read

Namna Ya Kumkafini (Kumvisha Sanda Maiti)

Baada ya kukatwa mapande hayo, kwanza utatandika ile shuka kubwa ya Namba 3: Na ndio ya kwanza, baadaye utatandika Kanzu Kanzu kwa kuikunjua upande mmoja, (na hii ni ya pili), baadaye utaliweka shuka kwa upana kwa kukunjua. Ukisha tandika yote hayo vipande vitatu vya vitambaa vilivyo wajibu, basi sasa atalazwa maiti juu ya mapande yote ya sanda.

Kwanza utamfunga shuka na kuondoa kile kitambaa ulichotumia wakati wa kumwoshea kuficha utupu wake.

Utaurejesha ule upande wa kanzu ulioukunjua kwa kupitisha kichwa cha maiti kwenye shingo.

Ikiwa umeshafanya mambo ya 'AL-HUNUUT' basi utaikunja hiyo shuka kubwa kwa kuiweka ncha moja juu ya pili, na kama bado hujampaka AL-HUNUUT na mambo yake basi fanya, ndipo umalize kumfunika.