read

Sanda Ya Maiti Iliyo Wajibu

Ni faradhi kuvishwa maiti mwanamume au mwanamke mkubwa au mdogo vipande vitabu vya nguo:

(1) Kanzu (2) Shuka (3) Shuka

(1) Kanzu: Bila kuishona, itobolewe sehemu ya shingo tu halafu kitumbukizwe kichwa. Kuanzia begani hadi nusu ya miguu kupita goti.

(2) Shuka: Kama anavyovaa mwanamume kutoka kitovuni

hadi magotini, na ni bora si wajibu kuanzia kifuani hadi chini ya magoti.

(3) Shuka: Kitambaa kikubwa cha kumfunika mwiIi wake wote mzima mbele na nyuma kwa urefu hata uweze kufunga pande zote mbili (upande wa kichwa na upande wa miguu) na kwa upana, ncha moja iweze kuja juu ya ncha va pili

SUNNA: Si wajibu bali ni sunna (a) Kuvishwa mwanamume kiIemba, mwanamke sidiria na ushungi (b) Nguo nyeupe isiyokuwa na rangi yoyote (c) Nguo iwe ya pamba (d) Ni bora kama aliwahi kuhiji basi 'IHRAMU' itumiwe au nguo za kusalia ambazo akisali nazo.

SANDA: Kwa kiasi kilichofaradhi lazima gharama yake na gharama ya vitu vya kumwoshea maiti, maji, Sidri, Kafuri, ardhi pa kuzikiwa na gharama zake zote haya hutoka katika asili ya mali ya maiti kabIa ya kulipwa deni au kufuatwa wasia wake. Na yako mambo ya sunna katika sanda ikiwa ameusia sanda itolewe katika theluthi (1/3) ya mali yake, au ameusia theluthi ya mali atumiliwe yeye basi sanda itatolewa humo, na kama hakuusia theluthi (1/3) basi kiasi kilichowajibu kitatolewa katika asili mali.

Sanda ya mke juu ya mumewe hata ikiwa mke anayo mali ya kutosha, na vivyo hivyo yule mke aliyeachwa kwa mara ya kwanza au ya pili na bado yupo katika eda, mume lazima atoe sanda. Ikiwa mtu mwingine yoyote ametoa sanda ya yule maiti (mwanamke) basi faradhi humuondokea mume.

Ni sunna kwa kila mwislamu kutayarisha SANDA yake na kuiweka nyumbani, pia ni sunna kuiangalia hiyo sanda kila mara. Mtukufu ,Mtume (s.a.w.) amesema, "Mwenye kutayarisha sanda yake, huwa kila siku zipitazo kila huandikwa thawabu kila apoiangalia, na kwa kufanya hivyo hatahesabiwa miongoni mwa waliomsahau Mwenyezi Mungu.