read

Mlango Wa 5: Utungaji Wa Mimba

Vyakula Vinavyopendekezwa

Chakula anachokula mtu sio tu kwamba kina athari kubwa katika mwelekeo wa kiafya wa mtu, bali katika nafsi, moyo na akili vilevile. Kwa hiyo, inapendekezwa sana kwamba wazazi watarajiwa wajihadhari na vyakula vilivyoharamishwa, na hata vile vyakula ambavyo kuvila kunakuwa na wasiwasi.1

Kwa nyongeza, baadhi ya vyakula pia vimependekezwa makhsusi kabisa na Maimam kwa ajili ya mtoto mzuri na halali.

Kabla ya kutungwa mimba ya Hadhrat Fatimah (a.s.), Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu alikaa mbali na Hadhrat Khadijah kwa muda wa siku 40. Katika muda wa siku hizi 40, alifanya vitendo vya ibada na kufunga, na futari yake ilijumuisha chakula ambacho kililetwa kutoka mbinguni. Inapendekezwa kula vyakula vifuatavyo kabla ya kujaribu kutunga mimba:

1. Chicory – Aina Ya Majani Kwa Saladi

a. Imependekezwa kwamba baba atumie kula hiyo chicory.2

2. Komamanga

a. Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba: “Kula komamanga ni sababu ya uongezekaji wa utengenezaji wa manii kwa wanaume na kunafanya mtoto (anayezaliwa) kuwa mzuri na mwenye afya bora pia.3

b. Imesimuliwa kutoka kwa Imam ar-Ridhaa (a.s.): “Ulaji wa komamanga tamu unamfanya mwanaume kuwa na nguvu zaidi katika tendo la ndoa na kunaathiri sana uzuri wa mtoto.4

3. Qawoot

Qawoot ni unga au poda inayotengenezwa kutokana na usagaji na uchekechaji wa mchanganyiko ufuatao kwa viwango vinavyowiana: Ngano iliyokaangwa, shayiri iliyokaangwa, mbegu za ufuta zilizokaangwa, mbegu za tikiti la kawaida na za tikitimaji zilizokaangwa, mbegu za tikiti lenye mikunjo (Deep Ribbed Melon) zilizokaangwa, mbegu za Purslane zilizokaangwa, mbegu za Coriandor zilizokaangwa, mbegu za katani zilizokaangwa, mbegu za shamari (kiungo jamii ya karoti) zilizokaangwa, mbegu za mpopi zilizokaangwa, mbegu za dengu zilizokaangwa, ufuta, mbegu za Pistachio, kahawa, iliki, mdalasini, lozi/badamu, sukari.

Kwa vile mchanganyiko huu haupatikani katika nchi nyingi, inashauriwa kwamba vitu hivyo vilivyotajwa hapo juu viwe vinaliwa vyenyewe kimoja kimoja, kwa mfano pistachio na badamu.

b. Imependekezwa kwamba wote baba na mama wale qawoot: Imesimuliwa kwamba mtu mmoja alimwambia Imam as-Sadiq (a.s.):
“Ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, mtoto wa kiume ndio kwanza amezaliwa ambaye ni dhaifu na mwenye akili pungufu.” Imam ali- jibu akasema: “Kwa nini hamkuwahi kula qawoot? Kuleni qawoot na washaurini familia zenu kufanya hivyo pia. Kwa hakika, qawoot inafanya mnofu kukua na mifupa kuwa imara, na mtoto wa kiume hatazaliwa kutokana nanyi isipokuwa kwamba atakuwa mwenye nguvu.”5

c. Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): Kula qawoot pamoja na mafuta ya mzeituni na nyama kunamnenepesha mtu, kunafanya mifupa kuwa imara, kunaufanya mwili kung’ara na wenye nuru (Nur tukufu) na kunaongeza nguvu na uwezo wa kujamiiana.”6

