Maswali Na Majibu

Kisha yule asiyeruhusu kukusanya Sala mbili amepinga kwa hoja mbali mbali huku akitumia Hadithi ya Ibnu Abbas na za wengine kama hoja katika suala hili. Zifuatazo ni hoja zake na majibu yake:

Ya Kwanza: Mgongano Wa Hadithi Ya Kukusanya Na Ile Ya Hanashu:

Habari za kukusanya zinapingana na habari aliyoitoa At- Tirmidhiy toka kwa Hanash toka kwa Ikrima toka kwa Ibnu Abbas toka kwa Mtume alisema kuwa:
“Atakayekusanya kati ya Sala mbili bila udhuru wowote atakuwa kaja kwenye mlango kati ya milango ya madhambi makubwa.”1

Nasema: kuwepo Hanash katika mapokezi yake ni dalili tosha juu ya udhaifu wa riwaya hii, na Hanashi ni lakabu ya Huseini bin Qaysi Ar-Rahbiy Al-Wasitwiy na yeye ni dhaifu mkubwa!

Ahmad amesema: “Huachwa.”
Bukhari amesema: “Hadithi zake hukanushwa wala haiandikwi Hadithi yake.”
Abu Zar'ati na Ibnu Mu'ini wamesema: “Ni dhaifu.” An- Nasaiy amesema: “Si mkweli.”

Marat amesema: “Huachwa.” As-Saadiy amesema: "Hadithi zake hukanushwa sana.”
Ad-Daruqutniy amesema: “Huachwa.” Na Al-Dhahabiy ameiweka Hadithi hii katika fungu la Hadithi zinazokanushwa.2

Al-Uqayly amezungumzia Hadithi yake: “Atakayekusanya kati ya Sala mbili bila udhuru wowote atakuwa kaja kwenye mlango kati ya milango ya mad- hambi makubwa.” Akasema: “Haifuatwi wala haijulikani isipokuwa kupitia yeye, wala haina chanzo. Imesihi toka kwa Ibnu Abbas kuwa Mtume alikusanya kati ya Adhuhuri na Al-Asr.”3

Ninaongeza kuwa katika mapokezi yake yumo Ikrima ambaye naye ni dhaifu, Hadithi zake haziwi hoja.

Ya Pili: Mgongano Wa Hadithi Ya Kukusanya Na Ile Ya Usiku Wa Harusi

Huenda mtu akadhani kuwa riwaya zinazoruhusu kukusanya Sala mbili kwa halisi zinapingana na Hadithi ya usiku wa harusi aliyoipokea Muslim.

Al-Alusiy ameinukuu ndani ya tafsiri yake toka kwa Ibnul-Hamam kwa kusema: “Ibnul-Hamam amesema: ‘Hakika Hadithi ya Ibnu Abbas inapingana na aliyoyapokea Muslim katika Hadithi ya usiku wa harusi kuwa Mtume alisema: Usingizini hakuna uzembe bali uzembe ni katika hali isiyo ya usingizi kwa mtu kuchelewesha Sala mpaka uingie wakati wa Sala nyingine.”

Al-Alusiy baada ya kunukuu maneno haya ya Ibnul- Hamam alisema: Kuna nukta nyingi za kuhoji.4 Katika mdahalo huu kuna nukta nyingi za kuhoji bali za kujibu.

Kwanza: Hadithi ya harusi haijumuishi kukusanya kwa kutanguliza bali inahusika na kukusanya kwa kuchelewe- sha tu kwani alisema: “Kuchelelewesha Sala mpaka uingie wakati wa Sala nyingine.”

Pili: Kitendo cha Ibnu Abbas kinaonyesha kuwa kuku- sanya kwa Mtume kulikuwa kwa kuchelewesha kwa mujibu wa riwaya aliyopokea Muslim kama ilivyotangulia kuwa: Siku moja Ibnu Abbas alitutolea muhadhara baada ya Al-Asr mpaka lilipokuchwa jua na nyota zikaan- za kuonekana. Watu wakawa wanasema: ‘Sala! Sala! Mara akaja mtu mmoja wa koo ya Bani Tamim huku akisisitiza: Sala! Sala! Ndipo aliposema Ibnu Abbas: ‘Je unanifundisha Sunna? Eee usiye na mama we!’

