenye ile sehe- mu ya kutahiriwa kwake au zaidi, hata kama kumwaga manii hakuku- tokea, josho la janaba linakuwa ni wajibu kwao wote.5

2. Kama baada ya kujamiiana mwanaume hakufanya Istibraa (kujikamua) kwa ajili ya kutoa manii (ambayo ni kiasi cha kukojoa tu) na kisha akachukua josho, na baada ya hapo akaona utokwaji na kitu na hakuweza kutambua kama ni manii au hapana (yaani mkojo) itachukuliwa kwamba ni manii na kwa hiyo Ghusul-Janaabah itakuwa ni wajibu kwake tena.6

3. Kama mwanaume anatokwa na manii kwa kupitiwa usingizini.7

Nyakati Ambazo Ghusl Al-Janaabat Haliwi Wajib

1. Kama mtu anatia shaka kwamba dhakari yake imeingia mpaka sehemu aliyotahiriwa ama laa, hapo josho la janaba haliwi wajib kwao wote.8

2. Yale maji, unyevunyevu ambao unatolewa na mwanaume wakati wa kunyegereshana unaitwa Madhii na ni masafi kiibada. Yale majimaji yanayotoka baada ya kumwaga manii yanaitwa Wadhii, nayo ni masafi kiibada. Ule uoevu ambao wakati mwingine hutoka baada kukojoa unaitwa Wadii, ni msafi kiibada (isipokuwa ukikutana na mkojo) na hakuna mojawapo kati ya haya linalohitajia Ghusl. Iwapo mtu atafanya Istibraa baada ya kukojoa na kisha akatoa uoevu na akatia shaka kwamba ni mkojo au moja kati vioevu vilivyotajwa hapo juu, uoevu huo ni msafi kiibada.9

3. Kama mtu anashughulika katika kujamiiana mara moja na akataka kujishughulisha tena mara moja au mbili katika usiku mmoja, josho sio wajibu kwa kila mara baada ya kila tendo moja.

4. Kama mtu amemwaga manii katika usingizi wake na angependa kushughulika na kujamiiana, sio wajibu kwake kuoga josho kisha ndipo ashiriki katika tendo hilo. Ni makruh hata hivyo kujishughulisha katika tendo hilo katika wakati wa hali hiyo.10

Kanuni Muhimu Za Josho (Ghusl)

Taratibu Za Josho (Chini Ya Bafu Ya Manyunyu)

a.) Mtu kwanza ni lazima alete nia ya Ghusl na kisha aoshe kichwa na shingo halafu mwili mzima.

Ni bora kuosha upande wa kulia kwanza na kisha upande wa kushoto. Mwili hauwezi kuoshwa kabla ya kichwa11

b.) Hakuna madhara kama wakati wa kuosha shingo mtu akaosha sehemu kidogo ya upande wa kulia wa mwili wake.12

c.) Kama sehemu ya mwili imenajisika, sio muhimu kwanza kuifanya tohara ndipo uchukue Ghusl; bali wakati unapooga josho sehemu hiyo inaweza kutoharika.13

d.) Endapo sehemu yoyote ya mwili imeachwa na ukavu (hata kwa ukubwa wa kichwa cha sindano) josho hilo linakuwa ni batili.14

e.) Tofauti na wudhuu, katika Ghusl ni sawa kutochunga muwaalaat, yaani, baada ya kuosha kichwa na shingo, mtu halafu anafanya kitu kingine (kwa mfano, kuupaka mwili sabuni), ni sawa kwake kurudi tena kuosha mwili baada yake; sio lazima kwa josho hilo kuanzishwa upya kuanzia mwanzo kabisa.15

f.) Shuruti zote ambazo zinatengua wudhuu, vilevile zinatengua Ghusl.

g.) Kama mtu atatokea kukojoa wakati wa josho au kutokwa na ushuzi, sio lazima kwa josho kuanza upya; josho hilo hilo linaweza kumaliziwa. Hata hivyo, kama mtu atataka kuswali, basi kwa mujibu wa tahadhari ya wajib, wudhuu lazima uchukuliwe hapo kwani hairuhusiwi kuswali kwa tohara ya josho hilo hilo.16

h.) Ghusl yenye nia nyingi kama inavyohitajika, mustahab na wajib, kwa mfano, Ghusl ya sunna ya Ijumaa inaweza kufanywa wakati mmoja na Ghusl ya Janaba.17

i.) Baada ya Ghusl ya Janaba kufanyika, mtu lazima atawadhe kwa ajili ya Swala. Hii ndio hali kwa majosho yote ya wajibu. Kama nia nyingi zitaingizwa, kwa mfano nia ya mustahab na wajib, hapo tena wudhuu sio lazima.18