4. Quince (Tunda Aina Ya Pea)

a. Imesimuliwa kwamba Imam as-Sadiq (a.s.) alimuona mtoto mzuri na akasema: “Inaelekea kabisa kwamba huenda baba wa mtoto huyu alikula lile tunda quince – aina ya pea wakati wa usiku wa kutungwa kwa mimba yake.”7

b. Imesimuliwa pia kutoka kwake yeye (a.s.) kwamba: “Kula quince kwenye usiku wa kutunga mimba kunafanya uso (wa kijusi) wa kupen- deza na mzuri, na moyo kuwa na nguvu na imara.”8

c. Hadithi nyingine kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) anasimulia kwamba: “Yeyote atakayekula quince juu ya tumbo lenye njaa, chanzo cha uzal- ishaji wa mbegu (manii) inakuwa safi na yenye afya, na mtoto wake atakuwa mzuri na mwenye mwenendo mwema.”9

d. Imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikata tunda lake la quince vipande vipande na akampa Ja’far ibn Abi Talib kimoja na akamwambia: “Kula! Quince hii inaleta mng’aro wa rangi na kumfanya mtoto kuwa mzuri.”10

Vitendo Vinavyopendekezwa

Ni muhimu sana kutambua kwamba vyingi ya vitendo vilivyotajwa katika sehemu hii ni sawa na vile vilivyodokezwa kwenye mlango wa Taratibu za mahusiano ya kujamiiana, pamoja na nyongeza ya jinsi zinavyoathiri mtoto aliyetungwa kwenye mimba.

Hali Ya Kimawazo:

Hali ya mawazo na moyo ya wazazi ina athari muhimu sana kwa mtoto. Matukio yafuatayo yanaakisi umuhimu wa hali ya kimawazo wakati wa kutunga mimba na matokeo yake

a.) Wakati Nabii Musa (a.s.) alipokuwa akifanya kazi kama mchungaji wa kondoo kwa Nabii Shu’aibu (a.s.), walifanya mapatano kwamba kon- doo yoyote kutoka kwenye kundi kondoo hao ambao watakuwa na rangi mbalimbali (wote wakiwa na rangi nyeusi na nyeupe), watalipwa kwa Nabii Musa (a.s.) kama mshahara wake. Baada ya mapatano haya, Nabii Musa (a.s.) aliifunika fimbo yake na ngozi yenye rangi na akaacha baadhi ya sehemu kama zilivyokuwa, akaning’iniza nguo (aba) yenye rangi kama hizo hizo juu ya fimbo hiyo na kisha akaiweka fimbo hiyo juu ya uwanja wa malisho. Wakati wa kuzaa, kondoo hao wata- iangalia fimbo hiyo.

Mwishoni mwa mwaka, ulipokuwa ni wakati wa kuchukua malipo, Nabii Shu’aib (a.s.) aliona kwamba wengi wa watoto wa kondoo walikuwa na rangi mbalimbali! Nabii Musa (a.s.) akaeleza kwamba haya yalikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya kuiangalia ile fimbo na nguo wakati
wa kuzaa.11

b.) Katika familia ya kiafrika, ambamo mume na mke wote walikuwa na ngozi nyeusi, walipata mtoto mwenye rangi ya hudhurungi (kama ile ya Mhindi mwekundu wa Marekani). Walipokuwa wakilitafiti hili, wanasayansi wakagundua kwamba yule mume alikuwa na rafiki Mhindi wa Marekani na alikuwa ameweka picha ya rafiki yake huyo ukutani. Ule wakati wa kutunga mimba, macho yake yaliangukia kwenye ile picha na akawa anamfikiria rafiki yake huyo; wazo hilohilo likawa na athari kwenye manii na mtoto mwenye rangi ya hudhu- rungi, sawa na ile ya rafiki yake, ndipo akazaliwa.12

Kwa hiyo, wakati unapojaribu kutafuta kutunga mimba, inapendekezwa kwa kukokotezwa kabisa katika Uislam kwamba vitendo vilivyopen- dekezwa hapo chini vinashikwa ili kutunga mimba ya mtoto safi na mzuri.

