read

Thawabu Ya Kwenda Kuzuru Makaburi Ya Ndugu Zetu Mumineen (Wenye Imani)

Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliwaambia Masahaba: "Watuzeni maiti wenu? Wakauliza, "Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu tuwatuze nini maiti?" Akajibu Sadaka na Dua, tena akaendelea kusema, "Hakika roho za wenye imani siku ya Ijumaa kwenye mbingu ya kwanza sawa na mahala walipokuwa wakikaa majumba yao na kila mmoja wao hupiga kelele kwa sauti ya kuhunisha na kulia na husema, Enyi watu wangu, watoto wangu, baba na mama yangu na majamaa zangu, tuonee huruma na Mwenyezi Mungu Atakuoneeni huruma, kwa mali hiyo mliyo nayo ilikuwa mikononi mwetu, sasa haipo mikononi mwetu, mateso na hesabu tunafanyiwa sisi na faida yake wanafaidi wengine". Na kilamoja (roho) humpigia kelele jamaa zake.

Tuonee huruma kwa kutoa sadaka 'dirham' moja (pesa za zama zile) au kwa kutoa mkate kumpa maskini, au kwa nguo kumvisha asiekuwa na nguo, na Mwenyezi Mungu atakuvisheni nguo za "Janah" (Pepo). Baadaye Mtukufu Mtume (s.a.w) akalia na Masahaba pia wakalia, na kilio kilimshika kwa wingi hata hakuweza kusema. Baadaye akasema "Hao ni ndugu zenu katika dini (Imani) sasa wameshageuka udongo na mifupa imesagika baada ya kuishi humu duniani kwa raha na furaha, basi wanapiga kelele na kusema, "Ole juu yetu, laiti katika uhai wetu tungali toa sadaka na kutenda mazuri kwa (pesa zetu) hizo tulizokuwanazo katika njia ya Mwenyezi Mungu leo tusengelikuwa muhutaji wenu". Basi wanarudi wanyonge na huku wanpiga kelele, "Haraka toeni Sadaka kwa maiti wenu".

Inafaa kwa Mwislamu kila wiki kwa uchache hasa siku AIhamisi awakumbuke wafu wake kwa kufika kwenye makaburi yao, hii ni Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) akiwaamrisha Masahaba wake kuzuru makaburi.

Amepokea Bi Aisha (R.A.) na Abu Hurayrah (R. A.) kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.) amesema, "Amekuja Jibrili kwangu na akaniambia kwamba "Mola wako Anakuamrisha uende kwa watu wa 'AL-BAQEE' makaburini mwa watu wa Madina na uwaombee waghufuriwe". Nikasema (Aisha), "niseme nini ninapofika makaburini?" Akasema, Sema, "AS-SALAA-MU ALAA AHLID-DIYAAR, MINAL MU'MINEE-NA- WAL MUS-LIMEEN. YARHAM UL-LAA-HUL MUSTAK-DIMEE-NA-MIN-NAA, WAL MUS-TA'A-KHIREEN, WA IN-NAA IN-SHAA-AL-LAAHU Bl-KUM, LAA-HI KUUN.

Licha ya kuwepo wapokezi wa hadithi kuhusu jambo hilo kutokana na wanachuoni, wa Ki-Shia vile vile wamepokea hadith hizo wanachuoni wa Ki-Sunni nao ni: Bwana Muslim katika Saheeh yake, na Bwana Bayhaki katika 'Sunan' yake na pia Bwana Ahmad Bin Hambal, Bwana Abudaud, Bwana Tirmizi, Bwana Nasaina Bwana Baghawi.

Ni sunna unapofika kwenye kaburi uelekee Qibla, weka mkono kwenye hilo kaburi na soma mara saba (7) sura ya Innaa Anzalnahu (5:97) na pia bora usome sura ya AL-FAATlHA (S:1) na sura ya AL-FALAQ (5:113) na WAN-NASI (S:114) na sura ya QUL-HUWL-LAAHU (S:112) na Ayatul-Kursi kila moja mara tatu.

Ni sunna unapoingia makaburini usome:

"BlS-MIL-LAA-HIR-RAH-MAA-NIR RAHEEM, ASSALAA-MU ALAA AHLI LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, MIN AH-LI LAA-ILAA-HA IL-LAL LAAHI YAA AH-LA LAA-Llaa-HA, IL-LAL-LAAH, BI-HAK-KI- LAA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, KAY-FA WAJAD-TUM KAULA LAA-ILAA-HA-IL-LAL-LAAH MIN LAA ILAA-HA IL-LAL-LAAH, YAA LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAAH, BI HAK-KI LA-ILAA-HA IL-LAL-LAAH, IGH-FIR LIMAN KAA-LA LAA-ILAA-HA, IL-LAL-LAAH WAH-SHUR NAA, FIY ZUM-RATI MAN KAA-LA, LAA-ILAA HA IL-LAL-LAA-HU, MUHAM-MADUN RASUU-LUL-LAAH ALY-YUN WALIY-YUL-LAAH

Kwa kusoma haya Mwenyezi Mungu atambarikia msomaji thawabu ya kutenda mema ya miaka hamsini na kumsamehe madhambi yake na ya wazazi wake ya miaka hamsini.

Tunaomba kwa Mola Atupe tawfiki ya kuwakumbuka wafu wetu hasa wazazi kwa kuwatendea mambo ya heri kwa thawabu yao na kuwazuru makaburini kwa kuwa somea Fatha Amin. Na kwa kuzuru makaburi tutakumbuka kuwa kuna kufa (mauti), hao walikuwa kama sisi sasa hawajiwezi kujisaidia.