Tayammum

Nyakati Ambazo Tayammum Inaweza Kutendwa Badala Ya Ghusl

Kuna hali namna sita ambapo tayammam inaruhusiwa badala ya Josho, ambazo kwamba zifuatazo zinatumika sana kwa wanandoa:

1. Wakati Hayawezi Kupatikana Maji Ya Kutosha Josho

Kama mtu anaishi kwenye sehemu yenye makazi ya watu wengi, anapaswa kufanya juhudi ya kutosha katika kupata maji kwa ajili ya Josho, mpaka wakati ambapo huenda matumaini yote yatakapopotea.19

Kwa hiyo endapo mtu atahitaji kufanya Ghusl ili aweze kuswali, na kwa wakati huo hakuna maji yanayoweza kupatikana, bali mtu akawa na hakika kwamba kabla swala hiyo haijawa qadhaa maji yatapatikana, basi ni lazima mtu asubiri hadi yatakapopatikana maji ili Josho liweze kufanyika.

Tayammam haiwezi kufanyika katika hali hii hata kama muda wa swala (wa fadhila) utakuwa umeingia au kama swala ya jamaa inaswaliwa.20

Hata kama kuna dalili kidogo tu kwamba maji yatapatikana kabla ya wakati wa swala, mtu hawezi kufanya tayammam na kuswali mpaka labda mtu atakapopoteza matumaini kabisa kwamba maji hayatapatikana kabisa kabla ya swala hiyo kuwa qadhaa.21

Hata hivyo, kama mtu ana uhakika kabisa kwamba maji hayatapatikana kabla ya qadhaa, basi hapo mtu anaweza kufanya tayammum na kuswali kwa wakati wa mapema iwezekenavyo.22

2. Wakati Inapokuwa Ni Karibu Kuwa Wakati Wa Qadhaa

Mtu anapaswa kufanya tayammum pale wakati uliobakia kwa swala hiyo kuwa qadhaa ni mdogo sana kiasi kwamba kama mtu atafanya Ghusl, hakutakuwa na muda uliobakia kwa kutekeleza swala hiyo.23
Hata kama mtu atakuwa na mashaka kwamba kutakuwa na muda wa kutosha au laa utakaokuwa umebaki kwa ajili ya swala kama akichukua josho au wudhuu, anapasika kufanya tayammam.24

3. Hatari Kwa Afya

Kama mtu akihofia kwamba endapo atatumia maji ataugua maradhi fulani au madhara ya kimwili, au ugonjwa ambao tayari anaugua utaendelea kwa muda mrefu, au utakuwa mkali zaidi au ugumu mwingine zaidi utaweza kujitokeza, basi anapaswa kufanya tayammam. Kwa mfano, kama mtu ana ugonjwa wa macho ama sindano mahali ambapo maji hayaruhusiwi juu yake kwa masaa 24, tayammam inapaswa kufanyika. Hata hivyo, endapo mtu anaweza kuyaepuka madhara hayo kwa kutumia maji ya vuguvugu, aandae maji ya vuguvugu kwa ajili ya Josho.25

Utaratibu Wa Kufanya Tayammam

Tofauti na utambuzi wa kawaida, kufanya tayammam kwa kweli ni jambo rahisi na jepesi sana; ni rahisi zaidi kuliko kutawadha. Kunapaswa kutekelezwa kama ifuatavyo:

Hatua Ya Kwanza:

Tia nia ya kufanya tayammam (sawa na wudhuu ama Ghusl).

Hatua Ya Pili:

Kwa mikono yote kufunguliwa wazi na kunyooka kuelekea kile kitu ambacho tayammam inaruhusiwa juu yake (udongo, vumbi, mchanga na au jiwe); piga (au weak) mikono yote kwa pamoja, mmoja pembeni ya mwingine juu ya kitu hicho ambacho tayammam inafanyika juu yake.

Hatua Ya Tatu:

Nyanyua mikono yako na uiweke pamoja kama mtu anayeomba du’a, halafu weak vitanga vya viganja vyako juu ya paji la uso kuanzia maoteo ya nywele. Telezesha mikono yako chini juu ya nyusi na ncha ya pua, halafu vishushe viganja vyako kuelekea upande wa kulia wa paji la uso na halafu upande wa kushoto. Kisha rudisha mikono yako katikati ya paji la uso na uiteremshe yote kwa pamoja kuelekea puani, ukihakikisha na vidole pia vinaparaza juu ya nyusi na ncha ya pua. Paji lote la uso linapaswa kufunikwa hadi kwenye nyusi (inapendekezwa kushusha kupita zaidi ya nyusi).