1. Jaribu kutulia, kwani hili linasababisha muongezeko wa mzunguko wa damu na hivyo kupatikana mtoto wa kawaida. Imesimuliwa kutoka kwa Imam Hasan (a.s.) kwamba: “(Kama) kila wakati wa kutunga mimba, moyo unakuwa umetulia, mzunguko wa damu unakuwa wa kawaida na mwili unakuwa hauna fadhaa na wasiwasi wowote, basi mtoto atafanana na baba yake na mama.”13

2. Halikadhalika, uhusiano mzuri baina mume na mke na mvuto wa nguvu wa kimwili ni vya manufaa kwa mtoto, ambapo hofu na wasiwasi vitakuwa na matokeo tofauti, hasi juu ya mtoto.14

3. Kuwa mwenye wudhuu na kumdhukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwani hili linaleta utulivu na burudiko la moyo na lina athari chanya, nzuri kwenye manii na hivyo kupatikana mtoto mzuri.15

Mwenyezi Mungu analielezea hili ndani ya Qur’ani tukufu, katika Surat ar-Ra’d, aya ya 28:

الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُمْ بِذِكْرِ اللَّهِ ۗ أَلَا بِذِكْرِ اللَّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ {28}

“Wale walioamini na kikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, sikilizeni! Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, nyoyo hutulia!” (Ar-Ra’ad; 13:28).

4. Anza kwa Dua ifuatayo:

Imesimuliwa kutoka kwa Imam al-Baqir (a.s.) kwamba kabla ya kitendo chenyewe, soma yafuatayo:
“Ewe Mola! Niruzuku na mtoto, na umfanye awe mchamungu. Fanya kusiwe na ziada au mapungufu katika kuumbwa kwake, na umjaalie na mwisho mwema.”16

Hali Ya Mwili

Hali ya mwili ya wazazi pia ina athari na matokeo ya kutambulika juu ya mtoto, na inaweza kupelekea kwenye udhaifu na ugonjwa kwa mtoto kama mtu hatakuwa mwangalifu.

1. Usifanye mapenzi ule usiku unaporudi kutoka safarini, au usiku unaokusudia kusafiri asubuhi yake, kwani mtu kwa kawaida anakuwa mchovu na aliyechoka kwenye usiku wa siku hizi. Imesimuliwa vile vile kwamba hili linaleta matokeo ya mtoto kuwa mzururaji na mbea,17 na mtoto huyo atatumia mali yake katika njia potovu.18

2. Usifanye mapenzi katika masaa ya mwanzo ya usiku, ukiwa na mwili uliochoka na kushiba kabisa, kwani hili linapelekea mtoto kuwa mchawi na kuchagua dunia juu ya akhera.19

Bali fanya mapenzi katika masaa ya baadae kabisa ya usiku, wakati kuchoka kwako takriban kumeondoka, na tumbo lako liko tupu. Imegunduliwa pia kwamba mtoto anayetungiwa mimba katika masaa ya baadae ya usiku anakuwa na akili zaidi.20

Kinga Kutokana Na Shetani

Ili kuweza kuzizuia athari za shetani katika usiku huu muhimu, vitendo vifuatavyopia vinapendekezwa kufanyika:

1. Weka nia kwamba unajaribu kutafuta mtoto, kwa ajili ya radhi na mku- ruba kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu

2. Kabla ya kujishughulisha na tendo lenyewe, soma Qur’ani na umshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa neema aliyokupa.

3. Kabla ya kushughulika na tendo lenyewe, anza na: “Najikinga na shari za Shetani,” kwa sababu hili linakuhakikishia kwamba mtoto atakayezaliwa atakuwa hana sifa za shetani.

