read

Sunna Za Kumwosha Maiti

Awekwe mahala palipo juu, kama kitanda, au baraza n.k. na mahala pa kuwekea kichwa chake painuke zaidi kuliko miguu.

Alazwe chali, miguu na nyayo zielekee Qibla (kama tulivyotaja katika mambo ya hali ya 'IHTIDHARI'.

Maiti avuliwe nguo zote kwa upande wa chini (miguuni) hata ikibidi itatuliwe (ichanwe) lakini kwa idhini ya warithi wa maiti.

Aoshwe chini ya sakafu, au banda au hema asioshwe chini ya mbingu.

Uchimbwe "UFUO" wa kuingia maji ya kuoshea.

Mwili wake wote uwe wazi isipokuwa utupu wake.

Ufunikwe utupu wake hata ikiwa mkoshaji au watu wanaomuosha ni miongoni mwa wale wanaoruhusiwa kumwangalia.

Mkoshaji apitishe mkono wake juu ya tumbo la maiti kwa taratibu lakini ikiwa maiti mwenye mimba ambaye mtoto pia amekufa tumboni hairuhusiwi kufanya hivyo.

Mkoshaji asimame upande wa kulia wa maiti.

Aanze kuosha upande wa kulia wa kichwa cha maiti.

Mkoshaji aoshe mikono yake mara tatu hadi begani kwa kila 'GHUSLI' tatu.

Mwoshaji anapokuwa anaosha kiwiliwili cha maiti anatakiwa aseme hivi: "Ewe Mola! Hiki ni kiwiliwili cha mja wako mwenye imani (Mumin) na umetoa roho yake kutoka kiwiliwili chake, na umetenga kati yao, basi msamehe kwako." Hasa wakati anapomgeuza.

Asitangaze mwoshaji aibu yoyote aliyoiona mwini mwa maiti.