Hatua Ya Nne:

Nyoosha mkono wa kulia ukihakikisha kwamba kiganja chako kimeelekea chini, vidole na dole gumba vikiwa vimefungana pamoja na dole gumba halikuchimbiwa chini ya vidole. Halafu weka upande wa ndani wa mkono wa kushoto katika hali ya wima juu kidogo ya kifundo (yaani, kile kidole kidogo tu ndio kinapaswa kukandamizwa juu ya kifundo cha mkono wa kulia, kiganja cha mkono wako wa kushoto kikuangalie wewe).

Teremsha mkono wa kushoto (ukishusha kiganja chini), ukihakikisha maeneo yote ya ndani ya mkono wa kulia ziefunikwa. Rudia utaratibu huohuo juu ya mkono wa kushoto (bila ya kurudia kupiga mikono juu ya udongo tena).

Mambo Muhimu Kuhusiana Na Tayammam

a.) Kama utaacha hata sehemu ndogo tu ya paji lako la uso au sehemu ya nyuma ya mikono yako katika tayammam, kwa makusudi au kwa kusahau, au hata kwa kutokujua, tayammam yako itakuwa batili. Unapaswa kuwa mwangalifu lakini usizidi kuwa mahususia, kama itaweza kuchukuliwa vya kutosha kwamba paji la uso na nyuma ya mikono vimepakwa itakuwa imetosheleza.26

b.) Kama namna ya tahadhari, upakaji wa kichwa na mikono unapaswa kufanywa kuanzia juu kushuka hadi chini.27

c.) Ni Ihtiyat mustahab (tahadhari inayopendekezwa) kwamba hilo paji la uso, viganja vya mikono na sehemu za nyuma za viganja na mikono vinakuwa tohara.28

d.) Wakati wa kufanya tayammam, pete ni lazima zivuliwe na kizuizi chochote kwenye paji la uso au kwenye viganja au nyuma ya mikono navyo ni lazima viondolewe.29

Kuvitoharisha Vile Vitu Ambavyo Vimechafuliwa Na Manii

Nguo Au Shuka Za Kitanda

Kama mashuka ama chochote cha kuvaa kama nguo au taulo vikinajisika kwa manii vinaweza kutoharishwa katika njia zifuatazo:

A. Kutumia Maji Yanayotiririka

1. Kama kitu hicho bado kina ubichi kutokana na manii, mtu anapaswa kuwa mwangalifu kwamba kisigusane na nguo nyinginezo au vitu vinginevyo kwa sababu hapo navyo vitakuwa vimenajisika.

2. Mtu anapaswa kuosha kile kilichonajisika mara moja chini ya maji ya bomba (kurr) katika namna ambayo kwamba:

a.) Maji yanafika kwenye kila sehemu ya lile eneo lililonajisika.

b.) Kuwe hakuna dalili za yale manii hasa yaliyoachwa kwenye nguo (yaani, sugua na kukamua nguo wakati wa kufua kwa namna ambayo hakuna mabaki ya manii yanayoachwa kwenye nguo wala rangi yake).

3. Kama kitu chenyewe ni kipande cha nguo, hakuna haja ya kukipopotoa au kukikamua baada ya kuwa kimetoharishwa (kwa mtindo huo hapo juu), ingawa hili huwa linafanyika kutokana tu na mazoea.

4. Wakati kitu hicho kikiwa kimeoshwa mara moja na kuwa safi kitohara (kwa mtindo huo hapo juu) hii inatosha; hailazimiki kukiosha mara mbili au tatu.

5. Kama kitu kilichonajisika kinatoswa kwenye maji ya bomba yanayotiririka (kurr) au maji yanayotembea, kwa namna ambayo maji yanaz- ifika sehemu zake zote zilizonajisika, kinakuwa kimetoharika. Na katika suala la zulia au vazi sio muhimu kulikamua, kulipopotoa au kuliminya.30

B.) Kutumia Mashine Za Kufulia

Hukmu inayotumika kwenye mashine za kufulia ni ile ya maji ya kurr.31 Hivyo kitu ambacho kimekuwa najis kwa manii kinaweza kuwekwa moja kwa moja kwenye mashine ya kufulia, na madhali hakuna dalili ya manii iliyobakia baada ya mzunguko kukamilika, halafu kitu hicho kinachukuliwa kuwa kimetoharika, na hakihitaji kuoshwa tena, au kupopotolewa na kukamuliwa.

