read

Hukumu Katika Hall Ya "Ihtidhaar" (Kukata Roho)

Mambo anayofanyiwa mtu anapokata roho na baadaye: Mwislamu anapofika katika hali ya Ihtidhari (wakati wa ukata roho), mwanamume au mwanamke, mkubwa au mdogo; ni wajibu (ni fardhi) kwake kama anajiweza na anayo fahamu na kama si hivyo basi kwa wale watu waliohudhuria hapo wamlaze huyo mgonjwa chali, miguu na nyayo zake zielekee Qibla, na ikiwa haimkiniki kufanya hivyo kwa ukamilifu basi kadri itakavyomkinika waanye, na ikiwa haimkiniki kabisa basi wamkalishe kuelekea Qibla. Na kama hiyyo pia haimkiniki basi wamlaze mkono wa kulia au wa kushoto kuelekea Qibla.

Ni Sunna: Wakati ule waliohudhuria wamfahamishe na kumtamkia 'Shaadatain' na majina matakatifu ya Maimamu kumi na wawili [a] na itikadi zote za haki, akumbushwe (kwa utaratibu na upole si kwa haraka na ukali aweze kufahamu kwa kukaririwa kaririwa).... Na pia asomeshwe dua maarufu iitwayo, "KALIMAA-TUL FARAJ nayo ni hii:

LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAA-HUL HALIMUL KARIM, LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAA-HUL ALIYYUL ADHIM, SUB-HAA-NAL-LAA-HI RAB-BIS-SAMAA WAA-TIS-SAB-I, WA RAB-BIL ARA-DHIY-NAS-SABI-WAMAA FIY-HIN-NA, WAMAA BAY-NAHUN-NA, WAMAA TAH-TA-HUN-NA WARAB-BIL AR-SHIL ADHIYM WAL-HAMDU LIL-LAA-HI, RAB-BIL AA LAMIN, WAS SALA'A-TU ALAA MUHAMMADIN WA AALIHIT-TAYYIBEEN.

Ni Sunna: Wakati ule asomewe sura ya YAASIN, WAS-SAAFATI, AHZABI, AYATUL KURSI", na aya tatu za mwisho za sura ya BAQARAH, na pia kama iki Mkinika asomewe sura zaidi. Kwa kufanya haya yule mgonjwa atakata roho kwa raha bila ya taabu.

Mwenye Janaba na mwanamke mwenye hedhi (ujusi) wakati wa kukata roho wasije na wasimsogelee, kwani (Malaika hawatahudhuria ikiwa watu hao wapo hapo).