Kisha akasema: ‘Nilimuona Mtume amekusanya baina ya Adhuhuri na Al-Asr, na Magharibi na Isha.’ Abdallah bin Shaqiqi anasema: ‘Hilo likanitia shaka moyoni mwangu, mara moja nikaenda kwa Abu Huraira nikamuuliza, akathibitisha habari ya Ibnu Abbas kuwa ni kweli.”5

Ni Hadithi ipi kati ya hizo mbili inafaa kuchukuliwa? Hadithi inamaanisha kuchelewesha Sala ya Isha mpaka unaingia wakati wa Sala ya alfajiri, linalounga mkono maana hii ni kupatikana riwaya katika usiku wa harusi, usiku ambao mtu anajishughulisha na mambo mpaka wakati wa alfajiri unaingia.

Ya Tatu: Hadithi Ya Habib Bin Thabiti Si Hoja

Riwaya ya tatu aliyoitoa Muslim ndani ya upokezi wake yumo Habib bin Abi Thabiti.

Al-Khatabi ndani ya Maalimu yake ameizungumzia akasema: “Hadithi hii hawaisemi wanazuoni wengi zaidi wa sheria, upokezi wake ni safi isipokuwa hawakuzungumza kuhusu Habib.” 6

Anajibiwa kuwa: Kusema kuwa wanazuoni wengi wa sheria hawaisemi ni kweli, lakini wapo wanaoisema na kuitolea fat'wa, majina yao yameshatangulia.

Ama kuhusu wanazuoni wengi sababu ya kutokuichukua ima ni kwa kuwa kutenganisha ndio kunakubaliana na ubora (Ihtiyati), au kwa kuwa inatofautiana na hali aliyoendelea nayo Mtume.

Ama kuhusu ubora ni kuwa imeshatangulia kuwa katika mazingira yetu haya kutoa fat'wa ya kutenganisha ni kinyume na ubora, kwa sababu fat'wa hiyo inapelekea watu kuacha Sala.

Ama kuhusu kitendo cha Mtume ni kuwa yeye mwenyewe alikusanya ili aufahamishe umma wake kuwa kuendelea kwake kutenganisha ni Sunna wala si faradhi.

Ama aliyoyasema kuhusu dosari walizozungumza juu ya Habib bin Thabit ni kinyume na aliyoyataja Ad-Dhahabiy ndani ya kitabu Mizanul-iitidal kwani amesema:

“Watu wote wa Sahih Sita wametoa hoja kutumia Hadithi hii bila kusita. Akasema: Yahya bin Mu'ini: na jamaa wamethibitisha ukweli wake.”7

Zaidi ya hapo ni kuwa riwaya hii inapatikana ndani ya moja kati ya Sahih mbili ambazo masunni wameafikiana juu ya usahihi wa Hadithi zake na juu ya kufanyia kazi yaliyomo humo.

Na mwisho wa dua yetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Bwana wa wote.ulimwengu

Imetarjumiwa na:
Hemedi Lubumba Selemani

  • 1. Sunanut-Tirmidhiy: Juz. 1, Uk. 356
  • 2. Mizanul-Itidali, Juz. 1, Uk. 546 maelezo namba 2043
  • 3. Tahdhibut-Tahadhibu, Juz. 1, Uk. 538
  • 4. Ruhunil-Maani, Juz. 15 Uk. 134 tafsiri ya Aya: "Simamisha Sala lipindukapo jua"
  • 5. Angalia riwaya namba 6
  • 6. Maalimus-Sunan, Juz. 2, Uk. 55, Hadith Na. 1167
  • 7. Mizanul-Itidal, Juz. 10, Uk. 1690