4. Soma: “Bismillahir-Rahmaanir-Rahyim.”

5. Mkumbuke Mwenyezi Mungu kila mara, hususan wakati wa tendo lenyewe. Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Wakati wowote mtu anapofanya mapenzi na mke wake, Shetani anakuwa yupo. Kisha kama jina la Allah linakumbukwa, Shetani anakwenda mbali sana kutoka hapo, lakini iwapo tendo litatokea na jina la Allah halikutajwa, shetani anachukuwa nafasi kwa kuwa yeye ndie mwenye manii hayo.”21

Imesimuliwa pia kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Wakati wowote unapotaka kufanya mapenzi na mke wako, mkumbuke Mwenyezi Mungu. Kwa sababu yoyote ambaye hatafanya hivyo, na mtoto akazaliwa kutokana naye katika hali hiyo, basi atakuwa anatokana na ushirikina wa shetani. Na usafi au kukosa usafi kwa mtoto kunatambulika kutokana na mapenzi na uadui juu yetu sisi Ahlul-Bayt.”22

6. Soma Dua ifuatayo:

“Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Yeye Mmoja ambaye hapana mungu ila Yeye, Muumba wa mbingu na ardhi. Ewe Mungu wangu! Kama umenipangia katika usiku huu mrithi, basi usimfanye Shetani akawa na ushiriki, sehemu yoyote au fungu ndani yake mrithi huyo, na mfanye awe mu’min mwaminifu, msafi kutokana na Shetani na vitendo vyake viovu (utukufu wako ni mkuu)”23

“Kwa jina la Allah, na kwa Allah. Ee Allah! Muweke shetani mbali na mimi na muweke shetani mbali na kile ambacho una- nineemesha mimi nacho.”24

7. Kazieni mapenzi ya Ahlul-Bayt (a.s.) ndani ya nafsi zenu. Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Wakati mwingine Shetani huja karibu na wanawake kama waume zao.” Alipoulizwa ni namna gani ya kutambua iwapo kama Shetani anayo sehemu katika utungwaji wa mimba za watoto wetu au laa, Imam akajibu akasema: “Kwa njia ya mapenzi au chuki kwetu sisi (a.s.). Hivyo mtu yoyote anayetupenda sisi, Shetani hana sehemu katika kuzaliwa kwake, na yeyote ambaye ni adui yetu sisi, mbegu (manii) yake imetoka kwa Shetani.25

Imesimuliwa katika Hadith kwamba Shetani amesema: “Yeyote ambaye ni adui wa Imam Ali (a.s.), basi bila shaka yoyote mimi nilishiriki katika kile kitendo kati ya baba yake na mama yake.”26

Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Watieni msuku- mo (wafundisheni) mabinti zenu na wanawake urafiki wa familia ya Ali (a.s.) na (hivyo) kuwafanya wabaki na hali (ya moyo safi na kuwa mbali na Akhlaq iliyopinda, mbaya).27

Kiangalizo: Mapenzi juu ya Ahlul-Bayt (a.s.) hayamaanishi kwamba tutamke upendo juu yao tu basi, bali hasa ni kuwachukulia kuwa ni mfano wa kuigwa katika kila jambo la maisha yetu ya kila siku na kujitahidi kufanya kazi ya kuuelekea mfano wao.

8. Hakikisha uhusiano wako unaruhusiwa na ni halali. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Imam Ali (a.s.): “Ewe Ali! Yeyote yule anayenipenda mimi na wewe na Maimam kutokana na kizazi chako, basi (wanapaswa) wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhalali wake huo, kwa sababu haku- na yoyote bali wale ambao ni halali (wa kuzaliwa) ndio wanaotupenda sisi na hakuna yoyote bali wale ambao ni haramu (kwa kuzaliwa) ambao ni maadui zetu.”28

Kwa hakika, wakati wa kipindi cha Imam Ali (a.s.), njia ya kutambua iwapo kama watoto walikuwa wa halali ama laa ilikuwa ni kuwaleta karibu na Imam na kuona kama walimpenda ama hapana.29

Matendo Yasiyoshauriwa Kufanywa

Ni muhimu kufahamu kwamba vingi ya vitendo vilivyotajwa katika sehemu hii vinafanana na vile vilivyoelezwa kwenye mlango wa Adabu za mahusiano ya kujamiiana, pamoja na nyongeza ya jinsi vinavyoathiri mtoto anayezaliwa.

