read

Mambo Ya Faradhi Baada Ya Kuogeshwa Maiti Hadi Kuzikwa Kwake

Haifai wakati anapooshwa maiti kuweko moto au kiteso cha kufukiza wala wakati wa mazishi hadi mwisho.

AL-HUNUUT: Kupakwa maiti kafuri mahali maalum ni faradhi kwa Waislamu baada ya kumwosha na kupanguswa (afutwe vizuri kwa nguo kavu) maiti kabla ya kusaliwa na kuzikwa apakwe 'Kafuri' laini sehemu saba (viongo vya kusujudia) navyo ni kipaji, viganja viwili, magoti mawili, ncha za vidole gumba viwili. Na sunna kupakwa kwenye pua, vile vile sunna kuwekwa pamba kwenye utupu wa maiti na kila penye tundu. Wakati wa kupaka HUNUUT ni baada ya kuogeshwa na kupanguswa na kabla ya kuvikwa sanda au wakati wa kuvikwa sanda.

Ikiwa Kafuuri haikupatikana hatakumwoshea maiti, basi hapo faradhi ya HUNUUT inaondoka, na kama amekogeshwa na Kafuuri lakini haikuzidi kwa ajili ya HUNUUT basi si kitu.

AL-HUNUUT: Kupakwa maiti Kafuri ni faradhi kwa kila maiti mdogo, mkubwa mwanamke, mwanamume, huru au mtumwa isipokuwa maiti yule aliyekufa hali yuko katika Ihramu ni haramu kumpaka Kafuri. Kafuri lazima iwe mpya si kukuu yenye kupotea harufu yake, na pia lazima iwe laini iliosagwa.