read

Mawahhabiyah na Wauaji wa Imamu Husayn (a.s.)

Mara kwa mara baadhi ya watu wajinga husema kuwa wauaji wa Imamu Husayn (a.s.) walikuwa ni Mashia. Ingawa uwongo huo umekwisha kukomeshwa tangu zamani kwa thibitisho zisizopingika, bado uwongo huu ungali ukitembezwa huko na huko, ili kwenda kuitambua hoja hii yenye nguvu, na kuweza kutofautisha baina ya ukweli na uwongo, tutatoa hapa hakika tatu zitakazoongezea kwenye uamuzi usiopingika. Hakika hizi ni:

1. Ni madhehebu ipi yenye kumheshimu na kumfuata Imamu Husayn (a.s.) na ni madhehebu ipi yenye kumpinga?

2. Ni madhehebu ipi inayofikiria kuwa ni wajibu kumlaani Yazid na ni ipi yenye kumtii (au kwa ujumla kutomtakia laana Yazid)?

3. Ni madhehebu ipi inayosikitishwa na kujitenga na maamiri-jeshi wa majeshi ya Yazid yaliyomwua Imamu Husayn (a.s.) na ni ipi yenye kuwatukuza maamiri-jeshi hao na kuwafikiria kuwa ni viongozi wa kidini?

Kweli hizi tatu zitatusaidia katika kuwatambua wale wanaomshutumu na kumkana Yazid na Wafuasi wake wa kisiasa na wale wenye kuwatukuza na kumchukulia Yazid kuwa ni Khalifa apasikaye kutiiwa.