Vitendo Vya Makruhu (Vya Karaha)

Kwa vile vitendo vingine vina athari hasi, mbaya juu ya mtoto kama vile chuki dhidi ya Ahlul-Bayt (a.s.),30 inashauriwa kwamba vitendo vilivy- otajwa hapa chini viwe vinaepukwa:

1. Kuangalia kwenye sehemu nyeti za siri za mwanamke wakati wa kitendo chenyewe hasa, kwani hili linapelekea kwenye upofu wa mtoto atakayezaliwa.31

2. Kuzungumza wakati wa kitendo chenyewe (isipokuwa kwa kudhukuru Allah (s.w.t.).), kwani hili linapelekea kwenye ububu wa mtoto atakayezaliwa.32

3. Kuwa na hinna juu ya mwanaume, kwa vile hili husababisha ukhuntha wa mtoto anayezaliwa (yaani, msichana anakuwa na tabia za kiume na kinyume chake).33

4. Kufikiria au kutamani mwanamke mwingine wakati wa kitendo, kwa vile hili linapelekea kwenye wenda wazimu wa mtoto atakayezaliwa.34

5. Kufanya mapenzi mbele ya mtoto, ambaye ama anaweza kuona au kusikia sauti za kitendo hicho, kwani hili linaleta matokeo ya mtoto huyo kutokuja kuokolewa (kutoka kwenye moto wa Jahannam) na kuwa mzinifu.35

6. Kufanya mapenzi wakati ambapo kuna mtu aliyeko macho ndani ya nyumba, ambaye anaweza kuona au kusikia sauti za kitendo hicho, kwani hili linaleta matokeo ya mtoto kutokuja kuokolewa (kutoka kwenye moto wa Jahannam) na kuja kuwa mzinifu.36

7. Kufanya mapenzi kwa kusimama wima, kwani hili linapelekea mtoto kuwa na tatizo la kukojoa kitandani.37

8. Kufanya mapenzi juu ya paa la nyumba, kwani hili linaishia kwenye mtoto kuwa mnafiki, na mmbea (mzushi).38

9. Kufanya mapenzi chini ya mti wa matunda, kwani hili linapelekea mtoto kuwa muuaji na kiongozi wa udhalimu.39

10. Kufanya mapenzi chini wa mwanga wa moja kwa moja wa jua, kwani hili linapelekea mtoto kuwa masikini, hata mpaka kifo chake.40

11. Kufanya mapenzi wakati mwanaume yuko katika hali ya Muhtalim (yaani, anapokuwa na hali ya janaba kwa ndoto usingizini mwake) na kabla ya kuchukua Wudhuu au Josho, kwani hili linasababisha mtoto kuja kuwa mwendawazimu.41

Ni muhimu vilevile kuzingatia akilini vitendo vinginevyo vile vyenye karaha – Makruh – wakati wa taratibu za kawaida za mahusiano ya kujamiiana (kama zilivyoelezwa kwenye Mlango wa 2: Adabu za Mahusiano ya Kujamiiana). Hivi ni vifuatavyo:

1. Kuwa na Qur’ani au Majina ya Allah (s.w.t.). mwilini mwako.
2. Kufanya mapenzi ukiwa uchi kabisa (bila cha kujifunika).
3. Kufanya mapenzi barabarani au ndani ya boti.
4. Kuelekea au kukipa mgongo Qibla.
5. Kukataa kujamiiana (kwa sababu mbalimbali – za visingizio).

Kiangalizo: Mara mwanamke anapokuwa kaishapata ujauzito, inashauri- wa kujiepusha kutokana na kufanya mapenzi bila ya Wudhuu, kwani hili linasababisha mtoto kuwa masikini na upofu wa ndani42

Nyakati Zinazoshauriwa

Ni muhimu kutambua kwamba nyingi ya nyakati zilizotajwa katika mlan- go huu ni sawasawa na zile zilizotajwa kwenye mlango wa Taratibu za Kujamiiana, pamoja na nyongeza ya jinsi zinavyomuathiri mtoto anayezaliwa.