Hata hivyo, kama hatua ya tahadhari, linaweza kuwa ni wazo jema kukifanya kile kitu kilichonajisika kuwa kisafi kitohara kwanza (kwa njia ile ya pale juu) na kisha tukiweke kwenye mashine ya kufulia, kwa sababu kama mtu ataweka kitu hicho moja kwa moja ndani ya mashine ya kufulia, na kwa sababu yoyote iwayo manii hayo yakabakia kwenye nguo baada ya kufuliwa, haitakuwa safi kitohara, na endapo nguo hiyo itakutana na nguo nyinginezo zenye ubichi, nguo hizo pia zitakuwa zimenajisika

Godoro:

A. Kutumia Maji Yanayotiririka

Endapo godoro litanajisika kwa manii kwa sababu yoyote ile iwayo, inawekana kulifanya tohara kwa maji safi yanayotiririka kutoka kwenye bomba au mpira wa maji:

Kama mtu anataka kutakasa godoro kwa kutumia maji safi yaliyounganishwa kwenye chanzo cha bomba – kurr – (kwa mfano kwa kutumia mpira wa maji au bomba) hakuna haja ya kuyafuta maji hayo kwa kutumia nguo hiyo au mashine ya kivuta vumbi na kadhalika.

Mara tu yale maji ya kurr yanapolienea eneo lenye najis, litakuwa tohara (madhali ile najasat ayn – manii, itakuwa imeondolewa) [na maji hayo pia yatachukuliwa kuwa tohara].32

Ni muhimu kukumbuka yafuatayo wakati godoro linapokuwa limenajisika kwa manii: Manii hayo yanahamia tu kutoka kwenye godoro kwenda kwenye kitu kingine kupitia unyevunyevu unaobubujika (yaani, unapokuwepo ubichi mwingi katika kile kilichonajisika ambao unapenya kwenye kitu kingine na kukifanya kuwa najisi).

Hiyo najisi haihamishiki inapokuwa kavu, hivyo iwapo utaweka mwili au mkono wako juu ya godoro lenye najisi kavu, huo mkono au mwili wako hautakuwa umenajisika.

Kwa hiyo, inawezekana kulala juu ya godoro ambalo limenajisika bila ya nguo zako kunajisika, alimradi tu kwamba kile kipande ambacho kimenajisika kinabakia kuwa kikavu ili kwamba ile najisi haihamishiwi kwenye nguo hizo kutoka kwenye godoro hilo.

B. Kutumia Maji Machache Kuliko Kurr (Qaliil)

Maji machache kuliko kurr yanatumika katika hali ambazo imma maji ya kurr hayapatikani au kwamba huwezi kuweka kitu kama godoro chini ya maji ya kurr (chini ya bomba). Utaratibu wa kukifanya kitu kiwe kisafi kitohara kwa maji machache ni kama ifuatavyo:

Hatua Ya 1: Kuiondoa Najisi

Manii hayo ni lazima yaondolewe kutoka kwenye godoro hilo. Mbinu inayowezekana ya kufanya hili ni kwanza kumwaga maji kutoka kwenye gilasi kuenea kwenye eneo lote lililoingia doa. Halafu chukua taulo na liweke juu ya ile sehemu iliyolowa na tumia nguvu kuminya juu yake kwa namna ambayo maji hayo yananyonywa na kwamba hakuna manii yanayobakia. Taulo litakalotumika litakuwa limenajisika na litahitaji kuoshwa kitohara.

Hatua Ya 2: Kumwaga Maji Kuliko Kiwango Cha Kurr

Baada ya kuyaondoa yale manii, sehemu hiyo inatakiwa ifanywe kuwa tohara. Hili linafanywa
kwa kuchukua gilasi nyingine ya maji na kumwagia tena maji juu ya eneo lote tena (lile lililokuwa limenajisika).

Maji hayo ni lazima yakamuliwe na kuminywa yatoke kwenye godoro kabla halijawa tohara. Hili linaweza kufanyika kwa kuchukua taulo na kuliweka juu ya eneo lililoloweshwa kwa namna ambayo wakati nguvu inapoongezwa juu ya taulo hilo maji yote yananyonywa yatoke.

