read

Mgawanyo Wa Nyakati Ndani Ya Fiqhi Ya Kisunni

Huenda mtu asiyejua akadhani kuwa mgawanyo huu wa nyakati unahusu fiqhi ya Imamiyya tu, bali ni kuwa mgawanyo huu wa nyakati katika aina tatu unahusu fiqhi zote mbili japokuwa kunatofauti kuhusu muda wa wakati.

Ndani ya Sharhul-Muhadhabu An-Nawawiy amesema: “Tawi: Adhuhuri ina nyakati tatu: Wakati wa ubora, wakati wa hiyari na wakati wa udhuru, hivyo wakati wa ubora ni mwanzoni mwa wakati, na wakati wa hiyari ni baada ya wakati wa ubora mpaka mwisho wa wakati, na wakati wa udhuru ni wakati wa Al-Asr kwa mwenye haki ya kukusanya kwa ajili ya safari au mvua.”

Kisha akasema: Al-kadhi Huseini amesema: “Adhuhuri ina nyakati nne: Wakati wa ubora, wakati wa hiyari, wakati wa ruhusa, na wakati wa udhuru.
Hivyo wakati wa ubora ni pale kivuli cha kitu kilichosimama kitakapofikia robo ya kipimo cha kitu hicho, na wakati wa hiyari ni kitakapofikia nusu yake, na wakati wa ruhusa ni kitakapolingana kivuli na hicho kitu na hapo ndio mwisho wa wakati.

Na udhuru ni wakati wa Al-Asr kwa mwenye kukusanya kwa ajili ya safari au mvua.1

  • 1. Al-Majmuu Juz.3 Uk. 27