Nyakati Zinazofaa (Mustahab)

1. Usiku wa Jumapili (kuchea Jumatatu). Mtoto anayetungwa kwenye mimba usiku huu atakuwa mwenye kuridhika na chochote Mwenyezi Mungu Mtukufu atakachomjaalia nacho, atakuwa na kumbukumbu nzuri na atakuwa Hafidh (mwenye kuhifadhi) wa Qur’ani Tukufu.43

2. Usiku wa Jumatatu (kuchea Jumanne). Mtoto anayetungiwa mimba kwenye usiku huu atakuwa na ustawi au neema ya Uislamu, na fursa ya Shahadat na hatoadhibiwa pamoja na washirikina. Atakuwa na kinywa kilicho na harufu nzuri na moyo wa huruma. Atakuwa ni mtu mwenye kutoa sadaka na ulimi wake utasalimika na kusema uongo, kusengenya au kutoa shutuma za uongo.44

3. Usiku wa Jumatano (kuamkia Alhamisi) Mtoto anayetungwa mimbani kwenye usiku huu atakuwa mtawala miongoni mwa watawala wa Shari’ah, au mwanachuoni miongoni mwa wanachuoni
wa kidini.45

4. Mchana wa Alhamisi, wakati wa kumalizika kwa mchana. Huu ndio muda muafaka, bora kabisa na umependekezwa sana kwa ajili ya utun- gaji mimba. Shetani hatasogea karibu na mtoto anayetungwa kwenye mimba usiku huu mpaka anapokuja kuzeeka na usalama wa dini na dunia utakuwa wake.46

5. Usiku wa Alhamisi (kuchea Ijumaa). Mtoto anayetungwa mimbani kwenye usiku huu atakuja kuwa mubalighin, msemaji fasaha na msomaji wa Qur’ani.47

6. Siku ya Ijumaa, baada ya wakati wa Alasiri. Mtoto atakayetungwa mimbani wakati huo atajulikana sana miongoni mwa watu wenye busara na wanachuoni wakubwa.48

7. Siku ya Ijumaa, baada ya wakati wa swala Isha. Mtoto atakayetungwa kwenye mimba wakati huo atakuwa anatokana na watu wema na wanaofaa.49

8. Usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani.50

Nyakati Zisizopendekezwa

Ni muhimu kutambua kwamba nyingi ya nyakati zilizotajwa katika mlango huu ni sawasawa na zile zilizotajwa katika mlango wa Taratibu za Kujamiiana, pamoja na nyongeza ya jinsi zinavyoathiri mtoto anayezaliwa.

Nyakati Haramu

1. Wakati wa kipindi cha hedhi ya mwanamke, hata katika ile siku ya mwisho, mpaka tone la mwisho la damu litakapodondoka. Ujauzito bado unawezekana, na mtoto atakayetungwa mimbani atasumbuliwa na (phagedemic ulcers) – aina ya vidonda vya tumbo na ukoma.51

Imesimuliwa vile vile kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Hakuna adui kwetu sisi Ahlul-Bayt, isipokuwa yule ambaye amezaliwa kwa njia ya haramu na yule ambaye alitungwa mimbani wakati wa hedhi.52

Ni muhimu vile vile kuzingatia akilini vitendo vingine haramu wakati wa taratibu za kawaida za kujamiiana (kama zilivyotajwa katika Mlango wa 2: Taratibu za Kujamiiana): Hizi ni:

1. Wakati wa Nifaas
2. Wakati wa saumu katika mwezi wa Ramadhani
3. Wakati katika hali ya Ihraam
4. Wakati ambapo inaweza kusababisha madhara makubwa ama kwa mume au kwa mke.