Godoro hilo sasa limekuwa tohara. Kama rai iliyothibitishwa na sio tahadhari ya wajibu, taulo hilo na maji yaliyotolewa yatahesabiwa kuwa ni najisi.

Kama kitu chochote kinakuwa najisi kwa uchafu mwingineo mbali na mkojo, kitakuwa tohara kwa kwanza kuondoa ule uchafu na kisha kumwa- gia maji machache chini ya kiwango cha kurr, mara moja, na kuyaruhusu yamwagike. Bali kama ni nguo na kadhalika, inapaswa kukamuliwa na kuminywa ili kiasi chochote cha maji kilichobakia kiweze kumwagika.33

Kiangalizo: Ni muhimu kabisa kutambua kwamba hata kama sehemu ya juu ya godoro inafanywa kuwa safi kitohara kwa maji machache (qaliil) kwa kufuatilia mfano huo hapo juu, sehemu ya ndani ya godoro itakuwa najisi kutokana na kununi ya maji machache. Hata kama godoro hilo litawekwa kwa pembe, bila shaka yatanywea kwenye godoro hilo.34

PENDEKEZO: Ili kuepukana na kazi hii ngumu ya ziada na ugomvi wote wa kulisafisha godoro, kuna manufaa makubwa sana kwamba mtu awe anaweka tandiko la plastiki kati ya shuka na godoro, ili kwamba kama kiasi chochote cha manii kitavuja kwenye shuka hakitavuja kupita kwenye plastiki hadi kwenye godoro.

Mwili Wenyewe

Kama sehemu ya mwili inanajisika kwa sababu ya manii, inaweza kufanywa safi kitohara kwa kumwagiwa maji kiwango chini ya kurr juu yake mara moja kwa namna ambayo kwamba hakuna mabaki ya manii yanayoachwa kwenye mwili. Hili linaweza kufanyika kwa kusimama chini ya bomba la manyunyu.

Hata hivyo, kanuni hii ni tofauti kama najisi yenyewe ni mkojo, ambao kuuosha mara moja hakutoshi, mwili lazima uoshwe mara mbili. Sio lazima kuingia na kutoka kwenye maji ili kupata majosho mawili. Endapo sehemu iliyopata najisi inapanguswa kwa mkono kuruhusu maji kufika hapo tena, hiyo itatosha.35

 • 1. Islamic Laws – Shari’ah ya Kiislam; Kanuni ya 362
 • 2. Islamic Laws, Kanuni ya 1499
 • 3. Islamic Laws, Kanuni ya 1101
 • 4. Islamic Laws, Kanuni ya 361
 • 5. Islamic Laws, Kanuni ya 355
 • 6. Islamic Laws, Kanuni ya 354
 • 7. Islamic Laws, Kanuni ya 351
 • 8. Islamic Laws, Kanuni ya 356
 • 9. Islamic Laws, Kanuni ya 74
 • 10. Islamic Laws, Kanuni ya 362
 • 11. Islamic Laws, Kanuni ya 367
 • 12. Islamic Laws, Kanuni ya 369
 • 13. Islamic Laws, Kanuni ya 378
 • 14. Islamic Laws, Kanuni ya 380
 • 15. Islamic Laws, Kanuni ya 386
 • 16. Islamic Laws, Kanuni ya 392
 • 17. Islamic Laws, Kanuni ya 395
 • 18. Islamic Laws, Kanuni ya 397
 • 19. Islamic Laws, Kanuni ya 655
 • 20. Islamic Laws, Kanuni ya 723
 • 21. Islamic Laws, Kanuni ya 723
 • 22. Islamic Laws, Kanuni ya 723
 • 23. Islamic Laws, Kanuni ya 686
 • 24. Islamic Laws, Kanuni ya 686
 • 25. Islamic Laws, Kanuni ya 677
 • 26. Islamic Laws, Kanuni ya 710
 • 27. Wasa'ilush-Shi'a; Juz. 20, Uk. 109, namba 25163
 • 28. Islamic Laws, Kanuni ya 714
 • 29. Islamic Laws, Kanuni ya 715
 • 30. Islamic Laws, Kanuni ya 160
 • 31. Imethibitishwa na ofisi ya Ayatullah Sistani, Qum.
 • 32. Kanuni ya Desturi kwa Waislam huko Magharibi, Ayatullah Sistani.
 • 33. Islamic Laws, Kanuni ya 163
 • 34. Islamic Laws, Kanuni ya 163
 • 35. Islamic Laws, Kanuni ya 172