Nyakati Za Karaha (Makruh)

1. Kati ya asubuhi sadiki (Adhana ya swala ya al-Fajr) na kuchomoza kwa jua.53
2. Kati ya kuzama kwa jua mpaka kupotea kwa wekundu wa angani.54
3. Usiku wa kupatwa kwa mwezi.55
4. Mchana wa kupatwa kwa jua.56
5. Wakati wa tetemeko la ardhi (au matukio mengine yanayolazimu Swala – Salat al-Ayat).57

Kama atatungwa kwenye mimba katika nyakati hizo hapo juu, wazazi hawataona sifa yoyote wanayoipenda kwa mtoto wao, kwa sababu hawakuziona hizi ishara za Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa za muhimu.58

6. Katika tarehe ya mwanzo wa mwezi (isipokuwa mwezi mosi ya Ramadhani, ambapo ni mustahab), katikati ya mwezi (unapoonekana mwezi kamili) na mwishoni mwa mwezi (kunapokuwa hakuna mwezi), kwani itakuwa ni chanzo cha hali ya wendawazimu, ukoma mweusi na kupooza kwa mama na mtoto.59

Hadithi nyingine inasimulia kwamba kutunga mimba wakati wa mwanzo wa mwezi na katikati ya mwezi kunapelekea kwenye wendawazimu na mtoto kutawaliwa na Jinni,60 na kutunga mimba wakati wa mwisho wa mwezi kunaongezea uwezekano wa kuharibika kwa mimba.61

7. Baada ya swala ya Adhuhuri (mpaka takriban karibu na wakati wa Asr), kwani hii inapelekea mtoto kuwa na makengeza.62

8. Kati ya Adhana na Iqaamah kwani hii inapelekea kwa mtoto kuwa shauku ya kuua.63

9. Usiku wa Eid al-Fitr, kwani hii inasababisha katika mtoto kuwa chanzo cha maovu.64

10. Usiku wa Eid al-Udh’haa, kwani hilo linapelekea kwa mtoto kuwa na vidole (sita) 6 au (vinne) 4.65

11. Usiku wa nusu ya Shaaban (mwezi 15), kwani hili linapelekea kwenye mtoto kuwa na hali ya ndege mbaya (nuksi au kisirani) na alama nyeusi usoni mwake.66

12. Siku ya mwisho ya mwezi wa Sha’ban, kwani hii inapelekea kwa mtoto kuwa msaidizi na mkusanyaji kodi wa madhalimu.67

13. Usiku wa Ashuraa’.

Kupanga Mimba

Tunaweza kuhitimisha kutokana na yote hayo hapo juu kwamba lengo la mahusiano ya kijinsia ni la njia mara mbili: kuridhisha haja ya mtu ya kimaumbile na kuzaa.

Miongozo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.) kwa wazi kabisa inaonyesha urefu wa muda ambao mtu anaweza kuchukua ili kupata mtoto anayefaa. Mahusiano ya kijinsia kwa ajili ya utungaji mimba yanapaswa kufanywa kwa tofauti kabisa, vyote kiakili na kivitendo.

Wakati mwingine, inaweza kutokea kwamba kutokana na ukosefu wa taar- ifa au sababu nyinginezo, mazingira ya upatikanaji wa mimba ya mtoto yanakuwa hayakupangwa. Taarifa hiyo hapo juu inaweza kwa hiyo kuwa chanzo cha wasiwasi kwa ajili ya wazazi kuhusu matokeo yanayowezekana ya utungaji wa mimba katika nyakati na kwa vitendo visivyopendeza.

Ni muhimu kuzingatia akilini kwamba kuna mambo mengi yanayochangia katika utengenezaji wa mtoto, kama vile hali asili ya kurithi (genetics), lishe, hali ya kijamii, na kadhalika.
Taarifa zilizotajwa hapo juu ni baadhi tu ya haya mambo ambayo yanaweza kuathiri mtoto aliyezaliwa.

Kwa nyongeza, inawezekana kuyakinga matokeo ya kijyume yanay- owezekana kutokea kwa vitendo kama vile sadaka, kusoma Qur’ani na kutafuta tawasali (uombezi mtukufu) kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s.).68

 • 1. Surat al-Baqarah, aya ya 168: “Enyi watu! Kuleni katika vile vilivyomo ardhini vilivyo halali na vizuri.”
 • 2. Vilevile inajulikana kama Succory, huu ni mtishamba ambao mizizi yake iliyokaushwa, kusagwa na kukaangwa inatumika kama kighushi cha, au kitu mbadala na kahawa.
 • 3. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 25, Uk. 104, namba 31499
 • 4. al-Kafi, Jz. 5, Uk. 35
 • 5. Biharul-Anwar, Juz. 66, Uk.278
 • 6. Ibid, Juz. 104, Uk. 80
 • 7. Makatimul-Akhlaq, uk. 88
 • 8. Barqaa’i, Uk. 549
 • 9. Biharul-Anwar, Juz. 81, Uk. 101
 • 10. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 25, uk. 165 hadithi ya 31538
 • 11. Bahdasht Izdawaaj az Nazr Islam, Uk. 89
 • 12. Izdawaaj Asaan; Uk k. 245
 • 13. Biharul-Anwar, Jz. 14. Uk. 379
 • 14. Rayhaan-e Beheshtii, Uk. 33
 • 15. Rayhaan-e Beheshtii, Uk. 39
 • 16. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 117, Hadithi ya 25180
 • 17. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, uk. 253, Hadithi ya 25560
 • 18. Hilliyatul Muttaqin, uk. 112-114
 • 19. Ibid.
 • 20. Rayhaan-e Beheshtii, uk. 40
 • 21. Al-Kafi, Jz. 5, uk. 502
 • 22. Sharh Man laa Yahdhural Faqii, Jz. 8, Uk . 202
 • 23. Al-Kafi, Jz. 5, Uk. 503
 • 24. Al-Kafi, Jz. 5, uk. 503
 • 25. Tafsir Nur al-Thaqalayn, Jz. 3, Uk . 183
 • 26. Niyazhaa wa Rawabith Maadaraan wa Janiin, Uk. 76
 • 27. Sharh Man laa Yahdhural Faqii, Jz.3, Uk. 493
 • 28. Al-Amaali cha Sheikh Saduq, Jz. 7, Uk. 383
 • 29. Manaaqib ya Ibn Shahr Ashuub, Jz.3, Uk k. 207
 • 30. Biharul-Anwar, Jz. 39, uk. 278, Hadithi ya 87
 • 31. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 122, Hadithi ya 25197
 • 32. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 121, Hadithi ya 25195
 • 33. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 125, Hadithi ya 25205
 • 34. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
 • 35. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, uk. 133, Hadithi ya 25223
 • 36. Niyaazhaa wa Rawaabith Jinsii was Zanaashuii, Uk. 64
 • 37. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
 • 38. Ibid. (Hilliyatul Muttaqiin, uk. 112-114)
 • 39. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
 • 40. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
 • 41. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20 Uk . 148, Hadithi ya 25271
 • 42. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 148
 • 43. Hilliyatul Muttaqiin, Uk k. 112-114
 • 44. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
 • 45. Hilliyatul Muttaqiin Uk. 112-114
 • 46. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
 • 47. Hilliyatul Muttaqiin Uk. 112-114
 • 48. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
 • 49. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
 • 50. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
 • 51. Hilliyatul Muttaqiin, Uk 110
 • 52. Niyaazhaa wa Rawaabith Jinsii was Zanaashuii, uk. 69
 • 53. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 126-127, Hadihi ya 25207
 • 54. Ibid
 • 55. Ibid
 • 56. Ibid
 • 57. Ibid
 • 58. Niyaazhaa wa Rawaabith Jinsii was Zanaashuii, uk. 59
 • 59. Wasa’ilush-Shi’ah, Juz. 20, Uk 129, hadithi ya 25214
 • 60. Wasa’ilush-Shi’ah, Juz. 20, Uk. 129, hadithi ya 25212
 • 61. Wasa’ilush-Shi’ah, Juz. 20, Uk. 129, hadithi ya 25208
 • 62. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
 • 63. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
 • 64. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
 • 65. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
 • 66. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
 • 67. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
 • 68. Imethibitishwa na ofisi ya Ayatullah Sistanii, Qum.